Friday 30 September 2016

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI 01 OCT 2016

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh4yFLUnTKbUR-uMjfR23kwZGo0CaMdDFP3kevvmEarJBKCnVNDnPxNl6uxdPrhWwPGtFFPmpCuyh4AqOx-yBmsY9IktiDqx-6AH68fnAj1imicBRyZ5I4IXQbe5U-PvLcagDpyP-uc9Zw1/s1600/1.PNG

Nape amewatoa wasiwasi kuhusu upatikanaji wa tiketi kuelekea mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara kati ya watani wa Jadi Yanga na Simba

nna1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)  leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya matumizi ya tiketi za kieletroniki  kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara ya watani wa Jadi Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi leo ,2016.
nna2
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya upatikanaji  wa tiketi za kieletroniki  kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara ya watani wa Jadi  Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi leo ,2016 kushoto ni Meneja Mradi kutoka kampuni ya Selcom Tanzania Bw. Gallius Runyeta.
nna3
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akieleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya matumizi ya tiketi za kieletroniki  kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara ya watani wa Jadi Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi leo ,2016 kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw. Alex Nkenyenge.
nna4
Waandishi wa Habari wakifatilia mkutano huo.
nna5
Waandishi wa Habari wakifatilia mkutano huo.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Mashabiki wa soka nchini wameondolewa wasiwasi kuhusu upatikanaji wa tiketi kuelekea mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara kati ya watani wa Jadi Yanga na Simba na kuhakikishiwa kuwa mfumo wa upatikanaji tiketi uko vizuri na mpaka sasa tiketi zinaendelea kuuzwa katika maeneo mbalimbali.
 Wasiwasi huo umetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu matumizi ya tiketi za kieletroniki kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba.
Waziri Nape amesema kuwa kuna kuna taarifa kutoka mitaani kuwa kuna uwezekano wa mfumo huu kutofanya kazi  katika mechi hii na malalamiko ya watu wengi  kulalamika kukosa tiketi za mchezo wa kesho.

Tunda Man na Jaguar wa Kenya wafanya kolabo

 Image result for tunda man
Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Tunda Man amesema kolabo ambayo inakuja kutoka kwake ni ile aliyofanya na msanii wa Kenya, Jaguar.
Muimbaji huyo ameiambia FOFAM-MEDIA BLOG kuwa ana kolabo nyingi ambazo amefanya na wasanii mbalimbali lakini kolabo ambayo amepanga kuitoa hivi karibini ni ile aliyofanya na Jaguar.
“Kuna kolabo nyingi ambazo nimefanya na wasanii wa hapa pamoja na nje lakini kolabo ambayo mpaka sasa ipo kwenye mpango wa kutoka ni kolabo ambayo nimefanya na Jaguar, kwa hiyo mashabiki watulie kuna mambo mazuri yanakuja kutoka kwa Tunda Man,” alisema Tunda.

Pia muimbaji huyo amesema bado hajajua ni wimbo upi utaanza kutoka kati ya ‘Mwanaume Suruali’ pamoja na wimbo wa hiyo kolabo yake na Jaguar.

Wimbo wa ‘Mwanaume Suruali’ ameshindwa kuuachia hivi karibuni baada ya video ya wimbo huo kuzuiliwa kutokana na kumtumia video queen ambaye ni mke wa mtu

Kukanusha kwa taarifa zilizoenea kuhusu ajira Serikalini

Kuna tangazo ambalo linasambazwa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii lenye kichwa cha habari ‘’Sekretarieti ya Ajira yatangaza zaidi ya nafasi za kazi 1,000’’. Likionyesha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,101 kwa niaba ya waajiri mbalimbali Serikalini.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira anapenda kuwataafu wadau na wananchi wote kwa ujumla kuwa taarifa hiyo haina ukweli wowote na inalenga kuupotosha Umma, hivyo wananchi wote wanapaswa kuzipuuza.
Matangazo yote ambayo hutolewa na Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni lazima yaonekane kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz au portal ya Ajira ambayo ni portal.ajira.go.tz.

Mahakama yabariki urais wa Nkurunziza

 Image result for pierre nkurunziza
Uamuzi huo ulitolewa  na Mahakama ya Katiba ya Afika Mashariki (EACJ) kutokana na kesi iliyofunguliwa dhidi yake na asasi tatu za kiraia za Burundi, ambazo zilidai amejiongezea muda wa uongozi kinyume cha katiba.
Kupingwa kwa Rais Nkurunziza kuendelea kuwa rais kwa awamu tatu, kulisababisha kuibuka jaribio la kumpindua Mei, mwaka jana, chini ya Meja Jenerali Godefroid Niyombane.
Kutokana na kuongoza jaribio hilo, Meja Jenerali Niyombane alitimuliwa ukuu wa usalama, ikiwa miezi mitatu baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Mapema nchini humo, Mahakama ya Katiba ilimthibitisha Nkurunziza baada ya uteuzi wa chama chake cha CNDD FDD kumpitisha kupeperusha bendera katika uchaguzi mkuu.
Hukumuiliyosomwa jana na Jaji Isack Lenaola, ilithibitisha uhalali wa Rais Nkurunziza kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa awamu ya tatu kwa mujibu wa Katiba.

Taasisi 9 za serikali zakutwa na viashiria vya rushwa

 Image result for Takukuru
Taasisi tisa za serikali ikiwamo Taasisi ya Mifupa (MOI), Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, zimetajwa kuwa na viashiria vya rushwa.
Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma(PPRA) Matern Lumbanga.
Maeneo matano yaliyoangaliwa ni ukidhi wa sheria ya manunuzi ya umma, ukiukwaji wa sheria na taratibu za manunuzi, kupima thamani halisi ya fedha ilivyotumika, malipo yenye utata na viashiria vya rushwa.

