Sunday 24 December 2017

Rais Mnangagwa amteua mkuu wa jeshi aliyeongoza mapinduzi ya kumng’oa Mugabe

Jenerali wa Jeshi la Wananchi Zimbabwe ambaye aliongoza mapinduzi yaliyopelekea Robert Mugabe kung’olewa madarakani, ameteuliwa kuwa naibu kiongozi wa chama tawala cha ZANU-PF.
Constantino Chiwenga ameteuliwa na Rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa  ambapo hivi karibuni alistaafu kama mkuu wa jeshi, na kuenea kwa tetesi kuwa atapewa wadhifa wa kwenye serikali ya mpya ya Rais Mnangagwa.
Uteuzi huo unaonekana kama hatua ya kuelekea kutajwa kuwa makamu wa Rais baada ya makamu wa Makamu wa sasa wa Zanu PF, Kembo Mohadi ambaye alikuwa waziri usalama chini ya Robert Mugabe kuonekana kuelemewa.

Viongozi wa dini watoa tahadhari kwa ukiukwaji wa haki za binadamu

Wakati Watanzania wakijiandaa kusherehekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, viongozi wa dini wameeleza mambo manne yanayopaswa kuchukuliwa tahadhari na jamii mwaka 2018.
Wameyataja mambo hayo kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu, uhalifu, ubaguzi; na uvunjifu wa amani wakibainisha kuwa yalichukua nafasi kubwa mwaka huu.
Viongozi hao wametaka yadhibitiwe ili yasijitokeze tena mwakani. Kwa waumini wa Kikristo, huenda huo ukawa ndio ujumbe utakaotolewa kwa waumini katika ibada hizo za sikukuu za mwisho mwa mwaka.
Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Raymond Saba alisema matukio ya uvunjifu wa amani mwaka huu yalikuwa tishio, hivyo ni muda sahihi wa Watanzania kujifunza namna ya kulinda tunu ya Taifa.
“Amani ndiyo kila kitu, amani ikitoweka hakuna malengo yoyote yatakayotekelezwa, kwa hiyo jamii ijitafakari katika kipindi hiki kuhakikisha amani inadumu, matukio ya wizi, utapeli yatoweke kabisa katika jamii,” alisema.
Rais wa Baraza hilo, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa alisema jamii inatakiwa kujenga utamaduni wa kulinda amani ya nchi, kutenda haki na kuhimiza upendo.
“Tunaelekea kwenye Krismasi tujali haki, tujali amani ya nchi yetu na upendo. Tumwombe Mungu atuongoze zaidi katika kipindi hiki, atusaidie katika kilimo chetu kwa sababu mvua haijaanza kunyesha,” alisema.
Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Rajab Katimba aliwataka Watanzania kujitathmini na kutenda haki ili mwaka ujao uwe wa amani na kila mwananchi ajisikie huru kuishi katika nchi yake.
Alibainisha kuwa, mwaka huu umekuwa na matukio mengi ambayo yanaonyesha ukiukwaji wa haki za binadamu.
Aliyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni mauaji, baadhi ya watu kufungwa bila hatia na wengine kutoweka katika mazingira ya kutatanisha. “Tumeshuhudia matukio ya kuokotwa kwa miili ya watu kwenye fukwe za Bahari ya Hindi na watu kupotea. Hivi ninavyoongea kuna mwandishi mmoja (Azory Gwanda) naye amepotea. Tunataka viongozi wahakikishe haki inatendeka katika Taifa hili,” alisisitiza.

Kiongozi huyo ametaka Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa weledi ili kulinda haki za Watanzania na hasa wanyonge wasio na sauti, akisisitiza haki ndiyo msingi wa maendeleo ya Taifa lolote duniani.

“Bila haki Taifa linakufa. Uwanja wa siasa nao uwe huru ili vyama vya upinzani navyo vipate haki ya kufanya siasa kwa mujibu wa sheria na Katiba,” alisema.
Kwa mtazamo wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Jacob Chimeledya alisema sasa ni wakati wa kila Mtanzania kutambua thamani ya mtoto na kumlinda ili akue katika njia iliyo bora na baadaye kuwa msaada kwa Taifa.
Dk Chimeledya alimtaka kila mwananchi kuangalia namna atakavyogusa maisha ya mtoto kwa kila anachokifanya ili kumjengea mustakabali mwema kimaadili, kielimu na kimaendeleo.
“Maisha ya mtoto ni tunu kwa Taifa, hivyo akitunzwa ana faida kubwa baadaye. Mungu amepandikiza karama na vipawa kwa kila mtoto, kama hakutunzwa vizuri basi anapoteza karama na vipawa hivyo,” alisema.

Aliwataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wa kutunza watoto wao katika misingi ya haki, imani na maadili ya Taifa.
Akizungumzia mwaka huu, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema umekuwa na changamoto nyingi kwa sababu wananchi hawakuzoea kuona yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, ikiwamo matumizi mazuri ya rasilimali.
Alisema ni wakati wa wananchi kujipanga kuijenga nchi iwe yenye kujitegemea, isiyoyumbishwa na mataifa mengine na kulinda rasilimali za nchi kwa manufaa yao wenyewe, “Tujenge nchi yetu kwa pamoja maana nchi hii ni yetu sote. Tujenge umoja wa kitaifa, wanadini na wanasiasa tujenge utamaduni wa kuvumiliana,” alisema.
Kuhusu haki za binadamu alisema, “Watanzania hawapati maelezo ya kutosha kwa mambo kadhaa kama vile miili ya watu inayookotwa fukweni na wengine kutoweka. Hatutarajii kuendelea na hali hiyo mwaka ujao.”

Saturday 23 December 2017

ZILIZOTUFIKIA KATIKA MEZA YA FOFAM-MEDIA KUPITIA KURASA ZA MBELE MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 24 2017




Nabii wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering, Shepherd amnunulia Gari la Thamani Mwanae wa Miaka 4

Nabii wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering, Shepherd Bushiri, amemfanyia sapraizi mwanayae wa kike, Israella Bushiri mwenye umri wa miaka 4, baada ya kumnunulia gari aina ya Maserati Levante lenye thamani ya Sh milioni 926, kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa.
Bushiri alitumia ukurasa wake wa Facebook ku-share picha na kuandika maneno ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya pekee aliyomjalia kumpata binti yake huyo.
Nabii huyo ambaye mara nyingi anafanya kazi zake za uinjilishaji nchini Afrika Kusini aliandika: “Ninaona baraka zako Mungu kwa zawadi hii ya pekee uliyonipa katika maisha yangu. Ninasherehekea kuzaliwa kwa Mungu wangu na mwokozi wangu Yesu Kristo, na kuzaliwa kwa binti yangu wa kwanza, Israella Bushiri.

“Ninaona ni kama jana tu wakati mtoto huyu alipozaliwa na kumbeba mikononi mwangu, lakini leo naweza kumweka mabegani mwangu na akatulia mwenyewe pasipo kushikiliwa, nitamsaidia kwa kila ninaloweza akue na kufikia malengo flani,” aliandika Bushiri.


Mtoto Israella Bushiri.

Vita ya kufunga mwaka kati ya Real Madrid na Barcelona


Leo ni vita ya kufunga mwaka kwenye ligi kuu soka ya Hispania maarufu kama La Liga, nyota wawili kutoka timu mahasamu Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa Barcelona watakuwa wanawania kufunga mwaka wakiwa na mabao mengi zaidi.
Kwasasa nyota hao wana mabao 53 kila mmoja ambayo wameyafunga ndani ya mwaka huu wa 2017 katika mashindano yote. Wanaingia kusaka mabao mengine ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kumaliza mwaka wakiwa na rekodi ya kuwa na mabao mengi zaidi.
Kwa upande wa viwango timu hizo zote zinafanya vizuri pamoja na Real Madrid kuanza vibaya msimu, tayari imeshaanza kurejea kwenye ubora wake haswa ikipewa nguvu na ubingwa wa klabu bingwa ya dunia ilioupata wikiendi iliyopita.
Kuelekea mchezo wa leo utakaopigwa saa 9:00 alasiri, Barcelona ndio vinara wa ligi wakiwa na alama 42 huku wakiwa wameruhusu nyavu zao kuguswa mara saba tu katika mechi 16 huku Real wakiruhusu mabao 11 katika mechi 15 na wakishika nafasi nne wakiwa na alama 31.

