Friday 26 August 2016

DrooEuropa League: Man Utd kukutana na Robin van Persie

Manchester United watakutana na klabu anayochezea nyota wao wa zamani Robin Van Persie- Fenerbahce- pamoja na Feyenoord na Zorya Luhansk hatua ya makundi Europa League.
Klabu ya KRC Genk anayochezea Mtanzania Mbwana Ally Samatta imewekwa kundi F na Athletic Bilbao ya Uhispania, Rapid Vienna ya Austria na Unione Sportiva Sassuolo Calcio kwa ufupi Sassuolo ya Italia.
Southampton, klabu nyingine ya Ligi ya England inayocheza michuano hiyo, imepangwa kucheza dhidi ya Inter Milan, Sparta Prague na Hapoel Beer Sheva.
Dundalk ya Ireland nayo imepangwa na h Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar na Maccabi Tel-Aviv baada ya droo kufanywa Monaco.

Meneja wa United Jose Mourinho amesema hawafahamu vyema wapinzani wao Zorya, kutoka Ukraine, lakini amefurahia kuwekwa kundi moja na Fenerbahce na Feyenoord.

"Sote twafahamu kwamba shindano hili si kama Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya lakini kuwa na Manchester United ikikutana na klabu zenye historia ndefu kama vile Fenerbahce na Feyenoord ni jambo zuri kwetu," amesema.


Droo kamili:
Kundi A: Man Utd, Fenerbahce, Feyenoord, Zorya Luhansk

Kundi B: Olympiacos, Apoel Nicosia, Young Boys, Astana

Kundi C:
Anderlecht, St Etienne, Mainz, Qabala

Kundi D:
Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar, Maccabi Tel-Aviv, Dundalk

Kundi E: Plzen, Roma, Austria Vienna, FC Astra Giurgiu

Kundi F: Athletic Bilbao, Genk, Rapid Vienna, Sassuolo

Kundi G: Ajax, Standard Liege, Celta Vigo, Panathinaikos

Kundi H: Shakhtar Donetsk, Braga, Gent, Konyaspor

Kundi I: Schalke 04, FC Red Bull Salzburg, Krasnodar, Nice

Kundi J: Fiorentina, PAOK Salonika, Liberec, Qarabag

Kundi K: Inter Milan, Sparta Prague, Southampton, Hapoel Beer Sheva

Kundi L: Villarreal, Steaua Bucharest, FC Zurich, Osmanlispor

No comments:

Post a Comment