Wenger: Wachezaji wa Afrika wamenifaa sana katika soka

 Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameiambia BBC kuwa wachezaji kutoka nchi za Afrika wamekuwa wenye umuhimu mkubwa katika taaluma yake ya miaka 20.
Wenga alikuwa akizungumza wakati wa mkutano wake wa kawaida na waandishi wa habari kabla ya mechi ambapo pia alitunukiwa kwa kukiongoza klabu hicho kwa miongo mwili.


Akiwa mwenye uso uliotabasamu, Wenger amesena kuwa wachezaji kutoa Afrika wana moyo, wenye ubunifu na nguvu, masuala ambayo ni vigumu kuyapa kwenye mche Aliwataja wachezaji akiwemo Nwanko Kanu wa Nigeria, Kolo Toure wa Ivory Coast na gwiji raia wa Liberia George Weah, ambaye alikuwa meneja wake katika klabu ya Monaco nchini Ufaransa, kama wachezaji watatu waliokuwa na uswawishi mkubwa katika taaluma yake.

Taarifa ya wizara ya afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto

img-20160930-wa0039

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh. Geoffrey Idelphonce Mwambe amewasimamisha kazi watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni

 mkuus
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh. Geoffrey Idelphonce Mwambe amewasimamisha kazi watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao vizuri, uzembe na utovu wa nidhamu.
Mwambe amefanya uamuzi huo alipokuwa kwenye Mkutano na Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni leo Tarehe 29.09.2016, ambapo aliwataja Watumishi hao aliowasimamisha kazi kuwa ni Mkuu wa Idara ya Ugavi Bw. Genesius Rugemalira ambaye amesimamishwa kwa kushindwa kusimamia manunuzi ya Halmashauri na kuisababishia Serikali hasara ya Tshs. Mil 16, Daktari John Amita wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni aliyesimamishwa kazi kwa tuhuma za kupigana na daktari mwenzake hospitalini hapo, tuhuma za utoaji mimba, na uzembe uliopelekea kifo cha mama mjamzito.
Wengine waliosimamishwa ni Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni Bw. Mika Iloti kwa uzembe uliopelekea kifo cha Mama mjamzimzito, Msaidizi wa Ofisi Bw. Anthony Sanga kwa ufujaji wa mapato ya Halmashauri na Mtendaji wa Kijiji cha Makasuku Bw. Mussa Ndahani ambaye kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Kijiji chake wamekuwa wakitoa vibali vya uvunaji Misitu kwa Wafanyabiashara ya mbao bila kuzingatia sheria na taratibu kwa kofia ya zoezi la utengenezaji wa madawati linaloendelea.
Mh. Mwambe amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kuhakikisha Watumishi hao wanasimamishwa mara moja kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili ili hatua Zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Viongozi mbalimbali wahudhuria mazishi ya waziri mkuu wa zamani wa Israel, Shimon Peres

 Rais wa Ufaransa, Francois Hollande na Prince Charles wa Uingereza walikuwepo
Viongozi wa dunia wamehudhuria mazishi ya waziri mkuu na rais zamani wa Israel, Shimon Peres.
Mazishi hayo yamegubikwa na ulinzi mkali.

Orodha kubwa ya viongozi wa mataifa mengine uliwasili kwaajili ya kutoa heshima zao za mwisho.
Wapo Rais wa Marekani, Barack Obama, Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, Waziri wa mambo ya nje wa Misri, Sameh Shoukry na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani
.

 Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton alikuwepo kutoa heshima zake kwa Peres
 Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas alikuwepo pia kwenye mazishi hayo
 Askari wakiwa wamelibeba jeneza la mwili wa Shimon Peres
Rais Barack Obama akisalimiana na wageni

Pluijm: Simba, Maneno Yenu Yote Mwisho Kesho

 Image result for hans pluijm
Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm.
 Katika mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi ya Simba, Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amesema imetosha kuhusiana na vita ya maneno inayoendelea kati yao na kinachofuata atawanyamazisha wapinzani kwenye mechi yao hiyo.
Pluijm ameeleza zaidi kuwa wakati mwingine haifai kuongea maneno mengi kuelekea katika mchezo huo kwa kuwa kikosi chake
kinafahamu nini cha kufanya ili kunyamazisha maneno yote yanayoendelea mitaani kuanzia kwa mashabiki, wapenzi, wadau mpaka viongozi.

“Huu mchezo umewaweka wengi kwenye presha, sasa sitaki kuongea sana, kuna maneno mengi yameshaongelewa na hii ni kwa kuwa ni mchezo wenye presha kwa sababu ni moja ya utani wa jadi uliopo, sasa kwa upande wetu nadhani hatuhitaji kuongea zaidi ya kufanya kazi hiyo Jumamosi.

“Wachezaji wangu wanafahamu mashabiki wanataka nini na nini cha kufanya kuzima hii presha iliyopo kwa mashabiki na wapenzi wengi wa Yanga, kumeshakuwa na maneno mengi lakini sasa ni vizuri kukaa

NSSF,mkoa wa Arusha,umezifikisha taasisi Nne mahakamani,kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao

 Image result for nssf tanzania

Ahmed Mahmoud- Arusha

MFUKO wa hifadhi ya jamii  NSSF,mkoa  wa Arusha,umezifikisha taasisi Nne mahakama ya hakimu mkuu mkazi   Arusha,kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa vipindi tofauti zaidi ya shilingi bilioni moja.
 
Mwanasheria mwandamizi wa NSSF, Selestini Ntagale, ameiambia mahakama ya hakimu mkuu mkazi kuwa taasisi hizo zimeshindwa kuwasilisha malimbikizo ya michango ya wafanyakazi hao kwenye mfuko huo licha ya kukumbushwa mara kwa mara.
 
Aliiambia mahakama hiyo kuwa michango ni haki ya mfanyakazi lakini kampuni hizo zimekuwa zikiwakata kwenye mishahara na haziwasilishi michango hiyo hivyo NSSF,kulazimika kutumia sheria kwa kuzifikisha mahakamani ili mahakama iziamuru kuwasilisha michango hiyo.
 
Miongoni mwa kampuni hizo ni pamoja na ,Water Solution, Net Health, na Hotel ya Snow Crest zote za Arusha.
 
Ntagale, aliiambia mahakama hiyo kuwa Kampuni ya Pride Tanzania, tayari ndani ya siku mbili imeshalipa shilingi milioni 180 kati ya deni lake la milioni 709 .
 
Ntagale, alisema Hotel ya Snow Crest inadaiwa tangia mwaka 2015 ambapo imechelewa kutekeleza hukumu iliyotolewa na hakimu mkazi na hivyo NSSF kukaza hukumu ambapo kama itashindwa kutekeleza NSSF itaomba kibali cha mahakama cha kuiuza  hotel hiyo kwa njia ya mnada ili kulipwa malimbikizo yanayodaiwa.
 
Aidha taasisi zingine zikiwemo Water Solution inadaiwa shilingi milioni  83.143.813,Hotel ya Snow Crest inadaiwa shilingi 449 na Net Health, inadaiwa shilingi milioni 14, 743,376,madeni ambayo ni malimbikizo  yanayotokana na makato ya mishahara ya wafanyakazi ambayo hayajawasilishwa NSSF.
 
Wakili mwandamizi, Method Kimomogoro, ambae anaiwakilisha kampuni ya Pride Tanzania, ameaiambia mahakama kuwa wateja wake wanakubaliana na deni hilo na watalilipa ndani ya mwezi mmoja .
 
Kimomogoro, aliiambia mahakama kuwa mteja wake amepewa muda mfupi wa siku mbili  na baada ya kupata taarifa hiyo wamelipa kiasi hicho cha fedha hivyo anaomba apewe muda wa mwezi mmoja hadi Novemba 4 wawe wamemaliza kiasi kilichobakia.
 
Katika hatua nyingine mahakama imetoa  hati ya kukamatwa kwa kampuni ya Net Health, ambayo haikufika mahakamani hapo huku kampuni ya Water Solution imeyakataa madai hayo ya NSSF wakidai sio sahihi .
 
Akiahirisha kesi hiyo, hakimu mkuu mkazi, Augostino Rwizila, amewataka wadaiwa wate kulipa madeni yao ndani ya muda wa mwezi mmoja ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 4 mwaka huu.
Kwenye kesi hiyo kila mdaiwa ana kesi yake binafsi  kulingana na madeni yake ingawa zote zinasikilizwa na hakimu mmoja .
 
Kesi hizo ni kama ifuatavyo, Net Health kesi namba, 389/ 2016, Pride Tanzania limited, kesi namba, 388/ 2016, Water Solution kesi namba, 390/ 2016 na Hotel ya Snow Crest kesi namba 61/ 2015 .

Kikosi cha Taifa stars

Image result for boniface mkwasa
Kocha Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi ambacho kitasafiri mwishoni mwa wiki ijayo kwenda Addis Ababa, Ethiopia kucheza na wenyeji wetu kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Oktoba 8, mwaka huu.
Mkwasa maarufu kwa jina la Master amesema wachezaji aliowaita wataingia kambini Oktoba 2, 2016 kabla ya kuanza kukiandaa kuanzia Oktoba 3, 2016 ikiwa mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya mwishoni mwa wiki hii ambako Mwadui itacheza na Azam huku Mbao ikishindina na JKT Ruvu Oktoba 2, mwaka huu.

Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa ni hawa

Makipa

Deogratius Munishi – Young Africans

Said Kipao – JKT Ruvu

Aishi Manula – Azam FC

Mabeki

Shomari Kapombe – Azam FC

Juma Abdul – Young Africans

Vicent Andrew – Young Africans

Mwinyi Haji – Young Africans

Mohamed Hussein – Simba SC

David Mwantika – Azam FC

James Josephat – Tanzania Prisons

Viungo wa Kati

Himid Mao – Azam FC

Mohammed Ibrahim – Simba SC

Jonas Mkude – Simba SC

Muzamiru Yassin – Simba SC

Viungo wa Pembeni

Shiza Kichuya – Simba SC

Simon Msuva – Young Africans

Juma Mahadhi – Young Africans

Jamal Mnyate – Simba

Hassan Kabunda – Mwadui FC

Washambuliaji

Ibrahim Ajib – Simba SC

John Bocco – Azam FC

Mbwana Samatta – CK Genk ya Ubelgiji

Elius Maguli – Oman

Thomas Ulimwengu – TP Mazembe Congo

Mchezo huo utakaofanyika jijini Addis Ababa, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ethiopia (EFF), wameo

Hii ni faida kwa Tanzania kama itashinda mchezo huo kwa maana kina alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.

Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Ethiopia yenyewe inashika nafasi ya 126.

Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Ujerumani, Colombia na Brazil.

Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 34 kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Algeria, Senegal, Tunisia na Ghana.

Wastara apata shavu la ubalozi wa kampuni mpya ya simu

Wastara akionyesha mkataba
Malkia wa filamu Wastara Juma amepata shavu la kuwa balozi wa kampuni ya simu za mkononi ya KZG Tanzania yenye makao makuu yake nchini China.
Katika mkataba huo mwigizaji huyo atavuna kiasi cha tsh milioni 400 kwa miaka miwili akiwa balozi wa kampuni hiyo kwa matangazo na matamasha mbalimbali.
Akiongea na Filamu Central meneja mauzo wa kampuni ya KZG Tanzania, Raymond Kalikawe amesema kuwa kamapuni yao imelenga kusambaza teknolojia vyuoni kwani wana bidhaa nyingi ambazo zinatumika katika kufundishia wanafunzi hao.

“Leo pia tunazindua simu ya kipekee kabisa kufika hapa nchini Kzg Kimi ambayo inatumia betri ya ndani kwa ndani ambayo ina sifa ya kutengenezeka tofauti na zingine ambazo betri zake zikiharibika hazitengenezeki,”alisema Kalikawe.

Pia Wastara ameishukru kampuni hiyo kwa kumwamini na kutambua kuwa ana vigezo stahili kuwa balozi wao na kuahidi kuwa hatowaangusha katika kuitangaza kampuni hiyo sambamba na bidhaa zake zilizalishwazo na kampuni hiyo ambayo utengeneza simu, Computer na vifaa vingine vya teknolojia.
Uzinduzi huo ulisindikizwa na wasanii wa Bongo movie wakimpongeza Wastara kuingia mkataba huo.

Thursday 29 September 2016

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPT 30 2016

 
 

Bahati Bukuku kama kawaida na nyimbo za mafundisho kwa jamii - Hakuna ajuaye yatakayotokea kesho

Pato la Taifa limekua kwa jumla ya thamani ya Shilingi trilioni 11.7

ver1
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa taarifa ya Pato la Taifa Robo ya Pili (Aprili – Juni) ya Mwaka 2016 kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa ofisi hiyo Bi. Joy Sawe. Taarifa hiyo imeonyesha kuwa Pato la Taifa limekua kwa kasi ya asilimia 7.9 katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni 2016 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
ver2
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa taarifa ya Pato la Taifa Robo ya Pili (Aprili – Juni) ya Mwaka 2016 kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa wa Ofisi hiyo Daniel Masolwa. Taarifa hiyo imeonyesha kuwa Pato la Taifa limekua kwa kasi ya asilimia 7.9 katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni 2016 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
ver3
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya Pato la Taifa Robo ya Pili (Aprili – Juni) ya Mwaka 2016 leo jijini Dar es Salaam. Taarifa hiyo imeonyesha kuwa Pato la Taifa limekua kwa kasi ya asilimia 7.9 katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni 2016 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2015. (PICHA NA EMMANUEL GHULA)

Na Veronica Kazimoto-Dar es Salaam
 
Pato la Taifa limekua kwa jumla ya thamani ya Shilingi trilioni 11.7 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016 ikilinganishwa na Shilingi trilioni 10.9 katika kipindi kama hicho cha mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa amesema ukuaji wa pato la Taifa umetokana na shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo, mifugo, misitu na uvuvi ambapo shughuli  hizo zimekuwa  kwa asilimia 3.2 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 1.9 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Kwa upande wa shughuli za uchumi za viwanda na ujenzi, Dkt. Chuwa alisema kumekua  na ongezeko la asilimia 20.5 katika kipindi hicho ukilinganisha na ukuaji wa asilimia 11.2 mwaka 2015 katika shughuli za uchimbaji madini, mawe na kokoto.
Aidha shughuli za uzalishaji bidhaa na viwanda zimeongeza kwa asilimia 9.1 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016 ukilinganisha na kasi ya asilimia 5.2 ya mwaka 2015.
Shughuli za uchukuzi na uhifadhi, Dkt. Chuwa amesema kuwa shughuli hizo zimekua kwa kiwango cha asilimia 30.6 zikisababishwa  na usafirishaji wa abiria kwa njia ya reli na barabara ikiwa ni pamoja na usafiri wa UDART.
Vilevile, shughuli za fedha na bima zimeongezeka kwa kasi ya asilimia 12.5 ikilinganishwa na asilimia 10.0 iliyopatikana katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Dkt. Chuwa amefafanua kuwa  huduma za elimu zimekua kwa kasi ya asilimia 8.0 katika robo hiyo ya mwaka ikilinganishwa na aslimia 7.4 ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2015 ambapo ukuaji wa shughuli hii imetokana na ongezeko la wanafunzi waliodahiliwa mwaka 2016.
Kwa upande wa Nchi za Afrika Mashariki ambazo zimeshachambua na kutoa Pato la Taifa katika kipindi kinachoishia Juni 2016 ni Rwanda ambapo Pato halisi la Nchi ya Rwanda katika kipindi cha Aprili – Juni 2016 limeendelea kukua kwa asilimia 5.4 ikilinganisha na asilimia 7.2 ya miezi kama hiyo mwaka 2015.

Bomba la mafuta lalipuliwa Nigeria

Kumwagika kwa mafuta kumechafua mazingira nchini Nigeria
Kundi la waasi katika eneo lenye utajiri wa mafuta nchini Nigeria linasema kuwa limelipua bomba la mafuta kama sehemu ya kampeni yenye kichwa "tunamiliki ardhi zetu."

Afisa wa idara ya ujasusi nchini Nigeria, aliliambia shirika la habari la AFP kuwa bomba hilo lililipuliwa na kundi la waasi
Bomba hilo liko chini ya usimamizi wa kampuni ya Nigeria Petroleum Development , sehemu ya kampuni ya serikali ya Nigeria Petroleum Corporation.

