Saturday 31 December 2016

YALIOTUFIKIA MAGAZETINI LEO JUMAPILI JAN O1 2017


 

Fofam-media inawatakia kheri ya mwaka mpya 2017 kwa kuendelea kusoma Blog hii na kupata huduma za Sare za Shule Mahoteli na mambo ya ushauri

No automatic alt text available.

Talaka na Gardner ni moja ya mambo 4 anayoshukuru Lady Jaydee mwaka 2016

Lady Jaydee ameitaja talaka yake kutoka kwa aliyekuwa mume wake, Gardner G Habash, ni miongoni mwa mambo 4 anayoshukuru zaidi kwa mwaka 2016.
Jide ametumia Instagram kuyataja mambo hayo huku la nne akielezea kwa kuweka picha ya cheti cha ndoa na talaka hiyo kutoka kwa mtangazaji huyo wa Clouds FM.
Kwenye post hiyo pia Jide amezungumzia kwa mara ya kwanza video maarufu ya mwaka huu iliyomuonesha Captain akijigamba kumko*oza staa huyo kwa zaidi ya miaka 10.
“Sitegemei tena kauli za nilikufanyaje sijui miaka kadhaa, au emoji zisizo eleweka. Utoto huooooooo . Mtu aki move on hana haja kufanya utoto wote huo , uki move on hujali chochote,” ameandika Jide.
 

Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa amewaasa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza nchini kuzingatia kuwa utendaji wao wa kazi za kila siku

timi
Na Lucas Mboje, Dar es Saam
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa(pichani) amewaasa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza  nchini kuzingatia  kuwa utendaji wao wa kazi za kila siku uende sambamba na kasi ya Serikali ya Awamu ya tano ili kuleta ufanisi unaotarajiwa.
KAIMU Kamishna Jenerali, Dkt. Malewa ameyasema hayo jana wakati wa Baraza la Kufunga Mwaka 2016 na kuukaribisha Mwaka 2017 lililowahusisha baadhi ya Maafisa na Askari kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani pamoja na Magereza ya Mkoa wa D’Salaam.
Aidha, amewataka Maofisa na Askari wa Jeshi hilo kudumisha nidhamu wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kazi  ikiwemo kutekeleza mara moja Amri mbalimbali zinazotolewa na Viongozi wao wa Jeshi.
“Kila mmoja wenu atimize wajibu wake katika eneo lake la kazi kwa bidii, ari na moyo wa kujituma ili kuliwezesha Jeshi letu kupata ufanisi unaotarajiwa”. Alisisitiza Kaimu Jenerali Dkt. Malewa.
Wakati huo huo Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa  pia ametumia fursa hiyo kuelezea baadhi ya mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwa Mwaka uliopita 2016 ambapo Jeshi la Magereza limeweza kupata jumla ya leseni 102 za uchimbaji wa madini ya ujenzi kama vile chokaa, mawe, kokoto, mchanga na Murram katika maeneo mbalimbali ya magereza. Pia katika mwaka 2016 Jeshi limeweza kujenga nyumba 129 kwa njia ya kujitolea ambapo nyumba 231 zipo katika hatua mbalimbali ya ukamilishaji.

Aidha, Ujenzi wa nyumba 320 za makazi ya askari katika eneo la Gereza Ukonga maandalizi ya ujenzi yanaendelea na ujenzi wa nyumba hizo ni kufuatia ziara ya Rais Magufuli  Novemba 29 mwaka huu  ambapo alipokea taarifa ya uhaba wa nyumba za kuishi askari wa jeshi hilo na akaagiza Jeshi la Magereza lipatiwe Tsh. bilioni 10 haraka ili kupunguza tatizo hilo.
Shirika la Magereza na Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PPF wameingia Makubaliano ya Mkataba wa ubia katika mradi wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha kusakata ngozi pamoja na uwekezaji wa mashine za kisasa za kutengnezea bidhaa za ngozi katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Karanga, Moshi.
Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga kimepata Ithibati na hivyo kuwa na hadhi ya kuwa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji na mapema mwakani kinatarajia kudahili wanafunzi 30 katika fani ya Taaluma ya Urekebishaji ngazi ya cheti. 
Pamoja na Mafanikio hayo, Kaimu Kamishna Jenerali Dkt. Malewa ameelezea changamoto mbalimbali zinazolikabili Jeshi hilo ikiwemo ufinyu wa bajeti, makazi duni ya maofisa na askari, uhaba wa vitendea kazi, ukosefu wa pembejeo pamoja na madeni ya wabuni na watumishi wa jeshi hilo.

