Friday 11 December 2015

MALINZI NTAMPA USHIRIKIANO WAZIRI HABARI NA MICHEZO NA UTAMADUNI

 Na Kalonga Kasati

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameahidi kumpa Ushirikiano Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Joseph Magufuli ameteua Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CCm kuwa Waziri wa Habari,Utamaduni Wasanii na Michezo katika serikali ya awamu ya tano.
 
Katika salamu zake, Malinzi amempongeza Nape na kusema TFF ina imani nae katika Nafasi hiyo, na kuahidi kushirikiana katika Michezo na haswa katika kusukuma Gurudumu la maendeleoya mpira wa miguu Nchini.
Malinzi (kulia) ameahidi kumpa ushirikiano Waziri mpya wa Michezo, Nape Nnauye Picha kwa Hisani Ya Bin Zubeiry

Aidha pia Malinzi amewapongeza Paschal Kihanga, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Morogoro kwa kuchaguliwa kuwa Meya wa Manispaa hiyo, na James Bwire Mmiliki wa Shule ya Alliance mjini Mwanza kwa Kuchaguliwa Meya wa Manispaa ya Nyamgana.

Malinzi amewatakia kila la kheri katika nafasi Hizo walizozipata za kuwatumikia watanzania, Na kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu Nchini anawatakia kila la kheri na kuahidi kushirikiana nao.

  Wakati huo huo: Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) itafanya Mkutano wake wa Pili wa Baraza Kuu (Governing Council) jijini Dar es Salaam, Jumapili, Desemba 13 mwaka huu.

Mkutano huo utahudhuriwa na Marais/Wenyeviti wa klabu zote 40, ambapo 16 ni za Ligi Kuu ya Vodacom na nyingine 24 za Ligi Daraja la Kwanza ya Startimes na kutoa mwelekeo wa Bodi kwa kipindi cha miezi 12 ijayo.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel ndiye anayetarajiwa kufungua Mkutano huo utakaofanyika kuanzia Saa 10 kamili asubuhi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment