Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Bi. Beng’i Issa akizungumza na
waandishi wa habari pamoja na wafanyakaz wa baraza hilo hawapo pichani
alipozungumzia kuhusu mkakati wa mradi wa Milioni 50 zitolewazo na
Serikali kwa kila kijiji leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) wakifatilia kwa kwa
makini maelezo ya Katibu Mtendaji wa (NEEC) Bi. Beng’i Issa hayupo
pichani alipozungumzia kuhusu mkakati wa mradi wa Milioni 50 zitolewazo
na Serikali kwa kila kijiji leo jijini Dar es salaam.
Abushehe Nondo-Maelezo
Wananchi wametakiwa kuwa makini na
mtu au taasisi binafsi zinazopita na kuwadanganya kwa kuwatoza fedha za
usajili wa kikundi kwa ajili ya kufaidika na mpango wa Millioni 50 kwa
kila kijiji kama zilivyoahidiwa na Serikali ya awamu ya tano.
Akizungumza na waandishi wa
habari Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi Bi. Beng’i Issa amesema kuwa kuna taasisi binafsi zimejitokeza
na kuwatoza fedha za usajili wa kikundi ili kuweza kufaidika na mradi
huo kinyume na taratibu za Serikali.
Bi. Issa amesema kuwa hivi
karibuni kumekuwa na taarifa kutoka sehemu mbalimbali nchini kuwa baadhi
ya taasisi na watu binafsi wanawadanganya wananchi kuwa mpango wa
shilingi milioni 50 kwa kila kijiji zitapitia kwenye taasisi zao na
kuwatoza wananchi fedha za usajili.
“Wananchi wasirubuniwe na kutoa
fedha za usajili kwa ajili ya kupata fedha za mradi huo kwani hakuna
malipo yoyote na bado ugawaji huo haujaanza” alisema Bi. Issa.
Aidha Bi. Issa amesema kuwa mradi
huo bado haujaanza kutolewa kwa kuwa Serikali bado inapanga utaratibu
wa kuwafikia wananchi wa vijiji vyote nchini ili kunufaika na mradi
huo.
Mbali na hayo Bi. Issa ametoa rai
kwa watanzania wasihadaike na taasisi hizo na kutoa onyo kali kwa yeyote
atakayebainika kujihusisha na zoezi hilo hatua kali zitachukuliwa zidi
yake.
No comments:
Post a Comment