Friday 26 August 2016

Jamaa ashtakiwa kwa kumpa mbwa wake jina la Rais

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.

Mwanamume kutoka Nigeria ametiwa nguvuni baada ya kumpa  mbwa wake jina la Muhammadu Buhari
-Kabla ya kutiwa nguvuni  aliandika jina la Rais kwa pande zote za mbwa kutokana na upendo wa kazi ya Rais
Joe fortemeso Chinakwe alitiwa nguvuni baada ya kuonekana akitembea na mbwa wake aliyemwitwa Buhari.
Askari walidai kumtia nguvuni kwa kuvunja amani baada ya kutembea na mbwa huyo mahali ambapo Rais ameungwa mkono na watu wengi.
Kituo cha BBC kimeripoti Chinakwe alipendezwa sana na kazi ya Rais, jambo lililomfanya kumuita mbwa wake Buhari.
 Chinakwe amepokea vitisho vya kifo kutoka kwa watu asiowajua kutokana na tendo lake.
Mwanaume huyo mwenye miaka 30, amesema kuwa alimpa mbwa wake jina la Buhari kwasababu ya mapenzi yake kwa rais huyo

No comments:

Post a Comment