Eneo hilo lenye utajiri wa mafuta la kusini mwa nchi, limeshuhudia mashambulizi tangu Rais Muhammadu Buhari ambaye anatoka kaskazizi aingie madarakani mwaka uliopita.

Waasi wanataka wapewe mgao wa utajiri wa mafuta na pesa kutoka kwa mauzo ya mafuta kutumiwa kupambana na umaskini eneo hilo. Aidha wametaka kumalizika kwa uchafuzi unaosababishwa na sekta ya mafuta.

Samatta uwanjani leo kuiongoza Genk Vs Sasuolo

Mshambuliaji Mbwana Samatta, atakuwa na kazi wakati KRC Genk itakapokuwa inawavaa Waitaliano Sasuolo, kwenye mechi za makundi ya Ligi ya Europa.
Mechi hiyo ya Kundi F katika michuano ya Europa itakuwa ni hatua nyingine KRC Genk kujiweka vizuri katika michuano hiyo.

Samatta, alikosa michezo miwili iliyopita kwenye ligi kwa sababu ya majeruhi, lakini anarudi uwanjani kutaka kuisaidia klabu yake, iliyopoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Rapid Wien.
Genk endapo itashinda mchezo wa leo, itajiweka mazingira mazuri kupigania kutinga 16 bora, katika kundi F.

Serikali yatenga Bilioni100 ukarabati wa viwanja vya ndege

irin
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk John Magufuli imetenga kiasi cha sh. Bil. 100 katika bajeti ya mwaka 2016/17 kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa viwanja mbalimbali vya ndege nchini.
Rais Dk. Magufuli alisema hayo juzi katika sherehe za uzinduzi wa ndege mbili za Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Dash 8 Q400 zilizonunuliwa na serikali, kwenye Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo viwanja hivyo vitaboreshwa ili kuwezesha ndege hizo kutua bila wasiwasi.
Mhe. Rais akifafanua zaidi, alisema , kiwanja cha ndege cha Nduli kilichopo umbali wa kilometa 13 Kaskazini Mashariki mwa Manispaa ya Iringa, ambacho kipo kwenye kiwango cha lami kitakarabatiwa, ili ndege hizo zitue na kupaa bila tatizo.
Dk. Magufuli alisema, kiwanja cha Nduli Iringa ni kiunganishi kikubwa na JNIA na kitatumika kupeleka watalii wanaokwenda kutembelea mbuga ya wanyama ya Ruaha, wakitokea Mataifa mbalimbali duniani.
Alisema mbali na kiwanja hicho cha Nduli, pia kiwanja cha Musoma kitawekwa lami, ili nacho kiwe moja ya maeneo ndege hiyo itakwenda, na kurahisisha usafiri wa watalii watakaokwenda kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti. Kwa sasa kiwanja cha Musoma kipo katika kiwango cha changarawe na kinatumika kwa ndege mbalimbali kutua na kupaa.
Kwa mujibu wa Meneja wa Kiwanja cha ndege cha Nduli, Bi. Hannah Kibopile, kiwanja hicho kinapokea ndege ndogo zaidi ya saba zenye uwezo wa kubeba abiria 13, na kati ya hizo tatu zipo kwenye ratiba maalum ya kila siku na zilizosalia ni za kukodishwa na nyingine zinakwenda mbuga ya wanyama ya Ruaha.
Bi. Kibopile alisema ndege zinazotua kwenye kiwanja hicho zinatoka Jijini Dar es Salaam, Sumbawanga, Songea na Mbuga ya Ruaha.
Naye Kaimu Meneja wa Musoma, Bi. Faraja Mayugwa amesema kiwanja hicho kinapokea ndege zaidi ya nne kwa siku na nyingi zinakuwa za kukodi zinazopeleka watalii mbugani.
Katika hotuba yake, Rais Magufuli alisema “Hii ndege inaweza kutua katika kiwanja cha aina yeyote; na serikali itaendelea na ukarabati wa viwanja vya ndege vya pembezoni, ili viwe katika kiwango, ambacho ndege hizi zitatua na kuruka bila wasiwasi,”.
Akifafanua zaidi Dk. Magufuli alisema serikali inatarajia kununua ndege nyingine kubwa mbili zenye uwezo wa kubeba abiria 160 na 242, ambazo zitaanzia safari zake kwenye JNIA kwenda sehemu mbalimbali duniani kama China au Marekani moja kwa moja, ikiwa ni lengo la kupata abiria hao, ambao wengi wao watakuwa watalii wanaokuja nchini kutembelea vivutio mbalimbali. Bombardier inauwezo wa kubeba abiria 76.
Naye Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof Makame Mbarawa awali wakati akimkaribisha Mhe. Rais kuzungumza na wananchi katika ghafla hiyo ya uzinduzi wa ndege, alisema kwa kuanzia ndege hizo zitatua kwenye viwanja 11 vya ndege, ambavyo ni Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro (KIA), Zanzibar (AAKIA), Mwanza, Dodoma, Arusha, Bukoba, Kigoma, Tabora, Mbeya na  Mtwara.  Pia ndege hiyo itakwenda Comoro.
Mhe. Prof. Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuendelea kufanya upembuzi yakinifu kwa kuangalia viwanja  vingine vya ndege, ambavyo ndege hizi zitakwenda.