Solo Thang ajitetea kuhusu Chid Benz

SoloThang
Msanii mkongwe wa Hip Hop Bongo Solo Thang amejitetea kuhusu uamuzi wake wa kurekodi video akiwa na Chid Benz na kusema alichokifanya si 'kumchoresha' bali ni kumfariji na kutomnyanyapaa maana Chid mwenyewe ndiye aliyeomba kitu hicho kifanyike
Baadhi ya wadau wa muziki wa Bongo Fleva walitoa kauli zilizoonesha kulaumu kurekodiwa kwa Chid Benz akiwa katika hali ya kudhoofika wakidai kuwa ni kumdhalilisha.
Kamera ya eNewz ilmtafuta Solo Thang na kumuuliza nia yake ya kupost video hiyo ilikuwa ni nini? Solo alisema kuwa hakukusudia kumchoresha Chid Benz bali Chidi mwenyewe ndiye aliyetaka kurekodiwa video baada ya kukutana naye.

Alikiba ashinda tuzo Ufaransa, awabwaga Davido, Sarkodie, Yemi Alade na wengine

Fresh kutoka kushinda tuzo ya video bora ya mwaka (Aje) kwenye tuzo za Soundcity MVP za Nigeria, Alikiba ameongeza nyingine wikiendi hii.
Mkali huyo ameshinda tuzo ya Chaguo la Watu (Prix du Public) kwenye tuzo za Ufaransa za Wana Music Awards zilizotolewa Ijumaa hii.
“Hii ilikuwa ni tuzo pekee ambayo ilikuwa wazi kwa watu kupiga kura mwaka huu na msisimko uliozalishwa na tuzo hii umevuka matarajio yetu kwa kuwa na majadiliano zaidi ya 30,000 kwenye matangazo yetu kupitia mitandao ya kijamii,” waandaji wa tuzo hizo Wana Corp wameandika kwenye tovuti yao.
“Mshindi, Alikiba wa Tanzania aliweza kujikusanyia jamii kubwa ya mashabiki, ‘mashabiki damu wa Alikiba’ kuweza kuuchukua ushindi. Mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwa Alikiba akiwa na sahihi katika label kubwa ya Sony, kushinda tuzo ya kimataifa ya MTV Europe Music Awards kama ‘Best African Act’ na yote kwa yote kuwa na moja ya video bora za mwaka na Aje,” wameongeza.
“The main information of this “Public Prize” is to see that our small website created in France can have links with a country like Tanzania thanks to Alikiba. Just for that, we say thank you to all those fans who have mobilized: a new link between Paris and Dar-Es-Salaam has been formed,” wamesisitiza.

Kombe la Ligi ya Comoro.

como
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania bara Yanga ina mataji mawili ya Ligi Kuu Bara na lile la FA kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini wapinzani wao Ngaya Club ya Comoro wikiendi iliyopita walitwaa taji la nne.
Ikicheza dhidi ya Ngazi Club ya Anjuani Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Hombo uliopo Mutsamudu kisiwani Ngazija, Ngaya ilishinda mabao 2-1 na kutwaa ubingwa wa Kombe la Ligi ya Comoro.
Mataji mengine ambayo Ngaya imetwaa msimu huu ni Ligi Kuu ya Ngazija, Kombe la Ligi Ngazija na Ligi Kuu ya Comoro. Ngaya inafundishwa na Kocha Lucien Sylla Mchangama mwenye Leseni C ya ukocha ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf). 
Ngaya Club inapatikana katika mji mdogo wa Mde Bambao unaopatikana mita 400 kutoka Kusini mwa Mji Mkuu wa Comoro, Moroni. Mechi ya fainali ya Kombe la Ligi ilichezwa kwenye Uwanja wa Hombo uliopo Mutsamudu, Kisiwani Anjuani.
Comoro ni nchi inayoundwa na visiwa vinne ambavyo ni Ngazija, Anjuani, Moheli na Mayotte. Kila kisiwa hucheza ligi yake kisha mabingwa hukutana kucheza ligi ya kupata bingwa wa Comoro katika Ligi Kuu na Kombe la Ligi.
Febuari 11, mwakani Yanga inatarajiwa kucheza na Ngaya Club nchini Comoro mechi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kisha kurudiana Jumamosi ya Februari 18, mwakani jijini Dar es Salaam.

Simba kesho kuivaa Taifa Jang’ombe

simba-day-5
Kinara wa Ligi Luu Bara, Simba inaondoka leo saa 1:00 asubuhi kwenda Zanzibar kushiriki Kombe la Mapinduzi ambalo  limeanza jana, timu hiyo imetamba kuendeleza wimbi lake la ushindi kama ilivyo katika Ligi Kuu Bara.
Katika ligi kuu, Simba inaongoza ikiwa na pointi 44 ikifuatiwa na Yanga yenye 40 huku Azam FC ikiwa ya tatu na pointi 30.
Simba ipo Kundi A na timu za Taifa Jang’ombe, URA, KVZ, Jang’ombe Boys, inatarajiwa kucheza mechi yake ya kesho Jumapili dhidi ya Taifa Jang’ombe saa 2:30 usiku kwenye Uwanja wa Amaan, wakitanguliwa na mechi kati ya KVZ na URA saa 10:00 jioni uwanjani hapo.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amesema: “Tunataka kuendeleza kasi yetu ya ushindi kwenye michuano hii ya Mapinduzi, hatutazubaa, tutaifunga kila timu.
“Pia tumepanga kuwatumia wachezaji ambao hatuwatumii sana kwenye ligi ili wapate nafasi ya kuboresha viwango vyao.”
Kati ya wachezaji ambao hawapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Simba ni Laudit Mavugo, Frederick Blagnon, Hamad Juma, Peter Manyika na Novalty Lufunga.
Mayanja alisema wamepanga kutengeneza mzunguko wa wachezaji katika michuano hiyo na watatoa kipaumbele kwa wachezaji wa benchi.
“Tulichokipanga kama benchi la ufundi ni kuwapa nafasi ya kucheza wachezaji wetu wa akiba ambao hawakutumika sana, tunataka kuona uwezo wao wa ndani ya uwanja baada ya kukosa nafasi ya kucheza.

Bocco awapa mkono wa mwaka mpya mashabiki Azam FC

boe
Nahodha wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’, amewatakia mashabiki wa timu hiyo kheri ya mwaka mpya ‘2017’ unaoanza leo saa 6.00 usiku huu huku akiwashukuru kwa sapoti yao waliyoionyesha mwaka huu.
Bocco ametoa kauli hivi karibuni mara baada ya kumalizika kwa mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) dhidi ya Tanzania Prisons walioifunga bao 1-0, huku akifanikiwa kutupia bao hilo pekee lililorudisha morali ndani kikosi hicho baada ya kutofanya vizuri kwenye mechi mbili za ufunguzi wa mzunguko wa pili walipocheza ugenini na African Lyon (0-0) na Majimaji (1-1).
“Kwanza tunawashukuru mashabiki wetu kwa uvumilivu waliouonyesha, kwa sapoti waliotupa katika kipindi chote kigumu tulichopitia, kama wachezaji na timu kwa ujumla tunawaomba waendelee kuwa na moyo huo huo na pia tunawatakia kheri ya mwaka mpya (2017) na wamalize mwaka huu vizuri, tuendelee kuwa pamoja ili kuisaidia timu yetu iweze kufanya vizuri,” alisema Bocco wakati akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz
Bocco ambaye ameipatia mafanikio makubwa Azam FC kwa mabao yake muhimu tokea timu hiyo ikiwa madaraja ya chini hadi kupanda Ligi Kuu mwaka 2008, aliendelea kusema kuwa wamepitia changamoto nyingi sana kwa mwaka huu unaoisha huku akidai kuwa wamejifunza kupitia hayo na wanachoangalia kwa mwaka mpya ni kuipeleka mbele zaidi timu hiyo ili kufikia mafanikio.
“Changamoto zilikuwepo nyingi na ni sehemu ya maisha, sisi kama timu tunajua mpira unachangamoto zake na tumezipokea kama binadamu na sisi wachezaji changamoto iliyokuwa katika kazi yetu haikuwa ndogo na tunamshukuru Mungu kwa kuweza kutusaidia tumeweza kupigana nazo na hatukuweza kukata tamaa, kikubwa tunachofanya hivi sasa ni kuangalia mbele zaidi ili kuipatia timu mafanikio kwa mwaka unaokuja,” alisema.
Azam FC mbali na kuwa bingwa mtetezi wa michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup), inamaliza mwaka huu ikiwa imefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani pamoja na taji la Ngao ya Jamii baada ya kuichapa Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-1 kufuatia sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 90 za mchezo huo uliofungua pazia la ligi msimu huu.
Ujio wa Mapinduzi Cup
Wakati kikosi cha timu hiyo kikielekea mchana wa leo Jumamosi visiwani Zanzibar kwenda kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi, Bocco amesema kuwa wao kama wachezaji wanaenda kushindana na hatimaye kurejea na ubingwa wa michuano hiyo.
“Mashindano ya Mapinduzi si mageni kwa Azam FC, michuano hiyo si mepesi ni migumu, sisi kama wachezaji tunaenda kushindana naamini ni sehemu moja ya msimu huu ambayo tukiweza kuchukua kombe itakuwa ni faraja kwa klabu na mashabiki wetu pamoja na sisi wachezaji, tukitoka huko hata tukirudi kwenye ligi tutakuwa na morali nzuri ya kuendeleza ushindi kwenye ligi, michuano ya FA na Kombe la Shirikisho Afrika,” alimalizia Bocco.

