Thursday 10 December 2015

Magufuli atangaza baraza lake la mawaziri

 Na Kalonga kasati

BREAKINGNEWS3
Rais Magufuli
Rais Dk. John Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli hivi punde ametangaza baraza lake la mawaziri, amesema wizara nyingi wameunganisha na atakuwa na wizara 18, na watakuwa na mawaziri 19 tu, na baadhi ya wizara zitakuwa na manaibu waziri huku zingine hazitakuwa na manaibu waziri.
Magufuli: Baraza nitakalolichagua halitakuwa na semina elekezi, kama ni semina watajipa huko huko ndani, wenyewe.

Baadhi ya Wizara na Mawaziri wake:
Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora – Simbachawene na Angela Kairuki.


Wizara ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora ina mawaziri wawili ambao ni Mh. Simbachawene na Kairuki


Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Waziri wake ni Jenesta Mhagama


Wizara ya Mambo ya Nje na EAC/ Kimataifa – Augustino Mahiga, Naibu Waziri – Dk. Suzan Kolimba


Wizara ya Ardhi – William Lukuvi


Wizara ya Elimu Waziri bado hajapatikana, Naibu Stella Manyanya
Waziri wa Afya Jinsia na Watoto: Ummy Mwalimu, Naibu wake Kigwangalla

No comments:

Post a Comment