Thursday 30 November 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DISEMBA 01 2O17




Maofisa 2 wa zamani Argentina wahukumiwa kifungo cha maisha


Maofisa wawili wa zamani wa jeshi la maji la Argentina wamehukumiwa kifungo cha maisha kwa makosa ya ukiukaji wa haki za binadamu, waliyoyatekeleza kati ya mwaka 1976 na 1983 chini ya utawala wa kijeshi.
Kaptain Alfredo Astiz na Jorge Eduardo Acosta walikutwa na hatia ya kuhusika katika mauaji ya mamia ya wanasiasa wa upinzani.
Hawa ni kati ya washitakiwa 54, kati yao raia ni wawili, walioshitakiwa kwa makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu,na mauaji ya mamia ya wanasiasa wa upinzani,katika kituo chao cha mateso cha ESMA.
Ukatili huo ulifanyika,hapo ilikuwa ni shule ya ufundi makenika ya wanamaji hao.
Hatua hii inaatajwa na wemngi kuwa itaifanya Argentina kuheshimika zaidi kimataifa.

Rais Trump amshutumu waziri mkuu wa Uingereza Theresa May


Rais Donald Trump amemwambia waziri mkuu wa Uingereza Theresa May kuangazia ugaidi nchini Uingereza badala ya kumkosoa kwa kusambaza video za kundi la mrengo wa kulia la Uingereza ambalo linaeneza chuki.
''Usiniangazie sana mimi, angazia ugaidi unaotekelezwa na makundi yalio na itikadi kali ambao unatekelezwa nchini humo'', Trump alituma ujumbe wa Twitter.

Rais huyo wa Marekani awali alituma video tatu zenye chuki zilizosambazwa katika mtandao wa Twitter na makundi hayo nchini Uingereza.

Msemaji wa bi May alisema kuwa ni makosa kwa rais kufanya hivyo.

Marekani na Uingereza ni washirika wa karibu na wameelezewa kuwa na ''uhusiano maalum''.
Theresa May alikuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kumtembelea rais Trump katika ikulu ya Whitehouse.



Kanda za video zilizosambazwa na Trump ambaye ana takriban wafuasi milioni 40 awali zilikuwa zimechapishwa na Jayda Fransen, naibu kiobngozi wa kundi la Uingereza la Britain First, kundi lililoanzishwa na wanachama wa zamani wa mrengo wa kulia wa chama cha Uingereza cha BNP.
Bi Fransen mwenye umri wa miaka 31 ameshtakiwa nchini Uingereza mwa kutumia maneno ya kutisha, na matusi katika hotuba alizotoa katika mkutano mjini Belfast.

Marekani yaitaka dunia kusitisha biashara na Korea Kaskazini


Marekani imetoa wito kwa mataifa mbalimbai kukata uhusiano wake wa kidiplomasia na kibiashara na Korea Kaskazini, ikiwa ni hatua ya kupinga majaribio ya makombora ambayo yamekuwa yakifanywa na taifa hilo.
Balozi wa Marekani Nikki Haley, ametoa pendekezo hilo katika mkutano wa dharura wa baraza la usalama la umoja wa mataifa unaoendelea mjini New York.
Bi. Haley amesema kuwa Rais wa Marekani amemtaka Rais wa China Xi Jinping kusitisha biashara ya mafuta ghafi na Korea Kaskazini, kama sehemu ya kutekeleza hatua ya kuwekewa vikwazo kwa taifa hilo.

Kupitia hatua hii ya kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini tunapaswa kusitisha asilimia tisini ya biashara na Korea Kaskazini pamoja na asilimia 30 yamafuta yake.

Mwaka 2003, China ilisitisha kupelekea mafuta Korea Kaskazini ,muda mfupi baadaye taifa hilo likasogea katika meza ya majadiliano.
''Tumefikia hatua ya kuitaka China kuchukua hatua Zaidi katika hili, ni lazima isitishe kuipatia mafuta Korea Kaskazini," alisema Haley.
Wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wanakutana mjini Ne York kujadili hatua ya Korea kaskazini na majaribio ya makombora ya masafa marefu.

Rooney afunga bao la mwaka Everton

Everton, Wayne Rooney amesema bao alilofunga dhidi ya West Ham United litabaki katika kumbukumbu yake daima.

Rooney alisema hakuwahi kufunga bao maridadi katika maisha yake ya soka tangu alipoanza kucheza soka Everton, Manchester United na timu ya taifa ya England.

