Wednesday 30 November 2016

MAGAZETI YA LEO 01 DEC 2016

Arsenal kumkosa Oliver Giroud

Mchezaji wa klabu ya Arsenal, Mfaransa Oliver Giroud ataukosa mchezo wa EFL Cup dhidi ya Southampton na kwa kuwa majeruhi.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ameuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa Oliver Giroud atakosekana napia amezungumzia kuhusu mchezaji Debuch ambaye amesema kuwa alifanyiwa vipimo lakini bado majibu hayatoka.
Mshambuliaji Lucas Perez anatarajiwa kuanza baada ya kupona maumivu ya enka yaliyomuweka nje kwa wiki tano.

Msajili: Haiwezekani watumishi wa umma kuiba fedha za kwenye akaunti maalum

  Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru amesema haiwezekani kwa watumishi wa umma kuiba fedha zinazowekwa kwenye fixed deposit accounts(akaunti maalum) kwa sababu miamala ya benki ni ya uwazi.
 Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Mafuru alisema hizo ni tuhuma tu na Serikali imemwagiza CAG kuchunguza.
"Nimefanya kazi kazi kwenye taasisi za benki kwa miaka 20, sijawahi kuona watumishi wa umma wakichota hela kwenye fixed deposit account.
 Pale kwenye benki kuna miamala ya aina mbili tu, ya kuweka na kutoa. Usipoweka wazi wakati wa kuweka, siku utakapozitoa itaonyesha tu," alisema Mafuru.
 Alisema hakuna kosa kwa taasisi za serikali kuweka fedha kwenye akaunti hizo, lakini serikali sasa imeamua kuzihamishia BOT ili iwe rahisi kuzifuatilia.

Zaidi ya watu 16,000 wakosa makazi nchini Syria

Baadhi ya familia zilizokosa makazi nchini Syria
  Umoja wa matifa umesema takribani raia 16,000 wametawanyika nchini Syria baada ya majeshi ya serikali kusonga mbele kuukamata mji wa Aleppo uliokuwa ukishikiliwa na waasi.
Mkuu wa misaada ya kibinadamu wa umoja wa mataifa Stephen O'Brien amesema maelfu ya watu wengine wanatarajiwa kuukimbia mji huo kutokana na mapigano yanayoendelea na kuimarika katika siku zijazo.
 O'Brien ameonesha wasiwasi kuhusu hatma ya raia hao wanaoyakimbia mapigano na kuainisha kuwa yanatia shaka.majeshi na wapiganaji wa jeshi la Syria wamekamata theluthi mbili ya mji uliokuwa ukishikiliwa na waasi Mashariki ya Aleppo tangu mwishoni mwa juma.

Roma avurugwa na mashabiki

Roma
Msanii wa Hip Hop kutoka Bongo, Roma Mkatoliki, amesema anashangazwa na kitendo cha mashabiki kupenda zaidi muziki wa nje kuliko ule wa wasanii wa hapa nyumbani.
Roma amesema yeye kama msanii kitu kama hicho kinamuumiza na hajui iwapo ni thamani ya msanii imeshuka hapa nyumbani, au ni kweli muziki wa nje ni mzuri kuliko hapa nyumbani.
Kitendo hicho cha Roma kimeungwa mkono kauli ya MC Koba ambaye naye alishawahi kulalamika kitu kama hicho, na kusema kuwa kinaua muziki wa ndani na kupoteza matumaini ya wasnaii wa hapa nyumbani.

Bosi CIA amuonya Trump kuhusu mkataba wa nyuklia

 John Brennan
Katka mahojiano aliyofanya na shirika la utangazaji la Uingereza  BBC, John Brennan amemshauri Rais mpya kuihofia Urusi na ahadui zake na kuilaumu nchi hiyo kwa mateso makubwa ya binadamu nchini Syria.
Wakati wa Kampeni za urais nchini Marekani Trump alitishia kufuta makubaliano ya Nukilia yaliyofikiwa kati ya Marekani na Iran na kugusia kufanya kazi kwa karibu na Urusi.
Brennan atajiuzulu nafasi hiyo mwezi Januari baada ya kulitumikia shirika hilo kwa miaka minne.

Donald Trump

Mbunge Waitara awatembelea wahanga wa Bomoa bomoa Kivile

Picha mbalimbali za mbunge waitara akiwa na wahanga walio bomolewa nyumba zao katika eneo la kivule..









