Friday 18 December 2015

Naibu Wa Waziri Wa Afya Maendeleo Ya Jamii Dr Kigwangala Amewanyoosha Wachelewaji Kazini

 

  Naibu Waziri  Wa Afya Dr Hamis Kigwangalla Apitisha Mnyoosho Ofisi za Wizara ya Afya, Wachelewaji Waishia Getini!

 

IMG_9164
‘Ziara za Kushtukiza’ na ‘Minyoosho’ ni Majina ya kati ya Serikali ya Awamu ya tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli na Mawaziri wake wameingia na Kasi hiyo Hiyo Tangu Waapishwe.
IMG_9164
Leo ofisi za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam Zilikuwa na Ugeni wa ‘Surprise’ kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla.
Ugeni huo Haikuwa wa Heri Hata kidogo Sababu Wachelewaji Wote walijikuta Wakirudia Getini Baada ya Kigwangalla kuwaamrisha Walinzi Wayafunge Baada ya Muda wa kufika ofisini kupita.
IMG_9122Nitawajibika kazini. Kila Mtu atapaswa kuwajibika. Haya ndiyo Mahitaji ya wakati huu. Leo Nimefungia Wachelewaji “ kazini nje ya Geti.
IMG_9231
Nitaendelea kushughulika na Watoro na Watorokaji. Nasubiri Ripoti ya Watendaji kuhusu Trend ya Watumishi Wote Watoro, Wachelewaji kisha Nichukue Hatua Stahiki! Ili kazi ziende ni lazima Tuweke Nidhamu ya kazi Na Uwajibikaji Maofisini
IMG_9172
Hawa tu ndio wamefika ofisini?
Kwenye picha Nyingine, Naibu Waziri Huyo Ameandika: #HapaKaziTu . Tumefunga Geti la ofisi Za Wizara ilipofika saa 1:30 asubuhi. Tunataka Watumishi wa Wizara Wawahudumie Wateja wetu Kwa Tija na Ufanisi.”

No comments:

Post a Comment