Wednesday 31 May 2017

ZILIZOMUBASHARA KATIKA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 01 2017

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjKg6F9YaNqyo2L3j12OKbQC_YJ-GjO4xEWBvYO3NaYPrtgdOwza7FiOw41z6nlMrPRDW2te9eLrGZ5KfBYXr2j9SDFjBekTWxtN5kgTR6X0RqMWLEsinXTftn3OSmSAY2pqxcBylH70IY/s1600/New-Doc-2017-06-01_21.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjLMAqY-Fz_LLHiTktwmNGRYKz5BfGQDFflFMYu4cAZVrI7-4-ykPl08Md7r81ahLw5pGs4JaZOch0qha7s7KEmVZETa9z-ry0T2-ugqE-05ImCDsQx_BWzz9bnU4AxjlwqLzPnxrOUbH0/s1600/New-Doc-2017-06-01_22.jpg

Elimu zaidi inahitajika kuhifadhi mazingira nchini

maz
WAKATI Mataifa mbalimbali yanaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani yanayofikia kilele chake hapo Juni 5, 2017, takriban hekta 372,000 za misitu hupotea kila mwaka nchini Tanzania kutokana na shughuli mbalimbali. Mwandishi Beatrice Lyimo wa Idara ya Habari – MAELEZO anaelezea zaidi. Kwa miaka mingi siku ya Mazingira duniani imekuwa ikiadhimishwa kwa Wadau katika nchi mbalimbali kuchukua hatua chanya zinazohusu mazingira. Siku hii pia imekuwa ni sehemu ya kampeni ya utoaji elimu juu ya maswala yanayojitokeza kuhusiana na mazingira. 
Kauli mbiu katika maadhimisho ya mwaka huu inasema “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira” ikihamasisha jamii kuwa na urafiki endelevu na mazingira asilia ambapo kila mtu anapaswa kutambua, kufurahi, kujivunia na kulinda uzuri wa mazingira asilia na kuhamasishana ili kuyatunza na kuyahifadhi. 
Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingi Barani Afrika na duniani kwa ujumla imeendelea kuathirika kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli mbalimbali zikiwemo za kilimo, ufugaji, ujenzi n.k  Mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu aliagiza kutofanyika kwa maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika ambayo yalizoeleka na badala yake Watanzania waadhimishe siku hiyo kwa kufanya usafi. Mtazamo wa wengi kuhusiana na maelekezo ya Dkt. Magufuli ulilenga zaidi katika kubana matumizi mabaya ya fedha za Serikali. 
Pamoja na mtazamo huo Mhe. Rais aliona mbali zaidi, kwani usafi wa mazingira unasaidia kudhibiti milipuko ya magonjwa kama vile kipindupindu, ambayo yanaigharibu Serikali fedha nyingi zaidi ya zile ambazo zingetumika katika kufanikisha maadhimisho hayo. Hivyo uamuzi alioutoa Mhe. Rais utakumbukwa zaidi wakati huu ambapo nchi mbalimbali zinaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani. 

Niko tayari kuondoka Barcelona- Iniesta

Nohodha wa Barcelona, Andres Iniesta bado ana ndoto za kuzeekea kwenye Liga ya La Liga, huku akisema kwamba iwapo atatakiwa kuondoka yupo tayari kufanya hivyo.
Iniesta mwenye miaka 33 mkataba wake unamalizika katikati ya mwaka 2018 na hatima yake imebaki njiapanda. Msimu huu alianza mechi 13 za ligi msimu huu.
Kiungo huyo alisema bado ndoto zake ni kustaafu maisha ya soka akiwa kwenye klabu yake ya Barcelona ambayo alijiunga  tangu akiwa na miaka 12, akichezea timu ya vijana.

Mbowe amzuia Mbunge lucy kuchangia bungeni

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe amesema alipopata taarifa ya kifo cha Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo alijaribu kumzuia mtoto wa marehemu, Lucy Owenya asichangie bungeni  lakini alishindwa.
Mbowe ameyasema hayo leo Jumatano wakati akilitangazia bunge kuhusu kifo cha Mwenyekiti huyo wa Chadema, mkoa wa Kilimanjaro.
Owenya ni mbunge wa viti maalum wa chama hicho na mtoto wa kada huyo mkongwe wa Chadema.

Matukio Bungeni

sab1
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akiingia bungeni huku akiongozwa na askari wa bunge  Bunge ili kuanza  kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
sab2 sab4
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akisoma dua ya kuliombea Bunge katika  kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
sab5
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Dk.Medard Kalemani akiwasilisha Randama za Makadirio na Matumizi ya Wizara yake  kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
sab6
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
sab7
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
sab8
Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Mhe.George Masaju akifuatilia jambo kutoka kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk.Suzan Kolimba  katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira,Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama.
sab9
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Prof Jumanne Maghembe akimskiliza Mbunge wa Mtama(CCM) Mhe.Nape Nnauye katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
sab10
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Khamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
sab11
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
sab12
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe.Dk Charles Tizeba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
sab13
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Ritta Kabati akiuliza swali katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
sab14
Mbunge wa Arumeru Mashariki(CHADEMA) Mhe.Joshua Nassari akifurahi jambo na Mbunge wa Momba(CHADEMA) Mhe.David Silinde katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
sab15
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mhe.Catherine Ruge akiuliza swali katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017. 
sab16
Mbunge wa Iramba Mashariki(CCM) Mhe.Allan Kiula akiuliza swali katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.

Jumla ya Mizani 448 Yahakikiwa Mkoani Mwanza Ikiwa ni Maandalizi ya Ununuzi wa Pamba.

unnamed
Wakala wa Vipimo (WMA) Tanzania imeendelea na zoezi la utoaji wa elimu  pamoja na uhakiki wa mizani kwenye  makampuni mbalimbali  ya wafanyabiashara Mkoani Mwanza   katika  Wilaya za  Kwimba, Magu, Misungwi  na Sengerema ikiwa ni maandalizi ya msimu wa Pamba.
Akizungumza na Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoani Mwanza  Bwana Hemed Kipengele  alisema  jumla ya mizani 448 tayari imekaguliwa kutokana na  makampuni manne ambayo  tayari yamekagulisha mizani yake na imekutwa ikiwa sahihi  ambayo ni  ICK (T) LTD  ambao walikuwa a mizani 184, SM HOLDING wenye jumla ya mizani 85 pamoja na   NYANZA COTTON  ambao walikuwa na mizani 179. Meneje aliongezea kuwa zoezi hili la utoaji elimu pamoja na uhakiki wa mizani itakayotumika kununulia Pamba linaendelea kwa Mikoa yote inayolima  Pamba ambayo ni Shinyanga, Simiyu, Geita, Kagera, Tabora pamoja na Mara.
Bwana Kipengele alisema wanatarajia kutembelea jumla ya vijiji 101 ambavyo vina jumla ya vituo vya kuuzia Pamba 150 ili waweze  kutoa elimu na kufanya kaguzi za kushutukize kwa wanunuzi wa Pamba ili kuona kama mizani waliyopima na ikaonekana ni sahihi itaendelea kununua Pamba ya wakulima kwa vipimo sahihi.
 Meneja Kipengele  aliwasihi baadhi ya wakulima wanaolalamikiwa kuweka maji, kokoto pamoja na mchanga kwenye Pamba kwa ajili ya kuongeza uzito waache tabia hiyo mara moja  sababu Sheria ya vipimo ipo na inafanyakazi kwa pande zote mbili muuzaji na mnunuzi wote kwa pamoja hawatakiwi kufanya udanganyifu wowote katika biashara.
 Kipengele alisema Sheria ya Vipimo Sura 340 inawataka Wakala wa Vipimo  kuhakiki na kupiga chapa vipimo vyote vinavyotumika katika biashara pia Wakala wa Vipimo imeongeza na uwekaji wa  sticker kwa kipimo kitakachokuwa tayari kimehakikiwa ili iwe rahisi kwa wakulima kuona na kutambua mizani iliyokaguliwa na kuruhusiwa kwa biashara kwa mwaka husika.

