Monday 29 August 2016

Tahadhari ya kiafya yatolewa kupatwa kwa jua

Tukio la kupatwa kwa jua

Tahadhari imetolewa kwa wakazi wa mikoa ambayo itashuhudia kupatwa kwa jua kuwa kutazama jua moja kwa moja bila kutumia kifaa chochote kunadaiwa kuwa na madhara kwa mtazamaji kutokana na mionzi ya jua hilo.
Kupatwa kwa jua kunatarajiwa kutokea katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ya Njombe wilaya ya Wang'ing’ombe katika kijiji cha Litundu, Mbeya wilayani Mbarali katika kijiji cha Mpungarelini na mkoani Katavi ambako kupatwa kwa jua kutaonekana vizuri kwa zaidi ya asilimia 97.

Tahadhari hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani humo ikiwa zimebaki siku chache kutokea kwa tukio hilo la kihistoria.

Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa kuna jitihada mbalimbali zinazofanywa na halmashauri ya Waning'ombe kwa ajili ya kuweza kupata vifaa mahususi kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo bila kuacha madhara yoyote.

Tukio hilo la kupatwa kwa jua lilizinduliwa Julai 10 mwaka huu katika kijiji cha Litundu kwa mkoa wa Njombe ambapo macho ya dunia nzima kitalii yatatazama katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment