Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Wednesday, 4 April 2018

Tuzo ya Mchezaji bora EPL


VITA  kubwa  kwenye Ligi Kuu ya England sasa imehamia kwenye tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi hiyo am­bapo wanaume wawili wana­pambana vikali.
Vita hiyo ipo kati ya kiungo wa Man­chester City, Kevin De Bruyne, na mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah na mashabiki wa soka wamekuwa waki­gawanyika kwa kiasi kikubwa kutambua nani anaweza kutwaa tuzo hiyo.
Tayari De Bruyne, ameshaonyesha hofu yake juu ya mshambuliaji huyo wa Liverpool anayeon­goza kwa kupachika mabao kwa sasa kwenye Ligi Kuu ya England.
Mbelgiji huyo ameshasema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuwa Salah atachukua tuzo hiyo kutokana na kasi yake tan­gu alipotua Liverpool mwanzoni mwa msimu huu.
Salah ni kinara kwa kupachi­ka mabao kwenye ligi hiyo ak­iwa amefunga mabao 29 huku akionekana kutawala pia kwenye ligi zote kubwa barani Ulaya kuto­kana na mabao mengi aliyofunga.

De Bruyne ambaye amekuwa nguzo sahihi kwenye kikosi cha City msimu huu ambacho kinajiandaa kutwaa ubingwa wa ligi
hiyo ameshasema kuwa itakuwa vigumu sana kwake kumzuia Salah lakini kwa kuwa ni tuzo kila kitu kinawezekana.
Tuzo ambazo zina­wania na mastaa hao ni mbili, moja ya mchezaji bora wa mwaka wa Ligi Kuu England na ny­ingine ni mchezaji bora wa mwaka wa waandishi wa habari za soka.
Vita hii imekuja wakati ambapo mastaa hao wawili watakutana kwenye mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Dimba la Anfield.
Liverpool leo watakuwa wenyeji wa Man City kwenye mchezo huo ambao unaonekana utakuwa mgu­mu sana kwa timu zote mbili.
“Ndiyo kama mimi ndiye nita­pata tuzo ya Mchezaji Bora wa England litakuwa jambo zuri sana, lakini nafikiri kwanza kwa ajili ya timu.

“Kwa njia moja nafikiri kuwa nastahili kwa kuwa nimekuwa kwenye kiwan­go kilekile kwa muda mrefu.

“Nina furaha sana mwenyewe na nime­kuwa navutika sana kwa jinsi ambavyo nime­kuwa nikicheza msimu huu.

“ Nafikiri hakuna mch­ezo ambao kiwango changu kilikuwa chini, lakini ni vye­ma nikawa na hofu na mpinzani wangu kwa kuwa ame­kuwa bora kwa muda mrefu na amekuwa mfungaji mzuri, hali­takuwa jambo rahisi kuitwaa.

“Salah amekuwa kwenye kiwan­go cha juu sana kwa kipindi cha hivi karibuni na amecheza vizuri kwenye michezo aliyocheza.

“Kitakwimu ni ngumu kunil­inganisha naye, lakini kwa kuwa ni tuzo basi ngoja tuone mwisho utakuwaje,”alisema kiungo huyo wa City.

De Bruyne ndiye kinara wa pasi kwenye Ligi Kuu ya England na Ulaya kwa ujumla akiwa amefani­kiwa kutoa pasi 15 zilizozaa mabao ambazo ni nyingi kuliko mchezaji mwingine yoyote msimu huu.
Salah yeye anakwenda kwenye tuzo hiyo akiwa na rekodi nzuri ya kupachika mabao akiwa ndiye ki­nara kwa sasa Ulaya nzima baada ya kufunga mabao 29 akifuatiwa na Lionel Messi mwenye mabao 26.
City wanakwenda kwenye Dimba la Anfield, wakitambua kuwa Liver­pool ndiyo imekuwa kizuizi chao msimu huu kwani ndiyo timu pe­kee ambayo imefanikiwa kuwafun­ga kwenye Ligi Kuu England hadi sasa wakiwa wamepoteza mchezo mmoja tu.
Mbali na kuwafunga Liverpool, wamekuwa kwenye kasi nzuri sana msimu huu wakiwa wanaamini kuwa wanaweza kumaliza kwenye nafasi ya pili mbele ya Manches­ter United ambao nao wamekuwa wakiwania nafasi hiyo.

Friday, 1 December 2017

Neymar ajihakikishia Ubingwa Kombe la Dunia


Nyota wa Brazil Neymar Jr amesema atajitoa kwa uwezo wake wote kuhakikisha taifa lake linashinda Kombe la Dunia mwaka 2018 kwenye fainali zitakazofanyika nchini Urusi.

Kikosi chetu kwasasa ni bora tofauti na ilivyokuwa mwaka 2014 tuliposhindwa kuchukua ubingwa tukiwa nyumbani, nitacheza kwa uwezo wangu wote kuhakikisha tunarejesha heshima ya kutwaa ubingwa wa dunia”, amesema Neymar.
Nyota huyo anayechezea PSG ya Ufaransa ameongeza kuwa timu yao ni bora ndio maana ilipoteza mechi moja tu kwenye michuano ya kuwania kufuzu fainali hizo kupitia kundi la Amerika ya Kusini (CONMEBOL).
“Kufuzu kwa kupoteza mechi moja tu kwenye kundi gumu la CONMEBOL ni hatua nzuri na imetufanya tujiamini na tutafanya vizuri na hayatajirudia mambo yaliyotokea kwenye fainali za miaka minne iliyopita”.

Kwenye fainali za Kombe la Dunia 2014, Brazil iliondolewa kwenye hatua ya nusu fainali baada ya kukubali kichapo cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani ambayo iliibuka bingwa wa dunia kwa kuifunga Argentina kwenye mchezo wa fainali.

Wednesday, 11 October 2017

Lionel Messi awafikisha Argentina Kombe la Dunia 2018 Urusi

Lionel Messi scored his first hat-trick in World Cup qualifying matches
Lionel Messi alifunga mabao matatu na kuiwezesha Argentina kutoka nyuma ugenini dhidi ya Ecuador na kuwalaza 3-1 na kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Brazil walikuwa tayari wamefuzu.
Luis Suarez alifunga mabao mawili kuwawezesha Uruguay kulaza Bolivia 4-2 na kufuzu pia.
Colombia pia wamesonga mbele baada ya kutoka sare 1-1 ugenini Peru.
Peru walimaliza wa tano katika michuano ya kufuzu Amerika Kusini na sasa watakutana na New Zealand katika mechi mbili za muondoano za kufuzu.
Lakini nyota wa Arsenal Alexis Sanchez na taifa lake la Chile wako nje ya michuano hiyo baada ya kushindwa 3-0 ugenini Brazil.
Argentina walianza siku wakiwa nambari sita na kwenye hatari ya kutofuzu kwa mara ya kwanza tangu 1970.
Aidha, walianza vibaya katika mechi hiyo iliyochezewa mji ulio nyanda za juu wa Quito. Wenyeji walijiweka kifua mbele baada ya sekunde 38 kupitia bao la Romario Ibarra, bao la kasi zaidi ambalo Argentina wamewahi kufungwa michuano ya kufuzu Kombe la Dunia.
Hata hivyo, Argentina, waliomaliza wa pili Kombe la Dunia nchini Brazil 2014, walijikwamua wakisaidiwa sana na ustadi wa Messi.
Alisawazisha baada ya dakika 12 aliposhirikiana vyema na nyota wa zamani wa Manchester United Angel di Maria.
Bao lake la pili alilipata dakika nane baadaye na kisha akafunga la tatu na la ushindi kipindi cha pili.
Msiba kwa Chile
Chile, ambao wameshinda Copa America katika michuano miwili ya karibuni zaidi, walikuwa wanapigania kufuzu kwa mara yao ya tatu mtawalia baada ya kufuzu na kufika hatua ya 16 bora mwaka 2010 na 2014.
Walianza mechi za mwisho wakiwa nafasi ya tatu lakini walifungwa mabao mawili na Brazil katika kipindi cha dakika tatu kipindi cha pili kutoka kwa Paulinho na Gabriel Jesus.
Baada ya Peru kufunga bao la dakika ya mwisho la kusawazisha dhidi ya Colombia, Chile walihitaji kufunga kujipatia nafasi ya kucheza mechi za muondoano za kufuzu.
Dakika za mwisho, walicheza kwa kikosi chao chote akiwemo kipa Claudio Bravo, kwenye nusu ya uwanja ya Brazil.

