Wednesday 9 December 2015

SAMATTA NA ULIMWENGU WAKIWA JAPAN


Mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Mtanzania Mbwana Samatta (kulia) akiwa na mchezaji mwenzake wakati wa chakula cha jioni jana mjini Osaka Japan. Mazembe ipo mjini humo kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia, inayoanza kesho. Mazembe itacheza mechi yake ya kwanza Jumapili dhidi yaa mshindi kati ya Sanfrecce Hiroshima ya Japan na Auckland City ya New Zealand Uwanja wa Nagai mjini Osaka. Timu nyingine zinazoshiriki michuano hiyo ni River Plate ya Argentina, Barcelona ya Hispania, Guangzhou Evergrande ya China na Club America ya Mexico.
Mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Mtanzania Thomas Ulimwengu (kulia) akiwa na mchezaji mwenzake wakati wa chakula cha jioni jana mjini Osaka Japan.

No comments:

Post a Comment