Habari Picha

tb
 Mwenyekiti Kamisheni ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bahame Nyanduga akitoa utambulisho wakati wa mdahalo wa Taasisi za Serikali, Dini na Asasi za Kiraia kuelekea maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
tb-1
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad akisisitiza jambo wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Suzan Mlawi kwenye mdahalo wa Taasisi za Serikali, Dini na Asasi za Kiraia kuelekea maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
suzi
Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Suzan Mlawi akisisitiza jambo wakati akifungua mdahalo wa Taasisi za Serikali, Dini na Asasi za Kiraia kuelekea maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
sz
Baadhi ya washiriki wa mdahalo wa Taasisi za Serikali, Dini na Asasi za Kiraia wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Suzan Mlawi (hayupo pichani) wakati wa mdahalo wa Taasisi za Serikali, Dini na Asasi za Kiraia kuelekea maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
war
 Baadhi ya washiriki wa mdahalo wa Taasisi za Serikali, Dini na Asasi za Kiraia wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Suzan Mlawi (hayupo pichani) wakati wa mdahalo wa Taasisi za Serikali, Dini na Asasi za Kiraia kuelekea maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
wp
Washiriki wa mdahalo mdahalo wa Taasisi za Serikali, Dini na Asasi za Kiraia kuelekea maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Suzan Mlawi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
hoji
 Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa mdahalo wa Taasisi za Serikali, Dini na Asasi za Kiraia kuelekea maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Eliphace Marwa –Maelezo.

Rungwe amtaka Profesa Lipumba awaombe radhi wana-CUF, Watanzania

. Wakati pande mbili zinazosigana ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) zikiendelea kulumbana, Mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe amemtaka Profesa Ibrahimu Lipumba kuwaomba radhi Watanzania.
Rungwe ambaye alikuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, alitoa ushauri huo alipofanya mahojiano na gazeti hili jijini hapa. Akiuzungumzia mgogoro uliomo ndani ya chama hicho alisema busara inahitajika kurekebisha kasoro zilizojitokeza.
“(Profesa) Lipumba anatakiwa akubali kuwa alifanya maamuzi kwa pupa na alitumia zaidi uprofesa badala ya busara. Anatakiwa awaombe radhi wafuasi wa chama hicho na Watanzania kwa ujumla kwa uamuzi wake wa awali,” alisema Rungwe.
Agosti mwaka jana, Profesa Lipumba alimuandikia barua katibu mkuu wa chama hicho akimjulisha juu ya azma yake ya kujiondoa kwenye uenyekiti. Wakati akifanya hivyo, taifa lilikuwa likijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais.
Mwaka mmoja baada ya kuandika barua hiyo, Profesa Lipumba aliandika nyingine na kutengua uamuzi huo. Alitaka kurudi kwenye nafasi yake ya uenyekiti ili aendelee kukitumikia chama hicho.
Hatua hiyo ilileta mvutano miongoni mwa wanachama, viongozi na baraza la wadhamini ambao waligawanyika pande mbili, moja ikitaka mwenyekiti huyo arudi kwenye nafasi yake huku wengine wakipinga.
Mvutano huo ulikolea baada ya Mkutano Mkuu wa CUF kujadili na kupitisha barua yake yake ya kujiuzulu. Baadaye, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa iliingilia kati mgogoro huo na kutangaza kumtambua mwenyekiti huyo na sasa mgogoro huo upo Mahakama Kuu.
Wakati anajiondoa kwenye majukumu ya kila siku ya chama hicho na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida, Profesa Lipumba alieleza kutoridhishwa kwake na uamuzi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao alikuwa mwenyekiti mwenza kumkaribisha Edward Lowassa kuwa mgombea urais .
Kwa kuzingatia hayo yote, Rungwe alisema kwa mtu yeyote anayefuatilia mwenendo wa chama hicho na upinzani kwa ujumla, ataona kilichofanywa hakikuwa sahihi, hivyo ni muhimu wa mhusika kuwa muungwana kwa kuomba msamaha.
“CUF ilivurugika kwa muda huo lakini upinzani kwa ujumla umeimarika,” alisema mwenyekiti huyo wa Chaumma.

Trump kutangaza baraza lake la mawaziri

Trump

Rais mteule wa Marekani Donald Trump anajiandaa kutangaza mawaziri zaidi watakaohudumia utawala wake.
Ripoti zinasema kwamba Trump atamteua mshirika wake wa kibiashara wa zamani Steven Mnuchin kama waziri wa fedha.
Wawili hao walikuwa wanamiliki Goldman Sachs, kampuni ambayo Trump aliikashifu wakati wa kampeni zake.
Pia ameshiriki mazungumzo na Mitt Romney, ambaye anakisiwa kuwa mwaniaji wa wadhfa wa waziri wa mambo ya kigeni.
Bwana Romney aliyewania urais kwa tiketi ya chama cha Republican mwaka 2012, kwa wakati mmoja alimwita Trump mtu muongo