Tuesday, 10 October 2017

Iceland yafuzu Kombe la Dunia

Image result for Iceland timu ya taifa
Iceland imekuwa nchi ndogo zaidi kuwahi kufuzu kwa Kombe la Dunia baada ya kuwalaza Kosovo 2-0 na kumaliza kileleni kundi lao la kufuzu kwa michuano hiyo itakayofanyika Urusi 2018.
Iceland, ambao walifika robofainali Euro 2016, baada ya kuwaondoa England hatua ya 16 bora, ni taifa la raia 335,000 pekee.
Ndiyo nchi ya kwanza kufuzu kwa Kombe la Dunia ikiwa na idadi ya watu ambao ni chini ya milioni moja.
Gylfi Sigurdsson wa Everton na Johann Gudmundsson wa Burnley ndio waliofungia taifa hilo Jumatatu.
Sigurdsson aliwapa matumaini kwa kufunga muda mfupi kabla ya mapumziko na kisa akamsaidia Gudmundsson kufunga bao la kuwahakikishia ushindi.Iceland sasa wameshinda mechi saba kati ya 10 Kundi I la kufuzu kwa Kombe la Dunia.


Mkufunzi wa Iceland Heimir Hallgrimsson alikuwa na wasiwasi kwamba angetatizika kuwapa motisha wachezaji wake baada ya kufana sana Euro 2016 nchini Ufaransa.
“Bia ya kwanza baada ya sherehe huwa si nzuri. Jambo ngumu zaidi lilikuwa kuendeleza ufanisi baada ya sherehe yetu kubwa kutokana na ufanisi Ufaransa,” alisema.
“Na isitoshe, tulikuwa kwenye kundi lenye ushindani mkali lililokuwa na Croatia, Uturuki, Ukraine na Finland, nchi ambazo zinatuzidi kwa viwango vya soka.
“Ufanisi huu si mwisho bali ni safari ndefu ya kuelekea hadi kwenye mwisho wa safari.”
Meneja wa Kosovo Albert Bunjaki amesifu sana Iceland kwa ufanisi wao na kusema kuwa hilo litatia moyo mataifa madogo.
“Naipongeza timu yote ya Iceland,” amesema Bunjaki, ambaye taifa lake la Kosovo lina watu mara sita zaidi ya Iceland.

Kocha alimwa kadi nyekundu

 Mchezo wa SDL kati ya AFC Arusha na Pepsi zote za Arusha uliochezwa Jumatatu katika Uwanja wa Ushirika na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, umeibua malalamiko baada  ya mwamuzi wa kati kudaiwa kuharibu mchezo huo, huku kocha wa AFC akilimwa kadi nyekundu.
Mwamuzi Goodluck Simba kutoka Pwani alilaumiwa na AFC kuwa aliwapa Pepsi bao ambalo sio halali pamoja na kuwanyima penalti, katika mchezo huo kocha mkuu wa timu ya AFC, Gerald Totoo alioneshwa kadi nyekundu kwa kuondoka eneo lake wakati mchezo ukiendelea.
Totoo alisema baada ya kurudi katika eneo lake alishangaa kuoneshwa kadi nyekundu wakati hakufanya jambo lolote baya kwa mwamuzi wala kwa kamisaa wa mchezo huo

Sunday, 8 October 2017

Uholanzi yaikung'uta Belarus 3-1

Nahodha wa Uholanzi, Arjen Robben akienda chini baada ya kukwatuliwa na beki wa Belarus, Sergei Balanovich katika mchezo wa Kundi A kufuzu Kombe la Dunia kwa upande wa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Borisov Arena mjini Borisov. Uholanzi ilishinda 3-1 mabao yake yakifungwa na Davy Propper dakika ya 24, Arjen Robben kwa penalti dakika ya 84 na Memphis Depay dakika ya 90 wakati la wenyeji lilifungwa na Maksim Volodko dakika ya 55.

