Saturday 30 May 2015

EDWARD LOWASSA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS WA TANZANIA, JIJINI ARUSHA LEO


 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. SOURCE:http://issamichuzi.blogspot.com/
 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, kumsikiliza  Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia).

Bunge lachachamaa baada ya hotuba ya Waziri wa mambo ya Nje Mhe Bernadi Membe pamoja na hotuba ya upinzani.


China yatakiwa kusitisha ujenzi baharini

Uwanja wa ndege unaojengwa na China katika visiwa vya Spatry
Marekani imetaka kuwepo usitishwaji wa ujenzi wa miradi kwenye maeneo yanayozozaniwa katika bahari ya kusini mwa China.Waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter aliuambia mkutano mkuu wa ulinzi nchini Singapore kuwa tabia ya China eneo hilio imekiuka sheria za kimataifa
Carter amesema kuwa kuvihami kijeshi visiwa bandia ambavyo vinajengwa na China ni hatua inayoweza kusababisha mizozo ya kijeshi.
Matamshi yake yanakuja siku moja baada ya makao makuu ya jeshi la marekani kusema kuwa china imeweka silaha katika moja ya visiwa hivyo.
Bwana Carter anasema kuwa hakutakuwa na suluhu la kijeshi . Hata hivyo amesema kuwa Marekani itaendelea kuwa na jeshi lake katika eneo hilo.

Friday 29 May 2015

Mateso dhidi ya mahabusu Tanzania

Safu ya viongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Uamsho Zanzibar, ambao baadhi yao wamefunguliwa mashitaka ya ugaidi Tanzania Bara.





















Safu ya viongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Uamsho Zanzibar, ambao baadhi yao wamefunguliwa mashitaka ya 
ugaidi Tanzania Bara.
Watuhumiwa wa ugaidi walio kwenye magereza ya Dar es Salaam wanalalamika
 kuteswa kikatili na kudhalilishwa kijinsia wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola wakilazimishwa kukiri makosa wanayoshitakiwa.
Katika Mbiu ya Mnyonge, Mohamed Dahman anahoji ni kwa namna gani tuhuma kama hizi zinatolewa na kunyamaziwa kimya na mamlaka husika katika wakati ambapo dunia inazungumzia utawala wa sheria na haki za binaadamu, zikiwemo za wale walio mikononi mwa vyombo vya dola!
Kusikiliza makala nzima, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
SAUTI NA VIDIO KUHUSU MADA
Mbiu ya Mnyonge yalia na mahabusu Tanzania

Mapambano dhidi ya mauaji ya albino

Symbolbild Albinos in Afrika

Nchini Tanzania mauaji ya watu walio na ulemavu wa ngozi au albino yameripotiwa kuzidi kuongezeka. Wanasiasa, wasanii na wanajamii sasa wanaungana kuelimisha kuhusu mila hii potofu na kuhakikisha kuwa watu hawa wanalindwa.

BAJETI: Wabunge wamshukia Nyalandu

“Mheshimiwa Spika. Naomba Bunge lako tukufu likubali kupitisha makadirio ya matumizi ya jumla ya Sh81,964,541,000 kwa mwaka 2015/2016 kati ya fedha hizo, Sh74,255,391,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh7,709,150,000 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Fedha za matumizi ya kawaida zinajumuisha Sh45,235,955,000 za mishahara ya watumishi na Sh29,019,436,000 za matumizi mengineyo. Fedha za miradi ya maendeleo zinajumuisha Sh5,709,150,000 fedha za nje na Sh2,000,000,000 fedha za ndani.” Nyalandu 
  • Hotuba zote mbili, ya kamati na upinzani, zilieleza kushangazwa na kitendo cha waziri huyo kupinga watalii kulipa tozo mara moja kila wanapoingia katika Hifadhi ya Serengeti na Ziwa Manyara, badala yake kung’ang’ania walipe mara mbili, jambo ambalo ni kinyume na maelekezo ya Bunge.

Siku tatu za kishindo; watano kutangaza nia CCM



  • CCM ipo kwenye wakati mgumu wa kutafuta mrithi wa Jakaya Kikwete katika nafasi ya urais na mwenyekiti wa chama hicho kikongwe nchini baada ya Rais huyo wa sasa kuongoza nchi kwa vipindi viwili vya miaka mitano kila kimoja na hivyo kulazimika kuondoka Ikulu kutokana na utashi wa kikatiba.

Thursday 28 May 2015

Tanzania: Kampeni dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao

 Symbolbild Facebook


Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania TCRA inaendesha kampeni inayolenga kukabiliana na matumizi mabaya ya mitandao ya mawasiliano, ikiwemo ya simu na intaneti, maarufku kama "Futa-Delete-Kabisa.
Mkuu wa idara ya mawasiliano ya umma wa TCRA Inncocent Mungi anazungumza na Iddi Ssessanga kuhusu kampeni hii katika makala ya kinagaugaba. Kusikiliza makala hiyo bonyeza hapo chini.

