Monday 29 August 2016

Tamasha la Uhondo wa Zantel lakonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Dar es Salaam

zat1
:Meneja Habari na Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Winnes Lyaro (kulia)  akitoa maelezo kwa  baadhi ya wakazi wa Boko Basihaya nje kidogo ya Jiji la  Dares Salaam mwishoni mwa wiki kuhusu huduma mpya zitolewazo na kampuni hiyo ikiwa ni moja ya mikakati ya kampuni hiyo inayokuja na mtizamo mpya katika kuboresha bidhaa zake  na kutoa huduma bora kwa wateja. Ilikuwa ni katika tamasha lililopewa jina la Uhondo wa Zantel lililodhaminiwa na kampuni hiyo.
zat2
Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetesa na wimbo wake maarufu wa ‘Unanitega Shemeji’, Selemani Jabil ‘MsagaSumu’ akifanya vitu vyake wakati wa tamasha la ‘Uhondowa Zantel’ lililofanyika Boko Basihaya nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo lilidhaminiwa na Zantel.
zat3
Meneja Habari na Uhusiano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Winnes Lyaro (kulia)  akitoa zawadi kwa mmoja wa washindi wa maswali ya papo kwa papo wakati wa tamasha la ‘Uhondo wa Zantel’ lililofanyika Boko Basihaya nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Tamasha hilo lililodhaminiwa na Zantel kama sehemu ya mikakati ya kampuni hiyo inayokuja na mtizamo mpya katika kuboresha bidhaa zake na kutoa huduma bora kwa wateja.

No comments:

Post a Comment