Askari mwingine JWTZ aliyeshambuliwa DRC afariki Dunia

ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliyekuwa katika Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) amefariki dunia nchini Uganda wakati akipatiwa matibabu.
Askari huyo ni miongoni mwa askari 44 wa Tanzania waliojeruhiwa katika shambulio lililofanywa Desemba 7 mwaka huu na waasi wa The Allied Democratic Forces (ADF) katika kambi ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa (MONUSCO), na kusababisha vifo vya wanajeshi 14 wa Tanzania na watano wa DRC.
Msemaji wa Katibu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, alitangaza taarifa hiyo ya kusikitisha katika Makao Makuu wa UN, Mjini New York jana Desemba 22, 2017 usiku.
Katika taarifa iliyotolewa na MONUSCO leo, imeeleza kwamba mwanajeshi wa 15 wa Tanzania amefariki dunia akipatiwa matibabu mjini Kampala.

Watu 22 wahofiwa kufa maji na 115 kuokolewa Ziwa Tanganyika


Watu 22 wanahofiwa kufa maji katika Ziwa Tanganyika katika ajali ya boti iliyotokea iliotokea leo alfajiri.
Imeelezwa miili ya watu wanne imeopolewa na imetambuliwa na ndugu zao huku watu wengine 115 wameokolewa wakiwa hai baada ya boti kugonga mtumbwi.
Ofisa wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) Mkoa wa Kigoma, Amaniel Sekulu amesema ajali hiyo imetokea katika kitongoji cha Lubengela kijijini Msihezi, Kata ya Sunuka wilayani Uvinza.
Amesema mtumbwi uitwao Mv Pasaka uligongwa ubavuni na boti ya Atakalo Mola na kupasuka, hivyo kuzama ziwani.
Sekulu amesema mtumbwi ulikuwa umebeba abiria 137 waliokuwa wanakwenda kwenye mkutano wa injili katika Kijiji cha Sunuka.
Amesema  boti ilikuwa ikitokea Kigoma kwenda Kalya ikiwa imebeba abiria 65.
Sekulu amesema  boti na mitumbwi inayobeba abiria hairuhusu kufanya safari usiku.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Sweetbert Njewike akizungumzia ajali hiyo amesema  wanaendelea kuwatafuta watu ambao hawajaonekana waliokuwa wakisafiri na vyombo hivyo.
Amesema  shughuli za uokoaji zinafanywa kwa pamoja na vikosi vya Polisi, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kulikuwa na dosari zilizosababisha ajali hiyo.
Amezitaja dosari hizo kuwa ni ukosefu wa vifaa vya uokoaji, vifaa vya kuzima moto na boti kufanya safari usiku.
Diwani wa Sunuka, Athumani Chuma amesema ajali hiyo imeacha simanzi kutokana na mazingira iliyotokea.


Friday 22 December 2017

ZILIZOANGAZA LEO KUPITIA KURASA ZA MBELE MAGAZETI YA JUMAMOSI DESEMBA 23 2017




CUF upande wa Maalim Seif waibwaga kambi ya Prof Lipumba Mahakamani

 Image result for Maalim Seif Sharif Hamad
Mahakama ya Rufaa Tanzania imekubali maombi ya Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF) inayomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho,Maalim Seif Sharif Hamad katika shauri Namba 43/01/2017 kuhusu kumkataa Jaji Kihiyo kusikiliza shauri la msingi.
Taarifa hiyo ya maamuzi ya mahakama ya Rufaa, imetolewa mapema leo Disemba 22, 2017 kwa vyombo vya habari na Naibu Mkurugenzi wa Habari CUF, Mbarala Maharagande.
“Mahakama ya Rufaa imeipa ushindi Maombi ya Bodi ya Wadhamini ya CUF chini ya Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad katika shauri Namba 43/01/2017 (From Civil Application No.23/2017) kuhusu kumkataa Jaji Kihiyo kusikiliza shauri la msingi tajwa hapo juu.
“Shauri hili ndilo linalohoji uhalali na mamlaka ya Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi kumrejesha Lipumba katika nafasi ya Uongozi ndani ya CUF baada ya kujiuzulu na kukubaliwa kujiuzulu kwake na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CUF uliofanyika katika ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza Tarehe 21 August, 2017,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Jaji wa Mahakama ya Rufaa , Jaji Musa Kipenka amekubaliana na hoja za Mawakili Wasomi wa CUF Halfani Daimu, Juma Nassoro na Hashimu Mziray walizozitoa Mbele ya Mahakama hiyo.

