Showing posts with label MWANZO. Show all posts
Showing posts with label MWANZO. Show all posts

Friday, 15 December 2017

Upendo Peneza awashangaa wanaohama vyama na kuliingiza taifa hasara kubwa

 Image result for Upendo Peneza
Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema, Upendo Peneza amesema hana sababu za kuhama chama hicho kikuu cha upinzani nchini huku akiwashangaa wanaochukua uamuzi huo.
Peneza amesema kuhama chama kunasababisha hasara kwa Taifa kwa kuingia katika uchaguzi wa marudio huku akipendekeza uchunguzi ufanyike kwa waliohama ili kubaini ukweli wa sababu wanazozitoa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Desemba 15, Peneza amesema hajafikiria kuhama chama lakini anasikitika watu walioaminiwa na wananchi wakajiuzulu kwa kutoa sababu zisizoeleweka.

“Nimehusishwa mimi kuhama chama changu, sina sababu za kuhama ila ninachotaka ni hawa wanaohama watueleze sababu za kutuingiza katika hasara ya kurudia uchaguzi,” amesema Peneza.

“Sioni sababu ya kwenda kuunga mkono halafu utuingize gharama, yaani furaha zako utuingize sisi gharama, hapana…watueleze sababu zao,” ameongeza

Amesema kuna haja ya kupitia Katiba au kuendeleza mchakato wa Katiba ili kuwazuia kugombea wale wanaojiondoa kwa sababu zisizoeleweka.

Peneza amesema “kama unasema unaunga mkono, useme umewafanyia nini wananchi wako au kuunga mkono kwani lazima uchukue kadi ya chama kingine, Watanzania tunachezewa na watu na huu ni mchezo wa kisiasa unafanyika.”

Akizungumza kwa msisitizo, Peneza amesema “ninapinga haya kwa sababu pesa za wananchi hazitumiki vizuri, tunabana matumizi, tunapinga mafisadi halafu fedha badala ya kwenda katika maendeleo lakini tunakwenda katika uchaguzi.”

“Tusiharibu hela kwa kile wanachosema tunamuunga mkono, kama Rais atajenga daraja la Mwanza kwenda Sengerema, nitampongeza, kama chama changu kitanifukuza haya,” amesema Peneza

“Kiuhalisia shida bado kubwa, mbunge wa Siha angesimama akasema amenijengea shule, ametatua matatizo ya wakulima, ardhi sawa ila hayo hayajatekelezwa unamuungaje mkono.”

Kuhusu kuhusishwa kwake na kuhama, Peneza amesema wakati akigombea alijua kuna CCM yeye aliamua kuwa Chadema ingawa akadokeza kwamba hawezi kusema atakuwa Chadema maisha yote.

Thursday, 14 December 2017

ZILIZOMUBASHARA KATIKA MAGAZETI YA LEO IJUMAA DISEMBA 15 2017


\

Kiama kwa wabunge watakaotumia Gharama Kubwa katika chaguzi

 Image result for tume ya uchaguzi tanzania
Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa nchini, Sisty Nyahonza amesema sheria inaruhusu kuchukua mkondo wake kwa Mbunge yoyote atakayezidisha kutumia gharama kubwa katika chaguzi mbalimbali, ambapo amesema gharama ya juu ni milioni 88.
Hayo amesema kupitia kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio kuwa  sheria hiyo imeanza mchakato mwaka 2006 na kukamilika 2010, inasema mtu achaguliwe kutokana na uwezo wake wala sio pesa.

Gharama ya kuendesha kampeni za uchaguzi inatokana na ukubwa wa jimbo lenyewe lakini kuna kiwango maalumu ambacho taasisi imekipanga, kiwango cha chini kinaanzia milioni 33 huku kiwango cha juu ni milion 88.

''Kila jimbo lina kiwango chake , kama kiwango ambacho kimepangwa kikipita tunayo nguvu ya kuchunguza namna gani gharama kubwa imetumika ili muhusika achukuliwe hatua.

