Tuesday 30 August 2016

Ramos ashtushwa kuachwa kwa Casillas timu ya taifa ya Hispania

Beki kisiki wa Real Madrid, Sergio Ramos amesema ameshitushwa kuona kipa mkongwe wa Hispania, Iker Casillas hakuitwa kwenye kikosi hicho.
Casillas, hivi karibuni ameisaidia FC Porto kusonga mbele hadj kuingia kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ramos amesema amekuwa akizungumza na Casillas mara kwa mara, lakini kikubwa ni kukaa na kushirikiana na kocha.

“Lazima tuamini mipango ya kocha hats kama suala hilo linasumbua. Lakini kila mmoja wetu ameshituka,” alisema.


“Pia tutaendelea kusubiri kwa kuwa itafikia sikh, uamuzi utabadilishwa au vinginevyo. Ila kwa sasa, tutapambana kwa ajili ya taiga letu,” alisema Ramos ambaye alicheza kwa ushirikiano mkubwa na Casillas wakati akiwa kips wa Madrid, pia nahodha wake timu ya taifa ya Hispania.

No comments:

Post a Comment