
Azam waliichapa Yanga kwa penalti 4-1 katika mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kumaliza dakika tisini kwa sare ya mabao 2-2, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ameiambia FOFAMMEDIA kuwa,
waliwapa Azam ngao ambayo siyo yenyewe kutokana na kuchelewa kukamilika
kwa utengenezwaji wa ngao halali ambalo walitakiwa kupewa.
“Lile kombe ambalo tuliwapa Azam siku ile walipocheza na Yanga kwenye
Ngao ya Jamii halikuwa lenyewe, bali tulilitoa kwa ajili ya kuziba
nafasi ya kombe halisi ambalo lilichelewa kuja kutokana na kutokamilika
mpaka inafika siku ile, hivyo tukaona siyo vizuri bingwa akiondoka
mikono mitupu.
“Tumepanga kuwabadilishia na kuwapa kombe lao halisi ambalo walistahili
kupewa ambalo hili litakuwa na thamani halisi na mwonekano tofauti
kabisa na lile ambalo tulilitoa awali,” alisema Alfred.
No comments:
Post a Comment