Zlatan Ibrahimovic Aipa Man United Ushindi Dhidi ya Southampton
Ligi Kuu England iliendelea usiku wa August 19 kwa klabu ya Man United
kuwakabribisha Southampton katika dimba lao la Old Trafford kucheza
mchezo wao wa pili wa baada ya mchezo wao wa awali kuibuka na ushindi wa
goli 3-1 dhidi ya AFC Bournemouth ugenini.
Zlatan lifunga goli la kwanza baada ya kupokea krosi maridhawa kutoka
upande wa kulia na Wayne Rooney baadae tena Zlatan alifunga bao la pili
kwa njia ya penati baada ya beki wa kushoto wa Man United Luke Shaw
kufanyiwa madhambi na Jordy Clasie na mechi hiyo kumalizika kwa Man
United kupata ushindi wa 2-0.
No comments:
Post a Comment