Sunday 13 December 2015

COASTAL UNION NA WAGOSI WAKAYA KUPIMANA NGUVU LEO


Na Mwandishi Wetu

Ligi Kuu Bara leo inaendelea kwa mechi Mbili tu, lakini macho na Masikio ya wengi yatakuwa katika Mechi ya Mkwakwani Mjini Tanga.

Wenyeji na Wakongwe wa Mjini Coastal Union 'Wagosi wa Kaya' Wanakutana na Wenyeji Wenzao, African Sports 'Wana Kimanumanu' katika Mechi ya Ligi Kuu Bara inayowakutanisha Baada ya Misimu zaidi ya nane.


Imekuwa ni nadra timu hizo kukutana katika Ligi Kuu Bara Baada ya kuporomoka kwa muda mrefu na kusababisha hata nguvu ya soka la mji wa Tanga kuyumba.

African Sports imerejea Msimu huu katika ligi hiyo, Maana yake hii itakuwa ni Derby mpya ya mkoa wa Tanga na kila mmoja lazima atataka kushinda kwa kuwa zote mbili hazina mwenendo mzuri katika Ligi Kuu.

Mechi nyingine ya leo, Maafande wa JKT Watakuwa Wenyeji wa Maafande Wenzao wa Magereza au Prisons. 





No comments:

Post a Comment