Friday 26 August 2016

Ufahamu juu ya baraza ya vyama


Image result for jaji francis mutungi
Kumekuwa na changamoto  kwa baadhi ya vyombo vya habari kutokuwa na ufahamu mzuri kuhusu Baraza la vyama vya siasa na majukumu yake kisheria
Baraza la Vyama vya Siasa limeanzishwa chini ya kifungu cha 21B cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 ikiwa ni jukwaa la viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kukutana mara kwa mara kujadiliana masuala yanayohusu demokrasia ya vyama vingi na siasa hapa nchini kwetu.
Kila chama cha siasa kinawakilishwa na viongozi wawili wa ngazi kitaifa katika Baraza la Vyama vya Siasa, ambapo kiongozi mmoja anapaswa kutoka Tanzania Bara na mwingine Zanzibar. Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti wa Baraza huchaguliwa miongoni mwa wajumbe wa Baraza. Baraza la Vyama vya linaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za zilizotungwa na Baraza.
Baraza la vyama vya siasa lina majukumu yafuatayo:-

 
1.    Kumshauri msajili wa vyama vya siasa kuhusu migogoro baina ya vyama vya siasa;
2.    Kumshauri Msajili wa vyama vya siasa kuhusu masuala yenye masilahi ya kitaifa yanayohusu vyama vya siasa na hali ya siasa nchini;
3.    Kuishauri Serikali kupitia Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu kutungwa, marekebisho na utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa na sheria nyingine zinazohusu vyama vya siasa;
4.    Kushauri kuhusu uratibu wa shughuli za vyama vya siasa; na
5.    Kumtaarifu Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu masuala yoyote yanayohusu utendaji wa chama chochote cha siasa.
Kamati ya uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa inaundwa na Mwenyekiti wa Baraza, Makamu Mwenyekiti wa Baraza, wenyeviti wa kamati nne za Baraza na katibu wa Baraza.

No comments:

Post a Comment