Friday 11 December 2015

MEYA MPYA MBEYA



JIJI LA MBEYA LAPATA MEYA MPYA DAVID MWASILINDI (CHADEMA) DIWANI KATA YA NZOVWE

Meya Mteule wa jiji la Mbeya Diwani wa Kata ya Nzovwe(CHADEMA) Ndugu David Mwasilindi ambaye aliibuka kidedea kwa kupata kura 34 dhidi ya Mpinzani wake wa CCM aliyepata kura 14 katika uchaguzi uliofanyika Desemba 10 katika ukumbi wa Mkapa jijini humo. Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Ndugu Quip Mbeyela ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti katika Kikao cha Baraza la Madiwani ambacho kiliketi kufanya uchaguzi wa kumpata Meya wa jiji hilo pamoja na Naibu Meya katika Halmashauri ya jiji la Mbeya . 
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya jiji la Mbeya Dkt Samuel Lazaro akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani ambalo liliketi kwa ajili ya kumchagua Meya pamoja na Naibu Meya katika Ukumbi wa Mkapa jijini humo. 

No comments:

Post a Comment