Saturday 19 December 2015

Mechi Ya leo Kuamua Azam Kurudi kileleni au Kushuka

 Na Kalonga Kasati

Azam Fc inamenyana na Majimaji Uwanja Wa Majimaji mjini Songea leo katika Mchezo Ambao ikishinda inarejea kileleni Mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Azam FC ilishushwa kileleni na mabingwa Watetezi, Yanga SC baada ya ushindi wa 1-0 Dhidi ya African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumatano.
  Lakini leo Azam FC inakutana na Majimaji Ambayo mchezo wa mwisho ilifungwa 5-1 na Vibonde wenzao Toto Africans Uwanja wa Majimaji.
  Azam FC inapewa nafasi kubwa ya kushinda Mchezo wa leo na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, kutokana na ukweli kwamba Majimaji ni Timu Dhaifu.
  Mabingwa watetezi, Yanga SC nao pia Watashuka Dimbani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo kumenyana na Stand United ya Shinyanga, ambayo hakika na timu ngumu.
  Ikitoka kufungwa 2-0 nyumbani na Mwadui katika Mchezo wake uliopita, Stand inayoongozwa na kinara wa mabao wa Ligi Kuu, Elias Maguri inatarajiwa kupambana leo kuzinduka.
  Nao mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, Simba SC watakuwa Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza leo kumenyana na Toto Africans.  Toto imekuwa na kawaida ya kuifunga Simba SC Uwanja wa Kirumba na hilo linafanya Mchezo wa leo, uvute hisia za wengi. 
  Simba SC leo wanatarajiwa kuwa kamili, Baada ya wachezaji wake iliyowaingiza Dirisha dogo, Mganda Brian Majwega, Mkenya Paul Kiongera na wazalendo Novat Makunga na Hajji Ugando kuruhusiwa kucheza.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo ni kati ya Mwadui FC na Ndanda FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Kagera Sugar na African Sports Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora na Prisons na Mtibwa Sugar Uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya – wakati kesho JKT Ruvu Wataikaribisha Coastal Union Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam na Mbeya City Watakuwa wenyeji wa Mgambo JKT Uwanja wa Sokoine.

No comments:

Post a Comment