Friday 31 March 2017

ZILIZOGUSA KATIKA VICHWA VYA WATANZANIA MAGAZETINI JUMAMOSI APR 01 2017




Kesi ya malkia wa tembo kusikilizwa kuanzia Aprili 5 hadi 7, mwaka huu

Yang Feng Glan, maarufu kama Malkia wa tembo
Kesi inayomkabili raia wa China, Yang Feng Glan (66) maarufu kama Malkia wa tembo inayosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam itaendelea kusikilizwa kuanzia Aprili 5 hadi 7, mwaka huu.
Wakili wa Serikali, Elia Athanas alidai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa na kwamba mawakili wanaosikiliza kesi hiyo hawapo.
Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Hassan Kiangio alidai kuwa kesi hiyo imeahirishwa kwa mara ya pili tangu mshitakiwa Manase Philemon (39) kudai amepigwa na kuteswa wakati akichukuliwa maelezo yake, ambapo upande wa mashitaka ulitakiwa kuleta mashahidi ili kuthibitisha tuhuma hizo.
Hatua ya upande wa mashitaka kuleta mashahidi ni kusikiliza kesi ndogo ndani ya kesi kubwa baada ya shahidi Sajenti Beatus (46) kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kudai kuwa aliandika maelezo ya mshitakiwa huyo na baadaye mshitakiwa kupinga kupokelewa kwa maelezo hayo kwa madai kuwa aliteswa na kupigwa.
Kiangio alidai kuwa mashahidi watakaoletwa na upande wa mashitaka watathibitisha ni kwa namna gani maelezo hayo yalichukuliwa. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 5 hadi 7, mwaka huu, kesi itakaposikilizwa mfululizo.

FIFA yakubali kuwepo timu 48 kombe la dunia

Baada ya Rais mpya wa FIFA, Gianni Infantino kutaka kuwepo kwa timu 48 ambayo ilikua ni moja ya ahadi zake katika kampeni.
Chama cha soka duniani FIFA kimepanga kuwepo kwa michezo sita ili zipatikane timu zitakazoingia katika fainali za kombe la dunia mwaka 2020.
FIFA imefafanua ni kwa namna gani timu 48 zitaweza kushiriki michuano hiyo.
Rais wa shirikisho la soka Ulaya Aleksander Ceferin amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo na nchi za Ulaya zitawakilishwa vyema.
Kila mwanachama wa FIFA atakuwa na uwezo wa kuongeza walau timu moja katika michuano ya mwaka 2026.
Mwenyeji wa fainali hizi ataingia moja kwa moja kama ilivyokua awali.
Mapendekezo hayo yapo hivi
Afrika – 9 kutoka timu za awali 5
Asia – 8 kutoka timu 4 za awali

Ulaya – 16 kutoka timu 13 za awali

Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean – 6 kutoka timu 4 za awali

Bara la Oceania – 1 kutoka timu 1 ya awali

Amerika ya Kaskazini – 6 kutoka timu 4 za awali

Simba SC yakubali kudaiwa na TRA

Hatimaye Klabu ya Simba SC yajitokeza hadharani na kukiri kudaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kodi za nyasi bandia walizozitelekeza bandarini huku wakifurahia kuongezewa muda wa kulipa malipo hayo.
Hatua hiyo imekuja baada ya kampuni ya udalali ya MAJEMBE AUCTION kutangaza kuzipiga mnada endapo klabu hiyo itashindwa kwenda kulipia ushuru unaodaiwa.
"Simba inakiri kudaiwa na TRA kodi ya nyasi bandia, tunafanya juhudi zote kulipa kodi kwa wakati baada ya kuomba kuongezewa muda kulipa na TRA". Imeandika klabu hiyo kupitia mitandao yake ya kijamii ya twiiter pamoja na instagram asubuhi ya leo (Ijumaa).
Pamoja na hayo klabu hiyo imewataka mashabiki na wanachama wake kuendelea kuwapa ushirikiano katika mechi zao za kanda ya ziwa vile vile kupuuza maneno ya mitandaoni yanayoweza kuwa na lengo baya kwa Simba SC.

Peter Lijualikali:Nilichofanyiwa ni uonevu

 Image result for Peter Lijualikali
Siku moja baada ya Mbunge wa Kilombero (Chadema) Peter Lijualikali kuachiwa huru na mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam, ametoa ya moyoni na kusema kuwa alichofanyiwa ni uonevu.
Ameyasema hayo leo baada ya Waziri Mkuu Mstaafu, na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye, kukamilisha taratibu za kumtoa gerezani.

