Katika siku za hivi karibuni,
kumekuwepo na mitazamo tofauti miongoni mwa jamii kufuatia kuonekana kwa
askari polisi wakifanya mazoezi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kufuatia hali hiyo, jeshi la
polisi nchini, linatumia fursa hii kuwatoa hofu wananchi kwamba mazoezi
hayo ni ya kawaida kwa askari wa jeshi la polisi
Aidha, jeshi la polisi linawataka
wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa sababu mazoezi hayo
hayalengi kuzuia shughuli zozote halali zinazofanywa na wananchi.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment