Sunday 28 August 2016

Zaza atua Westham United

Mchezaji raia wa Italia na klabu ya Juventus, Simone Zaza amesajiliwa na klabu ya Westham kwa mkopo wa muda mrefu. Mshambuliaji huyu anakuwa mchezaji wao wa 11 kumsajili na anafikisha kiwango cha fedha za usajili zilizotumika na West Ham kufika paundi milioni 60.

Bilic kocha wa West Ham amekuwa akijaribu kuhakikisha timu yake inabaki katika mstari waliomalizia msimu uliomalizika. West Ham wameshasajili aina ya Ayew na Feghouli ambao tayari wanauguza majeraha huku pia eneo la ushambuliaji likiwa lina upungufu ikiwa pamoja na Andy Caroll kuumia.

Aidha taarifa zinasema Ener Valencia naye anaweza kuondoka klabuni hapo. Dili la Zaza litaigharimu West Ham kiasi cha paundi milioni 5 huku pia wakiwa na uwezo wa kuchagua kumsajili baada ya mkopo kwa kiasi cha paundi milioni 20.

No comments:

Post a Comment