Lijualikali amefutiwa mashtaka yake jana na mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam baada ya kukaa jela kwa zaidi ya siku 70 akituhumiwa kufanya vurugu katika uchaguzi wa mwaka 2015. Katika hukumu hiyo, Lijualikali alihukumiwa bila kupewa masharti ya faini.

Rais wa zamani Korea Kusini akamatwa

 Bi Park amepelekwa kizuizini Seoul
Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani wiki chache zilizopita Park Geun-hye amekamatwa na kuzuiliwa kuhusiana na tuhuma za rusha ambazo zilichangia kutimuliwa kwake kutoka madarakani.
Park, 65, alisafirishwa kwa gari hadi kwenye kituo cha kuwazuilia watuhumiwa wa uhalifu kusini mwa Seoul baada ya mahakama kuidhinisha kukamatwa kwake.
Bi Park anatuhumiwa kumruhusu rafiki yake wa karibu Choi Soon-sil kudai pesa kwa lazima kutoka kwa kampuni kubwakubwa.
Bi Park amekanusha madai hayo.
Rais huyo wa zamani aliomba radhi kwa umma wiki iliyopita, kabla ya kuhojiwa na maafisa wa mashtaka kwa saa 14.
Waendeshaji mashtaka walisema Jumatatu kwamba "wameamua kwamba ni vyema, kwa kufuata sheria na maadili nchini humo, kuomba kibali cha kumkamata".
Walisema ushahidi, ambao unapatikana katika diski za kompyuta huenda ungeharibiwa iwapo Bi Park hangekamatwa.
Bi Choi amefunguliwa mashtaka ya ulaji rushwa na tayari kesi dhidi yake imeanza.
Bi Park ndiye rais wa tatu wa zamani Korea Kusini kukamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika uhalifu, shirika la habari la Yonhap limeripoti.
Mahakama ya Seoul ilitoa kibali cha kukamatwa na kuzuiliwa kwa Bi Park anapoendelea kuchunguzwa kuhusu ulaji rushwa, kutumia vibaya mamlaka, kutumia mamlaka yake kushinikiza watu na kuvujisha siri za serikali.
Uamuzi wa mahakama ulitolewa baada ya kikao cha mahakama kilichodumu saa tisa Alhamisi. Bi Park alihudhuria kikao hicho.

Wafuasi wa Bi Park walikusanyika nje ya nyumba yake alipokuwa mahakamani
Video zilionyesha Bi Park akiwa amebebwa kwa gari jeusi aina ya sedan na kusafirishwa hadi kizuizini.


Rand ya Afrika Kusini yashuka kwa kasi

Fedha ya Afrika Kusini, rand, inaendelea kushuka thamani kwa kasi baada ya Rais Jacob Zuma kumtimua waziri wa fedha mwenye uzoefu mkubwa, Pravin Gordhan.
Zuma alitangaza uamuzi huo Alhamis hii kuwa anamuondoa Gordhan pamoja na mawaziri wengine. Wawekezaji walikuwa wameshaanza kuhofia kuwa Zuma angemtimua waziri huyo baada ya Jumatatu kumuamuru asitishe mikutano mingi na wawekezaji wa nje na kurudi nyumbani.
Hatua hiyo pia ilikuwa dhoruba kwa rand ambayo sasa imeshuka thamani yake kwa asilimia 8. Wachambuzi walionya mapema wiki hii kuwa kumuondoa Gordhan na mawaziri wengine kungekuwa na madhara.
Amekuwa waziri wa fedha kwa kipindi kirefu kuanzia mwaka 2009 hadi 2014 na kurudi tena December 2015. Zuma amteua Malusi Gigaba aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani kushika nafasi hiyo.

Lady Jaydee leo atafanya uzinduzi album yake mpya

  Image result for Lady Jaydee
Lady Jaydee leo atafanya uzinduzi wa album yake mpya na ya saba, Woman Ametangaza kubadilisha ukumbi wa awali na sasa utafanyika King Solomon Hall.
“Naomba kuwafahamisha mabadiliko ya Venue Ijumaa Woman Album Launch Itafanyika ukumbi wa King Solomon Hall , karibu na Best Bite (Ada Estate- Kinondoni) Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza,” ameandika Jide kwenye Instagram.
Album hiyo itakuwa na nyimbo kama Kamoba alioshirikiana na Hamoba wa Zambia, Together Remix akiwa na Spicy, Rosella akiwa na H_Art the Band, Unanichanganya akiwa na Naava wa Uganda na zingine.

Mbunge Viti Maalum Dkt. Elly Macha amefariki Dunia

 Image result for Elly Macha
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Viti Maalum (CHADEMA) akiwakilisha walemavu Dkt. Elly Macha amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, ambapo amesema mbunge huyo alikuwa akipatiwa matibabu mkoani Arusha.
"Taarifa ni za kweli, mbunge Viti Maalum Dkt. Elly Macha amefariki, lakini sijapata bado taarifa za kina, lakini ninachojua ni kwamba amekuwa akipatiwa matibabu kwa muda mrefu Arusha" Amesema Makene
Miongoni mwa wabunge wa kwanza kutoa taarifa za msiba huyo ni Lazaro Nyalandu ambaye kupitia mtandao wa twitter ameandika "Mbunge mwenzetu, Mhe. Dr. Elly Macha amefariki dunia leo.
Wabunge wote tumeguswa sana na tukio hilo. Upumzike kwa amani dada yetu mpendwa"

Thursday 30 March 2017

ZILIZOPEWA KIPAUMBELE KATIKA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MAR 31 2017




BALILE : NIMESHANGAZWA SANA NA MWAKYEMBE KUWA TAARIFA YETU KUHUSU MAKON...

Shy-Rose Bhanj:Sikuitwa kujitetea


Aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Shy-Rose Bhanji amelalamika jina lake kukatwa katika kinyang'anyiro cha kutetea nafasi hiyo katika muhula ujao bila kuhojiwa juu ya tuhuma zilizopeleka jina lake kukatwa.
Licha ya malalamiko hayo, pia Shy-Rose Bhanji ametumia fursa hiyo kuwapongeza watu waliochaguliwa kuwa wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi na kuwashukuru wabunge kwa kumpigia kura zilizomuwezesha kuwa miongoni mwa wagombea wanne wa mwanzo waliopata kura nyingi zaidi. 
"Ingawa jina langu limekatwa na Kamati Kuu ya Chama bila ya mimi nwenyewe kuitwa na kuhojiwa ili nipewe haki ya kujibu hoja zozote dhidi yangu, nawapongeza wote waliochaguliwa kuwa wagombea wa EALA kupitia CCM. Ninawashukuru sana Wabunge kwa kunipigia kura nyingi zilizoniwezesha kuwa miongoni mwa wagombea wanne wa mwanzo walioongoza kwa kura" aliandika Shy-Rose Bhanji
 

Bunge Afrika Kusini Kumng'oa Rais Zuma



Kiongozi wa upinzani Afrika Kusini, J. Malema kufungua kesi Mahakama ya Kikatiba akitaka Spika wa Bunge aanzishe mchakato wa kumng'oa Rais Jacob Zuma

Mallema

Clouds wamsimamisha Mtangazaji kwa kutangaza Habari ya Makonda


 Related image
Bodi ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) imekutana jijini Dar es Salaam leo Machi 30, 2017. Pamoja na mambo mengine imejadili mwenendo wa vyombo vya habari ndani ya wiki moja tangu tulipotoa msimamo wa kutotangaza habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Bodi imepitia habari za Mkuu wa Mkoa zilizochapishwa tangu ulipotolewa msimamo wa kumfungia. Bodi inapenda kawapongeza wahariri wote waliotekeleza kwa usahihi msimamo wa kutochapisha habari za Mkuu wa Mkoa kwa wiki nzima.
Bodi inapenda kusisitiza kuwa wahariri katika vyombo vya habari; magazeti, radio na televisheni waendelee na msimamo wa kususia habari za Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, hadi atakapotimiza takwa la kuomba radhi kwa tukio la kuvamia kituo cha Clouds.
Bodi inatoa wito kwa viongozi wa mitandao ya kijamii kuunga msimamo huu. Bodi inapenda kufafanua kuwa Mhe. Makonda amewekewa vikwazo Maalum (Smart Sanction) kwa mikutano atakayoiandaa au matukio atakayoyaongoza habari zake hatutazichapisha.

Kikao Cha Wadau Wa Afya Afrika Mashariki

Q
Picha ya pamoja ya mawaziri wa jumuiya ya umoja wa Afrika Mashariki Mara baada ya ufunguzi wa Kongamano LA kupanga jinsi ya kukabiliana na majanga.Kongamano hilo lilizinduliwa na Rais Pierre Nkurunzinza
Q 1
Mganga Mkuu wa Serikali toka Tanzania (wa kwanza kushoto)  Prof.Bakari Kambi akichangia mada katika mkutano huo uliokutanisha wadau wa afya kutoka Afrika mashariki.
Q 2
Baadhi ya wajumbe toka Kenya wakifuatilia mada zilizowasilisha kwenye mkutano huo.