Wanachama wa UN watupilia mbali vitisho vya Trump

 Image result for trump
Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimekaidi vitisho vya Serikali ya Marekani na kupiga kura ya ndiyo kuidhinisha azimio linalotupilia mbali tangazo la Rais Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya Israel.
Nchi wanachama 128 zilipiga kura ya ndiyo dhidi ya kura tisa zilizopinga, huku nchi 35 zikijiondoa kupiga kura.
Baada ya kura, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley aliyashukuru mataifa 65 yaliyopinga azimio hilo, yaliyojizuia kupiga kura au hayakuwapo wakati wa kupiga kura.
Marekani, Togo, Honduras na Guatemala ni mataifa ambayo yalipiga kura kupinga azimio hilo.
Mataifa ya Canada, Mexico, Rwanda, Uganda, Poland, Jamhuri ya Czech na Romania hayakupiga kura.
Kabla ya kura, Marekani ilitishia kuzuia misaada kwa mataifa yatakayopiga kura kuunga mkono azimio hilo.

Kim Jong Un amepiga marufuku kuimba, kunywa siku ya Krismasi

 Image result for Kim Jong
Rais Kim Jong Un wa Korea ya Kaskazini amepiga marufuku kuimba, kunywa vileo na kufanya mikusanyiko ya aina yote nchini humo wakati wa Krismasi mwaka huu.
Kwa mujibu wa shirika la ujasusi la Korea ya Kusini (NIS), hatua hiyo inakazia amri ya kupiga marufuku sherehe za Krismasi ya mwaka jana (2016) ikilenga kuzuia nguvu za upinzani nchini humo hususan sasa ambapo vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi hiyo vinaonyesha kuiumiza nchi hiyo.
“Korea ya Kaskazini imeanzisha mfumo wa jumuia za chama tawala kuripoti matatizo ya kiuchumi ya watu wanayokumbana nayo kila siku, na imepiga marufuku mikusanyiko inayohusiana na unywaji wa vileo, uimbaji na burudani nyingine, na imeimarisha udhibiti wa habari kutoka nje,” lilisema NIS.
Fursa za kuitumia sikukuu hiyo kueneza uelewano na furaha zinazidi kufifia katika taifa hilo linalodaiwa kutawaliwa kidikteta na ambalo limepiga marufuku dini zote isipokuwa maadhimisho ya familia iliyoasisi taifa hilo la kikomunisti. Mwaka jana, Kim aliwazuia Wakristo nchini humo kuadhimisha Krismasi na badala yake akawataka kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa bibi yake, Kim Jong-suk, aliyezaliwa siku ya mkesha wa Krismasi mwaka 1919.

Dudu Baya ameitaka Basata kuwachukulia hatua Wasanii waloenda kinyume na maadili

 Image result for dudu baya
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Dudu Baya ameitaka serikali kupitia Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kuwachukulia hatua wasanii wote ambao wameenda kinyume na maadali kwa mwaka 2017 ili mambo hayo yasije kujirudia mwaka 2018.
Dudu Baya akizungumza na E-Newz ya EATV amesema baadhi ya wasanii kwa mwaka huu wameitumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kuweka picha zisizo na maadili kitu ambacho kimefanya jambo hilo kujadiliwa kuliko muziki wao.
“Watu kama kina Nuh Mziwanda wanapiga picha za uchi uko na Shilole kipindi kile uko bafuni unaoga kuna aja gani kuonyesha mashabiki wako, kuna mtu gani asiyeoga hapa duniani. Ukija kama suala la mdogo wangu Young Dee namkubali sana lakini alipiga picha na Amber Lulu za kumshika makalio, huo ni ujinga,” amesema Dudu Baya.
Dudu Baya ameendelea kwa kusema wasanii watumie mitandao kwa manufaa ya kibiashara na endapo wakishindwa basi sheria ichukue mkondo wake.
“Nabahatika nakutana na Amber Lulu au Gigy Money namwambia ebu kaza kwenye kipaji chako ebu achana na upuuzi, sasa hivi mabinti wanaotaka kuingia kwenye movie au muziki wasije kwa njia walizopitia Amber Lulu na Gigy,” amesema.


Umoja wa mataifa wapinga maamuzi ya Trump

Mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa umepiga Kura ya kutoyatambua maamuzi ya Marekani ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Makubaliano hayo ya mkutano wa umoja wa mataifa yamefikiwa pamoja na vitisho vya Rais wa Marekani Donald Trump aliyetishia kuzikatia msaada wa kifedha nchi zote zitakazopinga msimamo wake.
Mataifa mia moja ishirini wameyapigiakura maazimio, baadhi ya mataifa hayo yakiwamo washirika wa karibu wa marekani yaani Japan, Uingereza na Ujerumani.
Canada na Mexico ni moja ya mataifa thelathini na tano ambayo hayakuhudhuria mkutano huo. Wapalestina wameiita hatua ya Umoja wa mataifa kuwa ni ushindi wa Palestina ingawa Israel imeyakataa matokeo.

Klabu ya Ajax Amsterdam yatimua benchi la Ufundi


Klabu ya soka ya Ajax Amsterdam ya Uholanzi imelitimua benchi lake lote la ufundi likiongozwa na kocha mkuu Marcel Keizer baada ya kufanya vibaya kwenye ligi ya nyumbani na ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ukiacha kocha mkuu Marcel Keizer, wengine waliofutwa kazi ni wasaidizi wake Dennis Bergkamp pamoja na Hennie Spijkerman.
Meneja mkuu wa timu hiyo ambaye ni golikipa wa zamani wa Manchester United Edwin Van De Sar amefutwa kazi pia, huku mkurugenzi wa ufundi Marc Overmars naye akitupiwa vilago.
Ajax inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 38 nyuma ya PSV yenye alama 43. Mlinzi wa zamani wa kimataifa wa uholanzi Michael Reiziger, na Winston Bogarde wamekabidhiwa timu kwa muda.
Makocha wanaotajwa kuchukua nafasi katika timu hiyo ni Ronald Koeman na Frank De Boer ambao wanatajwa huenda wakapewa timu kwa
mkataba mrefu.

Thursday 21 December 2017

ZILIZOPEWA NAFASI KUBWA KATIKA KURASA ZA MBELE MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 22 2017




Lukuvi amaliza mgogoro wa Ardhi Vingunguti

  Image result for lukuvi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameumaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya wakazi wa Mtaa wa Mtambani Vingunguti na mwekezaji kampuni ya PPM.
Waziri Lukuvi amesema Serikali haitambui uwekezaji uliokuwa ufanyike na kwamba, mwekezaji hakufuata utaratibu hivyo kusababisha mgogoro huo.
Eneo hilo la eka 228 lina jumla ya nyumba 4,000 na wakazi 70,000.
"Hatuzuii mtu kuuza mali yake, tunachosimamia haki itendeke na utaratibu ufuatwe lakini katika mchakato huu mambo yamekwenda ndivyo sivyo," amesema Lukuvi leo Alhamisi Desemba 21,2017.
Amesema, "Kuanzia leo nasema haya maeneo ni mali ya wananchi kama anataka kununua aanze upya kufuata utaratibu uliowekwa, haiwezekani mtu anakuja kuwanunua watu 70,000 kienyeji."
Inadaiwa mwekezaji huyo alitaka kununua eneo hilo kwa ajili ya kujenga bandari kavu.
Kwa mujibu wa wananchi wa eneo hilo tangu mwaka 2012 mwekezaji huyo aliwazuia kufanya shughuli zozote za uendelezaji kwa kile alichodai ameshafanya tathmini.
Hata hivyo, hadi sasa hakuna kinachoendelea na malipo hayajafanyika.
Alipoulizwa kinachoendelea katika uwekezaji huo, meneja mradi wa PPM, Deogratius Chacha amesema wapo katika hatua za mwisho na malipo yangefanyika ndani ya siku 90.
Wakazi wa eneo hilo wamemwambia waziri Lukuvi kuwa mwekezaji amechukua pia leseni zao za makazi na picha.
Kauli hiyo imemfanya waziri Lukuvi kutoa agizo kwa meneja huyo kuwarudishia nyaraka wakazi wote hadi ifikapo kesho saa tano asubuhi.

Neema ya Maji kwa wakazi wa Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma

Vijijji vya Kwamtoro, Sanzawa na Mangasta vilivyopo Dodoma Wilaya ya Chemba wamepata neema ya Maji safi na salama baada ya mfadhili kutoka Abu Dhabi Bwana Jamal Mohamed kutoa msaada wa visima 4 vya Maji safi na salama kwa wananchi hao.