Mamia kupoteza ajira vituo mafuta

MAMIA ya watu walioajiriwa katika vituo mbalimbali vya kuuzia mafuta maarufu kama ‘petrol stations’ wako katika hatari ya kupoteza ajira zao , imefahamika.
Hali hiyo inatokana na kusuasua kwa mauzo ya bidhaa hiyo, huku chanzo kimojawapo kikitajwa kuwa ni matokeo ya hatua mbalimbali za Serikali ya awamu ya tano katika kubana matumizi.
Uchunguzi uliofanywa na Fofam-mediablog kwa siku kadhaa umebaini kuwa tishio hilo ni kubwa zaidi katika baadhi ya vituo baada ya wastani wa mauzo yake kwa siku kuporomoka katika siku za hivi karibuni hadi kwa kiwango cha takribani asilimia hamsini.
Aidha, uchunguzi huo umebaini kuwa hadi sasa, tayari baadhi ya kampuni zinazomiliki vituo vya bidhaa hiyo zimeanza kuchukua uamuzi mgumu wa kuviuza au kuvikodisha kwa watu wengine.

Mwanasayansi nguli adai baada ya miaka 1,000 dunia itateketea

 Dunia tunayoishi haitokuwa kama ilivyo sasa baada ya miaka 1,000.
Mwanasayansi nguli na mnajimu, Stephen Hawking, amesema binadamu hawatoweza tena kuishi katika ardhi ya dunia kwa miaka 1,000 nyingine, na chanzo kitakuwa yale yale, mabadiliko ya tabia nchi, mabomu na roboti.
Stephen Hawking
Akiongea kwenye chuo kikuu cha Oxford wiki kadhaa zilizopita, Hawking alisema njia pekee itakayotupa maisha zaidi, ni kuhama kwenye dunia hii na kwenda kutengeneza makoloni kwenye sayari zingine.
“Although the chance of a disaster to planet Earth in a given year may be quite low, it adds up over time, and becomes a near certainty in the next 1,000 or 10,000 years,” alisema.
“By that time we should have spread out into space, and to other stars, so a disaster on Earth would not mean the end of the human race.”

Pamoja na hivyo, Hawking alikuwa na maneno ya faraja: Remember to look up at the stars and not down at your feet. Try to make sense of what you see, wonder about what makes the universe exist,” he said. “Be curious. However difficult life may seem, there is always something you can do and succeed at. It matters that you don’t just give up.”

TFF ya kanusha taarifa ambazo zilisambaa katika mitandao

Zimekuweko taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari na mitandao kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeandaa shindano maalum mwezi Desemba.
Mwezi Desemba hakuna shindano lolote jipya litakalaondaliwa na TFF zaidi ya mashindano yake ya kawaida ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) na Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Michuano mingine inayosimamiwa na TFF ni Ligi Kuu ya Taifa ya Wanawake (TWPL), Ligi Kuu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 (TFFU20L), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), Ligi Daraja la Pili (SDL) na Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL).
Ikumbukwe tu kwamba kwa sasa, timu za VPL ziko likizo na ni wakati wa Klabu kufanya mchakato wa usajili wa Dirisha Dogo. Duru la pili lenye mizunguko 15 inatarajiwa kuanza Desemba 17, 2016 kama ilivyopangwa hapo awali.

Ajali nane za ndege zilizokumba timu za spoti

 Ndege iliyokuwa imebeba timu ya Brazil ilianguka nchini Colombia
Ndege iliyokuwa imebeba timu ya soka ya Brazil imeanguka wakati ilipokuwa ikikaribia mji wa Medellin nchini Colombia na kuwaua karibu watu wote 81 waliokuwa ndani yake.
Ndege hiyo ilikuwa na wachezaji wa timu ya Chapecoense, waliokuwa safarini kwenda kucheza fainali ya mashindano ya kimataifa ya vilabu vya Amerika ya Kusini.
Chapecoense ndicho klabu ya hivi punde kukumbwa na mkasa kama huo.
Mikasa mingine inayokumbukwa ni:
1949 Il Grande Torino
Mwezi Mei mwaka 1949 ndege iliyokuwa imeibeba timu ya Torino ilianguka eneo la milima karibu na Turin na kuwaua watu 31.
Wakati huo timu ya "Il Grande Torino" ilikuwa klabu kubwa nchini Italia baada ya kupata ushindi mara tano.
Kablu hiyo hikuweza kujikwamua kufuatia ajali hiyo ambayo iliangamiza karibu kikosi chote.

