Monday 31 July 2017

ZILIZOMUBASHARA KATIKA KURASA ZA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOST 01 2017




Waziri Mkuu Majaliwa amezungumza na Watumishi wa Umma wa Manispaa ya Mbeya

PMO_6985
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafisi wa Manispaa ya Mbeya kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya Julai 31, 2017.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla na Kulia ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson
PMO_7002
Baadhi ya Watumishi wa Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafsi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya julai 31, 2017
PMO_7007
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Emmanuel Kyabo taarifa zinaoonyesha ubadhirifu uliofanywa na baadhi ya watendaji katika ujenzi wa soko la Mwanjelwa jijini Mbeya ili afanye uchunguzi wa kina  na kumshauri Waziri Mkuu hatua zinazostahili kuchukuliwa kwa wanatakaobainika kuwa wamefanya makokosa. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Ummy Mwalimu:Tunaendelea kuchukua hatua kuhakikisha watanzania wanapata huduma za matibabu bila vikwazo

tot2
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akikabidhi kadi kwa mmoja wa watoto waliojiunga na bima ya afya ya watoto (TotoAfyaCard) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya  (NHIF) Spika Mstaafu Mama Anne Makinda na kushoto ni Benarld Konga Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa (NHIF). 
tot1
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akikata utepe wakati alipozindua bima ya watoto (TotoAfyaCard) kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amezindua (TotoAfyaKadi) Bima ya Afya kwa watoto. katika uzinduzi uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam aki, Kwa mujibu wa Taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), kati ya Watanzania 52m waliopo sasa (2017) watoto ni 26.7m (sawa na 51%). Mtoto ni mtu mwenye umri wa chini ya miaka 18.
Ummy Mwalimu anasema (TotoAfyaKadi) ni njia sahihi ya kuelekea Bima ya Afya kwa Wote nchini. Mpango huu unatoa Uhakika wa Matibabu kwa mtoto kwa Tshs 50,400/= kugharamia matibabu yake kwa mwaka mzima. Tena sio kwa Vituo vya Serikali bali pia vya Binafsi. Lakini pia si kwa Halmashauri au Mkoa unayoishi bali nchi nzima.

Waziri Mkuu Majaliwa:Waharibifu vyanzo vya maji kukiona cha moto

Waziri Mkuu amewataka watendaji kuwachukua hatua watu wote watakaokutwa wakiendesha shughuli mbalimbali kama za kilimo, ujenzi wa makazi na uchungaji wa mifugo ndani ya vyanzo vya maji kwa kuwa zinasababisha ukame.
Waziri Mkuu amesema wananchi lazima wazingatie sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60 ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.
"Hatuwezi kuruhusu Taifa likaangamia kwa ajili ya watu wachache wanaoharibu mazingira kwa kuendesha shughuli za kibinadamu ndani ya vyanzo vya maji. Ni marufuku kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka katika vyanzo vya maji, atakayekutwa atachukuliwa hatua za kisheria", amesema Majaliwa.
Mbali na hayo Mh. Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya iliyotengewa sh. bilioni 2.72 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji.
Amesema mkakati huo unatekelezwa kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Al Shabaab waua wanajeshi 24

Wanajeshi 23 wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika (AMISOM) na askari mmoja wa Somalia wameuawa katika mtego wa kuvizia ulioandaliwa na wapiganaji wa Al Shabaab Kusini Magharibi mwa Somalia.
Mapigano yalizuka baada ya wanamgambo wa Al-Shabaab kuvamia vikosi vya AMISOM mapema Jumapili katika Wilaya ya Bulamareer ya Mkoa wa Lower Shabelle kilomita 140 Kusini Magharibi mwa mji wa Mogadishu.
"Tumechukua miili 23 ya askari waliouawa wa AMISOM na askari mmoja wa Somalia kutoka kwenye eneo ambalo Al Shabaab waliweka mtego wa kuvizia na kuvamia,” alisema Ali Nur, naibu gavana wa Lower Shabelle.