Manispaa ya Temeke yagawanywa ni baada ya wilaya ya Ubungo na Kigamboni kuongezeka

Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo. 
Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo amesema Halmashauri ya Manispaa ya Temeke hivi sasa inagawanywa rasmi hali itakayowagawanya madiwani wa kata za eneo hilo pia.
Chaurembo akiwa katika tukio hilo  leo,  alisema mgawanyo huo umetokana na hatua ya serikali kuongeza wilaya za Ubungo na Kigamboni na kusema kuwa baadhi ya madiwani watabaki Temeke na wengine watakwenda Kigamboni.
Kwa sasa manispaa ya Kinondoni imeshagawanywa na kata 20 kati ya 34 zimebaki Kinondoni na kata 14 zipo Ubungo.

Taarifa ya CUF tawi chuo kikuu cha Mlimani

THE CIVIC UNITED FRONT (C.U.F - CHAMA CHA WANANCHI) JUMUIYA YA VIJANA (JUVICUF) C.U.F VYUO VIKUU TAWI LA CHUO KIKUU CHA DSM (UDSM-MLIMANI)

WITO KWA WANACUF
Chama cha wananchi C.U.F tawi la Chuo Kikuu UDSM kinapenda kuwajulisha wanacuf kuwa Ijumaa Septemba 30 wajumbe wa BARAZA KUU na WABUNGE wa C.U.F watawasili ofisi kuu za C.U.F taifa zilizopo BUGURUNI JIJINI DSM.

Katika msafara huo viongozi wakuu wa chama watakuwepo wakiwemo Katibu Mkuu taifa MAALIM SEIF SHARIFU AHMAD, mwenyekiti wa kamati ya uongozi CUF Mh JULIUS SUNDAY MTATIRO na viongozi wengine waandamizi wa chama.

Hivyo, Chama cha Wananchi CUF tawi la chuo kikuu cha DSM kinawaomba wanacuf wote kujitokeza kwa wingi mapema asubuhi kwenye ofisi hizo za BUGURUNI tayari kwa kufanya mapokezi makubwa ya viongozi hao wa chama ambao wanawasili ofisini hapo kwa lengo kuu la kupanga mikakati ya kukijenga chama.

Tunawaomba wanachama wote, vijana, wazee , akina mama, wanachuo wa CUF na wapenzi pamoja na wakereketwa wote wazalendo wa CUF kujitokeza kwa wingi wakiwa na vipeperushi vya chama, sare na kila aina ya vitu vyenye kuashiria upendo wa viongozi wetu wa CUF.

TUNAWAKARIBISHA WANACUF WOTE MAKAO MAKUU BUGURUNI KWA MAPOKEZI.

CUF ILIJENGWA NA WANACUF, IMEJENGWA NA WANACUF, INAJENGWA NA WANACUF NA ITAJENGWA NA WANACUF.

TUNAWATAKIA MAANDALIZI MEMA YA MAPOKEZI.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa na :-

Mwl Razaq Mtele Malilo.
Katibu CUF vyuo vikuu tawi la Mlimani-UDSM.

Profesa Tibaijuka akataa zaidi ya Sh 200 milioni za tuzo

Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anne Tibaijuka. 
. Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anne Tibaijuka amesema amepata tuzo nchini Marekani ikiwa ni kuthamini mchango wake akiwa Umoja wa Mataifa lakini akakataa kuchukua fedha dola 100,000( zaidi ya Sh 200 milioni) ambazo huambatana na tuzo hiyo.

Trump apoteza $800m kipindi cha mwaka mmoja

 Bw Trump hupenda sana kuwakumbusha wapiga kura kwamba anafadhili kampeni yake binafsi
Mfanyabiashara tajiri wa New York anayewania urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amepoteza $800m ya utajiri wake katika kipindi cha mwaka mmoja, kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Jarida hilo linasema kwa sasa utajiri wa Bw Trump ni $3.7bn (£2.7bn).
Forbes wanasema kushuka huko kwa thamani ya utajiri wake kunatokana na 'kudorora kiasi' kwa biashara ya nyumba na ardhi katika soko la New York.

Bw Trump, ambaye wakati mmoja liandika kitabu kwa jina Midas Touch (Mguso wa Midas: Midas aliaminika kubadilisha kila alichogusa kuwa dhahabu), amekuwa akisema kwamba rais wa Marekani kwa sasa anaweza kuwa mtu mwenye busara katika biashara na majadiliano.

Wakati wa mdahalo wa urais Jumatatu, alisema: "Nina mapato makubwa ... wakati umefika kwa taifa hili kuwa na mtu anayefahamu mengi kuhusu pesa."

 Mapema mwaka huu, hoteli mpya ya Trump ilifunguliwa Washington DC, karibu na White House
Alipoteza vipi $800m?
Forbes, ambao wamekuwa wakikadiria utajiri wa Bw Trumo kwa zaidi ya miongo mitatu, wanasema hilo limetokana na kudorora kwa soko la nyumba, afisi na ardhi New York.
Kati ya majumba 28 ambayo yalichunguzwa na Forbes, 18 yalishuka thamani, likiwemo jumba maarufu la Trump Tower linalopatikana Manhattan.
Jumba lake lililo 40 Wall Street na kilabu chake cha Mar-a-Lago kilichopo Palm Beach, Florida, pia vilipoteza thamani, kwa mujibu wa Forbes.
Lakini majumba saba ya Trump, likiwemo jumba la pili kwa urefu San Francisco, yalipanda thamani.

 Ametumia pesa ngapi kwenye kampeni?

Inakadiriwa kwamba amewekeza $50m, pesa zake binafsi, kwenye kampeni kufikia sasa.

Forbes wanakadiria kwamba matamshi yake dhidi ya wahamiaji wa Mexico yalimgharimu $100m kupitia mikataba aliyopoteza kwenye mashirika makubwa kama vile NBC Universal, Univision na Macy's.

