Tuesday 31 January 2017

ZILIZOBUBASHARA LEO KATIKA MAGAZETI YA FEB O1 2016


 

Gazeti la MwanaHALISI lamuomba Radhi Rais Magufuli

Misikiti yafungwa nchini Uholanzi

Misikiti mikubwa yafungwa nchini Uholanzi
Misikiti mikubwa minne nchini Uholanzi yafungwa kwa muda baada ya tukio la shambulizi la msikiti mjini Quebec nchini Canada .
Kwa mujibu wa shirika la habari la Uholanzi ni kuwa baada ya shambulizi la Canada maafisa wakuu wa misikiti hiyo minne walifanya mkutano wa dharura .

Baadaye misikiti hiyo mikubwa iliyopo katika miji ya Amsterdam, Rotterdam, Hague na Utrecht ilitangazwa kufungwa kwa muda na kwa ajili ya usalama .
Takriban watu 6 walifariki baada ya watu 3 kuingia katika msikiti mmoja Canada na kushambulia waumini waliokuwa wanafanya sala ya usiku ,8 wameripotiwa kujeruhiwa katika shambulio hilo .

Ufaulu umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015

 Image result for Charles Msonde
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo ufaulu umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.
Dkt. Charlse Msonde, Katibu Mtendaji NECTA
Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.
Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa watahiniwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya mtihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.
Aidha amesema baraza hilo limefuta matokeo ya watahiniwa 126 waliobainika kufanya udanganyifu ikiwa ni pamoja na watahiniwa 58 wa shule, 58 wa kujitegemea na watahiniwa 10 wa QT. Pia baraza hilo limefuta matokeo ya mtahiniwa mmoja aliyebainika kuandika matusi kwenye karatasi yake ya majibu.
Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60

Kwa upande wa masomo, amesema ufaulu katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic Mathematics, Physics, Biology, Commerce na Book keeping umepanda kwa kati ya asilimia 0.12 na 8.08 ikilinganishwa na mwaka 2015.
Somo lililoongoza kwa ufaulu ni Kiswahili ambapo asilimia 77.75 wamefaulu na somo la mwisho ni Basic Maths ambalo asilimia 18.12 ya watahiniwa wa shule wamefaulu.

Kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 5 ni wasichana na 5 ni wavulana wakiongozwa na Alfred Shauri kutoka Feza Boys ya Dar es Salaam
Kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa, shule 6 zinatoka katika mkoa wa Dar es Salaam

Azam FC Bocco, Kingue, Sure Boy ni Majeruhi


BAADA ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, kuanza rasmi mazoezi jana jioni kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Ndanda, daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa, amezungumzia hali za kiafya za baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi.
Wachezaji wa Azam FC waliokuwa majeruhi ni nahodha John Bocco ‘Adebayor’, Stephan Kingue waliopata majeraha ya misuli ya paja kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Simba, ambao matajiri hao walishinda bao 1-0 lililofungwa na Bocco.
Wengine wanaouguza majeraha, ambao waliukosa mchezo huo ni kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, kipa Mwadini Ally (nyama za paja) na beki Shomari Kapombe, ambaye ni mgonjwa lakini hivi sasa akiendelea vema.
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz mara baada ya mazoezi ya jana, Mwankemwa alisema kuwa Bocco na Kingue watakaa nje ya dimba kwa muda wa wiki mbili tokea jana, huku Sure Boy akitarajiwa kuanza rasmi mazoezi leo na Mwadini akipumzishwa kwa siku tatu kuanzia jana.
“Bocco hali yake inaonekana kuimarika vizuri tokea alipopata majeraha hayo ya kuchana msuli wa nyuma ya paja, Stephan (Kingue) kwa upande wake naye amechana msuli wa mbele ya paja, hivyo wote watakaa nje ya dimba kwa muda wa wiki mbili kutoka sasa (jana) na wataanza mazoezi mepesi baada ya wiki moja,” alisema.
Daktari huyo bingwa mzoefu, alisema hali za wachezaji wengine ziko vizuri kabisa kuendelea na mikikimikiki ya maandalizi kuelekea mechi zijazo za ligi pamoja na michuano mingine.