Bi Nkinga amewahimiza Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, kuzingatia sheria, kanuni

Pix 1
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akizungumza na washiriki wa mkutano wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) aweze kufungua mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017. 
Pix 2
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni Mwenyekiti wa mafunzo (kulia) Bw. Paschal Mahinyika akiwatambulisha washiriki wa mafunzo ya kudhibiti viashiria hatarishi kabla ya kukaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) aweze kufungua mafunzo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Pix 3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) akizungumza na Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Pix 4
Washiriki wa mafunzo ya udhibiti wa viashiria hatarishi kutoka vyuo vya Maendeleo ya Jamii vinavyosimsmiwa na Wizara wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati wa uendeshaji wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Pix 5
Watendaji kutoka Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kutoka kulia ni Mkurugenzi Utawala na Rasilimali Watu Utawala na Rasilimali watu Bibi Deodata Makani , katikati ni Mkurugenzi wa Ugavi na Manunuzi Bibi Martha chuma na kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani Bibi Lightness Mchome wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani) katika  ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017
Pix 6
Mkurugenzi Utawala na Rasilimali Watu Utawala na Rasilimali watu kwa kutoka Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Deodata Makani akitoa somo juu ya masuala ya kuzingatia kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Pix 7
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni mwenyekiti wa mafunzo Bw. Paschal Mahinyika(kulia) wakati wa mafunzo ya ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo vya maendeleo ya Jamii yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Pix 8
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiwasilisha mada kuhusu uaandaaji mzuri wa Bajeti kwa Wakuu wa Vyuo vua Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo ya ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo hao yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Pix 9
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati waliokaa)akiwa akiwa na wakufunzi wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini wakati wa mafunzo ya udhibiti wa viashiria hatarishi mahala pa kazi yaliyofanyikakatika Ukumbi wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo leo 31.7.2017.
  Picha na Erasto Ching’oro WAMJW
Na Erasto Ching’oro WAMJW
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Bibi. Sihaba Nkinga amewahimiza Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji wao wa kazi katika kuendesha vyuo wanavyovisimamia.
Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao  kuhusu udhibiti wa viashiria hatarishi vya utendaji na utawala ikiwa ni pamoja na  kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha katika utendaji wao wakazi wa kila siku ili kuepuka hoja za ukaguzi wa fedha.
Amesisitiza kuwa wakuu wa vyuo ni watumishi wa Umma na wanapaswa kuzingatia weledi mahala pa kazi kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zote za utumishi wa Umma katika kutimiza majukumu yao.
“Niwatake Wakuu wa Vyuo mliopo hapa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika kundesha vyuo mnavyoviongoza tuondokane na dosari katika suala la udhibiti wa Fedha katika matumizi” alisema Bibi Sihaba.
Aidha, Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga, amesema kuwa mara baada ya mafunzo haya maalum, Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini vitaweza kufuta hoja zote za ukaguzi mahala pa kazi kutokana na kufanya kazi kwa kufuata maadili, maarifa na miongozo na weledi unaotakiwa katika uendeshaji wa vyuo.

Vladimir Putin kukosesha ajira 755 wa ubalozi wa Marekani

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza wafanyakazi 755 wa ubalozi wa Marekani nchini Urusi kusitisha shughuli zao kufikia Septemba mosi mwaka huu.
Urusi imeidhinisha hatua hiyo kwa ghadhabu kufuatia vikwazo vipya vilivyopitishwa na bunge la Marekani dhidi yake, kwa tuhuma za kuingilia uchaguzi wa taifa hilo mwaka jana.
Marekani kwa upande wake, inasema imesikitishwa na uamuzi huo, na inapima athari na kutafakari namna ya kujibu hatua hiyo
Hatua hii ya Urusi imekuja baada ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi kuidhinishwa kwa wingi wa kura na mabunge yote ya congress nchini Marekani Jumanne, licha ya kwamba Ikulu ya White house ilipinga kura hiyo.
Rais huyo wa Urusi ameapa kuwa upo uwezekano wa kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Marekani.
Akizungumza kwenye televisheni ya taifa ya Urusi, rais Putin alisema kuwa alitarajia uhusiano baina ya Moscow na Washington ungebadilika na kuwa mzuri, lakini hilo haliwezekani kwa sasa
Akizungumza na wakati wa ziara yake nchini Estonia, makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence, alisema anatumai kwamba mienendo ya serikali ya Urusi itabadilika.