 Ivana na Donald Trump mwaka 1989
Utajiri wake kamili?
Utajiri wake kamili haujulikani. Alipowasilisha taarifa zake za kifedha kwa Tume ya Dola ya Uchaguzi, alisema ana "zaidi ya dola bilioni kumi."
Lakini Forbes wanasema utajiri wake ni $3.7bn, Bloomberg wanasema anamiliki $3bn nao Fortune wanasema ana $3.9bn.
Moja ya sababu inayochangia hili ni kwamba Bw Trump pia huhesabu thamani ya jina lake, ambalo anakadiria kwamba thamani yake ni karibu $3.3bn.

Trump na mkewe Melania na watoto wao wakati wa mkutano wa kampeni

Marekani yazuilia mali ya maafisa wawili wa DR Congo

 Jenerali John Numbi, (kushoto) akiwa na Jenerali Christian Damay wa jeshi la Ufaransa baada ya kikao na wanahabari mjini Kinshasa 14 Julai 2006.
Serikali ya Marekani imetangaza kwamba itazuilia mali ya maafisa wawili wakuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Marekani inawatuhumu wawili hao, mkuu wa zamani wa polisi Jenerali John Numbi na afisa mkuu wa jeshi Meja Jenerali Gabriel Amisi ajulikanaye kwa majina ya utani kama Tango Fort au Tango Four kwa kuwa "tishio kwa uthabiti na kuhujumu shughuli za kidemokrasia".
Wizara ya fedha ya Marekani imesema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kuzidi kwa vitendo vya ukandamizaji dhidi ya wapinzani, sana kwa kutumia nguvu
.
Kwa mujibu wa kituo cha redio cha Virunga Business, ingawa Jenerali Amisi bado anahudumu, John Numbi hajatekeleza majukumu rasmi kwa miaka mingi tangu kuuawa kwa mtetezi wa haki za kibinadamu Floribert Chebeya. Jenerali Numbi alisimamishwa kazi Juni 2010 baada ya kifo cha mwanaharakati huyo.
"Maafisa hawa wa serikali ya DR Congo wamejihusisha katika vitendo vya kuhudumu shughuli za kidemokrasia na kukandamiza haki za kisiasa na uhuru wa watu wa Congo, na kuzidisha hatari ya kuenea kwa ukosefu wa uthabiti DR Congo na eneo lote la Maziwa Makuu," kaimu mkurugenzi wa idara inayoangazia mali ya raia wa nje ya Marekani John Smith amesema kupitia taarifa.
Miezi minne iliyopita, mkuu wa polisi wa Kinshasa Celestin Kanyama pia aliwekewa vikwazo.
Bw Numbi anatoka Kolwezi, mkoa wa Katanga na anadaiwa kutumia nguvu na kuwatisha wapinzani wakati wa uchaguzi wa majimbo uliofanyika Machi 2016.
Anadaiwa kutishia kuua wapinzani wa wagombea wanaomuunga mkono Rais Joseph Kabila iwapo hawangejiondoa. Wagombea watatu wanadaiwa kujiondoa kutokana na vitisho hivyo.

"Ingawa si afisa wa serikali ya DR Congo tena, Numbi bado anaaminika kuwa mshauri wa Rais Kabila mwenye ushawishi mkuu," taarifa ya Marekani imesema.

Jenerali Amisi, ajulikanaye pia kama Tango Fort
Jenerali Amisi anadaiwa kuwa kiongozi wa kundi la kijeshi linalosimamia mikoa ya Bandudu, Bas Congo, Equateur na Kinshasa, ambao walitumiwa kuzima maandamano ya kisiasa, hasa yaliyoandaliwa na upinzani na mashirika ya kiraia Januari 2015.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa watumishi waliohamishiwa wilaya mpya ya Kibiti mkoani Pwani kuripoti katika vituo vyao

kibt1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa watumishi waliohamishiwa wilaya mpya ya Kibiti mkoani Pwani kuripoti katika kituo chao cha kazi na watakaoshindwa kutekeleza watakuwa wamejifukuzisha kazi.
Amesema mtumishi yeyote aliyehamishiwa wilaya hiyo ambaye anaishi nje ya Kibiti anatakiwa arudi na kuishi kwenye makao makuu ya wilaya na si vinginevyo.
“Tayari nimemuagiza ndugu Zuberi Samatabu  Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani kuhakikisha anasimamia watumishi wote wa wilaya hiyo wanaoishi nje ya wilaya hiyo  waishi Kibiti na si Ikwiriri,” amesema.
Kauli hiyo ya Waziri Mkuu ilifuatia taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Alvera Ndabagoye ambaye alimueleza Waziri Mkuu  kuwa ni watumishi wanane pekee kati ya  74  waliopangiwa kufanya kazi kwenye wilaya hiyo wameripoti  katika kituo cha kazi
Ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa nyumba za watumishi amemuagiza Mkuu wa  Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuzungumza na watendaji wa mifuko ya hifadhi  ya jamii kwenda wilayani huko kuwekeza katika miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi.