Friday, 6 October 2017

Ujerumani yafuzu kwa Kombe la Dunia 2018

Germany walihitaji kutoka sare au kushinda kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018
Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia Ujerumani wamefuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Urusi baada ya kulaza Ireland Kaskazini 3-1 mjini Belfast.
Sebastian Rudy alifunga bao dakika ya pili, Sandro Wagner akaongeza la pili baadaye, naye Joshua Kimmich akafunga la tatu mechi ikikaribia kumalizika.
Josh Magennis alifungia Ireland Kaskazini bao la kufutia machozi kwa kutumia kichwa dakika za lala salama.
Ujerumani wamefuzu wakiwa viongozi wa kundi lakini Ireland Kaskazini wanasalia bado na matumaini ya kufuzu kupitia mechi za muondoano za kufuzu Novemba.
Vijana hao wa Michael O'Neill watamaliza mechi zao Kundi C nchini Norway Jumapili, wakilenga kumaliza wakiwa miongoni mwa timu nane bora zitakazomaliza nafasi ya pili kati ya makundi tisa ya kufuzu.

Wednesday, 4 October 2017

Arsene Wenger apatwa na hofu Barcelona kuhamia Epl

Masuala ya kisiasa yanayoendelea nchini Hispania tayari yameleta habari nyingi za kisoka, lakini kubwa ni uwezekano wa vilabu vya Catalunya kuhamia katika ligi zingine ikiwemo Epl.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anaonekana kutofurahia habari za Barcelona kuhamia katika ligi kuu ya Uingereza huku akihoji Barcelona watahamiaje wakati kuna vilabu vya Scotland havijahamia hadi leo.
Wenger amesema haitakuwa sahihi kwa FA kuruhusu jambo hilo kutokea huku wakivikatalia vilabu vya nchi jirani ya Scotland kuhamia katika ligi hiyo.
Sii hivyo tu lakini mzee Wenger ameonya kuhusu mbio za ubingwa wa Epl kwamba zinaweza kuwa ngumu mno kama miamba hiyo ya La Liga itapewa ruhusa kujiunga na ligi kuu Uingereza.

Saturday, 30 September 2017

Man U yazidi kupasua mawimbi Chelsea wakishikwa shati na Man City

Timu ya Manchester United imezidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kutafuta ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kupata ushindi mnono wa jumla ya magoli 4-0 dhidi ya Vibonde Crystal Palace mchezo uliopigwa kwenye dimba la Old Traford.
Magoli ya Man United yakifungwa na Fellaini aliyefunga mawili dakika ya 35 na 49,Juan Mata dk 3 na Lukaku 86.
Kwa Matokeo hayo Man United wanabaki kwenye nafasi yao ya pili wakiwa na alama 19 sawa na Man City wakiwa wanatofautiana magoli ya kushinda na kufungwa Vijana wa Mourinho wamefunga magoli 21 na kufungwa mawili huku Guardiola akiwa ameshinda magoli 22 na kufungwa mawili.
MANCHESTER UNITED (4-2-3-1): De Gea 6; Valencia 7, Jones 7, Smalling 6.5, Young 7; Matic 6, Fellaini 8; Mata 7.5 (Herrera 76 mins, 6), Mkhitaryan 5.5 (Lingard 66, 6), Rashford 7 (Martial 71, 7); Lukaku 6 
Subs not used: Bailly, Blind, Romero, Darmian
Goals: Mata 3mins; Fellaini  35, 49; Lukaku 86 
CRYSTAL PALACE (4-3-3): Hennessey 6; Ward 5.5, Sakho 6, Delaney 5.5, van Aanholt 6; Townsend 6, Milivojevic 6, Puncheon 5.5 (Riedewald 69, 5.5); Cabaye 6.5, Sako 6.5 (Ladapo 74), Schlupp 5.5 (McArthur 69, 6) 
Subs not used: Speroni, Lee, Mutch, Kelly
Referee: Mike Dean 6
Attendance: 75,118
Kevin De Bruyne sent the travelling fans into raptures with his brilliant finish to put City ahead in the second half
Katika uwanja wa Darajani wenyeji Chelsea wamepoteza mechi yao baada ya kufungwa goli 1-0 na Manchester City huku Chelesea wakipata pigo kutokana mshambuliaji wao Moratta kupata majeraha.
Goli la ushindi la Man City limefungwa na Kevin De Bruyne kipindi cha pili kwa shuti kali na kumshinda mlinda mlango dakika ya 67 Courtois
The Belgian scored with a well placed shot from the edge of the box which left Thibaut Courtois with no chance