Man United ndio klabu yenye thamani kubwa Ulaya


Manchester United ndio klabu yenye thamani kubwa barani Ulaya ikiwa na thamani ya Yuro bilioni 3 kulingana na kampuni ya biashara ya KPMG.
Mabingwa hao wa kombe la Yuropa wanaongoza katika orodha ya thamani ya Kampuni ya KPMG, ikiwa mbele ya mabingwa wa Uhispania Real Madrid na Barcelona.
Utafiti huo uliangazia haki za kupeperusha matangazo, faida, umaarufu, uwezo kimchezo na umiliki wa uwanja.
Katika utafiti huo uliofanyiwa timu 32, vilabu vya Uingereza vilitawala orodha hiyo vikijaza nafasi sita kati ya 10 bora.
Andrea Sartori ambaye ni mkurugenzi wa maswala ya michezo katika kampuni ya KPMG amesema kuwa kwa jumla thamani ya soka imekuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
''Huku hilo likielezewa kufuatia kuimarika kwa matangazo, operesheni za biashara za kimataifa, uwekezaji wa vifaa vya umiliki wa kibinafsi, vifaa vya kisasa pamoja na usimamizi mzuri ni vigezo muhimu vya ukuaji huo'', alisema.
Kuhusu haki za matangazo, ligi kuu ya Uingereza inaongoza ligi nyengine za Ulaya ijapokuwa ligi nyengine zimeweka mikakati kupigania mashabiki wa kimataifa.
Vilabu kumi bora vyenye thamani ya juu kibiashara

1.Manchester United -Euro3.09bn

2.Real Madrid - Euro2.97bn

3.Barcelona - Euro2.76bn

4.Bayern Munich - Euro2.44bn

5.Manchester City - Euro1.97bn

6.Arsenal - Euro1.95bn

7.Chelsea - Euro1.59bn

Ndesamburo amefariki Dunia leo

  Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema) Philemon Ndesamburo amefariki dunia Ghafla leo, wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi.
Katibu wa Chadema, Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amethibitisha kifo hicho na kueleza kuwa wataendelea kutoa taarifa zaidi juu ya kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe.

IGP Sirro atangaza dau la milioni 120

Siku kadhaa baada ya Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani kutangaza zawadi ya Sh. milioni tano kwa mwananchi ambaye atafanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa 12 ambao limedai wanajihusisha na mtandao wa mauaji yanayoendelea katika Wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji, Basi hii Leo Mei 31, 2017 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Sirro ameongeza dau hilo mpaka kufikia shilingi Milioni 10.
Katika mkutano wake wa Kwanza na Vyombo vya Habari Jijini Dar es salaam tangu aapishwe, IGP Sirro amewaambia waandishi wa habari kuwa Jeshi hilo linaendelea kuwasaka watuhumiwa hao.
Kwamujibu wa ripoti Polisi imepata picha za baadhi ya watuhumiwa na fununu za mahali wanapopenda kutembelea mara kwa mara.
Kamanda Lyanga aliwataja watuhumiwa hao pamoja na mwanzilishi wa mtandao huo wa mauaji kuwa ni Abdurshakur Ngande Makeo, Faraj Ismail Nangalava, Anaf Rashid Kapera, Said Ngunde na Omary Abdallah Matimbwa.
Wengine ni Shaban Kinyangulia, Haji Ulatule, Ally Ulatule, Hassan Uponda, Rashid Salim Mtulula, Sheikh Hassan Nasri Mzuzuri na Hassan Njame.
Hata hivyo ripoti za jeshi hilo zinasema, waimegundua kuwa watuhumiwa hao hupendelea kutembelea maeneo ya kisiwa cha Simbaulanga, kisiwa cha Saninga katka kijiji cha Nchinga na kijiji cha Mfesini kata ya Nyamisati pamoja na maeneo mbalimbali ya wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga.