Serikali imetoa shilingi milioni 17 na kampuni ya simu ya Halotel imetoa shilingi milioni 15 kwa waathirika wa tetemeko Kagera

sd1
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiongea na wawakilishi wa familia waliopoteza ndugu zao (hawapo pichani) kwa tetemeko la ardhi lililotokea mapema Septemba 10 mwaka huu Bukoba mjini wakati wa kukabidhiwa rambirambi iliyotolewa na Serikali milioni 17 pamoja na kampuni ya simu ya Halotel ambayo imetoa shilingi milioni 15.kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa
sd2
Yusta Jonas mkazi wa Hamugembe Manispaa ya Bukoba akipokea rambirambi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu ambayo imetolewa na Serikali pamoja na kampuni ya simu za mkononi ya Halotel.
sd3
Mzee Vedasto Kato kutoka mtaa wa Hamgembe Manispaa ya Bukoba akipokea rambirambi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu ambayo imetolewa na Serikali pamoja na kampuni ya simu za mkononi ya Halotel.
sd4
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (katikati aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa wanafamilia waliofiwa na ndugu zao wakati wa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, mwaka huu.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba)

Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba
Familia 15 zilizofiwa na ndugu zao 17 wakati wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani wa Kagera zimepokea rambirambi ya jumla ya shilingi milioni 32 ikiwa ni mkono wa faraja kwa msiba uliwafika familia hizo na taifa kwa ujumla.
Rambirambi hiyo imetolewa mjini Bukoba na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kwa niaba ya Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya simu za mkononi nchini ya Halotel ili kuwashika mkono wafiwa hao kwa kupoteza ndugu na jamaa zao.
Katika rambirambi hiyo, Serikali imetoa shilingi milioni 17 na kampuni ya simu ya Halotel imetoa shilingi milioni 15 ambapo kila familia ya mfiwa amepokea shilingi 1,000,000 kutoka Serikalini na shilingi 885,000 kutoka kampuni ya Halotel.
Hatua hiyo inapelekea kila familia ya mfiwa kupokea jumla shilingi 1,885,000 ambapo familia mbili zilizopoteza ndugu zao wawili wawili wamepokea jumla ya shilingi 3,770,000 ikiwa ni rambirambi kwa kila ndugu aliyefariki wakati wa tukio hilo la tetemeko la ardhi.
Akikabidhi rambirambi hiyo kwa familia hizo, Mkuu wa Mkoa wa huo akiwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa mkoa Meja Jenerali Mstaafu Kijuu amesema kuwa Serikali imetoa rambirambi hiyo kwa lengo kuwapa pole wafiwa hao kutokana na kuwapoteza ndugu na jamaa zao wakati wa tetemeko hilo lililotokea  Septemba 10, mwaka huu.

Airtel na Puma washirikiana kununua mafuta kwa kutumia huduma ya Airtel Money Tap Tap

1
MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso  wakibadilishana mikataba mara baada ya kuasini makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi ya Aiter Money Tap Tap , Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay.
2
MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso  wakiasini  mkataba wa makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi ya Aiter Money Tap Tap , Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay jijini Dar es salaam.
4
Baadhi ya maofisa wa Puma na Aiter wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye kituo cha mafuta cha Puma Oysterbay jijini Dar es salaam.
5
Meneja Rasilimali Watu wa Puma Tanzania Bi Loveness Hoyange pamoja na maofisa wengine wa kampuni hiyo na kampuni ya Kampuni ya simu ya Aitel wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
6
Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matindekulia na baadhi ya maofisa wa kampuni ya Aitel na Puma wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
7
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso kulia na  MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti  wakishuhudia wakati mmoja wa wateja wa Aitel Money na Puma akijaziwa mafuta  kwa kutumia huduma ya  Airtel Money Tap Tap katika kituo cha mafuta cha Puma Oysterbay jijini Dar es salaam.
 
Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti amesema  wanalo jukumu la kuhakikisha huduma wanazitoa kwa ajili ya  Watanzania zinakuwa salama wakati wote ikiwa ni sehemu ya kuunga  mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuhamasisha kutumia  njia za kieletroniki kwenye malipo ya fedha.
Corsaletti alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa  huduma mpya inayojulikana kwa jina la Airtel Money Tap Tap ambayo  inamuwezesha mteja wao anapotaka kununua mafuta kwa kutumia  kadi ya Airtel badala ya kutoa fedha taslimu akiwa kituo cha mafuta.
Alisema wanahisi kwamba wanawajibu wa kufanya huduma zao kwa  usalama, senye ufanisi na rahisi zaidi kwa wateja wao na kufafanua ni  hatari kubeba fedha wakati wote maana ni rahisi kuhatarisha maisha.
Aliongeza hivyo ili kufanya jamii ya Watanzania inakuwa salama wakati  wote imeona kuna haja ya kuwa na huduma hiyo ambayo  itamuwezesha anayehitaji kununua mafuta kwenye vituo vya Puma  vilivyopo maeneo mbalimbali ya Dar es salaam wanatumia kadi za Airtel  kununua mafuta.
“Milango yetu iko wazi kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma zetu  na kuna jambo lolote ambalo tunaweza kulifanya ili jamii yetu  kuwa  salama wakati wote.Hivyo kuna umuhimu wa kuwa na matumizi ya  kadi ya Airtel katika kununua mafuta kwenye vituo vyetu vya  Puma,”alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu huduma ya Airtel Money Tap Tap, Corsaletti  alisema chini ya utaratibu huo mtu yeyote aliyejisajili na huduma ya  Airtel Money atakuwa na uwezo wa kulipia bidhaa za Puma katika vituo  vyake vyote nchini kwa kutumia kadi  ya huduma ya Airtel Tap Tap   badala ya kutumia fedha kwa ajili ya huduma kama hizo.
“Kadi hii imeundwa kwa namna ambayo wakati wa kutumika kufanya  malipo , hupunguza fedha kwa kiasi cha malipo kutoka katika akaunti  ya Airtel Money ya mnunuzi kwenda kwenye akaunti  ya muuzaji. “Kadi hii itakuwa inauzwa kwa bei ya Sh 2, 000 kwenye vituo vyote vya  Puma Dar es Salaam na maduka yote ya Airtel Tanzania .