1958 Ajali ya Munich
 Ndege iliyokuwa imebeba timu ya Manchester United ilianguka mjini Munich
Ndege iliyokuwa imebeba timu cha Manchester United ambayo ilikuwa wakati huo ilijulikana kama "the Busby Babes" ilianguka ilipokuwa ikipaa wakati timu ilikuwa ikirudi kutoka mechi ya bara ulaya dhidi ya klabu ya Red Star Belgrade.
Wachezaji 8 wa United na watu wengine 15 waliaga dunia.

1961 timu ya kuteleza kwenye theluji ya Marekani
Wanachama wote 18 wa timu ya kuteleza kwenye theluji ya Marekani walikuwa miongoni mwa watu 73 waliokufa baada ya ndege yao kuanguka karibu na uwanja wa ndege wa Brussels wakati ilipokuw ikitua.
Timu hiyo ilikuwa safarini kwenda mji wa Prague, huko Czechoslovakia, kushiri mashindano na dunia ambayo wakati huo yalifutwa.
1972 Alive
Siku ya Ijumaa tarehe 13 Oktoba mwaka 1972, ndege iliyokuwa imebeba timu ya Old Christians ambayo na timu ya raga ya Uruguay, ilitoweka ilipokuwa safarini kutoka mji wa Montevideo kwenda Santiago nchini Chile.

 Manusura wa Old Christians walikutana nchini Chile miaka 30 baada ya ajali
miezi miwili baadaye jeshi la wanahewa wa Chile waliwapata manusura 14 kutoka kwa ajali hiyo.
Wengine wawili walikuw wametembea kwa siku 10 kabla ya kukutana na wafugaji katika milima ya Andean.
Mkasa huo ulindikwa kwenye vitabu na baadaye kutengenezwa vilamu ,ALIVE, iliyoeleza jinsi manusura walikula nyama ya binadamu kuepuka kufa njaa.
M 1979 FC Pakhtakor Tashkent
Mwezi Agosti mwaka 1979 wanachama 17 wa timu ya soka la Pakhtakor Tashkent waliuawa wakati ndege yao iligongana na ndege ngingine katika anga ya Ukrain.
Watu wote 178 waliokuwa ndani ya ndege zote mbili waliangamia.
Timu zingine kwenye muungano ya usovieti zilichangia wachezaji wa klabu hiyo kukiwezesha kumaliza msimu.
1987 Alianza Lima
Timu ya soka ya Alianza Lima, moja ya vilabu vyenye mafanikio makubwa zaidi ilikuwa ikirejea mjini Lima wakati ndege yao ilianguka kwenda baharini dakika chache kabla ya kutua
Timu yote wa Alianza Lima iliyokuwa miongoni mwa watu 43 iliangamia. Ni rubani tu wa ndege hiyo aliyeweza kunusurika.
1993 Timu ya Soka ya Zambia
Wanachama 18 wa timu ya taifa ya Zambia waliuawa wakati ndege ya jeshi la Zambia ilianguka karibu na Gabon tarehe 28 mwezi Aprili mwaka 1993, walikuwa wikielekea kucheza mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Senegal.
Ripoti rasmi kuhusu mkasa huo miaka kumi baadaye ilitaja matatizo ya kimitambo kwenye injini moja ya ndege hiyo.
2011 timu ya magongo ya Lokomotiv Yaroslavl
Timu hiyo ambayo ilikuwa ndio mabingwa mara tatu nchini Urusi ya Lokomotiv Yaroslavl, iliangamia kwenye ajali ya ndege mwezi Septemba mwaka 2011.

Mabaki ya ndege yalipatikana kwenye mto uliokuwa karibu
Ndege hiyo ilikuwa ikielekea nchini Belarus kwa mechi ya kwanza ya msimu wakati ilianguka na kushika moto.
Wachezaji 36 na maafisa waliaga dunia pamoja na wahudumu 7. Mchezaji mwingine aliaga dunia akiwa hospitalini.

Tuesday 29 November 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOV 30 2016

 

Watumishi wa TAKUKURU Waliotumbuliwa tangu Mwaka jana Kwa Kukiuka Agizo la Rais Warejeshwa Kazini

Watumishi waandamizi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) waliosimamishwa kazi baada ya kusafiri nje ya nchi kinyume na agizo la Rais John Magufuli, wamerejeshwa kazini baada ya takriban mwaka mmoja kupita.
Msemaji wa Takukuru, Mussa Misalaba aliwataja watumishi hao kuwa ni Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma, Mary Mosha na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Ekwabi Mujungu ambao wamerejeshwa baada ya shauri lao kusikilizwa na ofisi husika.
“Shauri lao lilishughulikiwa na Ofisi ya Rais kutokana na vyeo vyao, wamerejeshwa ofisini na kuanza kazi Novemba 14,” alisema.


Ukweli kuhusu wacheza soka wa nchi za Afrika

 Wacheza soka wengi barani Afrika wanataka kumfanana Samuel Eto'o (kushoto)
Utafiti mkubwa kuhusu masuala ya soka duniani unaonyesha kuwa maisha miongoni mwa baadhi ya wanasoka wa afrika, yana tofauti kubwa na maisha ya wale walio na bahati ya kusakata soka kwenye vilabu vikubwa duniani.
Chama cha wacheza soka wa kulipwa cha kimataifa (Fifpro) ambacho ni sawa na chama cha wafanyakazi, kimefanya utafiti wa dunia nzima kwa karibu wanasoka 14,000 kwenye nchi 54, ambao ni utafiti mkubwa zaidi kuwai kufanywa.
Zaidi ya wachezaji soka 3000 ambao walishiriki kwenye utafiti huu ni kutoka nchi 13 za barani Afrika zikwemo, Botswana, Cameroon, Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, Misri, Gabon, Ghana, Ivory Coast, Kenya, Namibia, Afrika Kusini, Tunisia na Zimbabwe.
Huku vijana wengi wa Afrika wakiwa na ndoto ya kusakata soka sawa na Didier Drogba au Samuel Eto'o, takwimu zilizokusanywa na Fifpro zinaonyesha ukweli kuhusu maisha ya wacheza soka barani Afrika
Dhuluma za kimwili
Baadhi ya masuala ya kushangaza yaliyotokana na utafiti huo ni kuwa dhuluma za kimwili dhidi ya wachezaji barani, ndizo mbaya zaidi duniani
Wacheza soka nchini Ghana wako kweye hatari ya kushambuliwa kimwili mara kumi zaidi, na maafisa wa nyadhifa za juu kuliko wachezaji wengine.
Nchini Afrika Kusini na Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, uwezekano wa wachezaji kushambuliwa ni mara tatu zaidi kuliko viwango vyote duniani.
Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ina uwezekano wa juu wa wachezaji kushambuliwa na mashabiki, wakati wa siku ya mechi huku Kenya ikichukua nafasi ya pili.
Utafiti pia ulionyesha kuwa wachezaji walio katika nafasi ya kuamrishwa kufanya mazoezi peke yao wako barani Afrika.
Mishahara duni
Katika upande wa malipo, asilimia 100 ya wanasoka nchini Ghana walisema kuwa walilipwa chini ya dola 1000 kwa mwezi.
Wachezaji wenye malipo bora zaidi barani Afrika ambao wanalipwa zaidi ya dola 1000 kwa mwezi, ni kutoka nchini Morocco, licha ya wao kukumbwa na changamoto za kukosa kufahamu hatma yao.

 Licha ya mafanikio ya vilabu kama Zamalek (juu), Misri ina malipo duni kwa mujibu wa utafiti
Ligi ya Misri inaonekana kuwa bora zaidi barani Afrika, kufuatia vilabu vyake viwili kushinda kombe la klabu bingwa barani Afrika.
Klabu ya Al Ahly imeshinda vikombe vinane , Zamalek vitano na TP Mazembe ya DRC pia ina vikombe vitano.
Licha ya hilo ligi ya Misri huwa na malipo duni zaidi kati ya ligi 13 zilizofanyiwa utafiti barania Afrika
Zaidi ya asilimia 90 ya wachezaji walisema kuwa walilipwa chini ya dola 1000.
Nchini Gabon, ambayo ndiyo itakuwa mwaandalizi wa mechi za taifa bingwa barani Afrika mwezi Januari, asilimia 96 ya wachezaji walilalamikia kucheleweshwa kwa mishahara.
Mikataba
Afrika ina wachezaji wengi zaidi wasio na mikataba, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, asilimia 40 ya wachezaji wanasema kuwa hawana makaratasi ya mikataba.

 Wacheza soka wa Afrika mara nyingi hupigwa picha wakisaini mikataba ng'ambo, lakini wenzao barani Afrika hawana mikataba
Nchi tatu ambazo zina matatizo ya mikataba ni pamoja na Cameroon kwa asilimia 65, Gabon kwa asilimia 60 na Ivory Coast kwa asilimia 60.
Matumaini
Utafiti huo, hata hivyo unaonyesha kuwa kuna matumaini.

 Wacheza soka nchini Ivory Coast hupewa muda mrefu zaidi wa kupumzika
Upande wa likizo zilizolipwa, Ivory Coast na Namibia ni mfano mzuri, kwa kuwa nchi hizo huwapa wacheza soka likizo za zaidi ya siku 30 zilizolipwa kila mwaka.
Hii ni tofauti na Misri ambapo asilimia 93 ya wachezaji wanasema kuwa wao hupewa chini ya siku 10 za likizo inayolipwa kila mwaka.
Nchini Tunisia asilimia 99.5 ya wachezaji hupewa siku moja kila wiki ya kupumzika.
Uhakika wa kazi
Wachezaji wengi barani Afrika uhofia hatma ya maisha yao ya baadaye.
Wakati wachezaji waliulizwa ikiwa walihisi kuwa na wasiwasi kwa kazi zao, 11 kati ya nchi 13 zilikuwa za Afrika.
Licha ya utajiri wao, Morocco na Gabon zina asilimia kubwa.
La kushangaza ni kuwa wachezaji nchini Zimababwe, nchi ambayo shirikisho la Kandanda linakumbwa na matatizo ya kifedha, hadi kutimuliwa kutoka kwa kombe la dunia la mwaka 2018 baada ya kushindwa kumlipa kocha, wachezaji walihisi kuwa na uhakika wa kazi kuliko nchi zingine 13 za bara Afrika.
Kupanga matokeoUtafiti wa awali wa Fifpro, unaonyesha kuwa kukosa kuwalipa wachezaji mishahra huenda ikawa sababu ya kuwepo visa vya kupanga matokeo.
Malipo duni yamesababisha kuwepo majaribio mengi ya kupanga matokeo ikiwa ni asilimia 8.3 kutokana na utafiti
Licha ya asilimia 10.1 kusema walifahamu kuhusu visa vya kupanga matokeo kwenye ligi, asilimia hiyo ilikuwa ya juu kidogo kuliko ya nchi za ulaya ambayo ni 9.8.
Nchi tatu kati ya nchi tano zilizoripoti visa vingi zaidi vya kupanga matokeo ziko barani Ulaya.
Rekodi mbaya ya DRC
Nchi ambayo hakuna mchezaji angependa awe mchezaji wa kulipwa ni Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Asilimia 89 ya wachezaji nchini DRC hawana mikataba.

Idadi ya wachezaji ambao wameshambuliwa na wachezaji wengine ni mara tatu zaidi nchini DRC.
Mmoja kati ya wachezaji wanne aanasema kuwa ameshambuliwa wakati wa siku ya mechi.
Mmoja kati ya wachezaji watano anasema kuwa amedhulumiwa na wachezaji wenzake na mara nyingi amelazimishwa kusaini mikataba
Dalili nyingine ya mazingira mabaya ya kazi ni kuwa zaidi ya nusu ya wacheza soka nchini DRC, wanasema kuwa wana siku moja ya kupumzika kila wiki.

Khadija Yusuph amtaka Leila Rashid kumfuata mumewe

Khadija Yusuph
Msanii wa taarabu nchini Khadija Yusuph amemsihi wifi yake Leila Rashid kuachana na maswala ya muziki na kumfuata mume wake Mzee Yusuph kwa kuwa tayari mume wake kashaenda hija na ni dhambi kuacha kumsikiliza mume wake.
Akiongea ndani ya eNewz Khadija amesema ni vizuri Leila kumfuata mume wake kwa kuwa haoni sababu ya yeye kuendelea kuwa na kundi la Jahazi wakati mume wake Mzee Yusuph ameamua kumrudia Mungu na kuachana na maswala ya muziki.
Hata hivyo Khadija Yusuph amewaambia mashabiki waendelee kusubiria maamuzi ya Mzee Yusuph mwenyewe juu ya maamuzi ya mke wake kuendelea na muziki wakati yeye kaamua kumrudia Mungu na kuachana kabisa na mambo ya dunia.

Uchaguzi wa urais Somalia waahirishwa tena

Rais anayeondoka Hassan Sheikh Mohamud
Uchaguzi wa urais nchini Somalia, ambao ulikuwa umeahirishwa kwa mara mbili awali, umeahirishwa tena kwa muda usiojulikana.
Mwenyekiti wa bodi ya uchaguzi nchini humo Omar Mohamed Abdulle ameambia wanahabari mjini Mogadishu kwamba haiwezekani kwa uchaguzi huo kufanyika Jumatano wiki hii kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Sababu kuu ni kuchelewa kwa uchaguzi wa wabunge ambao wanafaa kukutana na kumchagua ras wa taifa hilo.
"Tarehe kamili haiku mbali. Wabunge watakapomaliza kuchaguliwa na wasajiliwe mnamo tarehe 6 au 7 Desemba, kila mmoja atafahamu tarehe kamili ya uchaguzi," alisema.
"Hautaki kugusia hilo kwa sasa. Hiyo itakuwa shughuli ya bunge na bunge ndilo litakaloamua ni wakati gani wa kumchagua spika wa bunge na rais. Lakini nawahakikishia jambo moja, kwamba uchaguzi huu usio wa moja kwa kwa moja unaitwa uchaguzi wa 2016, hii ina maana kwamba utafanyika 2016."