Serikali Yatenga Bil. 13.9 Kujenga Nyumba 1,157 za Walimu

Image result for Selemani Jafo
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Katika bajeti ya mwaka 2016/17, Serikali imetenga shilingi bilioni 13.9 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu 1,157 wa shule za msingi  nchini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ameyasema hayo leo, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge Viti Maalum, Mhe. Juliana Daniel Shonza juu ya mpango wa kuboresha miundombinu ya elimu vijijini kama vile nyumba za walimu pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya walimu.
“ Katika bajeti ya mwaka 2016/17, Serikali imetenga shilingi Bil. 13.9 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu 1,157 kwa shule za msingi na shilingi bilioni 11.14 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 661 kwa shule za sekondari,” alifafanua Jafo.
Aliendelea kwa kusema kuwa, Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMESII) imekamilisha ujenzi wa nyumba 146 kati ya nyumba 183 ambazo kila nyumba wataishi walimu Sita (6 multi-unit houses).
Aidha ameeleza kuwa ujenzi wa nyumba  hizo umegharimu shilingi bilioni 21.9 ambapo nyumba 37 zinaendelea kujengwa kwa gharama  ya shilingi bilioni 5.5 na zinategemea kukamilika tarehe 30 Aprili, 2017.
Kuhusu ulipaji wa madeni ya walimu, Jafo amesema kuwa Serikali imeendelea kulipa madeni kadri yanavyojitokeza na kuhakikiwa ambapo katika mwezi  Oktoba, 2015 Serikali ililipa madeni ya shilingi bilioni 20.12 kwa walimu 44,700 na shilingi bilioni 1.107 zililipwa mwezi February, 2016 kwa walimu 3221.

Benki ya KCB Tanzania yatoa mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali Mkoa wa Arusha.

SAD1
Meneja wa kanda ya kaskazini wa Benki ya KCB Tanzania Judith Lubuva, akiongea na wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hyo mkoani Arusha.
SAD2
Afisa Mawasiliano ya Umma wa benki ya KCB Margaret Makere akiongea na wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hiyo mkoani Arusha.
SAD3
Mwalimu wa Ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Nina Nchimbi akitoa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania kwa wanawake wajasiriamali wa mkoa wa Arusha.

SAD4
Meneja wa kanda ya kaskazini wa Benki ya KCB Tanzania Judith Lubuva (aliyekaa wapili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali waliohudhuria na kumaliza mafunzo ya ujasiriamali yalitolewa na benki hiyo katika mkoa wa Arusha.

Katika swala zima la kumkomboa mwanamke mjasajiriamali, Benki ya KCB Tanzania inaendelea na programu ya mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali yanayoitwa 2JIAJIRI. Programu hii inalenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika changamoto zinazosababisha biashara yake ishindwe kuendelea.
Benki ya KCB imepanga kufundisha wanawake wajasiriamali 315 kutoka mikoa ya Dar Es salaam, Mwanza, Morogoro, Arusha, Moshi na Zanzibar  ambapo matawi ya benki hiyo yapo.
Mafunzo haya ni bure kabisa, benki ya KCB inagharimia gharama zote. na yanahusisha Elimu ya Fedha (Financial Literacy), Kufikiwa huduma za kifedha (Financial Inclusion), Masuala ya Kisheria (Legal Framework), Ushindani wa Kibiashara (Business Competitiveness) na kuwa na sifa za kukopesheka (How to be bankable).
Zaidi ya mafunzo hayo, benki ya KCB itawapatia wanawake wajasiriamali hao maafisa watakao wafundisha kwa vitendo kwenye maeneo ya biashara zao. Maafisa hao watakua ni afisa fedha, afisa sharia na afisa masoko.
Kwako mwanamke mjasiliamali “JIULIZE KWANINI uhangaike wakati benki ya KCB tupo!”