Nahodha huyo wa zamani wa Man United na England aliiongoza Everton kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Goodison Park.

Nguli huyo alifunga mabao matatu ‘hat trick’ kwa mara ya kwanza tangu aliporejea Everton katika usajili wa majira ya kiangazi kutoka Man United.

Pia ushindi wa Everton ni ukaribisho wa kocha mpya Sam Allardyce ‘Big Sam’ aliyetua Goodison Park baada ya kuwa nje ya uwanja muda mrefu tangu alipojiuzulu kuinoa England.

Rooney alifunga bao la kwanza kwa shuti kali akiwa katikati ya uwanja dakika ya 66 akimtungua kipa mkongwe Joe Hart umbali wa mita 54.

“Hili ni bao bora zaidi kati ya mabao yangu niliyowahi kufunga. Ni mara ya kwanza kufunga ‘hat trick’ nikiwa Everton ni hili ndilo bao maridadi tangu nilipoanza kucheza soka,”alisema Rooney.
Mbali na kufunga mabao hayo, Rooney mwenye miaka 32 alikuwa nahodha katika mchezo huo na alicheza kwa kiwango bora dakika zote 90.
Pia alidokeza alifunga bao zuri kwa mkwaju wa penalti kwa kuwa anatambua udhaifu wa Hart tangu wakiwa wote timu ya taifa.
“Bao la kwanza lilikuwa muhimu. Nimejifunza sana kupiga penalti nyingi dhidi ya Joe Hart na najua jinsi ya kumfunga kwa kuwa anajua udhaifu wake,” alisema Rooney.

Taarifa ya TANESCO kuhusu itilafu katika gridi ya Taifa

 Image result for tanesco
Majira ya saa 7:20 leo hii Alhamisi Novemba 30, imetokea hitilafu kwenye Gridi ya Taifa na hivyo kusababisha umeme kukatika takriban kwenye mikoa yote iliyounganishwa kwenye Gridi hiyo.
Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, mafundi na wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO wameanza kufuatilia kujua chanzo chake hasa ni nini na taarifa Zaidi zitatolewa kila baada ya muda ili kuufahamisha umma na watuamiaji wa umeme
.

Wednesday 29 November 2017

ZILIZOPEWA NAFASI KUBWA KATIKA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 30 2017




Sasii kuchezesha michuano ya Kombe la CECAFA Challenge


Waamuzi wawili wa soka nchini wameteuliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa ajili kuchezesha michuano ya Kombe la CECAFA Challenge itakayofanyika nchini Kenya.

CECAFA imewataja mwamuzi wa kati Elly Sasii na mshika kibendera Soud Lila, kutoka Dar es Salaam kuwa sehemu ya waamuzi wa michuano ya CECAFA 2017.
Mbali na waamuzi hao, CECAFA pia imewateua kocha Sunday Kayuni ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF na Mjumbe Mteule wa Kamati ya Utendaji ya TFF Ahmed Iddi Mgoyi kuwa wajumbe wa Kamati ya Maandalizi.
Waamuzi hao wawili na wajumbe wawili wanatarajiwa kusafiri kwenda nchini Kenya Novemba 30 mwaka huu, tayari kwa kushiriki taratibu nzima za maandalizi hayo ambapo michuano itaanza Desemba 3 hadi 17 mwaka huu.

Tanesco yatolewa ufafanuzi kukatika umeme


Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa taarifa kwa wateja katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuwa baadhi ya maeneo hayana umeme kutokana na hitilafu iliyojitokeza.

Taarifa ya Tanesco imesema baadhi ya maeneo ya mikoa hiyo hayana umeme kuanzia saa 3:20 asubuhi ya leo Jumatano Novemba 29,2017 kutokana na mashine namba tatu ya kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia kituo cha Ubungo II kupata hitilafu.
“Mafundi wa shirika wanaendelea na jitihada za kutatua hitilafu hiyo kwa haraka ili kurejesha umeme katika hali yake ya kawaida,” imesema taarifa ya Tanesco.
Shirika hilo limesema litaendelea kutoa taarifa za maendeleo ya kazi hiyo.
Pia, Tanesco imetoa tahadhari kwa wananchi kutosogelea, kushika wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Majaliwa abaini mbinu chafu ya kutoa semi 44 Bandarini

Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa (mwenye Tai nyekundu) amefanya ziara ya kushitukiza katika Bandari ya Dar es salaam leo November 29, 2017 na kubaini Kampuni ya NAS ikitaka kutoa Semi Trela 44 bila ya kufuata utaratibu.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro kuwakamata, Bw. Bahman wa kampuni ya NAS na Wakala wa Kampuni ya Wallmark Bw. Samwel kwa kutaka kutoa bandarini magari makubwa aina ya semi tela 44 bila ya kulipa kodi kwa kutumia jina la Waziri Mkuu.