Alipoulizwa juu ya kujiridhisha kama kweli wagombea wametumia kiasi ambacho kimepangwa na taasisi hiyo amesema wana njia nyingi ikiwemo kushirikiana na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

''Tuna njia nyingi za kufahamu kama tuna shaka na matumizi ya kuendesha kampeni zimezidi, tunashirikiana na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa, tuna uwezo wa kufuata ripoti zote ambazo zimefanyika kupitia chama husika pamoja na kutafuta taarifa kwa wasamalia wema''.

Kwa uchaguzi ambao umefanyika mwaka 2015 kiwango cha chama cha siasa kimeruhusiwa kutumia kiasi cha bilion 17 kwa Rais, Wabunge na Madiwani.

Ambapo katika kampeni za Rais sheria inataka atumie shilingi bilioni 6 hadi mwisho wa uchaguzi, wakati madiwani wanaoishi mijini wametengewa milioni 8 huku wale wa vijijini watumie milion 6.

Tuesday, 12 December 2017

Korea kaskazini yaonesha kombora lingine hatari

Korea Kaskazini imetoa picha za jaribio la kombora lake jipya ambalo inadai kuwa linaweza kushambulia popote pale nchini Marekani.

Picha hizo zinaonyesha kiongozi wa Korea Kaskazini Ki Jong un na maafisa wengine kadha ya ngazi za juu jeshini wakisherehekea kombora la Hwasong-15 wakati likipaa.

Wengi wameshangazwa na ukubwa wa kombora hilo. Picha hii ambayo haijulikanai ilichukuliwa lini na iliyotolewa na vyombo vya habari vya taifa inaonyesha Kim akilikagua kombora hilo.
Michael Duitsman, mtafiti katika kituo kimoja alisema kuwa kombora hilo ni kubwa kuliko kombora la kwanza la Hwasong-14 "ni nchi chache tu zinaweza kuunda kombora kama hilo na Korea Kaskazini imejiunga nazo."
Pia linaonekana kuwa na kichwa kikubwa ikimaanisha kuwa linaweza kubeba bomu zito la nyuklia kwenye kichwa chake.
Yote haya yanaashiria kuwa kombora hilo lina uwezo kwa kusafirisha bomu la nyuklia kwa muda mrefu.
Lilisherehekewa kwa sigara
Kim mwenye furaha anaonekana akicheka kwa furaha  wakati kombora hilo linapaa. Linaaminiwa kuwa kombora la kwanza la Korea Kaskazini lililopaa mbali zaidi katika kilomita 4,475.

Monday, 11 December 2017

Kenyatta atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya 14 nchini Congo


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kupinga kitendo cha mauaji ya askari wake 14 waliokuwa wakilinda amani nchini Kongo, na kumpa pole kufuatia msiba huo mkubwa.
Katika barua hiyo, Rais Kenyatta amesema kushambuliwa kwa askari, ambao walikuwa wakihudumia kwa sababu nzuri ya kuanzisha amani ya kudumu nchini DRC ilikuwa mbaya, huku akiwapa pole watanzania na ndugu wa marehemu, na kuwaombea wale waliojeruhiwa waweze kupona haraka.
Uhuru Kenyatta ameendelea kwa kusema kwamba Kenya itaendelea kushirikiana na watu na serikali ya Tanzania katika kulinda amani ya Kongo na maeneo ya maziwa makuu, na kuangalia kesho bora ya maeneo hayo.
Rais Kenyatta amesema Kenya inathamini jukumu muhimu lililofanywa na watunza amani tangu imehusika katika mipango mingi ya kulinda amani.