Wednesday 27 May 2015

Makongoro Nyerere autaka urais.


Mtoto wa Baba wa Taifa, Charles Makongoro Nyerere.
Mtoto wa Baba wa Taifa, Charles Makongoro Nyerere amevunja ukimya juu ya uvumi ulioenea kwamba yeye ni miongoni mwa watu wanaotarajiwa kuchukua fomu ya kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu ujao kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kusema hata yeye anajisikia na yuko tayari kiafya, kiakili na ana nguvu ya kulitumikia Taifa kwenye nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa nchi.
 
Hata hivyo, Makongoro alisema kuwa dhamira hiyo ataiweka wazi kwa kuzungumza na wandishi wa habari siku mbili au tatu kabla ya tarehe iliyopangwa na CCM ya kuanza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
 
Makongoro aliyasema hayo juzi jijini Mbeya wakati akipokea kwa niaba ya familia ya Baba wa Taifa, Tuzo ya Uongozi uliotukuka na Uzalendo ambayo ilitolewa na viongozi wa dini za Kiislamu na Kikikristo mkoani Mbeya kwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwa lengo la kutambua mchango wake kwa Taifa la Tanzania.
 
Makongoro alilazimika kulisema hilo, baada ya watu mbalimbali waliokuwa wakizungumzia wasifu wa Hayati Baba wa Taifa kila mara kugusia uvumi unaomhusisha na kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.
 
“Kwa kuwa kuna maneno yanapita na mimi nimeyasikia, na kwa kuwa nanyi mmenitaka niseme ninachoweza kuwaeleza hata mimi najisikia na niko tayari kulitumikia taifa katika nafasi hiyo (urais), nimesikia CCM wametangaza ratiba ya kuchukua fomu, hivyo ninachoweza kuwathibitishia ni kwamba siku mbili au tatu kabla ya tarehe iliyopangwa na CCM kuanza kuchukua fomu nitazungumza na waandishi wa habari kuelezea uamuzi wangu juu ya suala hilo,” alisema Makongoro.
 
CCM tayari imetangaza ratiba na utaratibu kwa wale wanaotaka kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, na tarehe ya kuanza kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo itakuwa Juni 3, mwaka huu.
 
Aidha, alisema wiki ya kwanza ya kuanza kuchukua fomu za kugombea urais kupitia CCM, atakuwa mjini Dodoma kwa ajili ya ama kuwashuhudia wale wanaochukua fomu hizo au yeye mwenyewe kuchukua fomu.
 
Kwa kauli hiyo, Ni dhahiri kwamba mtoto huyo wa Baba wa Taifa ameingia rasmi kwenye orodha ya makada wa CCM walioonyesha nia ya kutaka kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini anachelea tu kukiuka kanuni na taratibu za Chama chake cha CCM kama atatangaza uamuzi wake mapema.

Saturday 23 May 2015

Yanga kujifua Zanzibar Kagame

Kikosi cha Yanga
Mabingwa mara tano wa Kombe la Kagame, Yanga wanataraji kuweka  kambi Zanzibar ya maandalizi ya michuano hiyo ya klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati itakayofanyika nchini Julai.
 
Wachezaji wa Yanga kwa sasa wapo mapumzikoni baada ya kutwaa ubingwa wa 25 wa ligi kuu ya Bara na kumalizika kwa msimu Mei 9.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Jerry Muro alisema maandalizi ya kambi hiyo yamekamilika.
Yanga itakuwa ikiwania kutwaa ubingwa mwingine wa Kombe la Kagame nyumbani kama inavyopewa nafasi kubwa, na kuwafikia watani wa jadi Simba kama klabu zilizobeba kombe hilo mara nyingi zaidi.

Kamati Kuu yasema akina Lowassa huru

  Lowassa: Ni safari ya matumaini
  Makamba: Safari ya ushindi imeanza
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakiwa kwenye kikao cha Kamati Kuu.
Hatimaye Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imewafutia adhabu makada sita wa chama hicho kwa kuanza kampeni za urais mapema kinyume na kanuni na taratibu za chama.
 
Waliofutiwa adhabu ni mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.

Hatimaye walemavu Mchikichini warejea kwenye vibanda vyao


Siku moja baada ya wafanyabiashara wenye ulemavu wa soko la Mchikichini jijini Dar es Salaam kufunga barabara baada ya kubomolewa meza za biashara zao, serikali imewaruhusu kuendelea na kazi eneo hilo huku ikifanya tathmini ya hasara iliyopatikana.
 
NIPASHE Jumamosi ilishuhudia jana meza za wafanyabiashara hao zilizovunjwa usiku wa kuamkia juzi zikijengwa upya.
 
Wafanyabiashara hao juzi walilazimika kufunga barabara ya Kawawa na Uhuru kwa saa sita baada ya kukuta meza zao za biashara zikiwa zimevunjwa.
 
Akizungumza na gazeti hili jana, mmoja wa wafanyabiashara hao ambaye anayejihusisha na uuzaji wa mabegi sokoni hapo, Mfaume Seleman, alisema kuwa viongozi wao walipokea barua kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.
Alisema barua hiyo imewataka waendelee kufanya shughuli zao katika maeneo waliyotoka au walipokuwa wakifanya biashara zao.
 
Alisema barua hiyo imeeleza kuwa, Serikali imeliona tatizo hilo na kulifanyia kazi kwa kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na uongozi wa wafanyabiashara hao.
 
Seleman alisema kuanzia jana viongozi wao wameanza kukutana na serikali kufanya vikao ili kupata ufumbuzi wa kudumu.
Barua hiyo ambayo NIPASHE imeona inaeleza kuwa, uchunguzi unafanyika na itakapobainika nini kilijiri kwa waathirika Halmashauri ya Ilala itakaa na waathirika ili kuweza kubaini hasara walizopata na fidia

Wednesday 20 May 2015

Wanafunzi UDSM wapigwa mabomu wakidai mikopo.

 
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Cosmas Mwaisobwa.
 
Jeshi  la Polisi Mkoa wa Kinondoni, limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya  Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), wanaoishi katika hosteli za Mabibo ambao walikuwa wakiandamana kudai fedha zao za kujikimu.

Bodaboda walalamikia Polisi.


Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova

Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda zaidi ya 50 wa jijini Dar es Salaam wameandamana hadi katika ofisi za gazeti hili kulalamikia unyanyasaji wanaofanyiwa na polisi jamii. 
Bodaboda hao kutoka maeneo ya Tanki bovu, Kawe na Mwenge wanadai kuwa wamechoshwa na unyanyasaji wanaofanyiwa na polisi jamii ambao wamekuwa wakiwakamata ovyo katika maeneo mbalimbali ya Jiji.
Kalos Meltus, alisema wamekuwa wakikamatwa na kutozwa faini kati ya Sh. 30,000 na 100,00 kila wanapoingia katikati ya Jiji na kudai kuwa wamegeuzwa mtaji wa baadhi ya viongozi kujipatia pesa.
Naye Erasto Matheo, alisema kuwakamata bodaboda katikati ya Jiji kunawaathiri kiuchumi kwa sababu wateja wao wengi wanakwenda mjini hivyo kuendelea kuwazuia ni kuwapa wakati mgumu kimaisha.
“Sababu inayotolewa kwamba sisi watu wa bodaboda tunashiriki vitendo vya uhalifu siyo kweli kwani licha ya kwamba tumekatazwa bado uhalifu unafanyika katikati ya Jiji,” alise

Watumishi kuongezewa mshahara asilimia 13.5.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Manejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani.

Serikali itaongeza mshahara wa watumishi wa umma kwa asilimia 13 .5 katika mwaka ujao wa fedha wa 2015/16.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Manejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani, (pichani),  alisema bungeni wakati akihitimisha mjadala wa bajeti ya ofisi hiyo. 
Hata hivyo, alisema ongezeko hilo litapandisha mishahara ya kima cha chini zaidi huku cha juu kikiongezwa kwa asilimia 3.0.
Awali wabunge wakichangia bajeti yake walitaka mishahara ikipandishwa iwanufaishe watumishi wa chini kwa vile inapopanda kwa asilimia 10 mtumishi wa chini ambaye mshahara wake ni Sh. 265,000 anapata nyongeza ya Sh. 30,000.
Hata hivyo, kwa wenye mishahara inyoanzia Sh. 3,000,000 wanafaidika zaidi kwa nyongeza ya 300,000.
Kombani alisema wenye mishahara minono wanalipa kodi kubwa ya mshahara ya lipa kiasi unavyopata (Paye) kwa asilimia 30.
Kwa kutumia maelezo hayo mtu mwenye mshahara wa Sh. 3,000,000, atalipa Paye ya Sh. 900,000.
Akizungumzia ajira ya walimu alisema taifa limeajiri walimu wa kutosha na sasa inajielekeza kwenye maeneo mengine ya kilimo na afya.
Alisema mwaka unaoishia wa 2014/15 walimu walikuwa 31,000 wakati sasa wataajiriwa 28,957.
Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye, alitaka sheria irekebishwe ili mawaziri wapewe pensheni.

Tuesday 19 May 2015

Tanzania yamshikilia muasi wa ADF

Polisi nchini Tanzania wamethibitisha kuendelea kumshikilia Jamil Mukulu ambaye ni kiongozi wa waasi wa ADF wa Uganda. Mukulu anayekabiliwa na tuhuma kadhaa ikiwemo mauaji amefikishwa mahakamani jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaa utaratibu wa kumrudisha Uganda ili akashtakiwe rasmi huko. Kiongozi huyo na kundi lake la ADF wanadaiwa kuhusika na uhalifu katika nchi za Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mahakama imempa hadi tarehe 22 mwezi huu kuwasilisha pingamizi lake au la atarejeshwa Uganda. Mwandishi wetu Kulthum Maabad amezungumza na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Tanzania, Diwani Athuman kuhusu hatua hiyo