Pia Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutowasikiliza wafanyabiashara wanaotaka kukwepa kodi kwa madai ya kupewa vibali vya msamaha wa kodi kutoka kwa viongozi wa juu Serikalini.

“Mtu asije hapa aseme amepewa kibali na Rais Dkt. John Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan au Waziri Mkuu cha kutaka kutoa mzigo wake bila ya kufuata taratibu. Akija mtu na taarifa hizo akamatwe mara moja na achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.”

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Novemba 29, 2017) alipofanya ziara ya ghafla bandarini baada ya kupata taarifa za mfanyabiashara huyo aliyetaka kuutapeli uongozi wa TPA kutaka kutoa magari hayo yaliyoingizwa nchini mwaka 2015 kutoka nchini Uturuki.

Hatua hiyo imekuja baada ya Bw. Bahman wa kampuni ya NAS kutaka kupata msamaha wa kodi kwa kuidanganya TPA kwa madai kwamba wamewasiliana na Waziri Mkuu na wasipotekeleza jambo hilo watapata matatizo.

Amesema Serikali inasisitiza watu kufuata sheria na taratibu za nchi ikiwa ni pamoja na kulipakodi ipasavyo na inataka watendaji wake wafanye kazi bila ya kubugudhiwa, hivyo amewataka wafanyabiashara kufuata sharia za nchi na kwamba Serikali haina ugomvi nao. Waziri Mkuu amefafanua kuwa mfanyabiashara huyo alitaka kuyatoa magari hayo bila ya kukamilisha malipo ya ununuzi kutoka kwenye kampuni Serin ya nchini Uturuki.

“Magari haya aliyalipia asilimia 30 tu kwa makubaliano ya kumaliza asilimia 70 iliyobaki baada ya kufika Tanzania na atakapokamilisha ndipo angepewa nyaraka ambayo inaonyesha jina la mwenye mzigo, aina ya mzigo na thamani (bill of lading) inasaidia mteja kufanyiwa tathmini ya gharama za kulipia ushuru, lakin huyu bwana hajafanya hivyo”

Waziri Mkuu amesema kitendo cha kuyasajili magari hayo bila ya kuwa na nyaraka hizo ni kinyume cha sheria na pia kinaweza kusababisha kampuni iliyouza magari hayo ya Serin kutolipwa malipo yaliyobaki.

Amesema jambo hilo halikubaliki kwa sababu linaweza kudhohofisha mahusiano mazuri iliyopo kati ya Tanzania na Uturuki kwani tayari kampuni hiyo imeshawasilisha malalamiko hayo katika ofisi za Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania.

“Uturuki wanawaamini sana wafanyabiashara wa Tanzania sasa huu ujanjaunja uliotumika katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuyasajili magari haya bila ya kuwa na bill of lading halisi unajenga sura mbaya kwa wafanyabiashara wengine waaminifu na watiifu wa sheria nawaagiza TRA kuchukua hatua kwa wahusika, hatuwezi kupoteza mahusiano na nchi kwa sababu ya utapeli wa mfanyabiashara mmoja.”
Pia Waziri Mkuu ametoa wito kwa Mawakala wa Forodha kuhakikisha wanakuwa makini katika kazi zao na Serikali haitawavumilia wababaishaji kwani inasisitiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo.

Awali, Mkurugenzi wa Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko alimueleza Waziri Mkuu kuwa pamoja na vitisho vya mfanyabiashara huyo kuwa wasipotekeleza matakwa yake watapata matatizo, lakini waliendelea kusimamia sheria na taratibu.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU JUMATANO, NOVEMBA 29, 2017.​

Kupitia ukurasa wa Ridhwani Kikwete ameandika haya

 Mbunge wa Chalinze kupitia CCM ambaye pia ni mtoto wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, ameonehsa kuguswa na kutoa yake ya moyoni baada ya Makamu wa Rais mama Samia Suluhu kwenda kumuona Tundu Lissu hospitali.
Kwenye ukurasa wake wa instagram Ridhiwani Kikwete ameandika ujumbe akisema kuwa Mama Samia ameonesha kuguswa kama mzazi kwa kitendo alichokifanya cha kwenda kumuona mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu.
"Sura yake Makamu wa Rais Mama Samiah Hassan inaonyesha kuguswa kama Mzazi. Wewe ni mzazi na Mungu aibariki Tanzania", ameandika Ridhiwani.
Hapo jana Makamu wa Rais mama Samia Suluhu alikwenda hospitali hapo kumuona Tundu Lissu ambaye amelzwa tangu Septemba 7 mwaka huu, baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya.