Friday, 29 September 2017

Manchester City yapata pigo kwa Aguero

MSAMBULIAJI wa Klabu ya Soka ya Manchester City na timu ya taifa ya Argentina, Sergio Kun Aguero, amepata ajali ya gari usiku wa jana akiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege nchini Uholanzi ambako alikuwa amehudhuria tamasha la muziki. 
Kwa mujibu wa ripoti, Aguero, 29, amevunjika mbavu na atakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili na atakosa mchezo dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini England klabu ya soka ya Chelsea utakaopigwa Jumamosi hii.
Picha zilizosambaa katika baadhi ya mitandao kutoka nchini Uholanzi zimeonyesha gari ndogo ambayo Aguero alikuwepo na dereva wake ikiwa imegonga nguzo katikati ya jiji la Amstedam huku ikiripotiwa kuwa hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya kuumia.
Awali aliweka picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ikimuonyesha yeye na msanii kutoka Uholanzi anayefahamika kwa jina la Maluma ambaye ndiye aliyemualika staa huyo wa Argentina katika tamasha hilo

Tuesday, 26 September 2017

Mbeya City yapata Kocha mpya

Image result for Nsanzurwimo Ramadhan
Klabu ya Mbeya City imefikia makubaliano na Kocha Nsanzurwimo Ramadhani kuwa Kocha Mkuu kwa mkataba wa awali wa Msimu mmoja wa ligi kuu ya Vodacom inayoendelea.
Kocha Ramadhan ni raia wa Burundi na anatarajiwa kujiunga na timu hiyo huko kanda ya ziwa inakoendelea na michezo yake ya ligi kuu.
Kocha Ramadhani amewahi kuwa kocha kwa nyakati tofauti katika vilabu mbalimbali nchini Burundi, Rwanda, Botswana, Malawi, Uganda, na Afrika ya Kusini, pia amewahi kuwa mshauri wa ufundi katika timu ya taifa ya Burundi na kocha msaidizi/kocha mkuu wa muda(caretaker) kwa timu ya taifa ya Malawi.
Imetolewa na
Shah Mjanja
Afisa Habari
MCCFC
0717282217

Lacazette aingia matatani

Mshambuliaji Alexandre Lacazette amekaguliwa kama anatumia dawa zinazozuiwa michezoni.
Lacazette raia wa Ufaransa, amepimwa ukiwa ni utaratibu wa kawaida ambao wachezaji mbalimbali hupimwa mara tu baada ya mchezo au wakati wa mapumziko.
Utaratibu huu ni “random” kwa kuwa unaweza kumuangukia yoyote. Ingawa Lacazette ambaye ambaye alifunga mabao mawili wakati Arsenal ikishinda 2-0 dhidi ya Wes Brom, amefanya mtandaoni kuwa gumzo baada ya kupiga mbili ndiyo maana ameangukia katika vipimo hivyo.

Monday, 25 September 2017

Sakata la Neymar na Cavanni lachukua sura mpya

Bado habari za Edison Cavanni na Neymar zinaendelea kutawala vichwa vya habari, baada ya mvurugano uliotokea wiki chache  zilizopita inasemekana wafalme hawa wawilu walipatana na Neymar aliomba msamaha.
Lakini sasa kumeibuka jipya, inasemekana mabosi wa klabu ya PSG walikaa chini na Edison Cavanni na kumuomba amruhusu Neymar kupiga penati huku pia wakitaka kumpa kiasi cha pesa ili kukubali.
PSG walitaka kumpa Cavanni kiasi cha €1million ambayo ni pesa ambayo wangempa Cavanni mwisho wa msimu kama akimalizia mfungaji bora lakini sasa wakataka kumpa kiasi hicho ili amuachie Neymar kupiga tuta.
Edison Cavanni amekataa kiasi hicho cha pesa na hii inamaanisha kwamba hayuko tayari kumuachia mtu mwingine apige penati na anaona ni bora akose kiasi hicho cha pesa kuliko kuacha kupiga penati.
Inadaiwa kwamba baada ya Neymar na Cavanni kugombana ilimbidi tajiri wa PSG Nasser El Khaifi kukaa na Cavanni ili kujaribu kumshawishi kuhusu kumpa Neymar penati lakini Cavanni amekataa.
Mbaya zaidi inadaiwa kwa sasa kumeanza kuwa na makundi katika klabu hiyo kwani kuna kundi kubwa ndani ya PSG linalomsuport Cavanni huku kikundi kingine kidogo kinachoundwa na Wabrazil pekea yao wakiwa wanamuunga Neymar.

