Siku chache baada ya mshambuliaji wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya
Ureno Cristiano Ronaldo kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia
inayotolewa na moja ya gazeti nchini Ufaransa “Ballon d’Or” kumeibuka na
mijadala mingi juu ya mabadiliko ya tuzo hizo kama ni ile inayotolewa
na Shirikisho la soka la Dunia (FIFA).
Kwa sasa Ronaldo atakuwa ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya nne nyuma ya
mshambuliaji wa FC Barcelona, Lionel Messi ambaye anaoangoza kwa
kunyakuwa Ballon d’Or mara nyingi kuliko mchezaji yeyeto katika historia
ya tuzo hizo baada ya kushinda mara tano katika miaka tofauti.
Ballon d’Or ilianza kutolewa rasmi mwaka 1956 kwa mchezaji bora wa mwaka
kutoka bara la Ulaya, huku kura za kumpata mshindi zikipigwa na
waandishi wa habari za michezo kutoka nchini ufaransa kwa kushirikiana
na chama cha soka cha nchini humo kama ilivyofanyika kwa mwaka huu.
Mwaka 1995 tuzo hizo ziliendelea kukua na kuhusisha wachezaji wote
wanaocheza katika klabu za Ulaya tu na kumfanya George Weah kuwa
mwafrika wa kwanza kushinda tuzo hizo kabla ya mwaka 2007 tuzo hizo
kuhusisha wachezaji kutoka kila pembe ya Dunia.
Katika kipindi chote hicho cha utoaji wa tuzo hiyo kubwa FIFA wao
walikuwa na tuzo yao ya mchezaji bora wa mwaka kabla ya mwaka 2010 rais
wa FIFA wa wakati huo, Sepp Blatter alipoamua kuifanya Ballon d’or kuwa
tuzo ya mchezaji bora wa dunia inayotolewa na FIFA.
Tuzo hiyo iliyofahamika kama FIFA Ballon d’Or ilianza kutolewa kuanzia
mwaka 2010-2015 ambayo mshindi alikuwa anapigiwa kura na wajumbe
wanaochaguliwa na FIFA katika mkutano maalumu, huku ikihusisha pia
kupata kikosi bora cha dunia kwa mwaka.
Mwaka 2016 raisi wa sasa wa FIFA, Gianni Infantino aliamua Balloon d’Or
iendelee kuwa tuzo inayojitegemea kama ilivyokuwa hapo awali, huku FIFA
nao wakiwa na tuzo zao za mchezaji bora wa mwaka ambazo zinatarajiwa
kutolewa mwezi Januari mwakani.
No comments:
Post a Comment