Taarifa ya Mamlaka ya hali ya Hewa

Marekani wafanya majaribio mfumo wa kutegua mabomu

Mfumo wa kutegua makombora wa Marekani ICBM
Marekani kwa mara ya kwanza imefanikiwa kuufanya majaribio mfumo wake wa kudungua makombora ya masafa marefu ICBM kulingana na maafisa.
Mfumo huo wa ardhini uliwekwa katika kambi moja ya kijeshi mjini California na kudungua kombora la masafa marefu kulingana na kitengo cha ulinzi wa makombora MDA.
Pentagon imesema kuwa majaribio hayo yalikuwa yamepangwa muda mrefu uliopita, lakini yanajiri huku kukiwa na wasiwasi mkubwa na Korea Kaskazini.
Majaribio hayo yamefanyika baada ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio kombora lake la tisa mwaka huu.
Mkurugenzi wa kitengo hicho cha ulinzi wa makombora Admirali Jim Syring amesema kuwa jaribio hilo ni hatua muhimu.
''Mfumo huu ni muhimu kwa ulinzi wa taifa letu na jaribio hili ni thibitisho kwamba tuna uwezo mkubwa dhidi ya tishio'', alisema siku ya Jumanne.
Lilikuwa jaribio la kwanza dhidi ya kombora la masafa marefu kwa mfumo huo wa ardhini GMD.
Mfumo huo ulirushwa kutoka Kwajalein Atoll katika kisiwa cha Marshal juu ya anga ya Pacific, kitengo hicho kilisema katika taarifa iliotolewa.

Tuesday 30 May 2017

ZILIZOGONGA VICHWA VYA HABARI KATIKA KURASA ZA MBELE MAGAZETINI LEO MEI 31 2017




Yaliojiri leo Bungeni Dodoma Mei 30 2017

NAJMA
Mwenyekitiwa Bunge la JamhuriyaMuunganowa Tanzania Mhe. Najma Giga akiongoza kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
ISAC
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
PIX 3 Mhe Waziri Mkuu na Sakaya
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Mbunge wa Kaliua(CUF) Mhe.Magdalena Sakaya katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
PIX 4 Ndalichako
Waziri wa Elimu,Sayansi  na Teknolojia Mhe,Prof.Joyce Ndalichakoakijibumaswalimbalimbaliyawabungekatikakikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
PIX 5 Mhe.Kairuki
WaziriwaNchiOfisiyaRaisUtumishinaUtawala Bora Mhe.AngelinaKairuki akijibu maswali mbalimbaliya wabungekatikakikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
PIX 6 kigwangala
NaibuWaziriwaAfya,MaendeleoyaJamii,Jinsia,WazeenaWatotoMhe.KhamisKigwangallaakijibumaswalimbalimbaliyawabungekatikakikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
PIX 7 Mhe.Kolimba
NaibuWaziriwa Mambo yaNjenaUshirikianowaAfrikaMasharikiMhe.Dk.SusanKolimbaakijibumaswalimbalimbaliyawabungekatikakikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
PIX 8 Mhe.Mwijage
WaziriwaViwanda,BiasharanaUwekezajiMhe. Charles Mwijageakijibumaswalimbalimbaliyawabungekatikakikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
PIX 9 Mhe.Mpango
WaziriwaFedhanaMipangoMhe.Dk.PhilipMpangoakisomaHotubayaMakadirioyaMapatonaMatumiziyaWizarayaFedhanaMipangokwamwakawaFedha 2017/2018 katikakikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.  
PIX 10 Mhe.Faida
MbungewaVitiMaalum (CCM) Mhe.FaidaBakarakiulizaswalikatikakikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
PIX 11 Mhe.Amina Mollel
MbungewaVitiMaalum (CCM) Mhe.AminaMollelakiulizaswalikatikakikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
PIX 12 Mwakyembe na Wambura
WaziriwaHabari,Utamaduni ,SanaanaMichezoMhe.Dk.HarrisonMwakyembe akizungumza jambo naNaibu wake Mhe.AnastaziaWambura katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.
PIX 14 Mhe Mhagama na Msigwa
WaziriwaNchiOfisiyaWaziriMkuuSera,Bunge,Ajira,Kazi,VijananaWatuwenyeUlemavuMhe.JenistaMhagamaakijadilijambonaMbungewaIringaMjini(CHADEMA) Mhe.PeterMsigwa katika kikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017. 
PIX 15 George Masaju
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.GeorgeMasaju akifafanua jambo katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11leoMjini Dodoma Mei 26, 2017.Kushoto kwakeni Waziri waNchi Ofisi yaWaziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira,Kazi,VijananaWatuwenye UlemavuMhe.JenistaMhagama naKulia niNaibuWaziri waNishati naMadiniMhe.Dk.MedardKalemani.
PichazotenaDaudiManongi,MAELEZO,DODOMA.

