Thursday 31 August 2017

ZILIZOMUBASHARA KATIKA KURASA ZA MBELE MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPT 01 2017




Kesi ya Sethi yahairishwa hadi September 14, 2017

Upande wa utetezi umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi amewekewa ‘Puto’ tumboni kutokana na ugonjwa unaomkabili hivyo asipohudumiwa inavyotakiwa anaweza kupoteza maisha.
Mbali ya Seth, mwingine ni Mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya TSh 309,461,300,158.
Wakili wa utetezi, Joseph Mwakandege amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa mteja wake Seth anatakiwa apelekwe Hospital ya Taifa Muhimbili lakini hadi sasa hajapelekwa na ni dhahiri upande wa mashtaka umedharau amri mbili za Mahakama.
”Ugonjwa uliosababisha Seth atakiwe kwenda Muhimbili ni baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa ambapo tumboni kwake kumewekwa Balloon ‘Puto’ hivyo asipohudumiwa ipasavyo inaweza kusababisha kifo, naomba mshtakiwa apelekwe Muhimbili kwa sababu ni Hospitali ya juu na yenye vifaa na watalaamu wa kutosha“
Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali Vitalis Peter amedai kuwa Magereza hawapangiwi wampeleke wapi mshtakiwa ambaye ni mgonjwa bali wana utaratibu, Hospitali na watalaam wao.
”Mshtakiwa alianza kupelekwa Hospital ya Magereza, kisha Hospital ya Amana ambapo alikutana na daktari mtalaam kutoka Muhimbili na aliweza kumuangalia afya yake, hivyo hoja ya kwamba hatujatekeleza amri ya Mahakama sio kweli.”

Mpinzani wa Kagame, apotea Rwanda

Aliyekuwa mpinzani wa Rais wa Rwanda, Diane Rwigara.
Diane Rwigara, aliyekuwa mpinzani wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwenye mchakato wa uchaguzi uliopita amepotea. Ndugu zake wamelitupia lawama jeshi la polisi wakilihusisha na tukio hilo.
Mjomba wa mwanasiasa huyo ameiambia BBC kuwa watu waliokuwepo wakati anachukuliwa wanadai alifungwa pingu na kuondoka na wanafamilia watano ambao wote walifikishwa kwenye kituo cha polisi.
Hata hivyo, msemaji wa jeshi la polisi la nchi hiyo, Theos Badege amekanusha taarifa hizo akieleza kuwa jeshi hilo halikumkamata bali linachokifanya hivi sasa ni kumtafuta.
“Hao wanasema wanapotaka wao wawepo, na kwasababu kazi yetu ilikuwa kuwatafuta ambayo ni sehemu ya uchunguzi kama nilivyosema awali, hatufahamu walipo,” alisema Badege.

Serikali yataifisha magari yaliyoingizwa nchini kinyume na sheria



Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetaifisha jumla ya magari sita yakiwepo magari matatu aina ya Ranger Rover Sports yaliyoingizwa nchini kinyume na sheria baada ya watuhumiwa hao kukiri kuwa wamefanya kosa hilo.
Rais Magufuli mwezi Machi mwaka huu alipokwenda bandarini alikuta kuna makontena yenye magari ndani yake huku wamiliki wa makontena hayo wakidai  makontena hayo yalikuwa na nguo na mabegi  lakini baada ya kufunguliwa zilionekana gari za kifahari zikiwa kwenye makontena hayo, jambo ambalo lilionekana wamiliki wa mahari hayo walikuwa wakiingiza magari hayo kinyume na utaratibu na sheria za nchi.
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, DPP Biswalo Mganga amesema kuwa baada ya mahakama kuwakuta na hatia raia hao wakigeni ambao walidai kuwa kontena hizo zilikuwa na nguo na mabegi wakati ni magari hivyo serikali imetaifisha magari yao na sasa kuwa magari ya serikali.
"Rais hao wamekiri makosa yao yote mawili na kutokana na kukiri kwao mahakama imewatia hatiani na ikaamuru yale magari yote matatu kuyataifisha kuwa mali ya serikali na kila mmoja anatakiwa kulipa faini ya milioni 133 kufidia hasara ambayo serikali imepoteza na kila mmoja anatakiwa kulipa tena milioni tano kama faini ambayo mahakama imewalipisha , wakishindwa kulipa faini hiyo watakwenda jela miaka mitatu" alisema Biswalo

Ibada ya Hijja

Katika kuelekea ibada ya hijja wananchi wametakiwa kulaani vitendo vya kialifu ikiwemo utekajii wa watoto vinavyojitokeza nchini. 
Akizungumza jijini Dar es salaam kiongozi wa kiroho wa dhehebu la shia-ithina sheria nchin shekh hemed jalala amesema wananchi wanatakiwa kushirikiana na jeshi la polisi kutokomeza vitendo hivyo kwa ni vitendo visivyokubalika na dini yeyote 
Amefafanua kuwa uharifu unaojitokeza nchini ni wa kukemewa vikali na kila kiongozi wa dini katika maeneo yao ya ibada 
Aidha Jalala amesema ibada hii ya hijja itumike kusuluisha matatizo mbalimbali na kuleta amani maeneo yasiyo na amani

Habari Picha

PIX 1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 2..
Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi,Pascal Barandagiye, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi, ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 3.
Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi  Duniani (UNHCR) nchini Tanzania,Chansa Kapaya, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 4..
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akipitia nyaraka mbalimbali wakatiKikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi,Harrison mseke.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 5
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba(watano kulia), Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi,Pascal Barandagiye,(wasita kulia), na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi  Duniani (UNHCR) nchini Tanzania,Chansa Kapaya(wanne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Makubaliano ya ushirikiano

IMG_0892A
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dr. Inmi Patterson na Mkuu wa Huduma za Kitabibu wa JWTZ, Meja  Generali (Dk.) Denis Raphael Janga wakitiliana sini mkataba wa kitabibu kwa ajili ya huduma za matibabu ya VVU/UKIMWI nchini Tanzania.
IMG_0897A
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dr. Inmi Patterson na Mkuu wa Huduma za Kitabibu wa JWTZ, Meja  Generali (Dk.) Denis Raphael Janga wakibadilishana nyaraka mara baada ya kusaini kwa ajili ya huduma za matibabu ya VVU/UKIMWI nchini Tanzania.
IMG_0901
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dr. Inmi Patterson na Mkuu wa Huduma za Kitabibu wa JWTZ, Meja  Generali (Dk.) Denis Raphael Janga wakipiga picha ya pamoja na maofisa wa Ubalozi wa Marekani na Jeshi la Wananchi JWTZ mara baada ya kusiniana mkataba huo.

 Serikali ya Marekani kupitia Taasisi ya kijeshi ya Walter Reed (WRAIR) imesaini upya makubaliano ya ushirikiano na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) siku ya Jumanne, Agosti 29, 2017 katika sherehe ya kusaini tamko la pamoja la ushirikiano katika jitihada za kupambana na VVU/UKIMWI. WRAIR ni kitengo cha kikosi cha jeshi la Marekani kinachojihusisha na tafiti za kitabibu na kimefanya kazi moja kwa moja na JWTZ tangu mwaka 2004 kutekeleza programu za VVU/UKIMWI Tanzania.
Utiaji saini huo uliofanywa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dr. Inmi Patterson na Mkuu wa Huduma za Kitabibu wa JWTZ, Meja  Generali (Dk.) Denis Raphael Janga, unawakilisha dhamira ya pamoja katika upatikanaji endelevu wa huduma za afya na mpango mkakati wa kukabiliana na tishio la VVU/UKIMWI.
Makubalino ya awali, yaliyosainiwa mwaka Aprili 2011 yanabainisha ushirikiano wa pande hizo mbili katika kupunguza maambukizi mapya na kuboresha matibabu na huduma za kuzuia maambukizi.
Kupitia ushirikiano huu endelevu wa pande hizi mbili Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) unatoa nafasi kwa majeshi ikiwemo JWTZ kuelewa vizuri tishio la afya, tabia na mazingira hatarishi yanayohusiana na kuenea kwa maambukizi ya VVU.

Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini kufanyika tarehe 7 hadi 8 mwezi Septemba mkoani Dodoma

Pix 01
Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akieleza juu ya maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 7 hadi 8 mwezi Septemba.
Pix 02
Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi (kushoto) akionesha kwa waandishi wa habari picha yenye mashine ya kushindilia barabara ambayo imegunduliwa na wahandisi wa hapa nchini na kupewa jina la Magufuli One, kulia ni Msajili Msaidizi wa bodi hiyo, Mhandisi Benedict Mukama .
Pix 03
Msajili Msaidizi wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Benedict Mukama  (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akieleza juu ya maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 7 hadi 8 mwezi Septemba, kushoto ni Kaimu Msajili wa bodi hiyo, Mhandisi Patrick Barozi.

Dkt. Makongoro Mahanga Akamatwa na Kufikishwa Mahakamani



Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Dk Makongoro Mahanga amekamatwa na Polisi Mkoa wa Ilala kwa amri ya Mahakama Kuu na amefikishwa mahakamani.
Mahakama iliamuru Dk Mahanga akamatwe na kufikishwa mahakamani kwa kushindwa kutekeleza uamuzi unaomtaka amlipe mdai Kainerugaba Msemakweli Sh14 milioni.
Fedha hizo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli baada ya kushinda kesi ya madai ya kashfa ambayo Dk Mahanga alimfungulia kwa kumtaja kwenye kitabu chake kinachoitwa: “Mafisadi wa Elimu”.
Katika kitabu hicho anamtaja kuwa ni mmoja wa viongozi wenye shahada za udaktari wa kughushi.
Kati ya kiwango hicho cha fedha, Dk Mahanga ameshalipa Sh6 milioni hivyo anadaiwa Sh8 milioni.

Tamko la Kamati ya Nidhamu TFF kuhusu Msuva, Chirwa na Kaseke



Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemkuta na makosa ya utovu wa nidhamu aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga anayekipiga nchini Morocco, Simon Msuva ambaye imempa onyo kali la barua.
Mbali na Msuva, wengine waliokuwa wakijadiliwa na kamati hiyo kwa utovu wa nidha kwenye michezo ya mwisho ya Ligi Kuu Tanzania Bara ni Obrey Chirwa (Yanga) na Deus Kaseke (Yanga) ambao wamesamehewa.

Shirika la Posta Tanzania limekusanya madeni ya shilingi bilioni 7.6.

1.JPEG
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Prof. Norman Sigala King (katikati), akiongoza kikao cha Kamati yake na Shirika la Posta Tanzania (TPC), kilichofanyika mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi S. Kakoso.
2.JPEG
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng.  Edwin Ngonyani, akifafanua jambo kwa  Kamati ya Bunge ya Miundombinu  katika kikao chao na Shirika la Posta Tanzania (TPC), kilichofanyika mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Prof. Norman Sigala King na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Sekta ya Mawasiliano Eng. Angelina Madete.
3.JPEG
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Luteni Kanali mstaafu Haruni Kondo, akitoa taarifa ya Shirika hilo kwenye kikao chao na Kamati ya Bunge ya Miundombinu kilichofanyika mjini Dodoma. Kulia kwake ni mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Anna Lupembe.
4.JPEG
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Anna Lupembe (wa kwanza kulia), akichangia hoja katika kikao cha Kamati hiyo na Shirika la Posta Tanzania (TPC), kilichofanyika mjini Dodoma. Kushoto kwake anayesikiliza ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo Luteni Kanali mstaafu Haruni Kondo.

Shirika la Posta Tanzania (TPC), limefanikiwa kukusanya madeni ya muda mrefu kutoka kwa taasisi za Serikali, mashirika ya umma na sekta binafsi kiasi cha shilingi bilioni 7.6.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Shirika hilo kilichofanyika mjini Dodoma ambapo amesema makusanyo hayo ni kati ya jumla ya shilingi bilioni 12 ambazo Shirika hilo linadai wateja wake kuanzia mwaka 2011 hadi mwezi Juni mwaka huu.
“Hakikisheni mnamalizia makusanyo ya deni lililobaki, kwani Shirika linahitaji kuendelea na kupata faida kupitia makusanyo haya”, amesema Naibu Waziri Ngonyani.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Mhe. Prof. Norman Sigala King ameiomba Serikali kuliondoa Shirika hilo kwenye orodha ya mashirika yanayotaka kubinafsishwa.
Ameongeza kuwa Serikali ikitekeleza jambo hilo, italiwezesha Shirika hilo kujiendesha kibiashara, kuzalisha faida na kukabiliana na changamoto za ushindani kwenye soko.
Aidha, amelitaka Shirika hilo kuwa wabunifu katika utoaji wa huduma zake kwa wananchi kwa kutumia Teknolojia za kisasa zaidi badala ya kutumia mifumo ya kizamani.  
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika hilo Luteni Kanali mstaafu Bw. Haruni Kondo, ameiomba Kamati hiyo kuendelea kushirikiana na Shirika hilo na kulisaidia ili liweze kutoa huduma kwa wananchi kwa wakati na kwa ufanisi.
Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma yanaendelea na utekelezaji wa agizo la Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuhakikisha kuwa yanajiendesha kwa faida, kuongeza ukusanyaji wa mapato na kudai madeni ya muda mrefu ili fedha hizo ziweze kutumika kuwahudumia wananchi katika nyanja mbalimbali kama vile za elimu, afya na ujenzi wa miundombinu.