Ngasa kuanza ligi leo, Mbeya City ikiivaa Mbao

Image result for mrisho wa ngasa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi mbili kwenye viwanja tofauti.
Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga wenyeji Mwadui wataikaribisha Kagera Sugar ya Bukoba, wakati Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, wenyeji Mbeya City watawakaribisha Mbao FC.
Mchezo kati ya Mwadui na Kagera unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua ukikutanisha timu jirani kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa zinazoundwa na wachezaji wanaofahamiana vizuri.
Mjini Mbeya, wenyeji wanatarajiwa kumtumia kwa mara ya kwanza mchezaji wao mpya, Mrisho Ngassa waliyemsajili mwezi huu katika dirisha dogo la usajili kutoka Fanja ya Oman.
Ngassa, kiungo wa zamani wa Azam, Simba na Yanga alishindwa kucheza mechi mbili za awali za Mbeya katika mzunguko wa pili kutokana na kuchelewa kwa Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).

Aidha, Mbeya City pia inatarajiwa kumtumia kwa mara ya kwanza mshambuliaji wake, Zahoro Pazi ambaye pia alikwama kucheza kutokana na kuchelewa kwa ITC yake.

Ligi Kuu itaendelea kesho kwa michezo miwili, Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Toto Africans wataikaribisha Stand United na Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, African Lyon wataikaribisha JKT Ruvu.

Tathmini ya Uhalifu Dar kwa Mwaka Mmzima wa 2016

KIKOSI cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imekamata jumla ya watuhumiwa 13,626 na kuwafikishwa mahakamani kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo dawa za kulevya na ujambazi wa kutumia silaha kwa kipindi cha mwaka mmoja wa 2016.
Aidha, hali ya uhalifu wa kutumia silaha katika jiji la Dar es Salaam umepungua, ukilinganisha na mwaka uliopita wa 2015 na matukio yanayoongezeka kwa wingi ni ya ubakaji na ulawiti.
Akitoa tathmini ya mwaka mmoja, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha yamepungua kutoka 204 mwaka jana hadi 127 mwaka huu.
Idadi hiyo ni pungufu ya matukio 77, sawa na asilimia 37.7 huku matukio ya kutumia nguvu yamepungua kutoka 1,181 mwaka jana hadi 874 sawa na asilimia 26.
Kamishna Sirro alifafanua kuwa matukio ya mauaji, yamepungua kwa asilimia 11 ukilinganisha na mwaka jana, ambapo kulikuwa na jumla ya matukio 327 wakati kwa mwaka huu ni matukio 291 pungufu ya matukio 36.
Alisema matukio ya ubakaji, yameongezeka kutoka 972 mwaka jana hadi 1030 mwaka huu, sawa na asilimia sita wakati matukio ya ulawiti yameongezeka kutoka 310 mwaka jana hadi 383 mwaka huu sawa na asilimia 23.5.
‘’Kwa matukio ya ubakaji yaliyoongezeka ni 58 na ulawiti matukio yaliyoongezeka ni 73. Lakini wizi wa watoto umepungua kutoka 26 mwaka jana hadi matukio 19 mwaka huu sawa na asilimia 27,’’ aliongeza.
Kwa mujibu wa Sirro, matukio ya uvunjaji yamepungua kwa asilimia 5.7 ambapo kwa mwaka jana kulikuwa na matukio 5,677 na mwaka huu matukio 5,355 sawa na upungufu wa matukio 322.
Kwa upande wa wizi wa magari, umepungua kwa asilimia 18.1 kutoka matukio 392 hadi 321 mwaka huu huku wizi wa pikipiki ukipungua kutoka pikipiki 2,644 mwaka jana hadi 2,191 ambapo matukio 453 yamepungua sawa na asilimia 17.1.
Wizi wa mifugo umepungua kutoka 197 mwaka jana hadi 163 mwaka huu sawa na asilimia 17.3 ikiwa ni pungufu ya matukio 34.


UFC 207: Amanda Nunes amchakaza Ronda Rousey ndani ya sekunde 48

 Ronda Rousey hakuweza kuhimili makonde mazito toka kwa Mbrazil, Amanda Nunes aliyemchakaza kwenye pambano la UFC 207 la ubingwa wa bantamweight, lililofanyika Las Vegas, asubuhi ya Jumamosi kwa saa za Afrika Mashariki.
Pambano lilianza kwa Nunes kurusha makonde mfululizo kwa Rousey yaliyomwelemea na kuchakazwa ndani ya sekunde 48 tu za pambano hilo na kumfanya mwamuzi, Herb Dean asitishe pambano.