RC wa Morogoro apata ajali katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe amepata ajali katikati ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyopo wilayani Kilosa mkoani hapa.
Ajali hiyo ilitokea saa saba usiku wa kuamkia leo Jumatano ambapo inadaiwa gari la mkuu huyo wa mkoa lilimgonga mnyama aina ya Nyati na gari hilo kuharibika vibaya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urlich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa taarifa kamili ataitoa mara baada ya kukamilika.
Inadaiwa kuwa ndani ya gari hilo mbali na kuwepo mkuu wa mkoa pia aliambatana na mlinzi wake ambao wote kwa pamoja walitoka salama.

Korea Kaskazini yarusha kombora Kubwa zaidi

Taifa la Korea Kaskazini limefanyia majaribio kombora lake la masafa marefu lililoruka juu zaidi na kombora hilo tayari limeonekana kuhatarisha usalama duniani kulingana na waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani James Mattis.
Jaribio hilo la kombora mapema siku ya Jumatano lilianguka katika maji ya Japan.
Liliruka kwa urefu wa kilomita 4,500 na kusafiri umbali wa kilomita 960 kulingana na jeshi la Korea Kusini
Ni jaribio la hivi karibuni ambalo limezua hali ya wasiwasi, Mara ya mwisho kwa taifa hilo kulifanyia jaribio kombora lake ni mwezi Septemba, Wakati huo, kombora lake la mwisho lilikuwa la sita la nguvu za kinyuklia mwezi huo.
Korea Kaskazini imeendeleza mpango wake wa kinyuklia pamoja na ule wa utengenezaji wa makombora licha ya shutuma kutoka kwa jamii ya kimataifa.


Baraza kuu la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kukutana katika kikao cha dharura ili kuzungumzia hatua hiyo ya hivi karibuni.
Bwana Mattis amesema kuwa kombora hilo liliruka juu ikilinganishwa na kombo jingine lolote lile hapo awali.

''Korea Kaskazini ilikuwa ikiunda kombora linaloweza kuruka kutoka bara moja hadi jingine ambalo linaweza kurushwa eneo lolote lile duniani'', aliongezea.

Rais wa Marekani Donald Trump aliarifiwa kuhusu hatua hiyo wakati ambapo kombora hilo bado lilikuwa angani kulingana na Ikulu ya Whitehouse.''Tutalishughulikia''.

Tuesday 28 November 2017

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 29 2017


Kenya zazuka vurugu kuapishwa kwa Kenyatta


Mtaa wa Jacaranda jijini Nairobi, Kenya, leo umefungwa na polisi ili kuzuia mkutano wa umoja wa vyama vya upinzani nchini humo, National Super Alliance (NASA) uliopangwa kwa ajili ya kuwakumbuka wafuasi wake 27 waliouawa wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi wa marudio uliofanyika zaidi ya wiki moja iliyopita.
Mkutano huo ulipangwa kufanyika leo ambapo Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa kwa kipindi cha pili katika uwanja wa michezo wa Kasarani. Chumba vya kutunzia maiti katika jiji hilo pia kimefungwa na polisi ambapo watu hawatakiwi kufika hapo.




Polisi waliokuwa na zana zote za kuzuia fujo wamekuwa wakirusha mabomu ya machozi sehemu nyingi yakiwemo maeneo ya wafuasi wa NASA ambao wamefunga barabara kadhaa jijini humo.
Mpinzani mkuu nchini humo, Raila Odinga, amepinga mipango ya kumwapisha katika nafasi ya urais, akisema hilo linaweza kuleta vurugu na vifo zaidi.
Aliyasema hayo akionyesha mifano ya nchi za Ivory Coast na Gambia ambazo zilifanya hivyo kutokana na migogoro ya uchaguzi na hivyo kuwaapisha Alassane Quatara na Adama Barrow, hali aliyosema si sawa na ile iliyotokea nchini Kenya.




Pamoja na kuzuiwa kwa mkutano huo wa upinzani, inasemekana polisi wamepiga kambi karibu na makazi ya viongozi wa NASA, akiwemo Mbunge wa Dagoretti Kaskazini, Simba Arati.

Kenyatta atangaza neema Afrika Mashariki

Rais Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza neema kwa wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuruhusu kuingia nchini humo kwa kutumia kitambulisho cha taifa tu na kupewa haki zingine kama raia wa Kenya.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Rais Uhuru Kenyatta alipokuwa akilihutubia taifa mara baada ya kuapishwa , na kusema kwamba raia wa Afrika Mashariki watahudumiwa kama raia wa Kenya na kupewa haki zote za msingi ikiwemo kufanya kazi nchini humo, huku wale wa nchi zingine za Afrika watapewa viza akifika katika kiingilio chochote mpakani au viwanja vya ndege Kenya.
Pamoja na hayo Uhuru Kenyatta amesema hataweka masharti kwamba lazima mataifa mengine yafanye hivyo kwa wakenya watakaotaka kuingia kwenye nchi zao.

Samia Suluhu ahudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais Kenyatta

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo asubuhi tarehe 28 Novemba, 2017 amewasili Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba amepokelewa na Mhe. Balozi Robinson Njeru Githae wa Kenya na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Pindi Chana.

Sherehe za kuapishwa kwa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta zinafanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Nairobi

28 Novemba, 2017

Juventus yatawala tuzo za Gran Gala del Calcio 2016/17


Usiku wa Jumatatu hii katika mji wa Milan zilifanyika sherehe za utoaji wa tuzo za Gran Gala del Calcio katika ligi kuu ya nchini Italia, timu ya Juventus ndio imeongoza kuzoa tuzo nyingi zaidi.

Timu hiyo imefanikiwa kushinda tuzo ya timu bora ya Italia baada ya kutwaa taji la ligi kuu ya nchi hiyo kwa mara sita mfululizo huku pia ikitoa wachezaji saba katika kikosi cha timu bora ya ligi ya Italia kwa mwaka 2016/17.
Wakati huo huo kocha wa Napoli, Maurizio Sarri amefanikiwa kushinda tuzo ya kocha bora na golikipa wa Juventus, Gianluigi Buffon amefanikiwa kunyakuwa tuzo mchezaji bora wa Serie A ambapo msimu uliopitta tuzo hiyo ilichukuliwa na Leonardo Bonucci.



Gianluigi Buffon, Alex Sandro, Miralem Pjanic, Gonzalo Higuain na Paulo Dybala (wote kutoka Juventus), Dani Alves (PSG, msimu uliopita alikuwa Juventus), Leonardo Bonucci (AC Milan, msimu uliopita alikuwa Juventus).


Wachezaji wengine ambao wametajwa kwenye kikosi hiko ni pamoja na Kalidou Koulibaly, Marek Hamsik, Dries Mertens (Wote kutoka Napoli), na Radja Nainggolan (AS Roma).

Aubameyang sasa kufungashiwa virago Dortmund

Klabu ya Borussia Dortmund ipo tayari kuachana na straika wake Pierre-Emerick Aubameyang ambaye anawaniwa na timu za Liverpool pamoja na Chelsea.
Dortmund italazimika kumuuza Aubameyang ili kuepuka hasara ya kuondoka bure kwa mchezaji huyo, haya yanakuja baada ya timu hiyo kutoka sare ya mabao 4-4 katika mchezo wao wa derby dhidi ya Schalke katika ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani.
Mara baada ya mchezo huo meneja wa kikosi hicho, Peter Bosz amesema kufuatia utovu wa nidhamu unaoonyeshwa na straika huyo wa kimataifa wa Gabon  muda wa kubaki ndani ya klabu hiyo umekwisha.
Mlinda lango wa Dortmund, Roman Weidenfeller amesema meneja wa kikosi hicho, kachoshwa na ujinga unaofanywa straika huyo nakusema kuwa amepoteza kilakitu.

