
Rais mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki, amepangiwa kufanyiwa upasuaji kesho katika hospitali aliyolazwa nchini Afrika Kusini ili kuondoa damu iliyoganda kwenye mshipa mdogo wa damu uliopo sehemu ya shingoni.
Kwa mujibu wa chanzo kutoka Afrika Kusini madaktari wa hospitali hiyo ya Netcare Sunninghill Jijini Johannesburg walibaini damu hiyo iliyoganda katika eneo ambalo ni salama kitabibu.
Kitendo cha kuganda damu kwenye mishipa ya damu huwa ni jambo hatari sana, iwapo kitatokea kwenye maeneo ya mwili wa binadamu kama ya kwenye ubongo, moyo pamoja na mapafu.
Hata hivyo kiujumla vyanzo kutoka Afrika Kusini vimesema hali ya Kibaki kwa sasa ni zuri zaidi ikilinganishwa na wakati alipoondoka Kenya, ambapo kwa sasa anaweza kutembea mwenyewe.
No comments:
Post a Comment