Tuesday 30 August 2016

Lowassa: kitendo cha kukamatwa na Jeshi la Polisi kimenimarisha na kumpa nguvu zaidi za kudai Demokrasia.

 
Aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowassa ambaye ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CHADEMA, amesema kitendo cha kukamatwa na Jeshi la Polisi yeye na viongozi wenzie wakati wakifanya mkutano jana, kimemuimarisha na kumpa nguvu zaidi za kudai Demokrasia.
Katika waraka wake alioutoa kwa Waandishi Mapema leo, Lowassa amedai anafurahishwa na jinsi wanachama wa chama hicho wanavyowaunga Mkono.

 
Jana jioni baadhi ya viongozi wa CHADEMA walikamatwa na Polisi kwa kosa la kukaidi amri ya kutokufanya vikao vya ndani wala nje ya vyama vya siasa hadi hapo muongozo mwengine wa kiusalama utakapotolewa

No comments:

Post a Comment