Na Ally Daud-Maelezo
Idadi ya mauzo katika soko la hisa
Dar es salaam (DSE) imekua kwa asilimia 57 na kufikia shilingi bilioni
3.3 kutoka shilingi bilioni 2.1 wiki iliyopita kutokana na ukubwa wa
idadi ya mauzo.
Katika taarifa iliyotolewa na
Afisa Mwandamizi wa Masoko DSE Bi. Mary Kinabo imesema kuwa idadi ya
mauzo hayo yamekua kutokana na kupanda kwa idadi za hisa zilizouzwa
kutoka shilingi milioni 1.6 hadi kufikia shilingi milioni 2.2.
Aidha taarifa hiyo iliongeza kuwa
Benki ya CRDB imeendelea kuongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na
kununuliwa kwa asilimia 49 ikifuatiwa na Soko la hisa DSE ikiwa na
asilimia 43 na ya tatu ni kampuni ya Bia nchini TBL yenye asilimia 4.
Taarifa hiyo iliendelea kueleza
kuwa ukubwa wa mtaji wa soko umepanda kwa asilimia 0.67 na kufikia
shilingi trilioni 23.4 kutoka trilioni 23.2 wiki iliyopita na ukubwa wa
mtaji wa makampuni ya ndani umebaki kwa shilingi trilioni 8.4.
Mbali na hayo taarifa hiyo
imeeleza kwamba licha ya mauzo kupanda lakini viashiria vya soko katika
sekta ya viwanda vimeshuka kwa alama 19.47 baada ya bei za hisa kutoka
TBL kushuka kwa asilimia 0.66 huku sekta ya huduma za kibenki kupanda
kwa alama 29.89 kutokana na kupanda kwa kaunta ya DSE na NMB.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa
viashiria vya soko katika sekta ya huduma za kibiashara wiki hii imebaki
kwenye hali yake ya wiki iliyopita baada ya bei za hisa za Swissport
kubaki kwa shilingi elfu 3.543.
No comments:
Post a Comment