Friday, 8 December 2017

Kanisa la ufufuo na uzima labomolewa usiku

Kufuatia zoezi la serikali la kupanua na kuboresha miundo mbinu mbalimbali nchini hususan ya barabara katika jiji la Dar es Salaam ambapo imelazimu baadhi ya maeneo kubomolewa ili kupisha zoezi hilo la upanuzi, Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima nalo limekumbwa na kadhia ya kubomolewa.
Kanisa hilo lililoko jirani kabisa na Barabara ya Morogoro ambayo serikali imepanga kuipanua ili kurahisisha usafiri na kupunguza foleni, lilitakiwa kubomolewa kutokana na kuwa ndani ya eneo la hifadhi ya barabara hiyo.
Mchungaji Biyagaza wa Kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko chini ya Askofu Gwajima, ameeleza kuwa serikali iliwapatia notisi ya siku 30 ili wabomoe kipande cha jengo la kanisa hilo kilichopo ndani ya eneo la hifadhi ya barabara.

“Ni kweli tunayo notice ya mwezi mmoja ya kuhakikisha kwamba eneo ambalo ni hifadhi ya barabara tunaliacha. Na hifadhi ya barabara ni mita 90 kuanzia katikati. Bahati nzuri wale waliokuja kuweka alama zao walipofika hapa na wahandisi , mafundi na baadhi ya watu wa kanisani walikuwepo. Basi tukawaambia wapime mita 90 zinapoishia. Kwa hiyo wakapima mita 90 zilipoishia wakaweka alama, wakasema basi nyie mnaweza mkabomoa upande huu na upande huu mkauacha kwa ajili ya hifadhi ya barabara,” alisema Mchungaji Biyagaza.
“Sisi baada ya hapo tukaona tujipange kwa ajili kuachia eneo la barabara ili shughuli nyingine ambazo ni mpango wa maendeleo ya serikali ziweze kuendelea na sisi tuweze kuendelea na eneo letu vizuri. Kwa hivyo kile kipande chote ambacho ni cha barabara na tukaongeza ndani kidogo chote tumekiondoa. Na hili eneo linalobaki tunapaimarisha ili nyumba ya Bwana iweze kufanya kazi yake ya kutoa huduma za kiroho,” aliongeza.
Mchungaji Biyagaza alieleza japokuwa eneo la jengo limepungua, eneo lililobakia linaimarishwa ili kanisa hilo liweze kuendelea kutoa huduma za kiroho kwa waumini wake.

Monday, 4 December 2017

Mahakama ya kenya imesema haina Taarifa ya kuapishwa

Nairobi, Kenya. Mahakama imesema haijapata mawasiliano rasmi kutoka kwa Muungano wa Nasa kuhusu hatua ya kumuapisha kiongozi wake Raila Odinga.
Msajili Mkuu wa Mahakama, Anne Amadi amesema Mahakama haina taarifa kuhusu sherehe iliyopangwa kufanyika Desemba 12,2017.
“Hatujaarifiwa chochote kuhusu hafla ya kumuapisha Raila Odinga inayopangwa na muungano wa upinzani,” amesema.
Muungano wa Nasa umeanza matayarisho ya hafla ya kumuapisha kiongozi huyo kwa kuunda kamati ya kusimamia shughuli hiyo.
Kuteuliwa kwa kamati hiyo ya watu saba kumefanyika siku chache baada ya Odinga kutangaza Jumanne iliyopita kuwa ataapishwa kupitia mabunge ya kaunti, hatua ambayo Serikali imesema ni kinyume cha sheria.
Gazeti moja la Kenya limesema muungano huo umetuma kadi za mwaliko wa hafla hiyo iliyopangiwa kufanyika Desemba 12,2017 Taifa hilo litakaposherehekea siku ya uhuru.
Kadi za kidigitali za mwaliko zenye jina la Odinga hazionyeshi mahali hafla hiyo itafanyika.
“Umekaribishwa. Njoo ushuhudie rais wa wananchi Raila Amollo Odinga akiapishwa tarehe 12 Desemba saa sita mchana. Taarifa kuhusu itakapoandaliwa hafla hii itatolewa baadaye,” ndivyo inavyosomeka kadi hiyo ambayo inasisitiza kuwa inaruhusu mtu mmoja pekee kwa kila kadi.