Rousey hakuamini kama angeweza kudundwa katika muda huo mfupi na kuna wakati alitaka kuanguka wakati amesimama kutafakari kilichotokea ndani ya sekunde chache tu
.
 Hilo linakuwa pigo jingine kubwa katika career ya bondia huyo ambaye mwaka uliopita alipoteza tena pambano jingine dhidi ya Holly Holm kwa fedheha kubwa.
 Swali ambalo watu wengi wanajiuliza sasa ni iwapo Ronda ataendelea tena ngumi ama ataamua kustaafu kabisa.


Friday 30 December 2016

YALIOJIRI LEO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DEC 31 2016

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijwD1zwM9FS3znoJfpy0CUntJZitQt2zscrUH-UOfoBYM28K7Q35yTVgMTEhyDkz9KTUt8ZK1YeJCmf6wVOaEKtq3iQTj2KNmVQe8bNu4J1nfBzIAg09A5ZKIq2hdbDQ0EN63HSUMlL0pR/s1600/01.PNG


Usiumize kichwa kutafuta utapata wapi mahitaji haya jibu lako lipo hapa

Habari Picha

my
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Ruangwa wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya  hiyo kuhutubia mkutano wa hadhara Desemba 30, 2016.
mty
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya  Ruangwa Desemba 30, 2016.
mgu
  Baadhi ya wananchi wa mji wa Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipohutubia mkutano wa hadhara  kwenye uwanja wa Ofisi  ya CCM ya wilaya hiyo mjini Ruangwa Desemba 30, 2016.
mggra
    Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa wakigalagala kuonyesha furaha katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa, Desemba 30, 2016.
mggpo
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya mkeka kutoka kwa wananwake wa Ruangwa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Sheria ya Taifa ya Uchaguzi

guyu
Kwa mujibu wa kifungu cha 40 (6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ilipokea Rufaa moja ya kupinga Uteuzi wa Mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF) katika Uchaguzi Mdogo wa Bunge Jimbo la Dimani – Zanzibar.
Rufaa hiyo ilikatwa na Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bwana Juma Ali Juma akipinga Maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dimani aliyemthibitisha Mgombea wa Chama Cha Wananchi (CUF) Bwana Abdul Razak Khatib Ramadhani kuwa ni mgombea halali.
 Rufaa hiyo ilikuwa na sababu mbili ambazo ni:- (i) Hakurudisha Fomu za Uteuzi kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sheria na (ii) Hakudhaminiwa na Chama cha Siasa kugombea Ubunge. Katika kikao chake cha leo tarehe 30 Desemba, 2016, Tume imepitia Rufaa hiyo na kuona sababu zilizotolewa na mkata Rufaa hazina nguvu ya kisheria, kwa kuwa, Mgombea wa CUF amerudisha Fomu za Uteuzi kwa mujibu wa sheria na taratibu. Pia, Fomu zake za Uteuzi zimesainiwa na kugongwa muhuri wa Katibu wa Wilaya ya Magharibi B. Kwa mantiki hiyo, Tume imekubaliana na Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dimani – Zanzibar.  Hivyo, Mgombea wa CUF amekidhi vigezo na uteuzi wake ni halali na aendelee na kampeni za kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo.
Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume imepokea Rufaa tatu; kutoka Kata ya Kijichi – Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam, Kata ya Misugusugu – Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mkoa wa Pwani na Kata ya Ihumwa – Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Mkoa wa Dodoma.
Kata ya Misugusugu Halmashauri ya Mji Kibaha, Rufaa ilikuwa ni ya Mgombea wa CHADEMA Bwana Gasper Melkiory Ndakidemi dhidi ya mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Bwana Bogasi Hussen Ramadhani.
Katika Kata ya Kijichi, Rufaa ilikuwa ni ya mgombea wa CUF Bi. Khadija Abdallah Shamas dhidi ya mgombea wa CHADEMA Bwana Fredrick Felician Rugaimukamu.
Kata ya Ihumwa Rufaa ilikuwa ni ya Mgombea wa CHADEMA Bwana Magawa Edward Juma dhidi ya maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi.
Tume katika kikao chake cha leo tarehe 30 Desemba, 2016 imepitia Rufaa zote na imeamua ifuatavyo:
Rufaa ya mgombea wa CHADEMA Bwana Gasper Melkiory Ndakidemi katika Kata ya Misugusugu Halmashauri ya Mji Kibaha na ya mgombea wa CUF Bi. Khadija Abdallah Shamas katika Kata ya Kijichi,  hazina mashiko ya kisheria na zimekataliwa.  Hivyo, Tume inakubaliana na Maamuzi ya Wasimamzi wa Uchaguzi wa Halmashauri hizo na wagombea waendelee na Kampeni kwa mujibu wa Ratiba.
Kuhusu Rufaa ya Mgombea wa CHADEMA kutoka Kata ya Ihumwa, Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Tume, imepokea barua ya Msimamizi wa Uchaguzi, Manispaa ya Dodoma, ikiwa imeambatishwa na barua ya Mgombea wa CHADEMA kuiondoa Rufaa yake na kwamba anakubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ambayo yalimuengua. Pia, leo Tume imepokea barua za kujitoa Ugombea za wagombea wa CHADEMA na ACT – WAZALENDO katika Kata ya Ihumwa. Kwa maana hiyo Rufaa iliyokuwa imekatwa na mgombea wa CHADEMA Kata ya Ihumwa imeondolewa kwa kuwa mkata Rufaa ameiondoa na amejitoa ugombea kabla haijasikilizwa.
Mwisho, Tume inavisisitiza Vyama vya Siasa, Wagombea na Wananchi wote wa maeneo yenye Uchaguzi Mdogo kufanya Kampeni za kistaarabu kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Maadili ya Uchaguzi.
Imetolewa na:-
Jaji Mkuu (Mst. Znz) Hamid M. Hamid
MAKAMU MWENYEKITI
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
30/12/2016