Bujumbura,Burundi
Nchi wanachama wa Umoja wa Afika mashariki pamoja na sektarieti ya umoja huo(EAC) wamehimizwa kuharakisha mchakato wa kuhakikisha kada zingine za afya ikiwemo ya uuguzi na kada nyingine zenye sifa  na viwango vinavyofanana na madaktari kuajiriwa kwenye nchi yeyote ya Afrika Mashariki
Hayo yamesemwa jana na Waziri WA Afya,Maedeleo ya Jamiii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Kisekta la mawaziri wa Afya wa Afrika mashariki kwenye kikao cha 14 nchini hapa
Waziri ummy alisema amefurahishwa sana na hatua iliyofikiwa na  nchi wanachama wa Jumuiaya hiyo ambapo hivi sasas madaktari wanaotoka katika jumuiya hiyo kuajiriwa
Katika hatua nyingine kikao hivho kimejadili kuhusu kuimarishwa kwa mafunzo na usimamizi wa pamoja  wa waraalam wa afya,udhibiti wa magonjwa ya milipuko pamoja na magonjwa ya kuambukiza kama vile Ebola,Mafua makali ya ndege kifua kikuu(TB) na UKIMWI
Kuhusu kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto ,mawaziri wamekubaliana hao wamekubaliana kuongeza juhudi Zaidi ili kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto ndani ya Afrika Mashariki
“Bado Afrika Mashariki hatufanyi vizuri katika afya ya uzazi na mtoto na hivyo kusababisha kutofikia malengo ya kidunia ya Millenia yaliyowekwa,hivyo tuongeze jitihada katika hili”,alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy ameelekeza Tume ya Utafiti wa masuala ya Afya ya  EAC ihamie mapema makao makuu yake mjini hapa kama ilivyokubaliwa kwenye vikao vya baraza la mawaziri  vilivyotangulia
Wakati huo huo Waziri Ummy akiwa nchini humo ameshiriki uzinduzi wa kongamano la Kimataifa la afya ya Sayansi lililofunguliwa na Rais wa Burundi Mhe.Piere Nkurunzinza ambalo limeandaliwa na Kamisheni ya Utafiti wa Masuala ya Afya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Simba yashindwa kulipia ushuru wa Nyasi za bandia

nyasi
Makamu wa Rais wa klabu ya Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kweli suala la taarifa ya nyasi zao bandia kutaka kupigwa mnada, limewashitua sana.
Lakini akawataka mashabiki na wanachama wa Simba kutulia wakati uongozi unapambana katika suala hilo.
“Tokea nyasi hizi zimepita tulifanya juhudi ya kuomba msamaha kwa serikali, unajua nyasi hizi si kwa Simba pekee. Ni kwa kwa jamii yote kwa kuwa tunalenga kuendelea vijana ambao hawatakuwa faida yetu pekee.
“Lakini tumekuwa tukiendelea kupambana kuzitoa, tulishaanza ujenzi wa uwanja na suala la nyasi tu.
“Kuhusiana na taarifa kwamba zinataka kupigwa mnada, kweli linashitua. Unajua kawaida mzigo wako ukikaa bandarini baada ya siku 60, unapewa taarifa ya kupigwa mnada. Tunaendelea kulishughulikia hili,” alisema Kaburu.
Taarifa za Kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart inataka kupiga mnada nyasi bandia za Simba imesambaa kwa kasi leo asubuhi.
Imeelezwa kuwa nyasi hizo zitapigwa mnada leo nyuma ya “The Waterfront Sunset Restaurant and Beach Bar”.
11b0f606-fe04-40b3-9b02-9cd66b5ec220

Azam FC na Ndanda FC kumenyana Jumatano ijayo

azam-fc-vs-ndanda-fc_18csoma4t14vz1wisyt5qazcir

Robo Fainali ya tatu ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup 2016/2017), kati ya Azam FC na Ndanda FC itafanyika Aprili 5, 2017 saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, imefahamika.
Kadhalika, Robo Fainali ya nne ya mwisho ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup 2016/2017), kati ya Young Africans na Tanzania Prisons FC itafanyika Aprili 22, 2017 saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Washindi wa kila mchezo watasonga mbele kwenda Raundi ya Nane ambayo ni Nusu Fainali. Tayari klabu za Mbao na Simba zilitangulia hatua hiyo ya Nusu Fainali.
Mbao FC ya Mwanza nayo imetangulia hatua ya Nusu Fainali baada ya kuilaza Kagera Sugar mabao 2-1 katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera Machi 18, mwaka huu.