Saturday, 2 December 2017

Sosopi Mwenyekiti mpya wa Bavicha

 Image result for patrick Ole Sosopi
Baraza la Vijana Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamefanya uteuzi wa viongozi wake ili kuziba mapengo kufuatia baadhi ya viongozi wao kukihama chama hicho na kujiunga Chama Cha Mapinduzi hivi karibuni.
Katika uteuzi huo, Bavicha wamemteua Patrick Ole Sosopi kuwa Mwenyekiti mpya wa BAVICHA kwa atakayetumikia nafasi hiyo kwa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi kufanyika mwakani 2018, baada aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo, Patrobas Katambi kuhamia CCM.

Thursday, 30 November 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DISEMBA 01 2O17




Marekani yaitaka dunia kusitisha biashara na Korea Kaskazini


Marekani imetoa wito kwa mataifa mbalimbai kukata uhusiano wake wa kidiplomasia na kibiashara na Korea Kaskazini, ikiwa ni hatua ya kupinga majaribio ya makombora ambayo yamekuwa yakifanywa na taifa hilo.
Balozi wa Marekani Nikki Haley, ametoa pendekezo hilo katika mkutano wa dharura wa baraza la usalama la umoja wa mataifa unaoendelea mjini New York.
Bi. Haley amesema kuwa Rais wa Marekani amemtaka Rais wa China Xi Jinping kusitisha biashara ya mafuta ghafi na Korea Kaskazini, kama sehemu ya kutekeleza hatua ya kuwekewa vikwazo kwa taifa hilo.

Kupitia hatua hii ya kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini tunapaswa kusitisha asilimia tisini ya biashara na Korea Kaskazini pamoja na asilimia 30 yamafuta yake.

Mwaka 2003, China ilisitisha kupelekea mafuta Korea Kaskazini ,muda mfupi baadaye taifa hilo likasogea katika meza ya majadiliano.
''Tumefikia hatua ya kuitaka China kuchukua hatua Zaidi katika hili, ni lazima isitishe kuipatia mafuta Korea Kaskazini," alisema Haley.
Wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wanakutana mjini Ne York kujadili hatua ya Korea kaskazini na majaribio ya makombora ya masafa marefu.

Rooney afunga bao la mwaka Everton

Everton, Wayne Rooney amesema bao alilofunga dhidi ya West Ham United litabaki katika kumbukumbu yake daima.

Rooney alisema hakuwahi kufunga bao maridadi katika maisha yake ya soka tangu alipoanza kucheza soka Everton, Manchester United na timu ya taifa ya England.

Nahodha huyo wa zamani wa Man United na England aliiongoza Everton kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Goodison Park.

Nguli huyo alifunga mabao matatu ‘hat trick’ kwa mara ya kwanza tangu aliporejea Everton katika usajili wa majira ya kiangazi kutoka Man United.

Pia ushindi wa Everton ni ukaribisho wa kocha mpya Sam Allardyce ‘Big Sam’ aliyetua Goodison Park baada ya kuwa nje ya uwanja muda mrefu tangu alipojiuzulu kuinoa England.

Rooney alifunga bao la kwanza kwa shuti kali akiwa katikati ya uwanja dakika ya 66 akimtungua kipa mkongwe Joe Hart umbali wa mita 54.

“Hili ni bao bora zaidi kati ya mabao yangu niliyowahi kufunga. Ni mara ya kwanza kufunga ‘hat trick’ nikiwa Everton ni hili ndilo bao maridadi tangu nilipoanza kucheza soka,”alisema Rooney.
Mbali na kufunga mabao hayo, Rooney mwenye miaka 32 alikuwa nahodha katika mchezo huo na alicheza kwa kiwango bora dakika zote 90.
Pia alidokeza alifunga bao zuri kwa mkwaju wa penalti kwa kuwa anatambua udhaifu wa Hart tangu wakiwa wote timu ya taifa.
“Bao la kwanza lilikuwa muhimu. Nimejifunza sana kupiga penalti nyingi dhidi ya Joe Hart na najua jinsi ya kumfunga kwa kuwa anajua udhaifu wake,” alisema Rooney.

