Tuesday 22 December 2015

Madereva Wamehimizwa Kutotumia Kilevi Cha Aina yoyote Wanapokuwa na Abiria

Tanzania.
007.DODOMAShughuli ikiendelea ya kutoa Elimu kuhusiana Na Mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa Elimu kwa Madereva kutokutumia Simu na kilevi wakati wote Wakitumia vyombo vya Moto.Kampeni hiyo inaendeshwa na Jeshi la polisi la Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
Na Mwandishi Wetu 
Kampeni ya Usalama Barabarani ya kuwataka Madereva Nchini kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani,leo imefanyika katika Mkoa wa Dodoma.
Madereva Wameendelea kuhimizwa kutotumia Vinywaji vyenye Ulevi na kuacha Tabia ya kuongea na Simu au kutuma na kupokea ujumbe wa Maneno (sms) Wanapokuwa Wanaendesha vyombo vya Moto.

Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, SSP Nuru Selemani amesema kampeni Hii ni muhimu katika kupunguza Matukio ya Ajali “Watumiaji wa Barabara hii ya Mkoa wa Dodoma Ni Wengi Hususani Madereva Wa vyombo vya Moto Hawana Budi kuzingatia Maelekezo Ambavyo Tumekuwa Tukiwapa katika kampeni hizi ili Tupate Matokeo Mazuri kwa kupunguza Ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema
Alisema Madereva Wakizingatia Sheria za Barabarani kwa kiasi kikubwa Ajali Zinazoendelea kutokea kila Siku zitapungua Hususani katika kipindi hiki cha Msimu Unakoelekea wa Sikukuu na Aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na Tatizo Hili ambalo limekuwa Sugu .

Kwa upande wake,Kaimu Mkuu wa kanda ya kati wa asoko wa Vodacom Tanzania Heladius Kisiwani, alisema Vodacom itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono Jitihada za kuondoa Matatizo kwenye Jamii kama lilivyo tatizo hili la ajali ili kuhakikisha wananchi Wanaishi Maisha Murua na Marefu.”Tunatoa rai kwa Madereva Wote kuzingatia Sheria za Barabarani na kutokutumia simu Wakati wowote Wakiwa Wanatumia Vyombo vya Moto”.

Aliongeza kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu ya mkononi kupitia kampeni ya “Wait to Send” pia itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia Sheria za usalama barabarani.
Alisema kampuni hiyo itaendeleza kutoa Elimu kwa Mikoa mingine pia katika Uhamasishaji wa madereva kuzingatia sheria za barabarani katika miji ya Morogoro,Dar es Salaam na mikoa mingine na kampeni hizi zitaendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini.

Katika kampeni ya leo Wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na Askari wa Usalama Barabarani Walitoa Uhamasishaji kwa Madereva kuacha kuongea na Simu Wanapoendesha vyombo vya Moto na kuwagawia Madereva pete maalum Za kuwatahadharisha kutotuma Ujumbe wa Simu Za Mkononi Wanapokuwa Wanaendesha vyombo vya Moto pia Zoezi la kupima Madereva kubaini kama Wanatumia vilevi lilifanyika Ambapo Madereva Waliokutwa Wanaendesha Vyombo vya Moto Walichukuliwa Hatua kali za kisheria.

Baadhi ya Abiria Walioshuhudia kampeni hii Mkoani Dodoma Wamesema ni ya Muhimu itasaidia kupunguza Ajali Nchini.”Hivi sasa ajali Nyingi Zinazotokea Hapa Nchini Zinasababishwa Na Uzembe wa Madereva,kampeni Hizi Zikiendelea Zitapunguza Ajali kwa kiasi kikubwa”.Alisema Sunday Israel Mkazi wa Dodoma Aliyekuwa Safarini kuelekea Singida.

No comments:

Post a Comment