Tuesday 30 August 2016

TRA yaanzisha utaratibu wa wanafunzi kulipa kodi vyuoni

Mkurugenzi wa huduma na elimu ya mlipa kodi (TRA) Richard Kayombo

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeanzisha utaratibu wa kufungua klabu za wanafunzi wa kodi vyuoni ili kurahisisha utoaji na upatikanaji wa elimu kwa mlipakodi katika jamii.
Akizungumza na wanafunzi wa Chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro, Mkurugenzi huduma na elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo ameeleza lengo la kuanzisha Klabu hizo ni kutaka kuwajenga wanafunzi kuwa na misingi ya ulipaji kodi.

“Lengo ni kuleta elimu ya kodi kwa wanafunzi na kutambua kwamba nyinyi ni walipa kodi, kwa namna moja au nyingine kama alivyosema kiongozi mwingine hapo awali kwasababu mnanunua bidhaa,”, alisema Kayombo.

Aliongezea, hivyo mnavyonunua bidhaa mnakuwa mnachangia kodi, kama wanafunzi wote vyuo vyote nchini siku moja mkasema katika manunuzi yetu kila mtu anayenunua adai risiti, au tukasema usipo toa risiti tunasusa hatununui kwako wote nina hakika watatoa risiti”, aliongezea.

No comments:

Post a Comment