Waziri wa Afya, Maendeleo ya
jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa tatu kulia akitia
udongo kwenye kichanja cha nondo kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa
awamu ya pili wa jengo la hospitali ya Agakhan katika uzinduzi huo
uliofanyika jana jijini Dar es salaam, na wa pili kushoto ni Mwenyekiti
wa kamati ya bodi hospitali ya Agakhan Bi. Zahra Aga Khan.
Wafanyakazi na wadau mbalimbali wa
hospitali ya Agakhan wakimsikiliza kwa kwa makini Waziri wa Afya,
Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo
pichani wakati wa sherehe ya uzinduzi wa ujenzi wa awamu ya pili wa
jengo la hospitali ya Agakhan.
Habari/Picha Na Ally Daud
Serikali imeuomba uongozi Wa
Agakhan kujenga hospitali nyingine kubwa katika mkoa Wa Dodoma ili
kuendana na agizo la Rais Wa awamu ya tano Dkt.John Magufuli na
kuboresha huduma bora za afya Mkoani humo.
Akizungumza hayo wakati wa
ufunguzi wa awamu ya pili ya jengo la hospitali ya Agakhan Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
amesema kuwa Agakhan wanatakiwa wajenge hospitali nyingine kubwa mkoani
Dodoma ili kueneza Huduma bora za kiafya.
“Kutokana na Agizo la Rais Wa
awamu ya tano Dkt. John Magufuli la kuhamia Dodoma inabidi na nyinyi
mjenge hospitali kule” alisema Mhe. Ummy.
Mhe. Ummy ameongeza kuwa kwa
kujengwa hospitali hiyo Serikali itakua iokoa shilingi billion 20 mpaka
25 kwa ajili ya wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Aidha Mhe.Ummy amesema kuwa
anaushukuru uongozi Wa Agakhan kwa kuanza kujenga jengo ilo
linalogharimu Billioni 112 ili kuondoa kero kwa wagonjwa Wa magonjwa
yasioambukiza na kurahisiaha huduma na matibabu bora kwa wagonjwa
nchini.
Mbali na hayo Mwenyekiti wa kamati
ya bodi hospitali ya Agakhan Bi. Zahra Aga Khan amesema kuwa wanampango
Wa kumaliza jengo hilo kwa ajili ya kutoa Huduma bora za kiafya nchini
ili kutokomeza maradhi ya mara kwa mara.
“Tuna morali kubwa ya kumalizia
jengo hili ili tuweze kuboresha Huduma ya afya nchini kwa kutoa tiba
zenye uhakika na za kisasa” alisema Bi Zahra
No comments:
Post a Comment