Ziara ya Makamu wa Rais mkoani Mara

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kufanya ziara rasmi ya siku tatu kuanzia tarehe 05 Juni, 2017 Mkoani Mara. 
Kwa mujibu wa ratiba ya Mkoa, Mhe Samia atatembelea Wilaya ya Tarime, katika Kituo cha Afya cha Nyamwaga kinachojengwa na wananchi kwa msaada wa Mgodi wa Acacia North Mara. 
Pia, Mhe. Makamu wa Rais atapata fursa ya kutembelea Bonde la Mto Mara kunakokusudiwa kuanza kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari. Mchana siku hiyo hiyo atafanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Bisarwi; katika eneo hilo kunakusudiwa kujengwa kiwanda cha sukari. 
Aidha tarehe 6/6/2017 Mhe. Makamu wa Rais ataenda Wilaya ya Serengeti ambapo ataweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Wilaya; mchana atafanya Mkutano wa Hadhara katika Uwanja wa Mbuzi, Mugumu mjini. 
Tarehe 7/6/2017 Mhe. Makamu wa Rais atakuwa Musoma ambapo ataweka jiwe la msingi kwenye barabara ya km.9.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Musoma. Pia atatembelea kiwanda cha Samaki cha Musoma Fish Processors (T) Ltd na kufanya Mkutano wa Hadhara katika uwanja wa Mukendo Musoma Mjini. 

Mwita Waitara:Asilimia kubwa ya majibu Mawaziri ni uongo


Mwita Waitara Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) leo aliwashambulia mawaziri wa Rais Magufuli kwa kueleza kuwa majibu yao asilimia kubwa ni ya uongo,
Mwita ameelekeza mashambulizi hayo leo bungeni wakati alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa kudai kuwa majibu yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliani, Isack Kamwelwe ni asilimia tano tu ya swali lake na asilimia 95 ni uongo.
“Mimi ni mwalimu wa hisabati na kemia nimekuwa nisahihisha mitiani ya serikali na kama ningekuwa nasahisha mitihani ya mawaziri wewe ningekupa asilimia tano tu kati ya mia majibu niliyouliza imejibiwa asilimia tano tu yaliyobaki ni uongo.
“Inaonesha waziri hauna taarifa sahihi ya miradi ya maji ya kata nilizozitaja katika swali la msingi Je, huko tayari sasa uniletee taarifa sahihi.
“Je, kwa sasa hupo tayari nikukutanishe na akina mama ambao wanakumbana na adha ya kutafuta maji na kulazimika kununua maji kwa sh. 500 kwa ndoo ili uweze kusikiliza kilio chao juu ya kukosekana kwa maji?” alihoji Waitara katika swali lake la nyongeza.
Awali katika swali la msingi Waitara alitaka kujua serikali itakamilisha lini miradi ya maji ya kata za Chanika, Kipunguni na Majohe ili wananchi wa kata hizo na maeneo ya jirani wapate maji ya uhakika.


Matajiri Walivyomiminika na Magari ya Bei Mbaya kmzika Ivan wa Zari

  watu wengi walikuwa wakiomboleza kifo cha Ivan Semwanga, matajiri wakubwa na watu maarufu katika jiji la Kampala, waliitumia fursa hiyo kujitokeza na kuonyesha magari yao ya bei mbaya.
Wakati ibada ya mazishi ya Ssemwanga iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Paul la Namirembe mchana huu, matajiri wengi walijitokeza katika msururu mrefu ambao ulisababisha msongamano wa magari katika barabara ya Namirembe.
Pamoja na magari hayo kuwa ya bei kubwa, mengi yalikuwa na majina ya wamiliki wake badala ya namba za usajili na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa watu waliohudhuria mazishi hayo.
Matajiri maarufu kama Jack Pemba, Lwasa, Mugisha na  mwanamuziki  Bebe Cool, walikuwa miongoni mwa watu maarufu waliohudhuria ibada hiyo.
Ivan Semwanga alifariki katika Hospitali ya Biko Academy nchini Afrika Kusini, Alhamisi wiki iliyopita kutokana na ugonjwa wa moyo na anazikwa leo nyumbani kwao Kayunga.