TFF na KCB waingia mkataba wa thamani ya shilingi 325,000,000


Shirikisho la soka nchini TFF, leo Septemba 25 limesaini mkataba na benki ya KCB wenye thamani ya shilingi 325,000,000.
Akiongea wakati wa kusaini mkataba huo Rais wa TFF Wallace Karia amesema huo ni ushahidi kuwa shirikisho lina ushirikiano na wadau mbalimbali wa mpira nchini.
Aidha Karia amesema fedha hizo zitaelekezwa kwenye kukuza vipaji vya soka pamoja na maendeleo ya soka nchini kwa ujumla.

Thursday, 21 September 2017

Ligi ya Bundesliga

51487055-aubameyang-marcou-dois-gols-na-vitoria-do-dortmund-em-cima-do-monchengladbach
Kuna rekodi moja ya Bundesliga inayoziunganisha Borussia zote yaani Monchengladbach na Dortmund.
Wakiwa wanajiandaa kukutana katika dimba la Signal Iduna Park katika mechi kali ya wiki hii Siku ya jumamosi, kitu cha uhakika ni kwamba rekodi hiyo haitavunjwa.
Kwenye mechi ya mwisho wa msimu wa 1977/8, Monchengladbach waliingia uwanjani wakiwa na idadi sawa ya point na Cologne, lakini wakiwa nyuma kwa tofauti ya magoli 10 nyuma ya wapinzani wao ambao walikuwa wanatazamia kushinda kirahisi mchezo wao dhidi ya St Pauli.
Kwenye mchezo uliolalia upande mmoja zaidi katika historia ya Bundesliga, Monchengladbach walifunga mabao sita katika kila dakika 45 za mchezo bila majibu hivyo kupelekea matokeo ya 12-0 baada ya kipenga cha mwisho kulia. Ikiwa ni rekodi ambayo haijavunjwa hadi sasa ndani ya Bundesliga.
Tangu kipindi hicho Monchengladbach hawajakaribia hata kidogo kushinda ubingwa wao wa sita huku wapinzani wao wakishinda Ubingwa huo mara tano na kuwa ndio hasimu mkubwa wa Bayern Munich.
Japokuwa idadi ya zaidi ya watu 80,000 hawatarajii kuona rekodi ya mabao 12 ikivunjwa, wanaweza kutazamia mchezo ambao bado utakuwa na mabao mengi ukizingatia timu hizi zina uwezo mzuri wa kushambulia na soka la kuvutia. Michezo 5 ya nyuma waliyokutana umeshuhudia angalau idadi ya magoli manne kwenye kila mchezo.
Mfungaji bora wa msimu uliopita Pierre Emerick Aubameyang ameendelea kutikisa nyavu bila wasi, huku Monchengladbach wakiwa na vijana machachari Lars Stindl na Thorgan Hazard, ambao wanachezea timu za taifa, Ujerumani na Ubelgiji.
Mchezo huu pia utakuwa ni kwanza kwa kiungo Mahmoud Dahoud kukutana na timu yake ya zamani tangu alipojiunga na Dortmund majira ya joto. Nafasi yake katika kikosi cha Monchengladbach imejazwa na kinda kutoka Uswizi Denis Zakaria ambaye amepata sifa kedekede kutoka kwa kocha wake.
“Ni burudani unapomtazama Denis namna alivyozoea. Hakika ameshatulia ndani ya Bundesliga”, Kocha wa Monchengladbach Dieter Hecking alisema, “Lakini sasa anahitaji kuendelea kucheza vizuri bila kuonyeshwa kadi”, aliongeza.
Watazamaji kote nchini wataweza kutazama mchezo huu MUBASHARA kupitia Chaneli ya World Football Saa 1:30 Usiku Jumamosi hii.