Barakah The Prince ataja anachokiona kwenye label ya WCB

Barakah The Prince ameisifia label ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz na kudai kuwa iko wazi inafanya vizuri.
Alikuwa akizungumza na mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
“Wapo vizuri kwasababu wana empire yao, wana mashabiki wao wanafanya muziki wana mashabiki. Mtu yeyote ambaye yupo na empire yake na mashabiki wake ina maana anafanya kazi nzuri,” alisema muimbaji huyo.
“Kwahiyo wanajitahidi kufanya kazi nzuri na kuufikisha muziki sehemu,” aliongeza.

Hivi karibuni hitmaker huyo wa Siwezi alidai kuanzisha label yake mwenyewe iitwayo BANA na wasanii wa kwanza walio chini yake ni Lord Eyez na Naj.

Makubaliano ya kusitisha vita Syria yatekelezwa

 Iwapo mpango huo utafanikiwa licha ya visa vichache vya ghasia ,mazungumzo ya amani yataanza kufanyika nchini Kazakhstan
Makubaliano ya kusitishwa mapigano kote nchini Syria yameanza kutekelezwa.
Mapigano baina ya vikosi vya serikali na vile vya waasi, yamesitishwa kwingi lakini kuna ripoti kuwa yanaendelea kwa kiwango kidogo katika sehemu chache tu.
Hii ni kwa sababu makundi mengine hayajashirikishwa kwenye makubaliano hayo ya amani na mapambano bado yanaendelea dhidi la makundi ya Nusra Front, YPG , na vilevile lile la IS Makubaliano hayo yaliafikiwa kwa ushirikiano wa Urusi na Uturuki yakiungwa mkono na Iran, lakini Marekani haikuhusishwa.
Iwapo mpango huo utafanikiwa licha ya visa vichache vya ghasia ,mazungumzo ya amani yataanza kufanyika nchini Kazakhstan katika kipindi cha mwezi mmoja.

Rais Bashar al-Assad amekubali kuteeleza makubaliano hayo
Shirika la wachunguzi wa haki za kibinaadamu nchini Syria SOHR ,lenye makao yake huko Uingereza limesema kuwa maeneo mengi ya taifa hilo yalikuwa yametulia usiku kucha.
Lakini limeripoti vita vikali kati ya wanajeshi wa serikali na waasi katika mkoa wa kaskazini wa Hama.
Mkurugenzi wa shirika hilo Rami Abdel Rahman ameiambia AFP: makundi madogo ya waasi
pamoja na makundi yanayotii waasi hao yanajaribu kuharibu makubaliano hayo kwa sababu mpango huo unapuuzilia mbali uwepo wao.

Ronaldo akataa mshahara wa £1.6m kwa wiki kutoka klabu ya China

Ronaldo na mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane
Klabu ya Real Madrid ilipewa takriban pauni milioni 250 na klabu ya China ambayo haikutajwa jina ili kumnunua nyota wake Cristiano Ronaldo kulingana na ajenti wake Jorge Mendes.
Amesema kuwa nahodha huyo wa Portugal mwenye umri wa miaka 31 hana haja na mpango huo ambao ulishirikisha mshahara wa kila mwaka wa pauni milioni 85.
Ronaldo alisema kuwa anaweza kucheza kwa miaka mingine 10 mnamo mwezi Novemba baada ya kuandikisha mkataba mpya na Real Madrid hadi Juni 2021.
''Soko la China ni soko jipya.wanaweza kuwanunua wachezaji wengi, lakini haiwezekani kumnunua Ronaldo'', alisema Mendes.

