Tuesday 8 December 2015

Vijana wametakiwa kushiriki kesho katika kufanya usafi



Na Kalonga kasati
Umoja wa vijana wa chama chama cha mapinduzi mkoa wa kigoma(UVCCM)wamefanya usafi katika hospitali ya mkoa maweni sambamba na kuwafariji wagonjwa waliolazwa katika wodi mbalimbali hospitalini hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa  mbunge wa viti maalum kupitia umoja huo wa vijana Zainabu Katimba alisema kuwa wameamua kuwafariji wagonjwa na kufanya usafi hospitalini hapo ili kuendana na kasi yam he Rais john pombe magufuli  wa hapa kazi tu.

Sisi kama vijana tumeamua kusherekea kauli mbiu ya mhe Rais magufuli  ya hapa kazi tu kwa vitendo hii si kwa ajili ya siku ya uhuru tu kesho hili ni zoezi endelevu tutakuwa tunalifanya mara kwa mara alisema Bi Katimba.
Aliwataka wananchi wote bila kujali itikadi zao kumuunga mkono Mhe Rais kwa kujitokeza siku ya kesho na kufanya usafi katika maeneo yao kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuepekana na maradhi  ya milipuko  kama kipindupindu na mengine.

Naye Mwenyekiti wa umoja wa vijana (uvccm) mkoa Peter Msanjile alisema kuwa na zoezi hilo la usafi katika maeneo mbalimbali linatekelezwa  na vijana katika mikoa yote
Msanjile amempongeza Rais wa awamu ya tano John pombe magufuli kwa kazi nzuri anazofanya kwa kuwajibisha wahujumu uchumi

No comments:

Post a Comment