Taarifa ya TANESCO kuhusu itilafu katika gridi ya Taifa

 Image result for tanesco
Majira ya saa 7:20 leo hii Alhamisi Novemba 30, imetokea hitilafu kwenye Gridi ya Taifa na hivyo kusababisha umeme kukatika takriban kwenye mikoa yote iliyounganishwa kwenye Gridi hiyo.
Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, mafundi na wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO wameanza kufuatilia kujua chanzo chake hasa ni nini na taarifa Zaidi zitatolewa kila baada ya muda ili kuufahamisha umma na watuamiaji wa umeme
.

Thursday, 16 November 2017

Sayari mpya yagundulika


Wataalamu wa anga za juu wamegundua sayari isiyo na joto sana na yenye ukubwa unaokaribia sana na wa dunia.
Sayari hiyo inapatikana karibu na mfumo wetu wa Jua
Mandhari katika sayari hiyo ambayo imepewa jina Ross 128 b yanaifanya kuwa pahala pazuri pa kutafuta viumbe au uhai anga za juu.
Sayari hiyo inapatikana umbali wa miaka 11 kwa kasi ya miali ya jua, na ndiyo sayari ya pili kwa karibu zaidi ambayo ina mazingira yanayokaribiana na ya dunia.
Sayari ya aina hiyo iliyo karibu zaidi hufahamika kama Proxima b, na wataalamu wanasema mazingira huko hayaonekani kuwa mazuri sana kiasi cha kuweza kuwa na viumbe.
Proxima b iligunduliwa 2016, na huzunguka kwenye mzingo ulio kwenye nyota kwa jina Proxima Centauri, ambayo hufahamika kama "nyota nyekundu mbilikimo". Nyota hiyo huwaka sana na ina maana kwamba milipuko kwenye nyota hiyo huenda ikarusha miali nururishi yenye sumu kwenye sayari ya Proxima b.
Sayari hiyo mpya, Ross 128 b, huzunguka sayari ambayo haitofautiani sana na Proxima Centauri (pia ni nyota nyekundu mbilikimo), lakini hailipuki sana.


  • Mpango wa Marekani kupeleka watu Mars

  • Mpango wa kupeleka watu wakaishi Mars

  • Sababu ya chombo cha Ulaya kutoweka Mars
Mmoja wa waliogundua Nicola Astudillo-Defru kutoka kituo cha kutazama anga za juu chenye makao yake Geneva, Uswizi aliambia BBC kwamba kwa sababu Proxima Centauri hulipuka na kutoa miali nururishi yenye sumu, "nafikiri ndio, Ross 128 ni pahala pazuri zaidi pa uhai kunawiri."
"Lakini bado hatufahamu anga ya Ross 128 b iko vipi. Kwa kutegemea vitu vilivyo kwenye anga yake na uwezo wa mawingu kuakisi mwanga, huenda kukawa na maji ambayo yanaweza kufanikisha uhai kama hapa duniani, au iwe sayari kama vile Zuhura ambayo haiwezi kufanikisha uhai."



Sayari hiyo mpya iligunduliwa na darubini yenye uwezo mkubwa kwa jina Harps iliyopo katika kituo cha kufuatilia anga za juu cha La Silla nchini Chile.



Ingawa kwa sasa sayari hiyo ipo miaka 11 kwa kasi ya miali ya jua kutoka kwenye dunia, nyota asili Ross 128 inasonga kuelekea kwa dunia na huenda ikaipita Proxima Centauri na kuwa mfumo wa nyota ulio karibu na dunia zaidi katika kipindi cha miaka 79,000.