Samatta azidi kupasua anga

Wachezaji wa Kimataifa wa Tanzania mshambuliaji Mbwana Samatta, Simon Msuva na Abdi Banda wamefanya vizuri na vilabu vyao katika michezo ya katikati ya wiki.
Mbwana Samatta akiwa na KRC Genk ya Ubeligji wamefanikiwa kusonga mbele kwenye kombe la Ubelgji baada ya ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Cercle Brugge Uwanja wa Jan Breydelstadion mjini Brugge usiku wa kuamkia leo. Katika mchezo huo Samatta amecheza dakika 75.
Naye Mlinzi wa zamani wa Simba Abdi Banda akiwa na timu yake ya Baroka FC wamefanikiwa kupata ushindi  wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya wenyeji, Bloemfontein Celtic katika mchezo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Banda akicheza dakika 90.

Monday, 18 September 2017

Wayne Rooney kurejea Man u



Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema anaamini ipo siku nyota wa zamani wa timu hiyo Wayne Rooney atarejea klabuni hapo.
Mourinho amesema hayo mbele ya waandishi wa habari alipoulizwa kuhusu mapokezi ya Rooney kwenye mchezo wa jana kati ya Manchester United dhidi ya Everton ambapo mashabiki walimpokea nyota huyo kwa shangwe nyingi.
"Rooney hana tatizo na timu wala mimi sina tatizo na Rooney ndio mana tumesalimiana kwa furaha, naamini siku moja atarejea maana hapa ni nyumbani kwake hata mashabiki wamempokea vizuri"' amesema Mourinho.
Rooney jana alirejea kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Old Trafold tangu aondoke kwenye dirisha la usajili lililopita ambapo alirudi kwenye timu yake iliyomkuza ya Everton na jana ilikumbana na kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa United.

Sunday, 17 September 2017

Kikosi cha leo Simba SC dhidi ya Mwadui FC

Image result for simba sc
Kikosi cha leo Simba SC dhidi ya Mwadui FC
1.Aish Manula
2.Ally Shomary
3.Mohammed Hussein
4.Salim Mbonde
5.Juuko Murshid
6.James kotei
7.Nicholas Gyan
8.Mzamir Yassin
9.John Bocco
10.Emmanuel Okwii
11.Shiza kichuya
Benchi
-Emmanuel Mseja
-Method Mwanajli
-Jamali Mwambeleko
-Jonas Mkude
-Said Hamisi Ndemla
-Mwinyi Kazimoto
-Laudit Mavugo
Muda saa 10:00 uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Cristiano Ronald aweka mambo hadharani

Nyota wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo amerejea kwao Ureno jana Septemba 16. Katika urejeo wake huo Ronaldo ametembela klabu yake aliyoanzia maisha ya soka Sporting CP akiwa ameambatana na mpenzi wake Georgina Rodriguez.
Ronaldo alifika mapema kwenye uwanja wa Estadio Jose Alvalade na kukutana na viongozi wa klabu hiyo ambao walimkaribisha na kumtembeza maeneo mbalimbali ya uwanja.
Baadae Ronaldo aliketi jukwaani na mpenzi wake kwaajili ya kutazama mchezo wa ligi kuu ya Ureno kati ya timu yake ya Sporting CP dhidi ya ya Tondela ambapo Sporting CP ilishinda 2-0.

Friday, 15 September 2017

Mabadiliko kombe la Dunia



Shirikisho la soka la kimataifa FIFA limebadili utaratibu wa namna ya kupanga makundi katika fainali za Kombe la dunia 2018 nchini Urusi.
FIFA imesema wakati wa kupanga makundi itazingatia viwango vya soka ambavyo huwa inavitoa kila mwezi kwa timu za taifa ambapo sahani (pot) zote 4 zitapangwa kulingana na viwango kwenye orodha ya FIFA. Awali sahani ya kwanza pekee ndio ilikuwa inazaingatia viwango hivyo lakini sasa itakuwa ni kwa pot zote.
Pia FIFA imethibitisha kuwa itatumia viwango itakavyotoa mwezi Oktoba. Hii inamaanisha sahani ya kwanza huenda ikawa na timu za Ujerumani, Brazil, Ubeligji, Argentina, Ureno pamoja na wenyeji Urusi, lakini hadi sasa Brazil na Ubeligji pekee kwenye nchi za juu ndio zimefuzu.