Simba ‘kukutana leo Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini

Wachezaji wa Simba SC wanatarajiwa kukutana leo Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini,Dar es Salaam kujipanga kwa ajili ya kuanza mazoezi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Katibu Mkuu wa Simba SC, Patrick Kahemele alisema jana katika mazungumzo na Nipashe kwamba wachezaji hao watakutana chini ya Kocha Msaideizi, Mganda, Jackson Mayanja.
Alisema mazoezi rasmi yataanza Jumatano kwenye viwanja hivyo vya Polisi kwa kupokezana na mahasimu wao, Yanga SC ambao wamenza jana asubuhi.
“Mkutano wa leo utahusisha wachezaji ambao wanaishi Dar es Salaam pekee wakati tunasubiri wachezaji zaidi wakiwemo wa nje ya mji nan je ya nchi wawasili. Mazoezi yataanza rasmi Jumatano,”alisema Kahemele.
Aidha, Katibu huyo alisema kwamba kocha Mkuu, Joseph Marius Omog anatarajiwa kufika mwishoni mwa wiki kuanzisha programu kamili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
Simba SC ilimaliza mzunguko wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiwa kileleni kwa pointi zake 35, mbili zaidi dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC.

Binadamu mzee zaidi asherehekea siku ya kuzaliwa akiwa na miaka 117

 Emma Morano ndiye binadamu mzee zaidi aliye hai
Binadamu pekee aliye hai, ambaye inatambuliwa kwamba alizaliwa katika karne ya kumi na tisa, leo anasherehekea sikukuu yake ya 117 tangu kuzaliwa kwake.
Emma Morano, alizaliwa katika jimbo la Piedmont karibu na mji wa Milan, Italia tarehe 29 Novemba, 1899.
Wakati huo, kampuni ya magari ya Fiat ilikuwa tu ndiyo imeanzishwa. Klabu ya soka ya Milan nayo ilikuwa imeanzishwa wiki chache awali.
Ameshuhudia wafalme watatu wa Italia wakitawazwa na kuondoka, alizaliwa wakati wa utawala wa Mfalme Umberto wa Kwanza.
Aidha, katika maisha yake, kumekuwepo na Baba Watakatifu kumi na mmoja.
Isitoshe, alishuhudia Vita Vikuu vya Kwanza na vya Pili vya Dunia.
Mwaka huu, alitambuliwa kuwa mwanamke mkongwe zaidi aliye hai baada ya kifo cha Mmarekani Susannah Mushatt Jones mwezi Mei. Ndiye pia binadamu pekee aliye hai ambaye alizaliwa miaka 1800.
Bi Morano anasema sana amekuwa na maisha marefu kutokana na jeni.
Mamake aliishi hadi miaka 91. Dadake wengi pia walifariki wakiwa na umri mkubwa.
Anasema kwa kiwango fulani, lishe yake imechangia. Anasema amekuwa akila mayai matatu - mawili yakiwa mabichi, kila siku kwa zaidi ya miaka 90.
Alianza hayo alipokuwa mwanamke kijana, baada ya madaktari kugundua alikuwa na ugonjwa wa anaemia, ambapo mgonjwa hupungukiwa na seli nyekundu za damu au haemoglobini, muda mfupi baada ya Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia.
Siku hizi amepunguza na hula mayai mawili pekee, na biskuti kadha.
Hilo linaenda kinyume kabisa na ushauri wa sasa wa madaktari kuhusu jinsi ya kuishi maisha marefu na yenye afya, daktari wake wa miaka 27 Carlo Bava ameambia AFP.
"Emma hula mboga chache sana, na hali matunda sana. Nilipokutana naye alikuwa anakla mayai matatu kila siku, mawili mabichi kila asubuhi na moja la kupikwa mchana saa sita na kisha anakula kuku chakula cha jioni."
Licha ya haya, Carla anasema, mwanamke huyo anaonekana kuwa na "maisha tele"
.
 Kuna kipindi cha televisheni kilichoandaliwa kuangazia maisha yake Emma Morano
'Nioe au nikuue'
Jambo jingine ambalo Bi Morano anasema huenda limechangia maisha yake marefu, ni hatua yake ya kumfukuza mumewe mwaka 1938 baada ya mtoto wake wa kiume kufariki akiwa na miezi sita pekee.
Ndoa yao ilikuwa inaendelea vyema kwa mujibu wa Bi Morano.
Alikuwa amempenda mvulana aliyeuawa wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia na hakutaka kumuoa mtu mwingine.
Lakini aliambia gazeti la La Stampa, alipokuwa na miaka 112, kwamba hakuna na namna nyingine ya kufanya ila kuoa mtu mwingine.
"Aliniambia: 'Ukiwa na bahati utanioa, la sivyo nitakuua'. Nilikuwa na miaka 26. Niliolewa."
Baadaye, ndoa yao ilianza kuvurugika na akamfukuza mumewe ingawa hawakuvunja ndoa yao hadi mwaka 1978 mumewe alipofariki.
Bi Morano alifanya kazi hadi alipotimu miaka 75 na aliamua kutooa tena.
"Sitaki kudhibitiwa na yeyote," aliambia gazeti la New York Times.

