Tuesday 15 December 2015

Kubenea Amefikishwa Mahakamani leo

Na Kalonga Kasati


IMG_0852Mbunge wa jimbo Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea Amefikishwa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam Mapema hii leo akielekea katika Chumba cha kusomewa Shtaka la kutoa lugha chafu Dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 IMG_0854Mbunge wa jimbo Ubungo,(Chadema) Said Kubenea akiwa na Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, leo Mara Baada ya kusomewa Shitaka lililokuwa likimkabiri Katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.IMG_0863Mbunge wa jimbo Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam leo.

Baada ya Taflani iliyotokea Jana Jumatatu kati ya Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea wa Chadema na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda Eneo la Viwanda (EPZA) Mabibo jijini Dar hali Iliyopelekea DC Makonda kuwaamuru Polisi Wamuweke Chini ya Ulinzi Saed Kubenea na kumpeleka Kituo cha Polisi.
 
Leo Saed Kubenea amepandishwa kizimbani kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam na kusomewa Shitaka la kutoa lugha Chafu dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 
Hata hivyo, Kubenea amekana kufanya Kitendo Hicho na kesi yake Kuahirishwa hadi Disemba 29, Mwaka huu huku Uchunguzi Ukiendelea.

No comments:

Post a Comment