Thursday, 25 August 2016

Mashabiki wamliza Joe Hart

 Mechi ya marudiano ya klabu bingwa Ulaya kuwania kufuzu hatua ya makundi kati ya Manchester City dhidi ya Steaua Bucharest ilikuwa na hisia za aina yake kwa mlinda mlango wa Man City Joe Hart.
 Claudio Bravo akiwa tayari ameshatua katika timu hiyo na akitarajiwa kutangazwa muda mwishoni mwa juma hili, Joe Hart, 29, alipewa unahodha katika mechi ya usiku wa jana ambayo inatajwa huenda ikawa mechi yake ya mwisho akiwa mchezaji wa Manchester City.
 Alikuwa akishangiliwa na mashabiki kwa kila alichokifanya kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo huo.

Wakati wa kipindi cha pili katika mchezo huo, mashabiki wa Manchester City walisimama kwa pamoja na kuimba “Stand up if you love Joe Hart“.

 Alisajiliwa na Man City mwaka 2006 kutoka Shrewsbury Town, Joe ahart alionekana akijitahidi kuzuia machozi lakini akashindwa na kujikuta akiangua kilio.

No comments:

Post a Comment