Matokeo ya kidato cha nne 2016 na matokeo ya QT 2016 yametoka

Image result for MATOKEO KIDATO CHA NNE 2016Leo January 31 2017 Baraza la mitihani Tanzania ‘NECTA’ limetangaza matokeo ya kidato cha nne ‘CSEE 2016’ na matokeo ya mtihani wa maarifa (QT) 2016
Kwa urahisi unaweza kuyaona matokeo ya kidato cha nne kwenye link iliyoandikwa ‘CSEE 2016’ >>>CSEE 2016
Unaweza pia kuyatazama matokeo ya matokeo ya mtihani wa maarifa (QT) 2016  >>>(QT) 2016

Monday 30 January 2017

MAGAZETI YA LEO JUMANNE


 

Taarifa ya Ujenzi wa Bomba Jipya La Mafuta Safi La Tazama

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasikiliza Mawaziri wa Nishati kutoka Tanzania na Zambia wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi kutoka Tanzania mpaka Zambia, Mawaziri hao ni Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Mhe.Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Mhe.Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba (kushoto) mara baada ya kumaliza mkutano wa kumpa taarifa Makamu wa Rais ya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi, Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba (kushoto) mara baada ya kupokea taarifa ya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi litakalotoka Dar es Salaam, Tanzania mpaka Ndola, Zambia, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Tanzania na Zambia ambao ulifanya ziara ya kukagua pampu na bomba la mafuta la TAZAMA kutoka Ndola, Zambia mpaka Dar es Salaam Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba ambapo walifanya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi litakalotoka Dar es Salaam, Tanzania mpaka Ndola, Zambia.

Mwanahalisi lapewa Saa 24 kumuomba Rais Magufuli Msamaha

Mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini, Efrahim Mwaitenda amejeruhiwa kwa kupigwa risasi

Mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini, Efrahim Mwaitenda mwenye umri wa miaka 60 amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mgongoni na mtu au watu wasiofahamika.
 

Mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini (Aliyekaa) akipeleka hospitali)
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29.01.2017 majira ya saa 05:45 usiku katika kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha Mahenge, Kata ya Makwale, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya.
Amesema tukio hilo limetokea wakati akiwa amelala kitandani nyumbani kwake Ntembela ambapo mbinu iliyotumika ilikuwa ni  kukata wavu wa dirisha na kumjeruhi kwa kutumia silaha za kienyeji zinazotumia risasi za gololi.

Mwenyekiti huyo amefikishwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na hali yake inaendelea vizuri.
Lukula amewaambia waandishi wa habari kuwa nia ya shambulizi hilo ilikuwa ni kutaka kuumua na kwamba juhudi za kuwatafuta na kuwakamata wahusika zinaendelea 

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako ya kudhibiti uhalifu

kamanda
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya , Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Emmanuel G. Lukula

