Thursday 17 December 2015

Mkuu Wa Mkoa Wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo Washukia Watendaji

Posted Na Kalonga Kasati


9956
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema kwamba Hawezi kuwavulilia   Viongozi na Watendaji   ambao Wanafanya Hujuma katika Mfumo wa Stakabadhi Ghalani katika zao  la korosho  kwa Maslahi yao Binafsi Na Badala yake Suala hilo atalivalia  Njuga kwa kuwawajibisha kuwachukulia Hatua kali Za Kisheria ili iwe Fundishisho kwa Wengine Wenye Vitendo kama hivyo.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa ameitoa wakati wa mkutano Maalumu  na Wadau wa zao la korosho  wa Mkoa wa Pwani wa kujadili Mwenendo mzima wa Mfumo wa kukunua zao Hilo kwa kutumia njia ya Stakabadhi Gharani pamoja na changamoto Zinazowakabili Wakulima.

Ndikilo amesema kwamba anashangazwa kuona kuna baadhi ya viongozi na  Watendaji Wanashindwa tutimiza Wajibu wao ipasavyo Na kuanza kukwepa  Majukumu kwa Visingizio Ambavyo havina Tija, na kuamua kufanya Hujuma kwa  kupinga Mfumo huo kitu Ambacho amesema ni lazima atawashughulikia kikamilifu watu kama hao ambao Hawataki kuleta Maendeleo kupitia Sekta ya kilimo.

No comments:

Post a Comment