Wednesday 31 August 2016

Athari za chumvi katika mwili wa bindamu

 Image result for chumvi ya kula
Chumvi ni kiungo ambacho haipiti siku bila mtu kukitumia kutokana na uwezo wake wa kukifanya chakula kuwa radha nzuri katika ulimi.
Imeelezwa kuwa mbali ya kuwa umuhimu huo lakini kula chumvi vyingi kunasababisha madhara mengi kwa afya ya binadamu.
Chumvi inapandisha shinikizo la damu. Shinikizo la juu la damu (presha) ni sababu kubwa ambayo husababisha la kiharusi(stroke),kusimama kwa moyo,shambulio la moyo na magonjwa mengine mengi ya moyo kote duniani.

Kuna ushahidi wa kutosha wa kitafiti kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya ulaji wa chumvi kwa wingi na kansa ya tumbo, osteoporosis(hali ya mifupa kuwa rahisi kufunjika na tete kutokana na upungufu wa Kalsiamu na vitamini D),mawe ya figo,ugonjwa wa figo na mwili kupoteza maji.

Chumvi inaweza pia kuongeza dalili za pumu, magonjwa na ugonjwa wa kisukari.

Kiasi kidogo cha chumvi ni muhimu kwa afya zetu.Watu wazima wanahitaji chini ya gramu1(kijiko kidogo cha chai) kwa siku na watoto wanahitaji kidogo zaidi.

Watu wengi tunakula zaidi ya gramu 8 kwa siku za chumvi ambayo ni nyingi maradufu ya kiwango cha juu kinacho shauriwa cha gramu 6 kwa siku hivyo kutuweka katika hatari zaidi ya kukumbwa na magonjwa yaliyotajwa.

Punguza ulaji wa chumvi il uweze kupunguza hatari ya kupata shinikizo la damu na hatari ya magonjwa mengi. Ukiweza kupunguza na kufikia gramu 3 kwa siku basi unajiweka katika nafasi nzuri kiafya.

No comments:

Post a Comment