Siku ya kuzaliwa Rais Mugabe kuwa siku ya Taifa Zimbabwe

Serikali ya Zimbabwe imetangaza siku kuu mpya ya kukumbuka mchango wa Robert Mugabe ambaye aliondolewa madarakani wiki iliyopita.
Gazeti la serikali la Herald limesema sikukuu hiyo itakuwa ikiadhimishwa siku ya kuzaliwa kwa Bw Mugabe kila mwaka.
Uamuzi wa kusherehekea Siku ya Taifa ya Vijana ya Robert Gabriel Mugabe kila 21 Februari ulifanywa rasmi kupitia tangazo rasmi kwenye gazeti la serikali.
Tangazo hilo lilichapishwa Ijumaa – siku ambayo Rais Emmerson Mnangagwa aliapishwa kuwa rais, na kufikisha kikomo uongozi wa Mugabe wa miaka 37.
Serikali ya Bw Mugabe ilikuwa imeamua kutangaza siku ya kuzaliwa kwake kuwa sikukuu ya taifa mwezi Agosti, baada ya kampeni kutoka kwa mrengo wa vijana katika chama cha Zanu-PF.

Ziara ya IGP Sirro Bandarini


MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro, amefanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam, ili kufanya ukaguzi wa magari 31 ya Jeshi hilo ambayo Rais John Magufuli, alielekeza kukabidhiwa kwa Jeshi hilo ili kurahisisha utendaji wao wa kazi.


Akiwa Bandarini hapo IGP Sirro amekutana na kufanya mazungumzo na askari wa Jeshi hilo Kikosi cha Bandari ambapo amewataka kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ipasavyo pamoja na kutenda haki ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wateja.

Monday 27 November 2017

ZILIZOPAMBA KURASA ZA MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 28 2017




Papa aizuru Myanmar


Papa Francis ameanza ziara ya wiki nzima nchini Myanmar na Bangladesh leo Jumatatu, wakati wasiwasi unaendelea wa kimataifa kuhusu usalama na ulinzi kwa wasilamu wa Rohingya.
Anatarajiwa kukutana na Aung Sun Suu Kyi na mkuu wa jeshi Myanmar.

Hata kabla ya kuondoka Roma, Papa Francis alikuwa anakabailiwana kitendawili cha kidiplomasia: iwapo kuliita kundi dogo la waislamu Myanmar - Rohingya.
Ni jina lisilo tumika na serikali ya kiraia na jeshi - wakieleza kuwa ni wahamiaji haramu kutoka Bangladesh na kwahivyo hawapaswi kuorodheshwa kama mojawapo ya makabila nchinihumo.
Lakini mashirika ya kutetea haki za binaadamu wanamuomba awaite hivyo, yakieleza kuwa nilazima Papa Francis aoneshe huruma kwa watu walionyimwa uraia na tangu Agosti wamekabiliwa na kile kamishna wa haki za binaadamu katika Umoja wa mataifa amekitaja kuwa 'kinachoonekana kuwa mauaji ya kikabila'.
  • Amnesty:Burma yatega mabomu kuwazuia Rohingya
  • Mapungufu ya UN katika mzozo wa Rohingya
  • Wapiganaji wa Rohingya watangaza kusitisha mapigano, Myanmar
  • Myanmar yatakiwa kukoma kuwatesa Waislamu wa Rohingya
Zaidi ya WaRohingya 600,000 wamekimbilia mpakani - na wakimbizi wakielezea kukabiliwa na mauaji, ubakaji na kuteketezwa moto kwa vijiji - jeshi imekana tuhuma zote.

Meya Boniface wa Ubungo apata Dhamana

 Image result for boniface jacob
Meya wa Ubungo, Boniface  Jacob ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa polisi kwa takriban saa 15 akidaiwa kutaka kupanga njama za vurugu baada ya matokeo ya udiwani wa Kata ya Saranga kutangazwa.
Jacob ambaye pia ni diwani wa Ubungo (Chadema) alikamatwa na polisi jana Jumapili Novemba 26,2017 saa tano asubuhi katika kituo cha kupigia kura cha Mtakatifu Peter, Kimara.

Akizungumza leo Jumatatu Novemba 27,2017 baada ya kuachiwa na polisi, Jacob amesema alipokamatwa alipelekwa vituo vya Mbezi kwa Yusuf, Mabatini na baadaye Oysterbay alikokaa muda mrefu.

"Nimeachiwa saa 7:40 usiku kwa dhamana, hizi zote zilikuwa ni njama za kutunyima ushindi. Dhamana gani inatolewa usiku?” amehoji Jacob.

Amesema, "Hii ilikuwa mipango ili Chadema isishinde ila wakazi wa Ubungo wasivunjike moyo na haya, wamejionea hali halisi iliyofanyika na huu ni ushindi kwetu."