Monday 7 December 2015

RAIS MAGUFULI AMEVUNJA BODI YA BANDARI NA KUMFUKUZA KAZI KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI



Na Kalonga kasati
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John pombe magufuli amevunja bodi ya bandari nchini pamoja na kutengua uteuzi wa katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi Dk Shabani Mwinjaka pamoja na  Mkurugenzi mkuu wa bandari Awadhi massawe  na mwenyekiti wa bodi ya bandari Profesa Joseph msambichaka
Kuvunjwa kwa bodi hiyo kumetokana na uendaji mbovu wa mamlaka hiyo kwa muda mrefu na kitendo cha kutokuchua hatua za haraka katika vyanzo husika.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake waziri mkuu Kassim majaliwa ofisini kwake leo jijini Dar es salaam amesema kutenguliwa kwa uteuzi huo kutokana na ziara alizofanya bandari ya Dar es salaam  na kubaini kuwepo na mianya ya ukwepaji wa kodi ikiwemo makontena 2387 yaliyopitishwa kati ya machi na septemba mwaka jana.
Amesema upotevu huo kutokana na mfumo wa kupokelea malipo ambao unatoa mwanya wa kupoteza mapato ya serikali kutaka mfumo huo ubadilishwe kufikia desemba 11.
Waziri mkuu kassim majaliwa amesema kuwa kutokana na utendaji wa bandari huo mbovu iliwataja majina ya wahusika na upitishaji wa makontena hayo bila ya kuwepo na taarifa yoyote hivyo amewasimamisha kazi wasimamizi 8 wa bandari kavu (icd) ambao ni Happy god Naftari juma Prosper kimaro mkango ali John Elisante na James Kamwomwa.
Wengine ambao hakuwepo kwenye ripoti hiyo ni viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa makontena kutoka ndani ya bandari wahusika wakuu hao ni Shaban mngazija aliyekuwa meneja mapato Rajab  mdoe Mkurugenzi wa fedha  na mkuu wa bandari kavu ibin masoud kaimu mkurugenzi wa fedha Apolonia mosha meneja wa bandari msaidizi wa fedha



Na kalonga kasati
Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma nchini ambao ulizinduliwa agosti mwaka huu
Akiongea na vyombo vya habari leo katibu mkuu Hab mkwizu amesema utekelezaji huo umeanza rasmi disemba 2015 ambapo kila mtumishi wa ummaataweka saini ya kiapo kwa kuzingatia taratibu zilozoweka na mazingira ya taasisi husika
Utaratibu wa utekelezaji wa ahadi ya uadilifu kwa utumishi wa umma umetolewa kupitia waraka wa mkuu wa utumishi wa umma  wa mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa ahadi ya uadilifu kwa viongozi watumishi wa umma wa sekta binafsi wa tarehe 1 agosti 2015 alisema mkwizu.
Mkwizu aliongezea kwa kusema uanzilishwaji wa uadilifu ni mwendelezo wa uundaji wa vyombo vya kusimamia maadili baada ya ongezeko kubwa la ubadhirifu utoro sehemu za kazi kushuka kwa nidhamu katika kipindi cha miaka ya thelathini na tisini
Alivitaja vyombo vipengele ambavyo vilianzishwa kusimamia ahadi kuwa ni sektarieti ya maadili ya viongozi wa umma tume ya haki binadamu na utawala bora na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU)
Aidha Mkwizu amtoa kwa waajiri wote kuhakikisha kuwa utekelezaji wa ahadi ya uadilifu unakamilika ifikapo tarehe 31-12-2015 na utekelezaji wakekwa kila ifikapo juni 30 ya kila mwaka fomu ya ahadi ya uadilifu zinapatikana katika tovuti ya Rais.

No comments:

Post a Comment