Saturday 12 December 2015

SIMBA YANGA AZAM KUSAKA POINTI LEO



 
LEO ni Vita ya Pointi Baada ya Mapumziko ya Mwezi Mmoja Michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara itaendelea kutimua vumbi katika Viwanja sita Tofauti, huku Simba, Azam FC na Yanga kila moja Ikiingia katika Vita ya Namba Kusaka Pointi Tatu Muhimu.

Wakati vinara ya ligi, Azam ikiwa ni mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Yanga itakuwa mgeni wa Mgambo Shooting kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Azam inayoongoza kwa pointi 25 kwenye msimamo wa Ligi, inahitaji kushinda mchezo huo kama inahitaji kuendelea kushika usukani.

 Iwapo itapoteza mchezo huo itakuwa na hatari kubwa ya kushuka na kumpa nafasi anayemfuatia Ambaye ni Yanga wakitofautiana kwa pointi mbili Pekee.

Timu hizi mara nyingi zinapokutana hutoka sare lakini katika mchezo wa mwisho uliochezwa Mei, Mwaka huu, Simba walifunga mabao 2-1.

Aidha, Simba inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 21 nyuma ya Mtibwa Sugar yenye pointi 22 inayoshika nafasi ya tatu Zikitofautiana kwa pointi Moja.

Wekundu hao Wanaiombea Mtibwa ifanye Vibaya Katika mchezo Wa leo Dhidi ya Mbeya City na wao Washinde ili Washike Nafasi ya Tatu au Pili.

Lakini ikiwa Mtibwa itashinda na Yanga basi Wataendelea kubaki nafasi ya nne.

 Katika mchezo huo, Simba inatarajia kuwachezesha wachezaji iliyowasajili katika Dirisha dogo la usajili akiwemo, Brian Majwega Kutoka Azam, Novat Makunga kutoka African Sports ya Tanga na mshambuliaji, Hajji Ugando Kutoka Mtibwa B.

 Azam imemsajili Mchezaji Mmoja Pekee ambaye Ni kipa, Ivo Mapunda kwa ajili ya Kuimarisha Kikosi chao.

Kwa upande wa Yanga, Watakuwa na kazi ngumu Dhidi ya Mgambo ambao Wamekuwa Wakipigana Kuhakikisha wanabakiza pointi Tatu Nyumbani kwao Tanga. 

Yanga iliwahi kumfunga Mgambo 2-0 msimu uliopita.

Mchezo huo hautakuwa rahisi kama ambavyo Kocha wa Yanga, Hans Paluijm hupenda kusema kwani wana kazi ya kutafuta pointi tatu.

 Mabingwa hao watetezi wanacheza leo bila Donald Ngoma, Nadir Haroub, Salum Telela na Oscar Joshua walioachwa Dar es Salaam wakiwa Majeruhi.

Iwapo Yanga Watashinda Watakuwa kwenye nafasi Nzuri kama Azam Watashindwa kushinda dhidi ya Simba leo. 

Lakini vinara Azam wakishinda basi Yanga nayo ikashinda itaendelea kubaki nafasi ya pili. 

Lakini kama watapoteza au kutoka sare watatoa Nafasi kwa Mtibwa au Simba kupanda na yeye Atashuka.

Hivyo, ushindi ni muhimu kwao ili kuendelea Kujihakikishia nafasi ya kutetea taji lao. 

Mechi nyingine zitakazopigwa leo Kagera Sugar Wataikaribisha Ndanda FC Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora, Stand United Wakiongozwa na Kinara wa mabao Ligi Kuu, Elias Maguli Wataikaribisha Mwadui FC, Mbeya City Wataikaribisha Mtibwa Sugar na Majimaji Wataikaribisha Toto Africans kwenye uwanja wa Majimaji Songea.

Timu zote hizo Zinahitaji Ushindi kuzitoa katika Nafasi ilizopo na kujitoa katika Hatari ya Kushuka Daraja.

No comments:

Post a Comment