Vigogo wa TFF warudishwa Rumande tena


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amerejeshwa rumande kwa siku nyingine 11 baada ya kesi inayomkabili ya kugushi nyaraka na kutakatisha fedha kushindwa kuanza kusikilizwa kutokana na upepezi kutokamilika.
Malinzi anayetuhumiwa na mashtaka 28 tofauti pamoja na Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa na Mtunza Fedha, Nsiande Mwanga wanaokabiliwa na mashtaka matatu, wamepandishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu, Julai 31, asubuhi, chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Willbroad Mashauri, lakini kesi hiyo haikuweza kusikilizwa.
Mawakili wa upande wa Jamhuri ambao ndiyo walalamikaji, waliiambia Mahakama kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, hivyo washtakiwa hao kurejeshwa rumande hadi Julai 11.

Sunday 30 July 2017

ZILIZOSHIKA HATAMU KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 31 2017




Polisi yafanikiwa kutibua njama ya magaidi kuangusha ndege Australia

Polisi nchini Australia wametibua mipango ya kundi la magaidi ya kutaka kuangusha ndege, kulingana na Waziri Mkuu Malcolm Turnbull.
Majasusi wa Australia wanasema kuwa walipata habari kuwa watu hao walikuwa na njama ya kutumia mabomu ya kujitengenezea nyumbani.
Waziri Mkuu Malcolm Turnbull alisema kuwa mpango huo umevurugwa katika oparesheni kali iliyofanywa na kikosi maalumu cha kukabiliana na magaidi nchini.
Watu wanne wametiwa mbaroni kufuatia misako iliyofanywa kote katika mji wa Sydney na maafisa wa polisi waliojihami wakishirikiana na majasusi.
Mwanamke anayesema mumewe na mwanawe ni baadhi ya waliotiwa mbaroni amekanusha kuwa jamaa zake wanahusika na kundi lo lote la watu wa imani kali.
Usalama umeimarishwa katika uwanja wa ndege wa mji wa Sydney na kuenezwa katika maeneo mengine ya nchi.

Rais Trump aikosoa China kwa kutoichukulia hatua Korea Kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump amekosoa Uchina kwa kukosa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha kuwa Korea Kaskazini inasitisha mipango yake ya silaha za nukia.
Maoni yake yamechapishwa kwenye mtandao wa twitter siku moja baada ya Korea Kaskazini kufyatia kombora lake la pili linaloweza kusafiri kutoka bara moja hadi jingine mara ya pili chini ya muda wa mwezi mmoja.
Korea Kaskazini baadaye ilidai kuwa jaribio hilo linaonyesha kuwa silaha zake zinaweza kuishambulia Marekani.

Uwanja wa Ndege Songwe wanusurika kuteketea kwa moto

Taharuki imewakumba wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (Sia) mkoani Mbeya na wananchi wanaofanya shughuli kando mwa barabara kuu ya Tanzania -Zambia baada ya moto kuwaka ndani ya eneo la uwanja huo.
Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika ulitokea jana mchana na kaimu meneja wa uwanja huo, Jordan Mchami alisema iliwachukua takriban nusu saa kuuzima.
Alisema moto huo ulianzia katika eneo la barabara kuu ya Tanzania - Zambia umbali wa mita 600 kutoka maeneo yalipo majengo na eneo la kurukia ndege.
“Tumefanikiwa kuuzima, hakuna madhara yoyote katika eneo letu na si sahihi kusema uwanja umeungua. Ifahamike kwamba uwanja huu una eneo kubwa ambalo ni kama vile pori tu. Moto umetokea barabara kuu ya Tanzania -Zambia umbali wa mita 600 hivi hadi tulipo sisi,” alisema baada ya kuenea taarifa katika mitandao ya kijamii na maeneo ya jirani kwamba uwanja huo umewaka moto.
Alipoulizwa kuhusu cha moto huo Mchami alisema ulionekana kuanzia barabarani na walipofuatilia kwa kuwauliza kina mama wanaofanya biashara ndogondogo kando mwa barabara hiyo waliambiwa kuwa waliona lori lililokuwa limeegeshwa eneo ulikoanzia hivyo wanahisi huenda mtu au watu waliokuwa katika gari hilo walirusha kipande cha sigara na kusababisha nyasi kuwaka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohamed Mpinga alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, simu yake ilipokewa na msaidizi wake aliyesema kamanda yupo kwenye msafara wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Tetemeko dogo la ardhi latokea Karagwe

