Monday 29 August 2016

Misri imepitisha sheria kali dhidi ya Ukeketaji

Picha inayopinga ukeketaji

Mamlaka nchini Misri imeongeza adhabu kwa yeyote atakae walazimisha watoto wa kike kukeketwa. Sheria imependekeza kifungo gerezani kati ya miezi mitatu hadi miaka mitatu kwa mtu atakaepatikana na hatia.Huku baraza la mawaziri limepitisha mpango wa kifungo cha gerezani kati ya miaka mitano hadi saba.

Hukumu ya miaka kumi na mitano inaweza kutumika pale ambapo kitendo hicho cha ukeketaji kitasababisha ulemavu. Ukeketaji umekuwa ni suala lisilokubalika kisheria nchini misri tangu mwaka 2008 lakini vitendo hivyo vya ukeketaji vimekuwa vikienea kila uchao nchini humo.

No comments:

Post a Comment