Mahakama kuu imetengua hukumu ya Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali

 Image result for peter lijuakali
January 2017, Mahakama ya wilaya ya Kilombero ilimuhukumu kwenda jela miezi sita Mbunge wa jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali (30) kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Mwendesha mashtaka inspekta wa Polisi Dotto Ngimbwa aliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa, akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na mwenzie Stephano Mgata (35) walitenda kosa hilo machi mosi mwaka 2016 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani katika eneo la Kibaoni ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero.

Kufuatia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, Hakimu mkazi katika mahakama ya wilaya ya Kilombero Timothy Lyon aliwatia hatiani washtakiwa hao walipatikana na makosa. Aidha, Hakimu alisema kuwa mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Mbunge ambaye alikuwa na kesi tatu huko nyuma atatumika kifungo cha miezi sita jela kwa kuwa anaonekana kuwa mkosaji mzoefu.

Wednesday 29 March 2017

ZILIZOLETA GUMZO KATIKA MITANDAO YA KIJAMII NA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MAR 30 2017




Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imejizatiti kurudisha thamani ya huduma za bima

B
Kamishna wa Bima, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania Bw. Baghayo Abdallah Saqware akiongea na waandishi wa habari kuhusu mwelekeo wa sekta ya Bima nchini na mikakati ya kuendeleza na kupanua shughuli za bima nchini, leo Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa mamlaka hiyo Bw. Eliezer Rweikiza
B 1
Meneja TEHAMA, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Bw. Aron Mlaka akiwaeleza waandishi wa habari mikakati ya mamlaka hiyo ya kuongeza na kupanua matumizi ya Teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) katika kuboresha huduma zao.  Kushoto ni Naibu Kamishna wa Mamlaka hiyo Bw. Juma Makame. 
B 2
 Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti TIRA Bi. Adelaide Muganyizi akifafanua jinsi Mamlaka hiyo inavyotoa elimu kwa Umma pamoja na  umuhimu wa Bima wakati wa mkutano na waandishi wa habari, leo Jiji Dar es saam. Kushoto ni Naibu Kamishna wa Mamlaka hiyo Bw. Juma Makame.
(Picha na Georgina Misama).

Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imejizatiti kurudisha thamani ya huduma za bima kwa kubadilisha baadhi ya sheria na kanuni za bima  pamoja na kutengeneza mfumo wenye kutoa  tija kwa Wananchi, Serikali pamoja na Kampuni za Bima nchini.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Bima, Baghayo Saqware alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya namna mamlaka hiyo ilivyojipanga kurudisha thamani ya bima kwa wananchi na makampuni ya bima hapa nchini, leo Jijini Dar es Salaam.
Baghayo Saqware amesema kwamba moja ya kanuni na sheria zitakazoboreshwa ni pamoja na kupeleka biashara ya bima (Insurance business – risks) nje ya nchi badala ya kutumia makampuni ya ndani.
“Tutaweka kanuni itakayolazimisha Kampuni za bima hapa nchini kuongeza  mitaji au kutengeneza mfuko wa pamoja au mfumo wa makampuni kushirikina kimtaji ili kuweza kuandikisha na kubakisha sehemu kubwa au biashara yote ya bima nchini,” alifafanua Saqware.
Aliendelea kwa kusema kuwa utawekwa utaratibu wa kisheria utakaohakikisha waingizaji wa mizigo kutoka nje ya nchi wanakatia bima za mizigo yao kupitia kampuni za bima nchini.
Aidha amesema kwamba ikibidi mamlaka hiyo itabadilisha sheria ya bima nchini ili wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi (import  goods) iwe ni lazima kukatia bima nchini  ili kuongeza mapato ya kodi (VAT) pamoja na bima (Premium Levy).
Katika kurudisha thamani ya huduma ya bima kwa wananchi mamlaka hiyo itahakikisha makampuni yanayotoa huduma ya bima yanatoa huduma stahiki  kwa wateja wa bima pamoja na kuhakikish malalamiko ya wateja yanayofikishwa  katika mamlaka husika yanashughulikiwa kwa wakati.
Aidha, katika kupanua shughuli za bima mamlaka hiyo iko katika hatua za mwisho za kukamilisha bima ya kilimo, mifugo pamoja na bima za watu wenye kipato cha chini (Micro-insurance) pamoja na kukamilisha utekelezaji wa sera ya Taifa ya Bima.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe alivyopokelewa