  Image result for Kagera
Tetemeko lililodumu kwa takriban sekunde tano limetokea leo, Julai 30 saa nne asubuhi katika  Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kayanga wilayani Karagwe, lakini hakuna madhara yaliyoripotiwa  kutokea.
Ofisa wa Wakala wa  Jiolojia Tanzania, Gabriel Mbogani amesema ili kupata uhakika wa tetemeko hilo ni lazima kukusanya taarifa kwenye mitambo.
Amesema wananchi mkoani Kagera kwa sasa wapo makini  baada ya kupatiwa semina kutokana na tetemeko la Septemba mwaka jana ambalo lilisababisha madhara makubwa.
“Wananchi wa Bukoba baada ya semina tulizotoa  na kuwaonyesha ramani ya matukio ya tetemeko  wamekuwa na uelewa, hivyo hata likitokea dogo  kiasi gani lazima watoe taarifa,” alisema Mbogani.
Hata hivyo, amewataka wananchi kuendelea  kuchukua tahadhari kwa kuwa haijulikani ni muda  gani tetemeko kubwa linaweza kutokea kwa kuwa uzoefu ni kuwa huanza dogo na baadaye kuwa kubwa.

Ziara ya IGP Simon Sirro mkoani Singida kujua changamoto za Askari

1
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi wa Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Singida, wakati alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
2
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo na kuwataka wafanyekazi kwa kutenda haki na kusimamia misingi ya sheria na taratibu, IGP Sirro yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
3
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na kikosi cha Polisi wanawake baada ya kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili mkoani Singida, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.

Na Jeshi la Polisi Nchini
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, amemaliza ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na mkoa wa Singida, huku akiacha morali kwa watendaji wa Jeshi hilo hatua ambayo italiwezesha ieshi hilo kufanyakazi zake kwa weledi katika kukabiliana na matishio ya uhalifu na wahalifu.
IGP Sirro, amefanya ziara hiyo ikiwa ni mkakati wake aliojiwekea tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi hilo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa ili kujua namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi.
Katika mazungumzo yake IGP Sirro, amewataka askari na maofisa kutimiza wajibu wao kwa kutenda haki na bila uwoga wala kumuonea mtu muhali jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu katika jamii.

Daraja refu kuliko yote Duniani

Daraja lililotundikwa lenye mita 500 linalokisiwa kuwa refu zaidi duniani limefunguliwa katika mji wa Zermatt nchini Uswizi, Daraja hilo lenye urefu wa mita 494 kwa jina Europabrucke limetundikwa mita 85 juu .

Bodi za utalii ya Zermatt inasema kuwa ndio daraja refu zaidi duniani ,ijapokuwa daraja la mita 405 mjini Reutte Austria limetundikwa mita 110 juu kutoka ardhini, Daraja hilo linachukua mahala pa daraja jingine ambalo lilikuwa limeharibiwa na mwamba.

Daraja hilo jipya ambalo ambalo lina uzito wa tani nane limewekwa kifaa cha ambacho linalizuia kuyumbayumba ,kulingana na bodi ya watalii ya Zermatt, Daraja hilo lipo kati ya Zermatt na Grachen kusini mwa Switzerland.

