Saturday 28 February 2015

Friday 20 February 2015

INAWEZEKANA KUMALIZA MAUAJI NA UKATILI DHIDI YA ALBINO


Vitendo vya mauaji ya Albino na ukatili wowote unaofanywa dhidi yao ni vitendo visivyokubalika katika jamii yoyote ile. Ni ukatili, ubaguzi na ubinafsi wa hali ya juu ambao haupaswi kuvumiliwa kwa namna yoyote ile.

Wananchi wote wa Tanzania tunapaswa kuonyesha hisia na hasira zetu kali dhidi ya vitendo hivi vya kikatili. Bila kujali imani zetu, itikadi zetu na tofauti zozote za kijamii tunazoweza kuwa nazo lakini sasa kwa UMOJA wetu tupaze sauti kuu kabisa tuseme SASA BASI tusivumilie tena hali hii inayotia uchungu, hasira ma kujenga visasi.

Tukumbuke kwamba sisi sote ni binadamu bila kujali rangi zetu au mataifa yetu. tumetoka katika chimbuko moja tu la Adam na Eva (Hawa). Hakuna sababu ya namna yoyote ile inayofanya binadamu mmoja aishi kinyonge dhidi ya binadamu mwingine.

YAMESEMWA SANA, WALIOKEMEA WALIKEMEA SANA, WALIOONYA WAMEONYA SANA. SASA TUUNGANISHE NGUVU KAMA TAIFA TUSEME "HAPANA" UVUMILIVU UMEFIKA KIKOMO.

Serikali na mamlaka zake husika zifanye kazi zaidi na kwa kasi zaidi ya ile ya mwanzo. Hatua za makusudi za dharula zichukuliwe. Sheria dhidi ya uhalifu wa aina hii zitekelezwe mara moja dhidi ya wahusika pasipo kuwaonea huruma yoyote.

TUMECHOKA KUSIKIA VITENDO VYA KIFEDHULI KAMA HIVI NDANI YA TAIFA LETU

Sunday 15 February 2015

Tanzania na Kenya zimalize mgogoro

Bendera ya Kenya na Tanzania zikiwa pamoja 

Nyakaho Marungu Aongoza Kitaifa Matokeo Kidato Cha Nne

Mwanafunzi aliyeongoza kwa kufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne kitaifa mwaka jana, Nyakaho Marungu akipongezwa na mama yake Celestina Maro, nyumbani kwao Kitunda Dar es Salaam jana, muda mfupi baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kutangaza matokeo ya mtihani huo