Saturday 19 December 2015

Waziri Mkuu Ameanza kwa Kukagua vituo vya Mradi Huo Kuanzia cha Feri, Jangwani, Kimara na kumalizia na Morocco na kuwapongeza kwa kumaliza kujenga Vituo 15 Kati ya 27



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa Akisalimiana na watendaji Mbalimbali wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Waliofika Katika kituo cha Feri cha Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) leo Jijini Dar es Salaam. Picha Na Kalonga Kasati
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa Akitembelea Maeneo Mbalimbali ya kituo cha Feri jijini Dar es Salaam leo.Picha Na Kalonga Kasati

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa Akipanda basi la Mwendo wa Haraka mara Baada ya kutembelea Maeneo Mbalimbali katika kituo cha feri leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa Akiwa katika kituo cha Mradi wa Mabasi cha Jangwani kukagua Maendeleo ya Ujenzi ya kituo hicho ikiwa Ujenzi wa kituo hicho upo Hatua za Mwisho kukamilika.
Kituo cha Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka kikiwa kimekamilika na Mabasi yakiwa Nyuma ya kituo Hiki kwaajili yakisubiri kumalizika kwa barabara ili ifikapo Januari 10, 2016 kuanza kufanya kazi.Picha Na Kalonga Kasati
Mabasi ya Mwendo wa Haraka yakiwa kwenye Maegesho. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Mara baada ya kumalizia kukagua Ujenzi wa Barabara ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka katika kituo cha Morocco jijini Dar es Salaam.
Na kalonga Kasati
MRADI wa Mabasi yaendayo kasi (BRT) kuanza Januari 10, 2016 hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa wakati Akikagua  Ujenzi wa Miundo mbinu ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka leo jijini Dar es Salaam.


Pia Majaliwa Amewaagiza Watendaji wizara ya Tamisemi Ambao ni Wamiliki wa Mradi Huo  kusimamia Vyema ili Uanze kufanya kazi  kama ilivyo pangwa kwa kuwa Mabasi 120 Yalishawasili jijini Dar es Salaam.


Waziri Mkuu Ameanza kwa kukagua vituo vya Mradi Huo kuanzia cha Feri, Jangwani, Kimara na kumalizia na Morocco na kuwapongeza kwa kumaliza kujenga Vituo 15 kati ya 27 na Amewaagiza kumalizia vituo Vilivyo baki ili kufikia januari 10 Mwakani Mabasi yaanze kufanya kazi.

No comments:

Post a Comment