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. Mafanikio yaliyopatikana katika msako ni kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 29.01.2017 majira ya saa 23:45hrs katika kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha Mahenge, Kata ya Makwale, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. EFRAHIM S/O MWAITENDA, [60], mkazi wa Ntembela mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini, alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mgongoni na mtu/watu wasiofahamika  akiwa amelala kitandani nyumbani kwake, mbinu  ni kukata wavu wa dirisha na kumjeruhi kwa kutumia silaha za kienyeji zinazotumia risasi za gololi, nia ni kutaka kuumua. Mhanga amefikishwa Hospitali ya Rufaa na hali yake inaendelea vizuri. Juhudi za kuwatafuta na kuwakamata zinaendelea.
Aidha mnamo tarehe  29.01.2017 majira ya saa 10:30hrs, katika  mpaka wa nchi ya  Mlawi na Tanzania Kasumulu Wilayani Kyela, mfanyabiashara ajulikanae  kwa jina moja la JAPHET amekamatwa na kikosi maalumu  [Task Force ] ya  TRA , POLISI na MAAFISA WAKILIMO  akiwa anavusha mahidi kwa njia ya panya kutoka nchi jirani ya Malawi bila ya kufuata utaratibu wa sheria za uingizaji chakula nchini. Mahidi hayo yamekamatwa yakiwa kwenye gari moja aina ya canter na mengine yalikuwa yamehifadhiwa kwenye store. Wakati wa uchukuaji wa mahidi store kundi la wananchi walijitokeza na walianza kuwazuia maafisa wa TRA kupakia mahindi hayo kwa kile walichodai kuwa wanauziwa mahindi hayo kwa bei rahisi. Kutokana na hali hiyo  Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi hao. Hata hivyo hali baada ya muda ilirejea kuwa shwari. Ufuatiliaji wa karibu unaendelea ili kubaini wafanyabiashara wenye tabia kama hiyo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi EMANUEL G. LUKULA anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria pia anatoa onyo kwa wafanyabiashara wasiofuata sheria, kanuni na taratibu za kusafirisha bidhaa iwe kutoa au kuingiza kwani mkono wa sheria  utawafikia kwani Jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau wengine linaendelea kufanya misako ili kukomesha tabia hiyo. Aidha anatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa Jeshi la Polisi ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
[EMANUEL G. LUKULA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Obama anaweza kulipwa hadi shilingi bilioni 99 kuandika kitabu kipya cha maisha yake

Barack Obama amepumzika sasa baada ya kuitumikiaa Marekani kwa miaka minane kama Rais. Lakini, hiyo haimaanishi kuwa ametoka kwenye mzunguko wa fedha. Na tena, huenda akaanza kuingiza nyingi zaidi, asante kwa mikataba minono inayomuwinda kutoka kwa wachapishaji wa vitabu.

Yeye na mkewe Michelle, ni uamuzi wao tu, kukubali kusaini mikataba ya vitabu, yenye thamani ya kuanzia dola milioni 20 hadi 45. Fedha hizo, pamoja na matumizi mengine, zitamwezesha kugharamikia bili za ndege binafsi, sababu amewahi kudai kuwa hatopenda kusafiri na ndege za kawaida akistaafu.

Kwa mujibu wa New York Times, mawakala wa masuala ya vitabu wanadai kuwa Obama ana nafasi ya kuandika kitabu chenye thamani kubwa zaidi kuwahi kuandikwa na Rais yeyote.
Wengine wanadai kuwa Obama anaweza kuingiza zaidi ya dola milioni 12, na mkewe zaidi ya dola milioni 10.

Obama amewahi kuandika vitabu vitatu, “Dreams From My Father,” “The Audacity of Hope” na “Of Thee I Sing” ambavyo vimeuza zaidi ya nakala milioni 4 duniani na kumuingiza zaidi ya dola milioni 10.

Rais Trump atetea hoja yake kuhusu Wanaotaka kuingia Nchini Marekani

Rais Trump atetea hoja yake kuhusu usafiri 
Rais wa Marekani Donald Trump ameteta marufuku yake ya muda ya kusafiri kwa watu wanaotoka nchi saba alizoorodhesha.
Rais Trump amewalaumu waandishi wa habari kwa kuupoteza umma baada ya kusema sera hiyo imelenga nchi za Kiislamu peke yake.

Kwa mujibu wa habari Rais Trump amesema viza zitatolewa kwa wasafiri kutoka nchi zote ndani ya siku tisini.
Hata hivyo kiongozi wa wafanyakazi wa Serikali Reince Priebus amesema marufuku hiyo haitawahusu wenye kuhodhi kadi za Green ambao wana haki ya kisheria kuishi Marekani.
Sera hii imeonekana kupingwa vilivyo na nchi nyingi.

Mv Kigamboni yaendelea kutoa Huduma ya Usafiri katika Jiji la Dar es salaam

KIV1
Abiria wakipanda katika kivuko cha Mv. Magogoni kinachotoa huduma ya usafiri kati ya Ferry na Magogoni, leo Jijijini Dar es salaam.
KIV2
Abiria wakishuka kutoka katika kivuko cha Mv. Kigamboni kinachotoa huduma ya usafiri kati ya eneo la Magogoni na Feri, leo Jijijini Dar es salaam.

Kipa Kagera Sugar David Burhan amefariki dunia

David Burhan enzi za uhai wake. 
Kipa wa Kagera Sugar David Burhan amefariki dunia alfajiri ya leo wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Akizungumza  asubuhi , Meneja wa Kagera Sugar, Mohammed Hussein amethibitisha taarifa za kifo cha mchezaji huyo na kusema klabu imeondokewa na mchezaji wake muhimu.

“Ndio,Burhan amefariki saa 12 asubuhi ya kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu…ni huzuni lakini tunamwachia Mungu,” amesema Hussein na kuahidi kutoa taarifa zaidi baadaye kuhusu kifo cha mchezaji huyo.
Enzi za uhai wake mchezaji huyo pia aliwahi kuichezea Majimaji ya Songea na Mbeya City ya Mbeya.

Sunday 29 January 2017

ZILIZOONEKANA KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JAN 30 2017

 

Cesc Fabregas,Kelvin De Bruyne na Andre Iniesta ni wachezaji waliopiga Pasi nyingi

Cesc Fabregas,Kelvin De Bruyne na Andre Iniesta ni wachezaji wanaosifika kupiga sana pasi.Lakini msimu huu hawapo hadi sasa katika orodha ya waliopiga pasi nyingi.Lakini Paul Pogba,Herrera na Henderson ni wachezaji waliopo kwenye listi hii.Hembu tuone wachezaji 10 waliopiga pasi nyingi katila ligi 5 kubwa barani Ulaya.

10.Benjamin Andre.
Timu Rennes
Pasi alozopiga  1181
Pasi za kwenda mbele 671
Nafasi alizotengeneza 22
Assist 2

9.Ander Herrera
Timu Man United.
Pasi alizopiga 1185
Pasi za kwenda mbele 691
Nafasi alizotengeneza 25
Assist 3

8.Marco Verrati.
Timu Psg.
Pasi alizopiga 1192
Pasi za kwenda mbele 719
Nafasi alizotengeneza 22
Assist 2

7.Malang Sarr
Timu Nice.
Pasi alizopiga 1237
Pasi kwenda mbele 953
Nafasi alizotengeneza 3
Assist 1

6.Thiago Alcantara.
Timu Bayern Munich
Pasi alizopiga 1258
Pasi kwenda mbele 727
Nafasi alizotengeneza 25
Assist 3.

5.Wylan Cyprien
Timu Nice.
Pasi alizopiga 1260
Pasi za kwenda mbele 729
Nafasi alizotengeneza 23
Assists 3

4.Paul Pogba
Timu Manchester United.
Pasi alizopiga 1271
Pasi za kwenda mbele 760
Nafasi alizotengeneza 41
Assists 3

3.Marek Hamski
Timu Napoli.
Pasi alizopiga 1477
Pasi za kwenda mbele 713
Nafasi alizotengeneza 45
Assist 7

2.Jordan Herndeson
Timu Liverpool.
Pasi alizopiga 1533
Pasi za kwenda mbele 926
Nafasi alizotengeneza 28
Assists 4

1.Thiago Motta
Timu PSG
Pasi alizopiga 1623
Pasi za kwenda mbele 1148

Nafasi alizotengeneza 10
Assists 0

Maalim Seif Sharif Hamad:Nimepitia yote kasoro Kifo

  Image result for maalim seif
Leo January 29 2017 kupitia Funguka ya AzamTV, katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amehojiwa na kuzungumzia ishu mbalimbali ikiwemo za Profesa Lipumba, Zanzibar na maamuzi yake mengine.
Kweli Lipumba alijiuzulu na alipoonyesha nia ya kujiuzulu tulimfuata kwenda kumuomba sana asiondoke hasa wakati ule tulikuwa tunakabiliwa na uchaguzi lakini akaendelea na msimamo wake, hakufukuzwa
Lipumba kajiuzulu mwenyewe, amekaa baada ya miezi 10 anaandika barua kwamba anatengua jambo hili mimi sijawahi kuliona hilo Duniani

Fedha za ruzuku zimekwenda kwenye akaunti ambayo bodi ya wadhamini, katibu mkuu hawaijui
Ukiingia kwenye siasa lazima ukubali kutukanwa, kushambuliwa, kufungwa hata kifo, mimi yote nimeshapitia isipokuwa kifo-Maalim Seif.
Jimbo la Dimani kihistoria ni la CCM na sisi tuliingia kwenye uchaguzi tukijua tuna kazi kubwa’Ulikosa?

Natarajia muda mfupi ujao nitakuwa Rais wa Zanzibar’
Baada ya kuacha wadhifa safari zote za nje najilipia mwenyewe na siombi serikalini ingawa nina haki
Hakuna namna yoyote Zanzibar lazima vyama vishirikiane, hii itawaleta Wazanzibar pamoja
Haiwezekani chama kimoja cha upinzani kuishinda CCM lakini UKAWA itasaidia
Jecha alisema anafuta uchaguzi ametumia kifungu gani cha katiba, kama nilifanya kosa kutangaza matokeo kwa nini hawakunipeleka mahakamani?
Lipumba alidhani akijiuzulu wengi watamfuata lakini haikuleta athari CUF, uchaguzi 2015 tulishinda majimbo 10 TZ bara,
Mtu akijiuzulu atumpi tena nafasi, katiba yetu hairuhusu hivyo, Mtu anajiuzulu halafu anarudi unafikiri anarudi kwa mema
Siwezi kukiacha chama cha CUF wala sijafikiria kuunda chama kingine.

Ziara ya Rais Magufuli nchini Ethiopia

Mahakama yapiga marufuku amri ya Trump kurudisha wahamiaji makwao

Donald Trump
Mahakama moja ya New York imeridhia ombi la wanaharakati waliokwenda mahakamani kupinga amri za Rais Trump za kupiga marufuku wakimbizi wa Syria na raia wengine wa nchi sita za kiislamu kwamba wasiingie marekani, mionongi mwao nchi za Iran, Iraq, Somalia, Sudan, Libya na Yemen.
Sasa koti hiyo imeamuru wote waliozuiliwa kupitia amri hizo waachiwe .

Tayari kuna ripoti kutoka uwanja wa ndege wa John F Kennedy kwamba watu kadhaa wamezuiwa kuingia Marekani wakiwemo wale ambayo walikuwa wamepewa ruhusa kwenda kuishi marekani kupitia mpango wa green card.
Waandamanaji kwa upande wao waliokuwa uwanjani hao walipaaza sauti kusema 'let them in' yaana kutaka watu hao waruhisiwe kuingia.

Saturday 28 January 2017

Mkuu wa magareza akamatwa akitoroka Gambia

Maafisa wa polisi nchini Senegal wanasema kuwa wamemkamata mkuu wa magereza nchini Gambia Jenerali Bora Colley alipojaribu kuvuka na kuelekea Guinea Bissau.
Taarifa ya polisi inasema kuwa alikamatwa siku ya Jumatano na baadaye kukabidhiwa jeshi la Senegal.

Makundi ya haki za kibinaadamu yanasema kuwa kiwango kikubwa cha ukandamizi ulifanywa chini ya uongozi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh ikiwemo mateso pamoja na mauaji ya kiholela ambayo yalifanyika katika jela.
Senegal ilichukua jukumu muhimu la kumsihi rais Yahya Jammeh kuondoka nchini humo siku ya Jumamosi.

Trump kuteua jaji anayepinga utoaji mimb

Makamu wa rais wa Marekani , Mike Pence, ameuambia mkutano wa watu wanaopinga swala la utoaji mimba kuwa rais Trump mwenyewe atamteua jaji wa mahakama ya juu mwenye msimamo mkali dhidi ya tabia ya utoaji mimba.
Sera ya mwanamke kujiamulia kuhusu swala la utoaji mimba iliidhinishwa nchini tangu 1973.
Bw. Pence, akizungumza huko Washington amesema mkondo huo utabadilishwa na utawala mpya uliopo sasa.

Ni hivi majuzi tu ambapo utawala wa Trump ulitangaza kukata ufadhili kwa mashirika yote duniani yanaoshughulika na kutoa huduma za afya ya uzazi ambazo zinajumuisha pia huduma za utoaji mimba.

Kampuni ya Google imewataka wafanyikazi wanaofanya kazi katika mataifa ya kigeni kurudi nchini Marekani

 Image result for google image
Kampuni ya Google imewataka wafanyikazi wanaofanya kazi katika mataifa ya kigeni kurudi nchini Marekani kufuatia agizo la rais wa taifa hilo Donald Trump kuwazuia raia wa mataifa sitaya Kiislamu kuingia nchini humo.
Wahamiaji wa Syria wamepigwa marufuku kuingia nchini humo itakapotolewa ilani nyengine.

Visa za raia wa mataifa sita ikiwemo Iran na Iraq hazitatolewa kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo.
Googole imeambia BBC ina wasiwasi kuhusu agizo hilo na mikakati ambayo huenda ikawazuia watu wenye vipaji kuingia nchini Marekani.

Mwandishi wa BBC aneyesimamia maswala ya kibiashara Joe Lyam anasema kuwa agizo hilo la Donald Trump lina maana kwamba maelfu ya raia wa Iran,Iraq, Yemen, Syria,Somali na Libya hataruhusiwa kupanda ndege zinazoelekea Marekani hata iwapo wanamiliki Green Card.
Bw Trump amesema kuwa hatua hiyo itawazuia magaidi kutoingia nchini humo.

Lakini makundi ya haki za kibinaadamu yanasema kuwa hakuna ushirikiano kati ya wakimbizi wa Syria nchini Marekani na ugaidi.

Habari Picha

agaooo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na baadhi ya wanawake wa Njombe kabla ya kuondoka kwenye Ikulu ndogo  baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa huo  Januari 28, 2017. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Njombe, Luth Msafiri.
agao 11
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa wilaya ya Njombe, Luth Msafiri kwenye Ikulu ndogo ya Njombe baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa huo, Januari 28, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Serena Williams katika fainali za Australia Open

SERENAAA
Serena Williams sank to the court after sealing the match winning point to take the 2017 Australian Open
The 35-year-old Serena was her dominant self on the course and inserted her superiority 
The victory means Serena is the oldest winner of a Grand Slam tournament in the open era
Serena has now picked up an open era record of 23 Grand Slams and overtakes Steffi Graf  in the process
Serena returns serve on the backhand as the Daphne Akhurst Memorial Cup watches on from court-side
Using the full extent of her frame, Venus Williams covers ground across court to return a shot out wide
Venus holds her arms aloft after being unable to match the power of her younger sister on a shot
Venus put up a hard fight but couldn't overcome the might of her sister
As the sun set on the action the arena took on an ambient glow while the two sisters went toe-to-toe
Spectators shield their eyes from the son as the action gets under way
A packed stadium watched with bated breath as the two giants of the women's game went head-to-head