M
 Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Elisante ole Gabriel akiteta jambo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe na wakati waziri huyo alipowasili Ofisini kwake Mjini Dodoma.
M 1
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Naibu Waziri  wa Wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura wakati alipowasili Ofisini kwake Mjini Dodoma.
M 2
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akisalimiana na baadhi ya wakurugenzi na wakuu wa Taaisi zilizo chini ya Wizara yake  wakati alipowasili Ofisini kwake Mjini Dodoma.
M 7
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisini kwake Mjini Dodoma.
M 8
 Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisini za Wizara  Mjini Dodoma.
M 9
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (aliyesimama) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura.
M 10
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura(kushoto) akimkaribisha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) kuzungumza na waandishi wa habari Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel.
M 11
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mikakati yake katika kuiongoza Wizara.
M 13
 Baadhi ya wakurugenzi wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe(hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao alipowasilikatika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma.
M 14
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa Ofisini kwake Mjini Dodoma akitekeleza majukumu mbalimbali ya Wizara.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.

Harrison Mwakyembe: Nitawaunganisha wasanii ili waondoe tofauti zao

  Image result for harrison mwakyembe
Harrison  Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ana mambo mengi ya kufanya kwa sasa, lakini siyo ripoti ya mtangulizi wake, Nape Nnauye, 
Uteuzi wa Nape ulitenguliwa akiwa anatarajia kukabidhi ripoti ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kudaiwa kuvamia kituo cha Clouds Media.
Waziri Mwakyembe amesema hawezi kutoka na kauli za papara na matamko ya haraka haraka ambayo yanaweza kuleta matatizo siku za mbele.
Alisema ripoti ya Nape dhidi ya Makonda siyo kipaumbele kwake bali yapo mambo mengi ya muhimu ya kufanya badala ya kuhangaika na jambo hilo ambalo halijakamilika kisheria. “Nimekuwa naulizwa sana na waandishi wakati naapishwa. Kwanza hiyo ripoti yenyewe sijaiona, lakini hata nikiiona siwezi kuipeleka kwani haijakamilika, maana imehoji upande mmoja,” amesema Mwakyembe.
Mwakyembe amesema akiwa kama mwanasheria kwa mujibu wa ibara ya 13 ibara ndogo ya sita (a) na sheria ya jumla anaheshimu sana kanuni hivyo kitu chochote lazima kiheshimu katiba na haki kwani mtu hawezi kuwa hakimu katika suala lake mwenyewe.
Akizungumzia kuhusu kuboresha wizara yake, amesema atahakikisha anafanya kazi kwa karibu na watendaji wake ili kuifanya wizara hiyo kuwa na maendeleo ya haraka.
Amesema kuna mambo mengi ambayo hatahaikisha anayafanya ikiwa ni pamoja na kuhunganisha wasanii ili kuondokana na tofauti zao na badala yake waunganishe nguvu ya kufanya kazi zao.

Manchester United kumnasa Neymar Jr

Manchester United imepania kuhakikisha inamsajili nyota wa Barcelona, Neymar Jr kipindi cha kiangazi baada ya kuanzisha mazungumzo ya awali.
Hata hivyo, mchezaji huyo amekuwa akionyesha waziwazi mapenzi yake kwa timu yake ya sasa ya Barcelona, jambo ambalo limewafanya Manchester United kuingia mfukoni na kutangaza dau kubwa ambalo litamshawishi Neymar.
Licha ya kwamba Mashetani hao wekundu wa London wametangaza kufanya kufuru ya usajili wa dunia kwa kulipa fedha ya uhamisho wa Pauni 170 ili kuipata huduma yake, lakini mchezaji huyo bado amekuwa akisisitiza kwamba anafurahia maisha akiwa na miamba hiyo ya Hispania.

12 walioteuliwa na CCM kugombea ubunge Afrika Mashariki

CCM imepeleka bungeni majina ya wagombea 12 wa ubunge wa EALA. Wabunge watapiga kura kuchagua wabunge 6 ambapo 3 ni wanaume na 3 wanawake.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Polepole akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam ameeleza kuwa mchakato wa kuwapata wagombea ubunge wa EALA Kamati Kuu imezingatia Uadilifu, Uaminifu, Uzalendo, Uchapakazi, Maarifa ya mgombea na kuiishi Imani ya mwanachama wa CCM