''Cristiano ndio mchezaji bora duniani, ni kawaida kupata maombi'', aliongezea raia huyo wa Ureno.
Chini ya ombi hilo analodai Mendes, Ronaldo angepokea kitita cha pauni milioni 1.6 kwa wiki ikiwa ni mara tatu ya zaidi ya kitita cha uhamisho wa pauni milioni 89 zilizogharimu uhamisho wa Paul Pogba kutoka Juventus kuelekea Manchester United.

Mendes aliambia Sky Italia: Klabu ya China imetoa pauni milioni 257 kwa Real Madrid na zaidi ya Yuro milioni 100 kila mwaka kwa Ronaldo.
''Lakini fedha sio kila kitu.Klabu hiyo ya Uhispania ndio maisha yake''.
Hatua hiyo inajiri baada ya klabu ya Shanghai Shenhua kutoka China kuthibitisha kwamba imemsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez kutoka klabu ya Boca Juniors.
Shanghai inayofunzwa na aliyekuwa mkufunzi wa Brighton Gus Poyet ,wameripotiwa kukubali uhamisho wa pauni milioni 40 mbali na mshahara wa zaidi ya pauni milioni 310,000 kwa wiki

Ewura yabariki ongezeko la umeme

eura

Rc Ndikilo ameagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wafugaji wote waliongiza mifugo kuondoka haraka

kau
 
Kutokana na kuendelea kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hapa nchini ,mbunge wa chalinze Mh RIDHIWANI KIKWETE ameiomba serikali kuchukua hatua stahiki ili kulinda raia wake dhidi ya migogoro iyo.
Mkutano huu unafuatia hali mbaya ya mapigani baina ya wakulima na watugaji kama ambavyo imeripotiwa kwenye vyombo vya habari. Mapigano hayo ambayo yalianza siku nyingi , sasa yamefika pabaya baada ya matukio ya watu kuuawa, kuvunjwa viungo na hata wengine kukimbia makwao kwa sababu ya kile kilichoitwa kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafigaji.
kama ilivyoandikwa kwenye vitabu va dini kuwa ombeni nanyi mtapewa,kilio cha mbunge ridhiwani kikapokewa vyema na mkuu wa mkoa Mhandisi Ndikilo kwa kutoa siku 30 ,kwa wafugaji waliovamia maeneo ya wakulima kuondoa mifugo yao haraka iwezakanavyo,”Mlipokuja hamkugonga hodi hvyo na mnapoondoka msituulize mtaenda wapi,haiwezekani ufugaji wako mtu mmoja uwe kero kwa jamii inayokuzunguka hii si sawa”…alisema Ndikilo
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza kabla ya mkuu wa mkoa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo hajakaribishwa kuzungunza na Wananchi , Mbunge wa Chalinze Bwana Ridhiwani Kikwete alisema katika kijiji hicho kuna wafugaji ambao wameingiza mifugo kwenye ranchi kinyume cha Taratibu hivyo kutumia njia ya kijiji kama njia halali ya kupeleka mifugo yao mto Ruvu kuwanywesha maji. Vitendo hivyo vimepelekea wananchi wengi kupoteza mazao yao ; jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wakulima wa kitonga,hivyo ni vema serikali ikachukua hatua stahiki juu ya jambo hilo..
Rc Ndikilo katika hatua nyingine ameagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wafugaji wote waliongiza mifugo hiyo kuondoka haraka iwezekanavyo. Mifugo imekuwa mingi sana katika eneo hili la kitonga na mkoa wa pwani , mkuu wa mkoa alisema. Kwa mujibu wa sensa iliyofanywa kwa kuwahoji wafugaji wenyewe,walidai kuwa wana ngombe wapatao laki 5,lakini ukweli unaonesha kuwa kuna zaidi ya kiasi hicho. ” hata kama ukweli ndiyo uo , eneo la kufuga mkoa wa Pwani linauwezo wa kuchukua Ng’ombe laki 2 na Nusu. Hivyo kuna ziada ya mifugo laki 2 na nusu.
Wafugaji wa kwanza kuingia mkoa wa pwani waliiongia mwaka 1940 ambao walikuwa wamasai na tangu hapo ukawa mwanzo wa pwani kuwa na mifugo. “Operesheni ya kuondoa mifugo katika Bonde la Ihefi ndiyo iliyofungua mlango huo. Wafugajo walitengewa maeneo Lindi lakini wengi walishuka pwani kwa kuona Maji na majani.”, alisema Mkuu wa Mkoa. Sasa muda umefika tusimamie taratibu tulizojiwekea.
Akionekana kuchukizwa zaidi na vitendo vya wafugaji kuwanyanyasa wakulima ndikilo amesema ni vyema wafugaji wakaelewa kuwa kila mmoja ana wajibu wa kutii sheria ili watu waishi kwa amani na upendo. Katika Mkutano huo pia Mkuu wa Mkoa wa Pwani alitumia nafasi kuwaonya wote wanaojiona kuwa wako juu ya sheria na pia wale wanaojidai kuwa wao ndiyo mababa wa Kitonga kwa kuwa mbele ya sheria hakuna aliyejuu. Alitoa tahadhari kuwa atashughulika na hap wote na onyo kali kwa kiongozi wao Bwana Leki ambaye inasemekana yeye ndiyo anayewaita wenzake na kuwapa kibuli.
kwa upande wake mbunge wa chalinze mara baada ya kauli ya mkuu wa mkoa akawataka wananchi wa chalinze kutoa ushirikiano kwa serikali ili kurahisisha zoezi la kuondolewa kwa mifugo iliyoingia kinyemela.
wanakijiji cha Kitoga wakisikiliza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza kwa wananchi katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa maelekezo kwa wanakijiji baada ya kufika katika kijiji cha Kitonga kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimiana na watendaji mkoa wa Pwani baada ya mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza

Tamko la ndg. Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto kuhusu Rasilimali na Madeni

zit
Ndugu Watanzania, Kama mnavyofahamu kuwa ibara ya 132(4) na (5) na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria namba 13 ya mwaka 1995 inataka viongozi wote wa umma kujaza fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni. Tamko hilo huwasilishwa Sekretariat ya Maadili ya Viongozi kabla ya mwisho wa kila mwaka. Kama nifanyavyo siku zote, nawajulisha rasmi kwamba nimetimiza matakwa hayo ya katiba na sheria kuhusu Maadili ya Viongozi.
Inafahamika kuwa Chama Cha ACT Wazalendo, kwa mujibu wa Katiba yake na Azimio la Tabora, kimeelekeza kuwa Viongozi wake wote waweke wazi kwa Umma Tamko la Mali, Madeni na Maslahi. Kwa kufuata masharti ya Katiba ya Chama Cha ACT Wazalendo natangaza rasmi fomu zangu nilizowasilisha Leo Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Ni matumaini yangu kwamba itafikia wakati Daftari la Rasilimali na Madeni la Viongozi wa Umma litakuwa linawekwa wazi kwa Umma ili wananchi waweze kujua Mali, Madeni na Maslahi ya Viongozi wao na pale ambapo kiongozi ametoa habari zisizo sahihi au kuficha mwananchi aweze kutoa Taarifa kwenye Sekretariat na Baraza la Maadili liweze kufanya kazi yake ipsavyo.
Mfumo wa kuweka wazi Rasilimali na Madeni ya Viongozi wa Umma ni mfumo endelevu na muhimu kwenye vita vita dhidi ya ubadhirifu na ufisadi. Mataifa kadhaa duniani hutumia mfumo huu ( public disclosure of leaders’ assets and liabilities) kuwezesha mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Nchini Uingereza na Kanada kwa mfano, daftari la matamko ya Rasilimali na Madeni ya Viongozi lipo wazi kwa kila mwananchi kuona na huuzwa kwenye duka la vitabu la Bunge.
Namsihi Sana Rais John Pombe Magufuli kusaidia kufanya mabadiliko makubwa ya Sheria ya maadili ya Viongozi ili kurejesha na kuboresha Miiko ya Viongozi katika kuimarisha vita dhidi ya ufisadi nchini. Rais aliahidi kuweka wazi Mshahara wake alipokuwa anazungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV. Ninamkumbusha afanye hivyo na pia aweke wazi Mali, Madeni na Maslahi yake ya Kibiashara ili awe mfano kwa Viongozi wengine Nchini.
Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kigoma Mjini
30/12/2016

Waziri Nchemba atembelea WCB

 Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba wiki hii alitembelea ofisi ya WCB iliyopo Tandale jiji Dar es salaam na kujionea uwekezaji uliofanywa na label hiyo ambayo ipo chini ya Diamond Platnumz.
Waziri huyo kijana aliweza kuzungumza na viongozi wa label hiyo na kuangalia namna ambavyo serikali inaweza kudhibiti wizi wa kazi za wasanii.
Baada ya kumaliza mazungumza hayo, Waziri Nchemba kupitia instagram yake aliandika:
#Wizi wa kazi za wasanii #Jeshi la polisi kuongeza nguvu

Pia alisema kuwa serikali haitasita kuwapa msaada pale watakapokwama na kuhitaji usaidizi wa serikali.