Ne-Yo, Diamond Platnumz kupanda Jukwaa moja Uingereza

Msanii wa muziki wa Pop na RnB kutoka Marekani, Neyo  amemjumuisha Msanii kutoka Tanzania   Diamond Platnumz kwenye ziara yake ya kimuziki nchini Uingereza.
Orodha ya miji na kumbi atakazotumbuiza Ne-Yo na Diamond Platnumz kwenye ziara yake nchini Uingereza
Ne-Yo amethibitisha hilo na kutoa ratiba yake kamili ya Tour yake ambayo iliahirishwa mara mbili, mwishoni mwa mwaka jana na mwezi Machi mwaka huu baada ya kutokea mashambulizi ya kigaidi jijini Manchester nchini Uingereza.
Tour hiyo itaanza tarehe 13 hadi 23 Septemba mwaka huu na atatumbuiza miji nane nchini humo kote akiwa na Diamond Platnumz.
Hii inakuwa ni ziara kubwa ya kwanza kwa Diamond Platnumz kupewa shavu la kutumbuiza kwenye tour ya Msanii mkubwa duniani, hivyo watanzania tusubiri neema kwenye muziki wetu itakayopatikana baada ya ziara hiyo iliyopokelewa kwa mikono miwili na Waingereza.

Marekani kuongeza askari Afghanistan

wizara ya ulinzi nchini Marekani Pentagon imethibitisha Kuhusu uwepo wa askari kumi na moja elfu wa Marekani hukoAfghanistan, hii ni Idadi kubwa zaidi kuliko elfu nane na mia nne, kinyume na ilivyoainishwa awali.
Maofisa wa ngazi za juu kutoka katika wizara hiyo wanasema takwimu hiyo mpya ni pamoja na vitengo vya muda na kubadilisha pamoja na majeshi ya kawaida.
Taarifa hiyo inafuatia wizara hiyo ya ulinzi ikijiandaa kupelaka Kama askari elfu nne zaidi nchini Afghanistan ili kusaidia kupambana na askari wa Taliban na kuwasaidia Afghanistan kujinyakulia ushindi na hii ni kwa muujibu wa sera mpya iliyotangazwa na Rais Trump wiki iliyopita.

Liverpool waibomoa Arsenal, wamnyakuwa Chamberlain

Hatimaye aliyekuwa mchezaji wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain amefanikiwa kusaini mkataba wa kujiunga na Liverpool.
Mchezaji huyo amejiunga na Majogoo hao wa Anfield kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 40.
Awali Chamberlain alikuwa akiwaniwa kwa ukaribu na Chelsea ambayo hakufanikiwa kuipata saini yake.
Hata hivyo mchezaji huyo amewashangaza mashabiki wengi baada ya kukataa kuongeza mkataba mpya na Arsenal ambao ungemfanya kuweza kulipwa kiasi cha paundi 180,000 kwa wiki na badala yake amekubali kujiunga na Liverpool kwa kulipwa mshahara wa paundi 120,000 kwa wiki.

Vibaka mjini London wamevamia duka la Arsenal

Majanga yameendelea kuikumba klabu ya Arsenal ambapo safari hii watu wanaosadikiwa kwamba ni vibaka wamevamia duka la klabu hiyo lililopo uwanja wao wa nyumbani wa Emirates na kuiba.
Vibaka hao walivunja baadhi ya vitu ikiwemo bendera kubwa ya klabu hiyo iliyopo nje ya duka hilo na kisha kuzama ndani na kuiba baadhi ya bidhaa ambazo zilikuwemo ndani ya duka hilo usiku wa Jumanne.
Baada ya tukio hilo wezi hao walitoka njr na kupakia gari kisha kukimbia na kuwaacha watu walioko eneo na jirani hilo kushikwa na butwaa,muda mfupi baada ya tukio hilo polisi wa kitongoji hicho cha Islington walifika uwanjani hapo.
Polisi hao wamewataka raia wa karibu na eno hilo kutoa taarifa za kuwezesha kuwakamata waliofanya tukio hilo la kihalifu kupiga simu maalumu namba 101 kutoa taarifa.

Wednesday 30 August 2017

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOST 31 2017




Serikali Yaanza kukabidhi Leseni kwa Magazeti

PIX0
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi leseni ya usajili wa Gazeti la Daily News mwakilishi wa gazeti hilo Bi. Pudenciana Temba. Idara ya Habari imetoa imetoa leseni nne kwa ambapo leseni namba moja imetolewa kwa Jarida la Nchi Yetu linalotolewa na Idara hiyo, namba mbili imetolewa kwa HabariLeo, namba tatu Dailynews na nne imetolewa kwa Spotileo.Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Usajili Bw. Patrick Kipangula.
PIX1
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi leseni ya usajili wa Gazeti la HabariLeo mwakilishi wa gazeti hilo mhariri wa gazeti hilo Bw. Amir Mhando leo Jijini Dar es Salaam. Leseni hiyo imetolewa kufuatia kuanza kwa matumizi ya sheria mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.
PIX2
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayomiliki magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo Dkt. Jim Yonaz akisisitiza jambo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kutolewa kwa Leseni za magazeti ya Kampuni yake kumalizika leo Jijini Dar es Salaam.
PIX3
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimpongeza Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayomiliki magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo, Dkt. Jim Yonaz kwa Kampuni yake kuzingatia matakwa ya Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016  kwa kujisajili upya na kupatiwa leseni.
PIX4
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na wahariri wa magazeti ya HabariLeo, DailyNews, SpotiLeo yanayomilikiwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) pamoja na uongozi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mara baada ya kukabidhiwa Lesini za usajili wa magzeti hayo leo Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO

Na. Neema Mathias na Paschal Dotto- MAELEZO.
Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) imeanza rasmi utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari kwa kutoa leseni kwa vyombo vya machapisho yakiwemo Magazeti na Majarida.  
Akizungumza katika makabidhiano ya leseni hizo Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema  utoaji wa leseni ni utekelezaji wa agizo rasmi lililotolewa Agosti 23, 2017 lililowataka wamiliki wote wa machapisho kujisajili upya na kupewa leseni kwa lengo la kuifanya tasnia ya Habari kuwa taaluma rasmi kama zingine.
“Leseni hizo zimeanza kutolewa rasmi Agosti 23 na zoezi hilo litaendelea hadi Oktoba 15, 2017 na baada ya hapo wale amabo watachapisha magazeti  na majarida bila kuzingatia Sheria hiyo watakuwa wametenda kosa la jinai”, alisema Dkt. Abasi.
Katika zoezi hilo Dkt. Abbasi alitoa leseni kwa vyombo vinne ambavyo ni Jarida la Nchi Yetu linalomilikiwa na Idara ya Habari MAELEZO, gazeti la Daily News, Habari Leo pamoja na Spoti Leo ambayo ni magazeti ya Serikali.
Dkt. Abbasi ametoa wito kwa vyombo vingine vya habari ambavyo bado havijaanza taratibu za upataji wa leseni visisubiri hadi dakika za mwisho za mchakato huo ili kuepuka msongamano na usumbufu usio wa lazima.
“Nitumie fursa hii kuwaalika ambao hawajapata leseni wafanye haraka, Tanzania Standard Newspaper (TSN) walitimiza masharti ndani ya siku tatu ndio maana leo wamepata leseni hizo, hakuna urasimu wala nia mbaya ya kufungia baadhi ya machapisho kama wengi wanavyodai bali ni katika kutekeleza matakwa ya Sheria”, alisisitiza Dkt. Abbasi.
Kwa upande wake Mhariri Mtendaji wa TSN Dkt. Jim Yonazi ameviasa Vyombo vingine vya Habari kutekeleza agizo hilo ili kupata uhuru mpana katika uwajibikaji pamoja na kuwa mfano wa kutii Sheria bila shuruti ili taaluma ya habari iendelee kuheshimika kwa jamii.
“Ukifanya kazi kihalali unakuwa na uhuru wa kufanya kazi vizuri, ubunifu unaongezeka na unafanya biashara bila wasiwasi”, alisisitiza Dkt.Yonazi.

Twaweza watoa ripoti ya Huduma ya Afya nchini


Baada ya kutoa ripoti ya utafiti wa hali ya usalama nchini mwezi uliopita, asasi ya kiraia ya Twaweza leo asubuhi inazindua matokeo ya utafiti mwingine unaoangazia changamoto za sekta ya afya.
Matokeo ya utafiti huo uliopewa jina la Sauti ya Wananchi, ulifanywa kati ya Mei 11 na 25 mwaka huu kwa kuhusisha sampuli ya watu 1,801 wa Tanzania Bara.
Miongoni mwa mambo yanayotazamiwa katika utafiti huo wa mfululizo wa 19 wa Sauti za Wananchi ni iwapo changamoto katika sekta ya afya zimepungua katika uongozi wa Serikali ya Rais John Magufuli, ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Twaweza inasema ripoti ya mwezi huu ambayo utafiti wake ulifanywa kwa njia ya simu inaweka bayana takwimu za mtazamo wa wananchi juu ya upatikanaji wa huduma za afya na ustawi wa jamii.
“Ni mambo gani wananchi hukutana nayo wakati wanaenda kupata huduma ya afya? Wanasubiri kwa muda gani kuzipata huduma hizo na je, hukumbana na uhaba wa dawa, watumishi au vifaa wanapoenda kutibiwa” inaeleza taarifa ya Twaweza kwa vyombo vya habari.

Maporomoko yaua watu 30 DR Congo


Takriban watu 28 wamefariki kufuatia maporomoko kusini mwa mji wa uchimbaji madini wa Kolwezi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kulingana na chombo cha habari cha Actualite.
Eneo hilo ni muhimu kwa madini ya Shaba .
Maporomoko ya hivi karibuni katika eneo la kaskazini-mashriki yaliwaua watu 200, kufuatia mvua kubwa iliosababisha mlima kuangukia kijiji kimoja cha uvuvi katika fukwe za Ziwa Albert.

Waziri Mbarawa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa

1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akifafanua jambo kwa Eng, Emmanuel Raphael Wansibho Mkuu wa Kitengo cha Ujenzi wa Viwanja vya Ndege huku Meneja Ujenzi wa Kampuni BAM inayojenga uwanja huo ya Eng. Ray Blumrick (kulia), akifuatilia.
2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akiangalia ramani ya namna muonekano wa miundombinu ya jengo la tatu la abiria litakavyokuwa mara baada ya ujenzi wake kukamilika (kulia), ni mtaalaam wa ramani toka kampuni ya BAM ya Uholanzi inayojenga uwanja huo akifafanua.
3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa (katikati), akipata maelezo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria unavyoendelea kutoka kwa Meneja Ujenzi wa Kampuni ya BAM inayojenga uwanja huo Eng. Ray Blumrick (kushoto), ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika baadae mwakani umefikia asilimia 64 ya ujenzi wake na utahudumia abiria milioni sita kwa mwaka.
4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa (katikati), akipata maelezo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria unavyoendelea kutoka kwa Meneja Ujenzi wa Kampuni ya BAM inayojenga uwanja huo Eng. Ray Blumrick (kushoto), ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika baadae mwakani umefikia asilimia 64 ya ujenzi wake na utahudumia abiria milioni sita kwa mwaka.


Na Neema Harrison, TUDARCO
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, ambapo sasa utakamilika Oktoba 2018.
Mhe. Prof. Mbarawa aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea maendeleo ya mradi huo ulianza 2013, na sasa kuridhishwa na hatua waliyofikia.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo, Prof. Waziri Prof. Mbarawa amesema kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 64, na hatua iliyobaki ni ujenzi wa wa mifumo ya ndani ya jengo.
“Sote tumekuwa mashahidi nimekuwa nuikitembelea mara kwa mara ujenzi wa jengo hili na ninaridhika kwa kasi ya ujenzi wake, ambapo sasa tumefikia kwenye hatua nzuri na vitu vilivyobaki sio vikubwa kama ilivyokuwa wakati wanaanza, hivyo ni matumaini yangu hadi Oktoba mwakani (2018) jengo lote litakuwa limekamilika na serikali kukabidhiwa,” amesema Mhe. Prof. Mbarawa.
Hatahivyo, Prof. Mbarawa amesema serikali inatarajia kupata watalii wengi na serikali itapata mapato kupitia kodi na tozo za abiria wanaosafiri kutumia kiwanja hiki, pia wapangaji wanaotoa huduma mbalimbali yakiwemo maduka na usafiri wa magari.
Amesema serikali itaendelea kutoa fedha za ujenzi wa jengo hilo linalosimamiwa na mkandarasi BAM International ya Uholanzi, ambapo pia likikamilika litatoa ajira kwa Watanzania wengi.