Tuesday 8 December 2015

MNIGERIA WA YANGA SC KUTUA LEO USIKU



Na kalonga kasati
Kiungo wa kimataifa  wa niger issoufou bobacar garba sasa anatarajiwa kuwasili  leo usiku kwa majaribio ya wiki moja ya kocha Hans van der pluijm kutoa uamuzi awali garba ilikuwa awasili jana usiku lakini alichelewa kuunganisha ndege mijini Addis  abba Ethiopia
 Na kulazimika kulala hadi leo

Dirisha dogo la usajili wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara imefungwa disemba 15 na kweli  mholanzi pluijm aliyependekeza mchezaji huyo atakuwa na wiki moja tu ya kutoa majaribu juu ya mnigeria huyo aliyezaliwa februari 2 mwaka 1990 taarifa zinasema garba kwa sasa anacheza kwao baada ya kuondoka Tunisia ingwa hakupata nafasi ya kucheza ingwa yeye anasema ni hila visa si sababu ya uwezo 

Katika wasifu wake garba anatambulishwa kama kiungo lakini yanga wanasema wanaleta mshambuliaji
Na huyu atakuwa mchezaji wa pili kuletwa na kocha pluijm baada wa kwanza Joseph Zuttah ambaye hata hivyo aliachwa baada ya mechi saba
Garba aliyezaliwa mji waNiamey mwenye urefu wa futi 5 na nchi 6 kisoka alianzia klabu ya As fan ya kwao 2010 kabla ya kuhamia Thailand  ambako alichezea klab za Muangthong united mwaka 2011 na Phuket  mwaka 2012 alitua  club ya African ya Tunisia  ambako hakucheza mechi hadi anasimamishwa

Es Hammam ambako pia hakucheza  wasifu wake unaonyesha tangu ameondoka Es Hammam-Sousse hajapata timu nyingine lakini uongozi wa yanga sc umejiridhisha anacheza bingwa ya kwao As Douanes

Mwenyekiti wa yanga sc Yusuph manji ametoa agizo la kutosajiliwa mchezaji yoyote kutoka Uganda Kenya hata awe anaweza kucheza kama christiano Ronaldo itakuwa kazi bure

No comments:

Post a Comment