Shabiki avamia kiwanjani na kumtolea maneno makali Wenger

Pamoja na Arsenal kuitwanga Benfica kwa mabao 5-2 katika mechi ya kirafiki, bado kuna mashabiki hawamtaki katika klabu hiyo.
Shabiki mmoja alifanikiwa kupenya uwanjani wakati wa mchezo huo na kusema maneno makali dhidi yake akionyesha kumpinga kwake.
Hata hivyo shabiki huyo aliondolewa uwanjani na askari baada ya kuwa ameropoka maneno hayo makali dhidi ya Wenger.
Miezi michache iliyopita, Wenger aliongeza mkataba wa miaka miwili kuifundisha Arsenal licha ya kuwa mashabiki wakionyesha wazi hawamtaki au wamemchoka.

Saturday 29 July 2017

ZILIZOCHUKUA NAFASI KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 30 2017




Method Mwanjale nahodha mpya wa Simba

Image result for Method Mwanjali
SIMBA SPORTS CLUB
DAR ES SALAAM
29-7-2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Benchi la ufundi la klabu ya Simba,chini ya kocha wake mkuu Joseph Omog limefanya marekebisho kwenye eneo la unahodha wa timu.
Katika marekebisho hayo yaliyoridhiwa na uongozi wa klabu,beki wa kimataifa Mzimbabwe Method Mwanjale ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya Simba,akichukua nafasi ya Jonas Mkude atakaendelea kuwa mchezaji mwandamizi kwenye kikosi hicho,ambacho kwa sasa kipo nchini Afrika kusini kujiandaa na msimu mpya unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.
Kwenye mabadiliko hayo ya kawaida, benchi la ufundi pia limewateua Mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania na klabu ya Simba kwa msimu huu,Mohammed Hussein(Tshabalala)na John Raphael Boko kuwa manahodha wasaidizi wa timu hiyo.
 
Klabu inamshukuru sana Nahodha wake kwenye msimu uliopita na mchezaji wake mwandamizi,Jonas Mkude kwa kazi nzuri alioifanya muda wote alipokuwa Nahodha wa Timu.
Kwa sasa kikosi chetu kinaendelea na mazoezi na kila kitu kinakwenda vema huko kambini Eden Vale Johannesburg nchini Afrika kusini.
IMETOLEWA NA..
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI WA SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA

RC Makonda akabidhiwa ripoti ya wezi na Magari na vifaa Dar, 73 mbaroni

 Image result for paul makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekabidhiwa ripoti ya wezi wa magari pamoja na vifaa vya magari na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Lucas Mondya ikiwa ni miezi kadhaa toka mkuu huyo aliagize jeshi hilo baada ya matukio ya namna hiyo kushamiri ndani ya mkoa huo.
Akiongea na waandishi wa habari Jumamosi hii wakiwa ndani ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Lucas Mondya alisema katika opesheni hiyo kali jumla ya wahumiwa 73 wamekamatwa na kupekuliwa na kukutwa na vifaa mbalimbali vya magari ikiwemo side mirrors, taa za magari, power windows, radio, injector pump, starter na seat cover.

“Tarehe 19 mwezi wa saba mweshimiwa RC Makonda ulitoa maagizo kwa jeshi la polisi kwamba unatupatia siku saba kuhakikisha tunasambaratisha mtandao wa wezi wa vifaa vya magari pamoja na magari baada na sisi tumelitekeleza hilo tayari kuna watu 73 tunawashikilia, Kinondani wamekamatwa watuhumiwa 29, Ilala wamekamatwa wahutumiwa 33 na mkoa wa kipolisi Temeke wamekamatwa wahumiwa 11,”

Alisema jumla ya power windows zilizokamatwa ni 40, Raidio 12, Taa za magari aina mbalimbali 105, side mirrors 92, vitasa vya magari 109, wiper switch 7, Tampa 4, left pump3, Air cleaner 1, Booster 3, show grill 6, machine za kupandisha vino 1 na tyre used 2.

Pia alisema katika mahojiano na wahutumiwa wote waliokamatwa wapo walioshindwa kuvitolea maelezo vifaa hivyo ni namna gani na wapi wamevipata.

Wahutumiwa wote bado wanaendelea na mahojiano na uchunguzi bado unaendelea ili kubaini mtandao wote unaojihusisha na wizi huo wa vifaa vya magari ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahamani kwa hatua zaidi.