Daktari wake wa miaka 27, Carlo, anasema mwanamke huyo ana maisha tele
Ili kusherehekea siku hii muhimu, wakazi wa eneo la Pallanza karibu na Ziwa Maggiore, ambapo amekuwa akiishi, wanaandaa maonyesho ya mitindo yakiangazia karne tatu katika historia.
Profesa wa masuala ya msambojeni George Church ambaye hufanya kazi katika chuo cha matibabu cha Harvard pamoja na kundi lake la watafiti ambao wamekuwa wakifanya utafiti kuhusu umri wa kuishi, ameambia BBC kwamba binadamu wataendelea kuongeza muda wa kuishi.
"Nafikiri tutashuhudia ongezeko kubwa la muda wa kuishi katika miaka michache iliyopita kutokana na teknolojia, na pia utafiti unaofanyiwa watu wa kipekee kama vile Emma."

Emma bado yuko buheri wa afya.
Hata hivyo, hajaondoka nyumba yake ya vyumba viwili kwa miaka 20.
Carlo anahisi shinikizo kuhusu majukumu ya kumtunza mwanamke huyo mkongwe, ambapo anasema ni kama kuutunza Mnara wa Pisa.
"Ile siku utaanguka, kuna mtu atalaumiwa," aliambia AFP. "Emma atakapofariki, mimi ndiye nitakayewajibishwa."
Mtu aliyeishi muda mrefu zaidi duniani kwa mujibu wa Guinness alikuwa Mfaransa Jeanne Calment, aliyeishi miaka 122 na siku 164. Alifariki Agosti 1997.

Zimbabwe yazindua fedha zake kwa mara ya kwanza

Noti mpya za Zimbabwe.
Taifa la Zimbabwe limezindua fedha zake kwa mara ya kwanza tangu sarafu ya dola ya taifa hilo ifutiliwe mbali miaka saba iliyopita kufuatia mfumuko mkubwa wa kiuchumi.
Noti hiyo yenye dhamana ambayo ina thamani ya dola moja imezua hofu kuhusu kurudi kwa matumizi ya dola ya taifa hilo.
Noti hizo ambazo zilizinduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwezi Mei, zimesababisha maandamano makubwa katika kipindi cha muongo mmoja dhidi ya rais Mugabe .
Serikali imesisitiza kuwa noti hizo za dhamana siyo sarafu rasmi ya taifa hilo imezindua noti hizo ili kukabiliana na upungufu wa fedha na kusitisha matumizi ya dola ya Marekani ambayo inazidi kutolewa nje ya taifa hilo, hatua ambayo kundi la wafanyibiashara wameiunga mkono.

Monday 28 November 2016

Brazilian football team Plane crashes in Colombia Team At the airport be...

Ndege iliyobeba wachezaji wa Brazil yaanguka Colombia

Kabla ya kuanza safari timu hiyo ilipiga selfie hii.
  Ndege iliyokuwa imebeba watu 72, ikiwemo timu ya soka ya klabu ya Chapecoense ya Brazil, imeanguka katika sehemu ya milima nchini Colombia wakati inakaribia Mji wa Medellin.
Maelezo kamili ya ajali hiyo hayajafahamika lakini habari zinasema kwamba kuna 6 watu walionusurika.
Ndege hiyo ya kukodisha iliyokuwa ikitokea Bolivia, ilikuwa na timu ya soka ambayo ilikuwa icheze katika fainali ya Kombe la Amerika ya Kusini dhidi ya timu ya Atletico Nacional ya Medellin. Hivyo, fainali hiyo imeahirishwa

Ripoti zinasema ndege hiyo yenye leseni namba CP 2933, iliyoanguka muda mfupi kabla ya saa sita usiku, ilielezewa na Meya wa Medellin, Federico Gutierrez, kama “janga kubwa”, akiongeza kwamba inawezekana kuna watu walionusurika.