  • Proxima Centauri ni 'nyota nyekundu mbilikimo'; ni ndogo na pia haina joto sana kama Jua

  • Inakaribia zaidi lakini kuna uwezekano ikawa imeunganishwa kwa mvuto na Alpha Centauri A & B

  • Kwa mtu anayetumia jicho lake kutazama juu angani Alpha Centauri A & B huonekana kama nyota moja

  • Sirius A ndiyo nyota inayong'aa zaidi na inayotambulika kwa urahisi zaidi angani usiku

  • Jupiter ndiyo sayari kubwa zaidi mfumo wetu wa Jua. Iwapo ingelikuwa na uzito mara 80 zaidi ya sasa, basi ingegeuka na kuwa jua
  • Mambo muhimu kuhusu sayari ya Mars

  • Mmarekani wa kwanza kuizunguka dunia afariki

  • Japan yatuma mtambo wa kufagia anga za juu

Monday, 30 October 2017

IEBC kumtangaza Rais wa Kenya

  Kenya. Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatarajiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi wa marudio kwa kura ya utais uliofanyika Oktoba 26 na kutangaza ikiwa itaandaa uchaguzi katika majimbo 25 ambako uliahirishwa.
Makamu wa Rais wa tume hiyo, IEBC, Consolata Nkatha alisema jana jioni kwamba walikuwa wamepokea matokeo kutoka majimbo sita kati ya saba yaliyokuwa yamesalia na kwamba kufikia Jumatatu asubuhi matokeo yote yatakuwa yamejumlishwa.
“Tumepokea matokeo kutoka majimbo sita sasa na tutakuwa katika nafasi ya kutangaza matokeo ya mwisho kesho (leo) asubuhi. Tutafanya kazi usiku kucha kuhakikisha uhakiki na ujumlishaji unakamilika. Pia tutatangaza ikiwa tutaendesha uchaguzi katika majimbo 25 ambako uliahirishwa au la,” alisema Nkatha.
Majimbo hayo yaki kwenye kaunti ambazo tume iliahirisha uchaguzi ambazo ni Kisumu, Migori, Siaya na Homa Bay.
Mawasiliano na IEBC yamekuwa haba lakini inafahamika kwamba makamishna wa tume walifanya kikao cha saa kadhaa na wanasheria wao juzi kufikiria kama wajaribu kuitisha uchaguzi katika majimbo 25.
Jana jioni Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alisema tume yake ilikuwa imehakiki matokeo ya majimbo 259 kati ya 265, yakiwemo ya nchi za nje.
Kutoka katika majimbo hayo, Chebukati alisema watu 7,447,014 walijitokeza kupiga kura sawa na asilimia 43.04. Matokeo yaliyokuwa yakitangazwa moja kwa moja kutoka jengo la Bomas of Kenya Rais Kenyatta alijikusanyia kura 7,393,405 sawa na asilimia 98.3 ya kura halali.

Monday, 23 October 2017

Mnada wa Magorofa ya Lugumi kupigwa mnada Novemba 9,

Kampuni ya Udalali ya Yono imesema itapiga mnada kwa mara ya pili nyumba za kifahari za mfanyabiashara Saidi Lugumi baada ya ule wa kwanza uliofanyika Septemba 7 kukwama.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Scholastica Kevela amewaeleza waandishi wa habari leo Jumatatu kuwa lengo la mnada huo ni kufidia Sh 14 bilioni anazodaiwa Lugumi.
"Sio kweli nyumba hizi zimedoda ila thamani halisi katika mnada wa kwanza haukufikiwa na ndio maana tunarudia tena Novemba 9," amesema Kevela.
Amesema baada ya mnada wa awali kukwama walirudi kujipanga na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewapa maelekezo mengine ikiwamo thamani ya nyumba hizo.
Wateja hawajajitokeza kununua mali za Lugumi
"Wale wanaotaka majumba haya ya Lugumi waje siku hiyo na tayari Serikali kupitia TRA imetupa maelekezo mapya hasa thamani ya majumba hayo imepanda kuliko ya awali ilivyokuwa," ameongeza

Mkurugenzi huyo amesema nyumba hizo zitakazopigwa mnada ziko Mbweni JKT nyumba mbili na  nyumba moja ipo Upanga.