Bwana Jamal Mohamed alipata ujumbe kuwa Maeneo hayo kunashida ya Maji safi ndipo akaamua kujitolea kuwasaidia wananchi hao kwa kuwachimbia visima 4 vyenye urefu wa mita 150 kwenda chini vyenye thamani ya milion 35 kwa kila kimoja.
Mpaka sasa visima 3 vishakamilika na kimoja ndio kimeanza kuchibwa, Jumla ya msaada huo utagharimu milion 140 za kitanzanai.
Wananchi wameelezea furaha yao juu ya msaada hou nakudai kuwa shida ya maji ilikuwa nitatizo kubwa sana katika maeneo hayo ili kupata maji ili kuwa nilazima utembee kilometa 10 mpaka 15.
Kwa mujibu wa waataalamu wa kuchimba visima wanasema visima hivyo kila kimoja kinatoa lita 15,000 kwa saa na kwa mujibu wa wakazi wa maeneo hayo kutakuwa hakuna tena shida ya maji safi na salama.
Jumla ya visima vyote vitatoa maji lita laki 2 mpaka 3 kwa siku ambazo zitaweza kuhudumia watu zaidi ya 2000 mpya 3000 kwa siku.




Urafiki wawashukia wapangaji walioshindwa kulipa madeni yao


. Uongozi wa Kiwanda cha Urafiki umetangaza kiama kwa wapangaji zaidi ya 160 ukiwataka kulipa kodi la sivyo watawaondoa pasipo kuangalia hadhi ya mtu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Desemba 21,2017 naibu meneja wa kiwanda hicho, Shadrack Nsekela amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya wapangaji kushindwa kulipa madeni wanayodaiwa tangu mwaka 2015.
"Hakuna msalie mtume katika hili, tutawatoa wote bila kujali nani ni nani. Tumeanza kuwapa notisi tangu mwaka 2015 lakini hawalipi sasa tunawatoa," amesema Nsekela.
Amesema wapangaji waliopo katika kota za Urafiki jijini Dar es Salaam wanadaiwa kati ya Sh600 milioni na Sh1 bilioni.
Nsekela amesema wameanza kuwatoa wapangaji wa ofisi, huku wale wa makazi wakitakiwa kujiandaa wakati wowote nao watatolewa.
Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya udalali ya Yono, Scholastika Kevela amesema baada ya siku 14 watapiga mnada mali walizokamata ili kufidia deni.

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Heche

 Related image
Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini ameitaka serikali kuwa mfano mzuri kwa kutoa takwimu za ukweli na kwamba takwimu nyingi si za kweli na inapaswa kushughulikiwa.
Mbunge John Heche (CHADEMA) ametoa maoni yake hayo kupitia ukurasa wake wa twitter ikiwa ni siku moja baada ya Rais Magufuli kutoa onyo kwa watu wasiohusika kutoa takwimu kufanya kitendo hicho na kuagiza mamlaka husika kuwashughulikia watu hao.
"Serikali inatakiwa kuwa mfano mzuri kwa kutosema takwimu za uongo, lakini tukianzia kwenye takwimu zinazotolewa kuhusu ukuaji wa uchumi, idadi ya viwanda na mengine mengi nafikiri inatakiwa serikali yenyewe ndio ianze kushughulikiwa kwanza," Heche ameandika.
 Jana Rais Magufuli alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu Dodoma aliwataka wananchi kuwa makini na masuala ya takwimu na kuwapuuza watu ambao wanasema vyuma vimekaza ili hali watu wa Takwimu wanasema vyuma vimefunguka na kwamba mtu akikosea kutoa takwimu ameichafua nchi.


Rais wa orea Kaskazini, Kim Jong Un amepiga marufuku sikukuu ya Krismasi

Pyongyaung. Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amepiga marufuku mikusanyiko inayoashiria kusherehekea sikukuu ya Krismasi kama vile inayohusu unywaji na uimbaji.
Ametaka wananchi kutosherehekea sikukuu hiyo na wanaopenda kufanya hivyo, waitumie Desemba 24 kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa bibi yake aliyezaliwa siku kama hiyo mwaka 1919.
Kiongozi huyo ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinadhibiti mikusanyiko yote ambayo inaendana na maadhimisho ya Krismasi.
“Ni marufuku watu kukusanyika na kufanya mambo kama ya unywaji au kuimba katika sikukuu ya Krismasi,” chanzo kimoja cha habari kimenukuu taarifa ya kiongozi huyo.
Kim Jong Un amekuwa akichukua hatua kuzua kuenea kwa utamaduni kwa kigeni na amedhibiti vyombo vya habari kutotangaza taarifa zozote zinazoienzi sikukuu hiyo kama hatua ya kupiga marufuku Krismasi.