Monday 29 August 2016

Hatimaye Drake na Rihanna mambo hadharani

   ukufikie popote ulimepo wewe shabiki wa Robyn Rihanna Fenty ‘Riahanna’ ama Aubrey Drake Graham ‘Drake’. Kwa miezi kdhaa, kukuwepo na tetesi kuwa Rihanna na Drake wnatoka kimahaba licha ya wao kukanusha na kusema kuwa ni washkaji tu!
 Jana hali imekuwa tofauti baada ya mastaa hao kuamua kuanika hadharani mahusiano yao kwa kupeana malovee mbele ya maelfu ya mashabiki waliokuwa umefurika kwenye shoo ya ugawaji wa Tuzo za VMA nchini Marekani.

 

 Kwa sasa sio tena tetesi na mapicha picha ya Instagam tu, bali inasemekana wameamua kuwa wapenzi na kwamba wanataka wazae watoto.
 Drake na Rihanna waliwashangaz watu waliohudhuria shoo hiyo iliyofanyika jana Jumapili usiku baada ya wawili hao kukumbatiana na kupigana mabusu mbele ya umati huku wakigandana kwa sekunde kadhaa kabla ya kuachiana, kuwaacha mashabiki wakishangaa huku wakisema kwa hali ilivyokuwa inaonesha wawili hao wanataka kuishi kama mke na mme.
 Uhusiano waoulikole zaidi miezi michache iliyopita baada ya Rihanna kumshilikisha Drake kwenye baadhi ya nyimbo za albamu yake mpya ya AntiRihanna.
 Ijumaa iliyopita, Drake alifanya sapraizi kwa kununua bango la barabarani jijini Los Angeles na kuliandika maneno ya kumtakia kila la kheri mpenzi wake Rihanna kwenye tuzo hizo za MTV Video Vanguard Award zilizofanyika Jumapili usiku.

 Alichokisema Drake sasa
“Kwa mara ya kwanza nilikutana na Robyn Fenty mwaka,” alisema Drake, akielezea video walioshuti pamoja. “Wimbo uliitwa Pon de Replay na Director wa video hiyo aliikuwa Little X.
 Nilitambulishwa kwake kama mtoto anayecheza background music kwenye migahawa wakati watu wakila chakula chao cha jioni.

 Siyo rahisi kuamini kuwa miaka 11 baadaye sote watatu tumefanya kazi pamoja na kutengeneza wimbo wa Rihanna Work.”



No comments:

Post a Comment